"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, October 31, 2008

Usingizi Huwa mtamu

Sex husaidia usingizi kuwa mtamu hasa ikifanywa punde tu kabla ya kulala.
Utafiti unions kwamba tend Zima la ndoa huweza kupunguza joto na mwili kujisikia relaxed kitu ambacho hupelekea kupata usingizi mnono.

Wataalamu wanatoa tahadhari kwamba kufanya mazoezi ya nguvu kabla ya kulala si jambo zuri hata kama zoezi huwa linaupa ufanisi bado hufanya ushindwe kupata usingizi ila tendo la ndoa kabla ya kulala ni utaratibu mzuri kukupa usingizi mnono pia sex husababisha uwe na usingizi mzito (deep)

Homoni (norepinephrine, serotonin, oxytocin, vasopressin, nitric oxide na prolactin)
wanazozalisha mwanaume na mwanamke baada ya kufika kileleni (orgasm) huwezesha kuwapa relief fulani inayosababisha kulala usingizi.
Pia homoni ya prolactin husababisha mtu kujisikia ameridhishwa.

Pia watu wengi wakiwa kwenye tendo la ndoa huwa hawa- focus kwenye hivyo hupumua (breathing) so wakishamaliza wanakuwa na deni la oxygen matokeo yake ni kijisikia usingizi na kulala folilo au fofofo.
Pia wapo mwanaume na wanawake kutokana na tension ya kufika kileleni baada ya kushuka huwa wamechoka hivyo kupata usingizi wa kufa mtu.

Pia kemikali za Oxytocin, melatonin na vasopressin ambazo pia huzalishwa wakati wa kufika kileleni hupumua stress na mtu hujisikia relaxed then sleepiness.

Ukipanda mlima kwa miguu hasa kama ni mrefu lazima upate resting.

Ndoa Mpya

Inawezekana wakati wa uchumba alikuwa anaonja wine tu kwenye kijiko baada ya kuingia ndani ya nyumba analala njiani, nyumbani hadi aletwe, ni wako huyo! mtunze, mpende! Kuna mambo au vitu kama hujaolewa au kuoa huwezi kuelewa tukiongea hadi siku ukiwa kwenye ndoa na hata ukielewa huwezi kuamini hadi siku yakikukuta.

Ukweli ni kwamba ni muhimu kuelewa na kujifunza kwamba tunavyoongea ni uzoefu si hadithi.
Mara nyingi wanandoa wapya hukata tamaa kabisa kwani ni kama baada ya honeymoon mambo huanza kubadilika polepole na yale ulitegemea kuwa kama unavyotaka anakuwa tofauti kabisa.
Jambo ya msingi ni kufuata kanuni na kanuni mojawapo ni:


USITAFUTE MAKOSA KWA VITU AMBAVYO TANGU UCHUMBA ULIJUA ANAVIFANYA:
Inawezekana anakula sana kuliko ulivyotegemea, inawezekana anakunywa sana kuliko ulivyotegemea, inawezekana anapenda mahaba hadi unahisi nguvu kukuishia, au anatumia pesa ovyo kama maji, au yupo antisocial hadi unaogopa, au ni mvivu hadi unaona future haina maana kuwa na yeye, au anavuta sigara kama gari moshi, au anapenda michezo hadi unakosa muda wa kuwa naye, au ni mchafu hadi rafiki zako wanakusema, au ana kelele nyumbani hata hamuhitaji radio za FM au ana ganda kwenye TV kama vile ana mkataba na vituo vya TV au anatabia ambayo inakukera mimi siijui!
Inawezekana anakula sana hadi unaamua kuficha chakula chini ya kitanda lakini wapi ananusa utadhani ana sensor ya chakula.

Kumbuka wakati wa uchumba ilikuwa rahisi sana kwako kupuuzia matatizo (uliyoyaita madogomadogo) na vile vitabia vibaya kwa sababu ulitaka kuoana naye na kweli umeoana naye.
Labda ulidhani kwamba utambadilisha siku moja kwa siri au atabadilika, ni kweli wapo ambao hubadilika ila wa kwako imeshindikana.
Pia unajitahidi kumbadilisha matokeo yake anazidi kuzama kwenye hizo tabia mbaya
.

Bottom line ni kwamba ulimpenda ukakubali kuoana naye hivyo ulifahamu kwamba yupo hivyo sasa kelele nyingi za nini?

Kumbuka ulimkubali katika raha na shida, ugonjwa na afya.
Habari njema kwako ni kwamba hakuna unaloweza kufanya kumbadilisha isipokuwa kumkubali kwanza kama alivyo.
Pia fahamu kwamba tabia zake mbaya au vitu ambavyo unaona kwako ni usumbufu kamwe haviwezi kukufanya ujisikie vibaya hadi wewe mwenyewe uamue.

Ukitaka abadilike njia ni moja tu kumuomba yule aliyemuumba ambadilishe na njia sahihi ni maombi mbele za Mungu huku ukimpenda kuliko wakati wowote.

Upendo wako ndio unaweza kumrudisha kwenye mstari unaotaka na si vita, au kumlaumu au kumsema, au kupigishana kelele au kulalamika au kutukanana.

Mathayo 19:24-26
Kwa Mungu hakuna lisilowezekana.

Tutaendelea na kanuni Zingine…………………

Thursday, October 30, 2008

Ndoa inanichanganya!

Ni kweli ukiwa katika Kristo ndoa ni tamu Je, unapita katika ndoa ngumu hata unawaza sijui kesho itakuwaje?
Kila siku ikipita unaona afadhari ya jana kwa kwani ndoa ni ngumu, ipo ovyo, kupigana kila wakati, kitu kidogo basi mzozo mkubwa huzaliwa, nyumba ni moto, ni kudharauliana tu na visa kila iitwapo leo?

Kwa tabia mbaya alizonazo partner wako unajilaumu hata kwa nini ulichukua uamuzi wa kuoana naye.
Kila ukimtazama sasa hana mvuto kabisa, amechuja, ni mbaya na havutii, hapendezi tena na anakutia kichefuhcefu unatamani mlale vyumba tofauti au asafiri miaka isiyojulikana.

Unaanza kufikiria kuachana ndiyo njia rahisi na kwamba ni permanent solution.
Wakati huohuo mawazo yako na akili yako na moyo wako na nguvu zako zote umeelekeza nje, kwa partner mwingine ambaye unaamini kwa moyo wako kwamba ni mzuri, mtamu, yupo single, independent, loving, romantic, caring na ukiwa na yeye basi maisha yatakuwa matamu zaidi.

Hata umeamua kubadilisha marafiki ili kukubaliana na nafsi yako kwamba ukiwa na hao marafiki wapya ambao ni single na wenye tabia mpya kama yako basi dunia itakupa kile unahitaji.
You can not satisfy sin!

Ukweli ni kwamba mambo si rahisi kama unavyofikiria.
Pia ni kweli mawazo kama haya (mawazo ya kujenga nyumba kwa mabua) huwapata wengi sana kwenye ndoa zetu.
Hebu vuta pumzi, pumua upya na jikusanye na kuanza kufikiria upya hata kama ndoa unaona haina ladha, imekuwa upside down, umeshindikana na haina mwelekeo ukweli bado unaweza kuirudisha kwenye siku zake za honeymoon.

Wakati unaendelea kufikiria jinsi utakavyokuwa unajirusha na partner wako mpya katika viwanja mbalimbali, please fikiria kwanza watoto wenu (mtoto), pata picha jinsi utakavyowaambia watoto kwamba wewe na mwenzako mmeachana na wao sasa wanaishi na mzazi mmoja.
Fikiria jinsi ya kugawana picha zilizomo kwenye Album yenu ya harusi, Fikiria mtakavyoanza kugawana mali.
Fikiria utasema nini kwa Mungu maana uliahidi mbele zake na mbele za wandamu kwamba utaishi na hii ndoa hadi kifo kitakapowatenganisha.
Fikiria familia, ndugu, marafiki nk
Na cheti cha ndoa je, rings je?

Je, bado unamawazo ya kuachana naye?
Una uhakika hakuna mambo mazuri kwake kuliko mambo mabaya?
Usije kuwa unataka kubadilisha seat kwenye meli ya MV Bukoba ukaishia kuzama ziwa Victoria, au usije kuwa unabadili seat kwenye meli ya TITANIC najua waweza jua nini kilitokea.

Naamini unadhani kwa sura aliyonayo huyo partner 2 basi hutapata matatizo au migogoro yoyote.
Ukweli ni kwamba hata ukipata partner mpya kinachobadilika ni sura tu matatizo ni yaleyale kwani wote ni binadamu na ndoa imara si kukimbia matatizo bali kukabiliana nayo na kujifunza na kuendelea mbele.
Je, umeshaomba ushauri kwa kiongozi wako wa dini naye akashindwa? washauri wa mambo ya ndoa nao wakashindwa?

Tafiti zinaonesha wengi walioamua kuachana na kuanza ndoa mpya baada ya muda hukutana na matatizo makubwa zaidi na magumu zaidi kuliko yale ya kwanza na hutamani kama wangerudi kwenye ndoa zao za kwanza.

Kitakachokusaidia ni kubadilisha mtazamo (altitude) siyo kubadilisha ndoa na ukweli ni kwamba ni rahisi kubaki kwenye ndoa kuliko kuanza ndoa mpya.

Usije ukaruka majivu ukakanyaga moto!

Wednesday, October 29, 2008

Linapokuja suala la rangi wanawake huonekana wapo makini zaidi na wazuri zaidi kuchagua rangi za nguo kuliko mwanaume.

Pia utafiti uliofanywa na Professor Andrew Elliot (University of Rochester in New York) unaonesha kwamba mwanamke huvutia zaidi akiwa ametinga kiwalo (viwalo) chenye rangi NYEKUNDU.

Isssue ni kwamba ukiwa (mwanamke) mwanamke akiwa amepiga pamba rangi nyekundu huvutia zaidi kwa mwanaume na kuonekana sexy na si kwamba ataonekana intelligent la hasha.

Hii ina maana kama ni mwanamke umepata mwaliko kwenda sehemu (outing) na unadhani unahitaji mwanaume akuone sexy na attractive usisumbuke tinga kiwalo rangi nyekundu badala ya green, blue au white nk.

Tuesday, October 28, 2008

Machozi ni Dawa!

Kutoa CHOZI namna hii wakati mwingine husaidia ujisikie ahueni Kitendo cha kulia na kutoa machozi ni kitu kinachokubalika na tamaduni zote duniani.
Unapocheka au kulia mwili huweza kupitia mabadiliko ya kikemia na kifizikia pia kutoa machozi au kucheka vyote vina faida kihisia, kimwili na ki-emotions.

Watu wote tunafahamu kwamba kulia (kutoa machozi) huweza kutufanya kujisikia ahueni.


AINA ZA MACHOZI
Kawaida kuna aina tatu za machozi ambayo binadamu yeyote huweza kutoa:
1. Basal Tears:
Hii ni aina ya machozi ambayo huwezesha macho yetu kuwa na majimaji kila wakati (lubiricating tears) na kufanya macho yaone vizuri
2. Reflex Tears:
Haya ni machozi ambayo huweza kutoka pale kitu kinachowasha macho kama vile kitunguu, mabomu ya machozi huingia machoni.
3. Emotional Tears
Hii ni aina ya machozi ambayo hutoka kutokana na kuguswa hisia, au tukuto moyoni.

MACHOZI YAPI HUONDOA STRESS?
Wanasayansi wamegundua kwamba Emotional tears (aina ya tatu) huwa na kiwango kikubwa cha madini ya manganese na homoni za prolactin ambazo husaidia mliaji kujisikia ahueni baada ya kilio.

Ukweli asilimia 85 ya wanawake wanakiri kwamba baada ya kutoa machozi au kulia kujisikia relief na wapo relaxed.
Kulia (KUTOA MACHOZI) ni moja ya njia ya asili ya kuondoa stress ikiwa ni pamoja na kucheka, kutembea, kukimbia, kupiga kelele na pamoja na kufanya ishara mbalimbali.


Je unaamini kwamba njia nzuri ya kuondoa stress ni mwili wako mwenyewe?


INAKUWAJE?
Tunapokuwa stressed miili yetu inajaa kemikali ambazo huweza kuharibu hisia na mood.
Baada ya kulia (kutoa machozi) mwili huweza kuondoa hizo kemikali kwa kupitia machozi.

Unapotoa machozi huku upo emotional (hasira, stress, maumivu, umeudhika, umekwazwa, mawazo, umechoka nk) zaidi mwili huweza kutoa homoni za protein kama vile Leucine Enkephalin (hii ni natural pain killer), prolactin na adrenocorticotropic hizi hupunguza stress zaidi na kukufanya usijikia raha na ahueni.

JINSI YA KULIA AU KUTOA MACHOZI
Ukishaona una stress, au umekarisika au umeumizwa au una mawazo na unajisikia kutoa machozi au kulia, tafuta sehemu ambayo ni ya siri na peke yako, sehemu yenye utulivu harafu ruhusu kilio chenye machozi yanayotiririka yenyewe hadi chini kwenye cheeks (mashavu), hakikisha unaruhusu emotions zako za ndani kuhusika katika kulia kwako ili utoe machozi mengi na ya maana (content) kwani ni tiba bora zaidi na utajisikia bora zaidi na pia kujisikia kama umetua mzigo mzito ndani ya mwili wako.

Hii ina maana kwamba kama mtu (mume au mwanamke) anatoa machozi si vema kumzuia asilia badala yake mpe usiri au muda alie hadi achoke mwenyewe kwani hiyo ni dawa muhimu kwake.

Baada ya kutoa machozi yako hakikisha unakuwa na mood nzuri kwani machozi pia husaidia kukuwezesha ku-clear Mind.

Monday, October 27, 2008

Kwa nini wanawake hutoa machozi zaidi?

Moja ya imani mojawapo katika jamii ni kwamba wanawake ni viumbe wa machozi kama watoto.
Kama ni kweli kwa nini ni viumbe wa machozi zaidi kuliko wanaume?
Wavulana na wasichana wote hutoa machozi kiwango sawa (au kulia lia) hadi wakifikia miaka 12. Wasichana wakifikisha miaka 18 hulia mara 4 zaidi ya wavulana.
Sababu ya kwanza muhimu ambayo watafiti wengi wanaielezea ni kuhusuani na malezi, utamaduni, jamii kwamba mtoto wa kiume anavyolelewa huambiwa kwamba mwanaume hatakiwi kulia ovyo, anatakiwa kuwa imara, haruhusiwi kuonesha emotions zake, anahitaji kuwa tough, huru, mbabe na mtu wa kutoa majibu kwa kila kitu si kulia tu.
Wakati watoto wa kike kadri wanavyokuwa anafundishwa kuwa wanawake yaani kuonesha sifa na alama kwamba wao ni wanawake, wawe na huruma, waoneshe emotions zao nk.

Sababu ya pili ambayo wanatafiti wengi wanaivalia njuga ni hii ya tofauti ya homoni kati ya wanaume na wanawake.
Homoni ya prolactin ambayo imo kwenuy mammary glands kwa ajili ya kuzalisha maziwa hupatikana pia kwenye damu na glands za machozi.
Wavulana na wasichana wana kiwango sawa cha hiyo homoni hadi wakifikisha miaka 12 baada ya hapo homoni ya prolactin huongezeka maradufu kwa wasichana wanapofikisha miaka 18 asilimia 60 zaidi ya wavulana.

Pia kuna tofauti ya anatomy kwenye glands za machozi kwani mara nyingi mwanamke akitoa machozi huweza kutiririka hadi kwenye cheeks wakati wanaume hata machozi yakitoka bado huishia kwa wao kujifuta bila kutiririka kama wenzao wanawake.

Pia wanawake wanapokabiliana na frustration, stress, matatizo binafsi na mabadiliko ya homoni hasa yanayosababishwa na ujauzito, kuwa katika siku zake, menopause hivi vyote huweza kusababisha machozi kutiririka.

Pia kutoa machozi kwa wanawake kuna umuhimu wake kwani husaidia kuondoa kemikali ambazo zimesababishwa na stress na hivyo baada ya machozi hujisikia ahueni fulani.

Wengine wanasemaje?
Eti wanawake wana gene (inherited) sawa na ile ipo kwenye vitunguu so maumivu kidogo tu machozi huanza kutiririka.
Eti wanawake husikia maumivu ya kitu chochote zaidi kuliko wanaume ndiyo maana wana machozi mengi.
Wanawake hutoa machozi sana hasa wakiwa kwenye siku zao hasa kutokana na mabadiliko ya homoni mwilini.
Wanawake huwa wanafahamu nini cha kufanya wakiona mtu anataka kulia machozi tofauti na wanaume.
Kwenye sherehe (harusi) wanawake hulia kwanza ndipo hulewa, wakati wanaume hulewa kwanza ndipo hulia machozi

Marriage usually breaks up over little things.
It takes only a small nail to puncture a tire.
Small mistake by a mechanic can cause the crash of a giant airplane.
A misunderstanding can start a War.
One angry word leads to shooting.
Little things mean a lot because this is a level where we live

Friday, October 24, 2008

Hatua za Ndoa

Ndoa ni furahaBinadamu peyote aliyezaliwa na mwanamke mara nyingi maisha yake huathiriwa sana na muamuzi yake na uchaguzi anaofanya, na moja ya ushaguzi na maamuzi ni suala la ndoa.
Tangu wawili mume na mke wanapooana ndoa hupitia hatua mbalimbali hadi mmoja anapokufa na baadae mwenzake kufa baadae na ndoa kuwa historia.
Zifuatazo ni hatua muhimu ambazo ndoa nyingi hupitia si lazima ndoa ipitie kila hatua bali ni ukuleles cha hatua mbalimbali ndoa hupitia na kama upo kwenye ndoa unaweza kujua ndoa yako ipo stage ipi kati ya hizi nne muhimu.

1. MAHABA:
Wanandoa wote wamepitia hatua hii, kwani ndiyo hatua iliyowapa sababu ya kuamua kuoa kwa kupeana ahadi za kuishi pamoja hadi kifo kitakapo watenganisha.
Hapa maisha ni matamu, kupendwa ni kutamu na bila mwenzako (partner) maisha unaona hayana maana kabisa.
Kila mmoja yupo romantic ni raha.
Kila mmoja hutoa maneno matamu yenye Kuonesha mapenzi ya kweli kama vile "I mis you baby!" "You are mine", I love u nk, pamoja na kupeana vizawadi vya kila aina.
Hupeana ahadi za kushinda hata wanasiasa wanapongombea vyeo utasikia “nitakupenda milele‘, ‘hakuna mwanamke mzuri kama wewe‘, ‘hakuna mwanaume wa maana kama wewe”

Huwa kunakuwa na tofauti lakini tofauti hazionekani kwani humezwa na “fall in love”
Hata wakilala hukumbatiana kama wote ni mwili mmoja.
Wanandoa wengine hii hatua hudumu kwa muda wa kuanzia miezi sita hadi miaka mitano ya kwanza.

2. MAUZAUZA:
Katika hatua hii ya pili zile tofauti ndogondogo ambazo zilikuwa hazionekani sasa huanza kujitokeza na kwa mbali huanza kukera na kusumbua na kuudhi.
Vitu vile vile ambavyo Mwanzoni vilikuwa havina maana au vilikuwa havisumbui wala kuudhi sasa huanza kuudhi na kusumbua wanandoa.
Mmoja au wote huanza kulalamika kwamba mwenzake sasa hawi kama anavyotaka, hii ina maana sasa tofauti zinaanza kujitokeza na kuonekana.

Sasa spouse anaanza Kuonekana si perfect kama ulivyokuwa unadhani.
Ndoto za kuwa ulikuwa na bonge la partner zinaanza kuyeyuka kama barafu kwenye jua, unaanza kulinganisha na wengine.
Unaanza kujiuliza na kama kuna mtu alikushauri kwamba partner anatatizo unaweza kuanza kukumbuka ushauri wake hata kama hakuwa sahihi.
Wengine kwa hatua hii tu huanza kuwaza kuhusu talaka ingawa walio na hekima na hofu ya Mungu ndani yao huanza kuchukua hatua ili kupata solution.

3. MAJONZI, MATESO NA TABU
Waingereza wanaiita “misery”
Hapa kama mtu ni mlevi basi hujikita nakuweka mizizi na hali kuwa mbaya zaidi.
Hapa wengine ndo huanza extra marital affairs, na wengine husikia maneno yanayoumiza kutoka kwa spouse wao kiasi kwamba hujiuliza hivi huyu ndo Yule nilikubali kuishi naye?

Ndoa huingia kwenye majonzi, majuto, mawazo, stress, BP, depression, kukosa usingizi, katakana, kudundana, ngeu, kulala mzungu wa nne, wengine vyumba tofauti.
Hapa ndo talaka nyingi hutokea, ni hatua ambayo imeumiza watoto wengi sana ambao walikuwa na wazazi wawili na kujikuta wakiishi na single parent.
Ndoa huwa katika mtihani, ndoa huwa katika maumivu makali kama ya jino ambayo huathiri mwili mzima.

Inaweza kutokea Mwanandoa mmoja akawa anataka talaka au ndiyo huyo mmoja analeta kasheshe zote na mwingine ndo anataka mambo yaishe na kupata suluhu.
Hapa ni mahali ambapo mwanamke au mwanaume anahitaji Kuonesha uwezo,hekima ubunifu, moyo mkuu, kutokata tama, kuwa imara, kusimama imara ili kuhakikisha anabadilisha machungu yote kuwa furaha, amani, na upendo na ndoa kuwa imara kuliko mwanzo.
Wengi wanaoachana (talaka) kwenye hii hatua wakioa mwanamke mwingine au kuolewa na mwanaume mwingine baada yamuda hujikuta anaingia kwenye matatizo yaleyale na kuanza kujiona ana mkosi au bahati mbaya kupata iana ileile ya partner, ukweli ni kwamba hajui jinsi ya kupambana na matatizo ili kupata solution.

4. KUAMKA, KUCHAGAMKA NA FURAHA MPYA
Kumbuka wote wanaoishia hatua ya 3 na kuamua kutengana si watu wabaya, bali tatizo kubwa ni kwamba walikosa tools au walikosa kujua tools zinazotumika kujenga ndoa imara.
Ndoa imara si ile isiyokutana na dhoruba bali ni ndoa ambayo inazishinda aina zote na dhoruba nakuendelea mbele kwa kasi ya ajabu.
Hata kama ndoa imekondeana na kubaki mifupa ambayo hata mtoto wa chekechea anaweza kuhesabu mifupa, bado inaweza kutiwa stake na kuwa nene ikapendeza zaidi kuliko mwanzo.
Ndoa si romance kama tunavyoangalia kwenye magazeti na TV ndoa ni maisha halisi pamoja na kukutana na setback na kuzigeuza kuwa viungo vitamu kuifanya ndoa kuwa na furaha, amani na upendo kila siku.

Kwenye hii hatua Mwanandoa huanza kuaminiana kuliko kawaida kwa sababu wanajuana na pia wametoka mbali na wamepitia mengi na wamejifunza.

NB:
Si lazima ndoa yako ipitie hatua zote 4 unaweza kuwa kwenye hatua ya kwanza miaka yako yote kama utaruhusu Kristo kuwa kiongozi wa ndoa yako kwani kama yeye anavyolipenda kanisa basi mume na mke wanahitaji kuishi kwa mfano wa Kristo na kanisa.

Tuesday, October 21, 2008

Mwanamke tu!

Kufika kileleni hupunguza maumivu ya kichwa:
Kama unaumwa kichwa mara nyingi huwezi kujisikia kupata sex, hata hivyo kupata sex ni njia moja wapo ya kuondoa maumivu ya kichwa hasa kitendo cha kufika kileleni.
Unapofika kileleni (orgasm) kawaida mwili hutoa bio-chemical ambayo hufanya mwili u-relax na kuondoa maumivu pia huongeza idadi ya serotin ili kukupa sex appetite zaidi.

Sex wakati wa hedhi ni hatari kwa maambukizi ya bacteria.
Ingawa kufanya sex wakati upo kwenye siku zako kunakuhakikishia kutopata mimba bado ni wakati mzuri sana kupata maambukizi ya magonjwa.
Mwanamake anapokuwa hedhi kiwango acha acid/alkaline kinabadilika na kuwezesha bacteria kustawi vizuri kwenye uke.
Kawaida uke upo Acidic na bacteria hawapendi kabisa hayo mazingira, damu huongeza pH na kuwa alkaline zaidi hali inayoruhusu bacteria kustawi kwa kasi ya ajabu.
Wengine hutumia kinga!
Hata hivyo kwa nini usisubiri wako umalizi siku zako then uendelee kujirusha na mumeo?

Si sex mara kwa mara bali oral sex husababisha yeast.
Utafiti unaonesha mwanaume hawezi kumwambukiza yeast mwanamke kupitia sex, bali inatokana na mwanamke kuwa na upungufu wa kinga kupambana na yeast.
Kati ya wanawake na wanaume 200 waliofanyiwa utafiti ilionesha kwamba wanawake waliopata oral sex kutoka kwa waume zao walipata yeast au yeast ilijirudia tena.
Hii ina maana kwamba kama mwanamke anatatizo la kuwa affected na yeast kupata oral sex kwake ni risk kubwa zaidi kuendelea kuugua.
Pia asilimia 80 ya wanawake wanaougua yeast husababishwa na tofauti ya homoni (imbalance) mwilini, kuwa na sukari nyingi mwilini, stress, birth control pills nk.

Harufu kama ya mkojo kuzunguka uke si mkojo bali ni jasho.
Kwa kuwa jasho lina aina ya secretions zenye compositions sawa na mkojo ni jambo la kawaida mwanamke kujiona anaharufu ya mkojo kwenye sehemu zake za siri au nguo yake ya ndani (chupi)
Ni vizuri kuosha sehemu V- zone kwa maji na sabuni mara kwa mara baada ya haja ndogo na kupaka poda yenye asili wanga (cornstarch) ambayo huondoa unyevu au jasho, pia usivae kufuli aina ya Nylon ambazo huongeza joto na kusababisha kutoa jasho zaidi.
Ukiona harufu imepotea basi ujue ilikuwa jasho na si harufu ya mkojo na ukiona harufu bado vilevile mwone Daktari.


Monday, October 20, 2008

A man and a woman


EATING OUT
When the bill arrives, Mark, Chris, Eric and Tom will each throw in a $20, even though it's only for $32.50. None of them will have anything smaller and none will actually admit they want change back.
When the women get their bill, out come the pocket calculators.
MONEY
A man will pay $2 for a $1 item he needs.
A woman will pay $1 for a $2 item that she doesn't need, but it's on sale.
BATHROOMS
A man has five items in his bathroom: a toothbrush, shaving cream, razor, a bar of soap, and a towel from the Marriott.
The average number of items in the typical woman's bathroom is 337.
A man would not be able to identify most of these items.
ARGUMENTS
A woman has the last word in any argument.
Anything a man says after that... Is the beginning of a new argument.
CATS
Women love cats.Men say they love cats, but when women aren't looking, men kick cats.
FUTURE
A woman worries about the future until she gets a husband.
A man never worries about the future until he gets a wife.
SUCCESS
A successful man is one who makes more money than his wife can spend.
A successful woman is one who can find such a man.
MARRIAGE
A woman marries a man expecting he will change, but he doesn't.
A man marries a woman expecting that she won't change, and shedoes.
DRESSING UP
A woman will dress up to go shopping, water the plants, empty the garbage, answer the phone, read a book, and get the mail.
A man will dress up for weddings and funerals.
NATURAL
Men wake up as good-looking as they went to bed.
Women somehow deteriorate during the night.
THOUGHT FOR THE DAY
Any married man should forget his mistakes.
There's no use in twopeople remembering the same thing.

Sunday, October 19, 2008

Jumapili Njema


"Wewe ni Kimbilio la vizazi vyote"

Saturday, October 18, 2008

Wanapopiga picha tu!

Jamii zingine ukitaka mume na mke washikane mikono au kutabasamu waambie unawapiga picha, vinginevyo wanaweza kukaa miaka nenda rudi hakuna kushikana mikono kufurahiana, au kutabasamu acha kukumbatiana.What is Nonsexual Touch?
Here are more examples of affection and nonsexual touch in marriage:
Holding hands both privately and in public.
Nonsexual massage of neck, shoulders, back.
Hugs.
Sitting close to one another both privately and in public.
Kisses, especially unexpected kisses.
Holding one another.
Cuddling, snuggling.
Walking arm in arm.
Stroking.
Reaching across the table to touch hands.
Simple caring and tender gestures such as resting your hand on your spouse's leg.
Putting your hand on your spouse's shoulder.
Gentle caresses.

Why is Nonsexual Touch Important in Your Marriage?
Nonsexual touch and other signs of affection strengthens your marriage relationship, creates a comforting and calming atmosphere in your home, builds trust between the two of you, and deepens your intimacy with one another.
Do not let nonsexual touch become a thing of the past in your marriage!

Friday, October 17, 2008

Ua tu huweza kubadili hali ya upendo ktk ndoa yako
Mwanamke anahitaji alama za upendo kutoka kwa mwanaume.
Mwanaume anapompelekea mwanamke (mkewe) zawadi hii hudhihirisha kwamba mwanamke ana thamani na anamjali, mfano zawadi ya maua huonesha kwamba mwanamke ni mrembo na ana uzuri ambao mwanaume anaukubali.

Iwe zawadi kubwa au ndogo zote hutoa maana halisi ya mapenzi, humsaidia mwanamke kufahamu kwamba yeye ni mwanamke special, na kumpa zawadi mwanamke ni njia ya kumpa heshima na thamani ambayo mwanamke huhitaji kutoka kwa mume wake.

Kuna alama nyingi ambazo huonesha kwamba unampenda mke wako moja ni kumpa zawadi mbalimbali kama maua au kadi yenye ujumbe unaoelezea hisia zako kwake nk.
Ni muhimu mwanaume kuwa creative na innovative katika kuhakikisha penzi linazidi kunawiri kila iitwapo leo katika ndoa yako na unajitahidi kutoa hisia zako original pale unampa zawadi au kumwandikia text message (sms) yoyote, kitu cha msingi afahamu kwamba kuna mwanaume anayemjali.

Wanaume wengi huwa wanakuwa wataalamu na wajuzi sana wa kuwapelekea wapenzi wao zawadi motomoto na kadi zenye maneno matamu matamu mwanzo wa mahusiano (uchumba au ndoa) na baada ya muda wanaachana kabisa na hiyo tabia, hili ni kosa kubwa sana ktk masuala ya ndoa, kutoa zawadi hakuzeeki wala ku-expire hudumu na kudumu na kudumu, till death do us apart, ni njia muhimu sana ya Kuonesha unamjali mke wako.

Kama ni mwanamke unakumbukani lini mpenzi wako amekuletea zawadi?
Na kama ni mwanaume je, unakumbuka ni lini umempelekea mke wako zawadi?
Eti haya mambo yamepitwa na wakati!
Shauri yako!
Usione vinaelea vimeundwa!

Wanawake wengi kwenye ndoa au mahusiano hujisikia na kujiona hawapendwi na waume zao, hujisikia wanaume hawawajali, ukiangalia kwa undani moja ya sababu ni mwanaume ameacha kumpa zawadi hata ndogondogo, au maneno mazuri (notes) au kadi kama alivyokuwa anafanya mwanzo na kwa sababu ulikuwa unampa na ueacha anajiona humpendi tena, si ulikuwa unampa? sasa imekuwaje? unampelekea nani tena? maana ulikuwa na tabia ya kutoa zawadi.

Kiwango cha attention unayompa mke wako ni alama muhimu ya Kuonesha upendo wako kwake.

Mwanamke hujisikia anapendwa na kwamba unamjali pale mwanaume:-
Unampompa zawadi iwe ndo au kubwa,
Unapompa zawadi ya kadi yenye maneno mazuri yanayoelezea hisia zako kwake,
Unapomhudumia kwa kumjali,
Unapomsikiliza yeye na kujiona anasikilizwa,
Unapjitolea kumsaidia kazi ndgondogo na mambo ambayo anajisikia upo na yeye,
Unapompa plan za mambo mbalimbali mnayotaka kufanya pamoja kama familia iwe "outing", likizo, business n.k,

Pale unapomuuliza anavyojisikia hasa baada ya kazi au unapohisi emotions zake hazipo sawa,
Unapochukua muda wa ziada kuwa naye na kuwa kwa ajili yake,
Unaposhirikiana naye ktk huzuni au tatizo huku ukimfariji na kumkumbatia,
Unapompa nafasi ya kujisikia huru kwako hata kudeka (si wote)
Unapogundua kwamba amevaa amependeza mavazi na nywele na kumpa sifa anazostahili.
Unapom-surprise na zawadi au notes na
Unapompigia simu ukiwa umesafiri na kumuulizia anaendeleaje na jinsi gani utakuwa unaongea naye na kuwasiliana naye.

Thursday, October 16, 2008

Wengine wanavalisha miti viatu, Na wengine kupata kiatu chochote cha kuvaa ni muujiza!

Nguvu Mbili

Tatizo kubwa la wanawake wakiwa kwenye mahusiano (ndoa au uchumba) ni kwamba huwa wanasahau mahitaji yao na kujikuta wanavutwa na kuhusika zaidi na mahitasji ya wengine au wapenzi wao kihisia na kisaikolojia.

Challenge kubwa inaowakabili wanawake wote duniani wakishaiingia kwenye mahusiano ni uwezo wa kuimarisha sense of self, kujitambua, kujiamini, na kuanza na wao kwanza kabla ya mpenzi hasa linapotokea suala la mgogoro.
Wakati mwanamke hu-expand mwanaume hu-contract.
Kama ilivyo nguvu ya centripetal amabyo huhusika kuvuta kitu katikati (mwanaume) na nguvu ya centrifugal ambayo huhusika kuvuta kitu pembeni (mwanamke) kutoka katikati ndiyo ilivyo kwa mwanamke na mwanaume kwani mwanaume mara zote hurudi kwenye centerpoint hupungua, husinyaa, huongea kidogo, huongea kwenye point, wakati mwanamke yeye hupanuka kutoka katikati kwenda pembeni, huongea sana hata kama si point, huvutika kuongeza maongezi.

Ndiyo maana wanaume hulaumiwa sana linapokuja suala la mawasiliano kwani mwanamke na mwanaume wanapoongea mwanamke hu-expand maongezi na mwanaume hui-contract na kuongea kwenye point.

Kawaida mwanaume hufikiria kwanza (kwa ndani) kile anataka kuongea ili kujua kama ni point, wakati mwenzake mwanamke huendelea kuongea tu na anapoongea inamsaidia kuijua point,
Hii ina maana mwanamke huongea iliajue point na mwanaume hujua point ili aongee.

Bila kujua hii tofauti basi mwanaume asiyejali anaweza kusikitika sana kumsikiliza mpenzi wake na kuona alikuwa anaongea pumba au pointless na amempotezea muda wake au kuendelea kubishana kwamba mwanamke haongei point au kumkatisha kwa kuwa anachoongea hakielewiki.

Mwanaume anayejali husikiliza kwanza hata kama mwanamke anaongea kitu ambacho anahisi hakieleweki hata hivyo baadae ataelewa na mwanamke anajisikia mwanaume anamjali na kumsikiliza na maisha yanaenda

Wenzetu wanatunza joto!Wanaume wana ngozi nene kuliko wanawake, ndiyo maana wanawake huwahi kupata ndita (wrinkles) haraka na mapema kuliko wanaume wanapozeeka.

Wanaume wana damu nzito kuliko wanawake, hii ina maana kwamba wanaume huwa na damu yenye oxygen nyingi zaidi na kupelekea kuwa na energy kubwa zaidi pia wanaume hupumua na kuvuta hewa nyingi kuliko wanawake hii ina maana wanawake huvuta hewa mara nyingi na hupumua mara nyingi zaidi kuliko wanaume.

Wanaume wana mifupa mikubwa kuliko wanawake pia mifupa ya wanaume na wanawake imejipanga tofauti ndiyo maana kuna tofauti kubwa sana katika kutembea kwa mwanaume na mwanamke.

Wanaume wana misuli mingi kuliko fat katika miili yao hivyo kuwa rahisi kupunguza uzito, wanawake wana layer ya ziada ya fat ndani ya ngozi ambayo huwawezesha kuwa na joto la ziada hata wakati wa baridi hivyo wanawake huwa na energy reserve nzuri na joto la asili kuliko wanaume, ndiyo maana wakati wa baridi sehemu zingine kiwango cha wanawake kupata mimba huongezeka maradufu.
Guess why?
Malizia mwenyewe!

Wednesday, October 15, 2008

Moja ya usafri wa watoto wa shule huko India.
Kazi kwelikweli!

Hudhoofisha Afya

Kuolewa au kuoa ni kitu kingine na kujenga ndoa ni kitu kingine.
Ndoa yenye furaha huwa haijengwi siku ya ndoa au siku ya harusi au siku ya kuvalishana pete tu bali hujengwa kila iitwapo leo.

Ndoa inapokuwa na mgogoro mara nyingi (si zote) wanandoa huathirika zaidi na mara nyingi mwanamke huonekana ni makini na kuelekeza juhudi nyingi ili mahusiano yaendelee na kuwa yenye afya njema ( ingawa si wanawake)

Tafiti nyingi (mfano Doctor Robewrt W. Levenson PhD) University of California) zinaonesha kwamba migogro mingi ya mahusiano (Ndoa au uchumba) mara nyingi mwanamke ndiye huathirika zaidi.
Wanaume hata kama ndoa ina mgogoro bado huonekana wapo physically fit na mentally fit kabisa nakuendelea kujichanganya na wenzao kama vile hakuna linaloendelea ktk ndoa zao wakati wanawake ndoa ikiwa na tatizo basi kwa kumwangalia tu unaweza kupata ujumbe kamili achilia kukoswakoswa kugongwa na magari.

Why?
Wanawake na wanaume hutofautiana sana jinsi ya kukabiliana au kuchimbua (ku-process) hisia (feelings), tukuto (emotions) zinazotokana na mgogoro uliopo.
Wanaume huweza kuvumilia tukuto na hisia zao bila kutegemea mwanamke au kuegemea kwa mwanamke, hii ina maana kwamba mwanaume hujikana, hujiondoa, huwa hajali, hu-withdraw hisia zake au kujisikia kwamba ana mgogoro na matokeo yake haathiriki sana.

Wakati huohuo mwanamke yeye kwanza ni mtu wahisia na tukuto (feelings & emotions ) tatizo likitokea hujihusisha zaidi, huji-engage, hujitoa (dedicate), huji-commit kupata solution, hujiuliza maswali wengine watasemaje? huwaza zaidi kuhusu yeye na mpenzi wake na jinsi ya kusaidia mgogoro uishe, matokeo yake huathirika zaidi na hudhoofisha afya yake na kuweza kukumbwa na magonjwa kama shinikizo la damu, stress, depression, stroke, magonjwa ya moyo nk.

Mwanamke afanyeje?
Jambo la msingi ambalo mwanamke anaweza kufanya ndoa inapokuwa katika mgogoro ni kumuomba Mungu ampe hekima, busara na ushindi ili ndoa iwe katika mstari kwani ni jaribu na lazima ushinde, kila ndoa bora imejaribiwa na kuonekana imara, usione vinaelea vimeundwa.

Pia mwanamke anahitaji kuwa positive, kwamba anaweza na kwamba bado ndoa ipo, mume ni wake na aendelee kumpenda na kutamkia mambo mazuri mume wake kuliko kuwa na mtazamo negative.
Pia mwamke anahitaji kujiamini kwamba chanzo cha furaha yake ni Mungu hivyo hakuna binadamu anaweza kuondoa furaha yake hadi aamue mwenyewe.

Tuesday, October 14, 2008

Hata chini inawezekana!

Wengine akimeza pills hupoteza libido, wengine hupata kichefuchefu, wengine maumivu ya tumbo na nk. Linapokuja suala la uzazi wa mpango kawaida kuna vidonge ambavyo wanawake hutumia na humeza kwa mdomo (oral) hata hivyo Steve Goldstein, MD, Professor obstetrics and gynecology at NYU Medical Center in New York City anakiri kwamba "kuingiza vidonge vya mpango wa uzazi ukeni badala ya njia ya kawaida mdomoni hakuna tatizo na huweza kupunguza side effectsza birth control pills kama vile kujisikia kichefuchefu au kutapika".

Hii ni siri mpya ambayo imevumbuliwa na wanasayansi wa kiisrael na kuchapishwa katika gazeti la Contraception.

Madaktari walilinganisha makundi mawili ya wanawake waliokuwa wanatumia vidonge vya uzazi wa mpango, kundi moja kwa kumeza mdomoni na kundi la pili kuingiza ukeni na kuacha viyeyuke vyenyewe.
Wanawake waliotumia njia ya uke hawakupata kichefuchefu, wala maumivu ya kichwa, au matiti kubadilika kuwa laini zaidi, au kuwa na maumivu wakati wa hedhi, au maumivu ya tumbo tofauti na wale waliomeza mdomoni.

Hata hivyo kabla ya kuingiza hizo pills huko south pole au V- zone hakikisha umepata ushauri wa daktari hata kama unadhani hii njia ni bora kwako.

Monday, October 13, 2008

Je, Upweke ni Ugonjwa?

Saturday, October 11, 2008

Urembo na mvuto

Kijiji kwetu mwanamke mzuri ni yule anajua kushika jembe na kulima pamoja na tabia njema hata hivyo huko Thailand uzuri wa mwanamke ni Shingo yenye rings, hapo mchumba hakosi!

Suala la ndoa ni suala la kiutamaduni zaidi.
Katika jamii nyingi kuwa romantic na uzuri wa kimwili (physical attraction) jambo la muhimu sana.
Afya, umri na mwonekano pia huwa jambo linalotazamwa sana kila mmoja anapotafuta mwenzi wake.
Pia mwanamke kuonekana anavutia hutofautiana sana katokana na utamaduni, jadi na mitazamo ya jamii husika.
Kwa mfano kama umezaliwa huko Thailand, mwanamke anayevutia ni mwanamke mwenye shingo ndefu iliyovalisha rings (tazama picha hapo juu).
Pia kama umezaliwa jamii za Afrika au Amerika ya kusini na katika visiwa vya karibean, basi mwanamke mwenye umbo nene na makalio makubwa huonekana ndiye anayevutia kuliko aliye kimbaumbau ambaye huonekana mgonjwa.

Ingawa Ulaya na Amerika kaskazini pamoja na vijana wa kizazi kipya bado wanaona mwanamke mnene hapendezi na ana umbo lisilo na afya.
Na huko China mwanamke mwenye umbo la uso wa mviringo kama mwezi huwachanganya wanaume bado wanamke mwenye mguuu wa nguvu huonekana si lolote na wakati huohuo wanaume wenzao wa Afrika mwanamke mwenye mguu wa nguvu huonekana wa uhakika.
Pia suala la umri katika kuoana kwa sasa halina tatizo sana
Hata hivyo kutokana na kupanuka kwa mawasiliano ya mitandao na mwingiliano wa jamii globally mtazamo wa kizazi kipya kuhusu urembo na uzuri linakuwa suala kubwa na la kibiashara zaidi kwani wanawake na wanaume wengi sasa wanafanya upasuaji ili krekebisha mwonekano iwe mguu, matiti, makalio au uso na wengine hushinda saloon.

Uzuri na urembo wa kweli huanzia moyoni na tabia pamoja na kujifahamu kwamba kama ulivyo umekamilika na upo kwa ajili ya utukufu wa aliyekuumba.
Je, kwenu mwanamke mrembo ni yupi?

Friday, October 10, 2008

Ulimi nao mmm!

Maneno yetu huweza kubomoa ndoa kama mmomonyoko wa udongo! Utafiti unaonesha kuwa mtu mmoja kawaida huwa na maneno 5,000 ambayo hutumia kila siku kuongea kuhusu mawazo, hisia, matukio na mahitaji mbalimbali ya mawasiliano ya kila siku.

Na hayo maneno ambayo binadamu huongea kila siku yana nguvu ya ajabu mno hata kuweza kuponya au kuumiza, kutia moyo au kukatisha tamaa, kusifia au kulaumu, kuleta uhai au kuleta kifo, kuimairsha au kudhoofisha, kuleta ukweli au kuleta uwongo, kubariki au kulaani.

Pia maisha tunayoishi ni matokeo ya kile unaongea, hivyo basi kufanikiwa kwako au kushindwa kwako katika maisha au mahusiano mara nyingi ni matokeo ya matumizi ya kinywa chako.

Pia tafiti nyingi zinabainisha kwamba kinachoelezea mafanikio na kushindwa kwa mahusinao (ndoa) si uzuri wa mapenzi au kufanana kwa wahusika au kufanana kwa vitu wanavyovipenda au uchumi au umaskini au kiwango cha elimu cha wahusika bali ni maneno wanayoongea kila mmoja kwa mwenzake.

Wapo wanandoa ambao huongea maneno ambayo ni death sentence kwa ndoa zao au ni maneno yenye mtazamo hasi (negative) kwa kila jambo katika ndoa au mahusiano yao au kila kinachoongelewa wao huchuja na kuweka katika msimamo wa negatives.
Kumbuka maneno ya aina hii yasipobadilika huwa mfano wa seli za kansa kiasi kwamba huendelea kumomonyoa ndoa au mahusiano kama mmomonyoko wa udongo na huishia kuiua kabisa ndoa.

Kama ni mwanaume unahitaji kuongea maneno mazuri kwa mke wako kwa kadri unavyotaka awe.
Acha kuongea na kuendelea kusisitiza yale anafanya vibaya, jifunze kumsifia kwa mfano:-
“Mke wangu ni mzuri, mke wangu unapendeza, mke wangu una akili, mke wangu unanifaa, mke wangu ni mwanamke wa tofauti duaniani hakuna kama wewe, mke wangu ni mtamu, mke wangu una uwezo na hekima ya ajabu”

Na mwanamke naye ni hivyo hivyo lazima uongee maneno ya kujenga ndoa si kubomoa kama vile:-
“Eti mume wangu ni mbishi, mume wangu hunisikilizi, mume wangu hunijali, mume wangu huna akili, mume wangu huna lolote, mume wangu siku hizi hunivutii, mume wangu hanipendi nk”

Maneno unayotimia kwa mwenzi wako yanaweza kuumba hisia za furaha, upendo, ukaribu, sifa, kutia moyo, kufariji, kumpa nguvu, kumuinua pia maneno yako yanaweza kuumba hisia za maumivu na hasira na hatimaye kutoana ngeu.

"Words are, of course, the most powerful drug used by mankind."

Thursday, October 9, 2008

You can close the windows and darken your room, and you can open the windows and let light in.

It is a matter of choice.

Your mind is your room.

Do you darken it or do you fill it with light?

Eti Kwa simu hawajambo!

Mawasiliano ni jambo a msingi sana kwa jamii ya sasa (information society), Pia mawasiliano ni kiungo muhimu cha kuunganisha watu katika jamii iwe familia, biashara hata utendaji wa ofisi mbalimbali.

Linapokuja suala la mahusiano, mawasiliano ni jambo a msingi sana kati ya wawili wanaopendana na haliwezi kukwepeka.

Kawaida ili barua ifike kwa mhusika basi haina budi kuwa na anwani (address), vivyo hivyo ili watu wawili walio katika mahusiano waweze kuwa na mahusiano mazuri basi mawasiliano ni muhimu na bila mawasiliano ni sawa na barua isiyo na anwani kwani bila anwani watu wa posta watashindwa wapeleke wapi hiyo barua.

Kuna aia nyingi ya kuwasiliana kati ya mtu na mtu kama vile simu za mezani, simu za mkononi (cellular), ujumbe mfupi wa maneno (sms), barua (posta), kuonana (face to face) na email.
Utafiti unaonesha kwamba wanaume wanapenda sana kuwasiliana kwa kuonana (face to face) wakati wanawake wao wanapenda sana kuwasiliana kwa kutumia simu za mkononi (cellular) hii ina maaa kwamba wanawake hujisikia vizuri sana kupigiwa simu na kupiga simu zao (mobile) kuliko kuonana na kuongea.

Je, kuna ukweli wowote kwamba wan awake ni vinara wa kuongeakwenye simu za mkononi?

Joke:
Women are like cell phones.
They like to be held and talked to, but push the wrong button, and you'l............................

Wednesday, October 8, 2008

Raha na vikwazo!

Huanzia kwenye ubongo kwanza! Uumbaji wa Mungu ni wa ajabu sana hasa linapokuja suala la mahusiano Kati ya mwanamke na mwanaume katika ndoa.
Ili kuridhishana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume jambo la msingi ni kufahamu vizuri hatua kamili ambazo ili tendo la ndoa likamilike lazima zifuatwe na hasara zake.

Hata hivyo wakati mwingine wanandoa hujikuta katika mgogoro katika eneo lingine la ndoa na matokeo yake masuala ya kitandani pia huwa ovyo na zaidi kuanza kulalamikiana kila mmoja akimlaumu mwenzake.
Kawaida tendo la ndoa hupitia hatua tatu muhimu ambazo ni vizuri kila mwanandoa kufahamu na pia ni muhimu kufahamu kwamba kila hatua huwa na vikwazo vyake na hili lisipozingatiwa unaweza kujisikia wewe tu ndiye unayepunjwa kwenye ndoa.

Hizi hatua tatu muhimu kila moja ina uwezo wake na mzunguko wake binafsi na vikwazo vyake.
Hatua ya kwanza ni hamu (desire) ya tendo la ndoa na ili kupata hamu ya tendo la ndoa lazima ubongo uhusike kwani kwenye ubongo kuna mfumo maalumu wa fahamu (neural) ambao kutokana na hali iliyopo mtu hujisikia hamu.

Hatua ya pili ni kusisimka (excitement) hii ni hatuas ambayo baada ya kuwa na hamu damu huweza kusambaa sehemu muhimu kama vile matiti, uke au uume kwa ajili ya kuhakikisha sex inafanyika.

Hatua ya mwisho ni kufika kileleni (orgasm) hii hutokana na kukaza kwa misuli ya uke au uume na kutoa raha isiyoelezeka na baada ya hapo ni kama mwisho ya furaha ya tendo lenyewe.

Nini vikwazo vya hatua hizo muhimu?

Wasiwasi, hofu, mashaka, woga, kuogopa na uadui hupelekea mtu kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Fadhaa zozote kuhusu sex hupelekea kukosa kusisimka na kuwa tayari kwa mapenzi pia ku-concentrate kwenye skills na techniques au style za sex kuliko kufurahia tendo lenyewe hupelekea kushindwa kufika kileleni.

Kumbuka utendaji wa sex katika ndoa huonesha hali ya ndoa nzima katika mambo yote kwani mara nyingi ndoa ikiwa na mgogoro hata tendo la ndoa huwa ni bora liende, si kuridhishana bali wajibu na ukweli unabaki kwamba sex katika ndoa huelezea ndoa ipoje.

Kama kuna mgogoro ambao haujapata jibu au kutokuelewana katika ndoa basi mfumo mzima wa sex hubadilika.

Je, unajisikia raha na hamu kubwa na kusisimka kwa ajabu kama zile siku za kwamba wakati mnaoana?
Je, jinsi unavyoridhika na tendo la ndoa ni sawa na ulivyokuwa unategemea? Au ni kama wajibu na si kupeana raha?
Ukweli unao mwenyewe.

Uzoefu unaonesha jinsi wanandoa wanavyozidi kuishi pamoja; tendo la ndoa huwa zuri zaidi na la kuridhisha zaidi kuliko mwanzo au miaka ya mwanzo.

Tuesday, October 7, 2008

Kazi kwelikweli!

Monday, October 6, 2008

Ni kujitoa

Kuwa na mahusiano yenye afya kwenye ndoa au uchumba huhitaji nguvu za ziada wakati mwingine.
Hakuna kitu kizuri kama kuwa na mahusiano bora.
Pia hakuna kitu kizuri kama kupendwa na Yule unayempenda.

Hata hivyo kazi inahitajika kuhakikisha mapenzi yanadumu na kudumu kwani kuna milima na mabonde.
Pia bila kuvumiliana, kuchukuliana na kumtanguliza mwenzako kwa kusameheana na kutiana moyo bado mahusiano yanaweza kufika mahali yakashindikana.

Friday, October 3, 2008

Ngoma ya asili ilivyosababisha binti kubakwa kwenye sherehe ya mfalme

Mwaka huu mwezi uliopita, ngoma hiyo iliyoleta balaa baada ya binti mwenye umri wa miaka 14 kubakwa na kundi la vijana, ambao walimvizia alipokuwa amekwenda kununua vitafunwa baada ya ngoma kumalizika.
Licha ya ulinzi mkali wa Polisi na askari wengine wa usalama wanaokuwa wanawalinda mabinti hao bikira ambao hucheza nusu utupu mbele ya mfalme kama sehemu ya utamaduni, lakini vijana hao walifanikiwa kufanya kitendo hicho ambacho wanaharakati wa haki wanasema ni cha udhalilishaji.
Ngoma hiyo iliyokuwa ikichezwa mahususi kwa ajili ya sherehe za kutimiza miaka 60 ya mfalme wao Goodwill Zwelithini wa eNyokeni KwaNongoma. Wakati wa kucheza ngoma hiyo, huwashirikisha mabinti 20,000 kutoka maeneo mbalimbali ya ngome ya kifalme.
Soma: http://www.habarileo.co.tz/makala/?id=12637

Source: Ikunda Erick Daily News; Thursday,October 02, 2008 @20:04

Thursday, October 2, 2008

Ipi si Kweli

A:
Kuoana katika umri mdogo (teenager) hupelekea ndoa kushindwa mara nyingi zaidi ukilinganisha na wale wanaooana katika umri mkubwa (zaidi ya miaka 20)

B:
Jinsi wanandoa wanavyofanana katika imani, asili yao, malengo katika maisha, maono na tamaduni hupelekea kuwa na ndoa imara.

C:
Kuishi pamoja kabla ya ndoa imethibitika kwamba si lolote, hasa linapokuja suala la uimara wa ndoa ukilinganisha na wale wanaofunga ndoa kwanza then kuishi pamoja.

D:
Ndoa (kuoana) huwezesha mtu kuongeza kipato na utajiri zaidi kuliko kuwa single.

E:
Watu walio kwenye ndoa wana maisha yanayoridhisha zaidi linapokuja suala la tendo la ndoa kuliko wale ambao wapo single.

F:
Watu wanaoishi kwenye familia ambazo baba na mama wameachana (talaka) hata wakioa nao huishia kupeana talaka.

Harusi zingine kazi kwelikweli!

Wednesday, October 1, 2008

Wangari Maathai

Wangari Maathai ni mtoto wa tatu kati ya watoto sita, alizaliwa tarehe 1 April, 1940 katika kijiji cha Ihithe tarafa ya Tetu wilaya ya Nyeri Kenya.
Yeye ni mwanamke wa kwanza Africa kupata Nobel Peace Prize kutokana na kuchangia kazi za maendeleo endelevu na haki/demokrasi/wanawake


Anatoka katika kabila la Kikuyu na amewahi kuwa mbunge wa Mbunge la Kenya na Waziri wa Mazingira na Mali Asili katika serikali ya Rais Mwai Kibaki.

Elimu yake na kazi:
Baada ya kumaliza elimu ya msingi katika kijiji cha Ihithe alijiunga na Shule ya Sekondari ya Loreto Limuru Kenya ndipo akapata scholarship kwenda kusoma Marekani degree yake ya kwanza (BS, Biology, Mount St. Scholastica College, USA (1964) na baadaye MS, Biological Sciences, University of Pittsburgh, USA (1966) aliporudi Kenya then akarudi Kenya na kupata PhD (PhD, Anatomy, University of Nairobi (1971)
Amewahi kufanya kazi idara ya mifugo chuo kikuu cha Nairobi kuanzia mwaka 1971.
Mwaka 1977 alianzisha Green Belt Movement shirika lisilo la kiserikali lilijohusisha na upandaji miti na wamefanikiwa kupanda miti zaidi ya milioni 40 hadi sasa.

Ndoa yake:
Wangari aliolewa mwaka 1969 na Mwangi Muta mwanasiasa mojawapo Kenya walifanikiwa kupata watoto 3 ambao ni Waweru, Wanjira and Muta.
Mwaka 1980 ndoa ilivunjika na mumewe Mwangi alidai kwamba Wangari alikuwa mwanamke mgumu asiyekubali kuongozwa na mumewe na msomi mwenye jeuri katika ndoa yake.
Ingawa Wangari alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha ndoa inaendelea mume wake alitumia wanasheria wenye uwezo hadi jaji akaamua talaka itolewe.

Hata hivyo baada ya kuhojiwa na vyombo vya habari Wangari alikiri kwamba jaji hakumtendea haki na kwamba amekura rushwa, kitendo kilichosababisha atiwe jela miezi sita kuwa kumsemea vibaya jaji.

Katika suala la ndoa anasema kwamba yeye alipigana kufa na kupona ili ndoa isivunjike hata hivyo mume wake hakukubali na hii inatokana na mfumo dume wa kiafrika kwamba mwanamke akiwa amesoma, anakipato kikubwa basi mwanaume huwa hajiamini na kuona anapoteza madaraka yake katika ndoa.

Mambo magumu aliyokutana nayo:
Ndoa kuvunjika (talaka)
Kufungwa jela kwa kumwambia jaji alikuwa mla rushwa na mfumo mzima wa mahakama za Kenya
Kukataliwa kurudi kufundisha Chuo Kikuu cha Nairobi
Kufukuzwa kukaa katika nyumba ya chuo Kikuu bila kujua wapi kwa kwenda
Kutiwa jela kwa kupigania haki za Mazingira na siasa

Anashauri kwamba kama kweli things have fallen apart, haina haja kukaa achini na kuanza kuhuzunika na kuugulia maisha yako yote, amka, tembea na endelea na safari na mbele ya safari mambo yatabadilika na kuwa safi.

To Know That we Know What we Know, and to Know That we Do Not Know What we Do not Know; That is a True Knowledge.