"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, October 14, 2008

Hata chini inawezekana!

Wengine akimeza pills hupoteza libido, wengine hupata kichefuchefu, wengine maumivu ya tumbo na nk. Linapokuja suala la uzazi wa mpango kawaida kuna vidonge ambavyo wanawake hutumia na humeza kwa mdomo (oral) hata hivyo Steve Goldstein, MD, Professor obstetrics and gynecology at NYU Medical Center in New York City anakiri kwamba "kuingiza vidonge vya mpango wa uzazi ukeni badala ya njia ya kawaida mdomoni hakuna tatizo na huweza kupunguza side effectsza birth control pills kama vile kujisikia kichefuchefu au kutapika".

Hii ni siri mpya ambayo imevumbuliwa na wanasayansi wa kiisrael na kuchapishwa katika gazeti la Contraception.

Madaktari walilinganisha makundi mawili ya wanawake waliokuwa wanatumia vidonge vya uzazi wa mpango, kundi moja kwa kumeza mdomoni na kundi la pili kuingiza ukeni na kuacha viyeyuke vyenyewe.
Wanawake waliotumia njia ya uke hawakupata kichefuchefu, wala maumivu ya kichwa, au matiti kubadilika kuwa laini zaidi, au kuwa na maumivu wakati wa hedhi, au maumivu ya tumbo tofauti na wale waliomeza mdomoni.

Hata hivyo kabla ya kuingiza hizo pills huko south pole au V- zone hakikisha umepata ushauri wa daktari hata kama unadhani hii njia ni bora kwako.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hapo sasa kuna kazi kwa maana hii itabidi ukojoe kwanza aula uvumilie mpka vidonge viyeyeke au sijui inakuwaje kwani umesema huu ni ugunduzi mpya.

Lazarus Mbilinyi said...

Siyo mtaalamu sana wa elimu a uzazi ya wanawake ila najua kwa mwanamke mkojo una sehemu yake na uke ni sehemu yake hivyo hata ukikojoa bado pills haiwezi kuathiriwa na mkojo kwani ni njia mbili tofauti.
Ubarikiwe!