"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, October 27, 2008

Kwa nini wanawake hutoa machozi zaidi?

Moja ya imani mojawapo katika jamii ni kwamba wanawake ni viumbe wa machozi kama watoto.
Kama ni kweli kwa nini ni viumbe wa machozi zaidi kuliko wanaume?
Wavulana na wasichana wote hutoa machozi kiwango sawa (au kulia lia) hadi wakifikia miaka 12. Wasichana wakifikisha miaka 18 hulia mara 4 zaidi ya wavulana.
Sababu ya kwanza muhimu ambayo watafiti wengi wanaielezea ni kuhusuani na malezi, utamaduni, jamii kwamba mtoto wa kiume anavyolelewa huambiwa kwamba mwanaume hatakiwi kulia ovyo, anatakiwa kuwa imara, haruhusiwi kuonesha emotions zake, anahitaji kuwa tough, huru, mbabe na mtu wa kutoa majibu kwa kila kitu si kulia tu.
Wakati watoto wa kike kadri wanavyokuwa anafundishwa kuwa wanawake yaani kuonesha sifa na alama kwamba wao ni wanawake, wawe na huruma, waoneshe emotions zao nk.

Sababu ya pili ambayo wanatafiti wengi wanaivalia njuga ni hii ya tofauti ya homoni kati ya wanaume na wanawake.
Homoni ya prolactin ambayo imo kwenuy mammary glands kwa ajili ya kuzalisha maziwa hupatikana pia kwenye damu na glands za machozi.
Wavulana na wasichana wana kiwango sawa cha hiyo homoni hadi wakifikisha miaka 12 baada ya hapo homoni ya prolactin huongezeka maradufu kwa wasichana wanapofikisha miaka 18 asilimia 60 zaidi ya wavulana.

Pia kuna tofauti ya anatomy kwenye glands za machozi kwani mara nyingi mwanamke akitoa machozi huweza kutiririka hadi kwenye cheeks wakati wanaume hata machozi yakitoka bado huishia kwa wao kujifuta bila kutiririka kama wenzao wanawake.

Pia wanawake wanapokabiliana na frustration, stress, matatizo binafsi na mabadiliko ya homoni hasa yanayosababishwa na ujauzito, kuwa katika siku zake, menopause hivi vyote huweza kusababisha machozi kutiririka.

Pia kutoa machozi kwa wanawake kuna umuhimu wake kwani husaidia kuondoa kemikali ambazo zimesababishwa na stress na hivyo baada ya machozi hujisikia ahueni fulani.

Wengine wanasemaje?
Eti wanawake wana gene (inherited) sawa na ile ipo kwenye vitunguu so maumivu kidogo tu machozi huanza kutiririka.
Eti wanawake husikia maumivu ya kitu chochote zaidi kuliko wanaume ndiyo maana wana machozi mengi.
Wanawake hutoa machozi sana hasa wakiwa kwenye siku zao hasa kutokana na mabadiliko ya homoni mwilini.
Wanawake huwa wanafahamu nini cha kufanya wakiona mtu anataka kulia machozi tofauti na wanaume.
Kwenye sherehe (harusi) wanawake hulia kwanza ndipo hulewa, wakati wanaume hulewa kwanza ndipo hulia machozi

2 comments:

Bwaya said...

Asante kwa kulishughulikia swali vizuri. Kazi safi. Pongezi kaka. Ama kweli hapa ni kilima chenye utajiri wa elimu!

Yasinta Ngonyani said...

aise mimi nilikuwa sina habari hii asante sana. Nilichokuwa najua ya kwamba wanawake wana huruma kuliko wanaume. na ni kweli nimewahi kusikia wanaume hawalii kama wanawake kwa vile wa ni WANAUME