"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, October 29, 2008

Linapokuja suala la rangi wanawake huonekana wapo makini zaidi na wazuri zaidi kuchagua rangi za nguo kuliko mwanaume.

Pia utafiti uliofanywa na Professor Andrew Elliot (University of Rochester in New York) unaonesha kwamba mwanamke huvutia zaidi akiwa ametinga kiwalo (viwalo) chenye rangi NYEKUNDU.

Isssue ni kwamba ukiwa (mwanamke) mwanamke akiwa amepiga pamba rangi nyekundu huvutia zaidi kwa mwanaume na kuonekana sexy na si kwamba ataonekana intelligent la hasha.

Hii ina maana kama ni mwanamke umepata mwaliko kwenda sehemu (outing) na unadhani unahitaji mwanaume akuone sexy na attractive usisumbuke tinga kiwalo rangi nyekundu badala ya green, blue au white nk.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mm! kaka Mbilinyi mafundisho mazuri ila binafsi napenda rangi nyeusi na halafu nyingne zote kuliko nyekundu. Je mimi sio ..... na wala sikuwa sina wazo hilo kama navaa rangi hii nitaonekana sexy. mawazo yangu

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta leo umenifurahisha kwani ni mara yangu ya kwanza kusikia wewe ni moja ya wanawake wachache wanaopenda rangi nyeusi inapendeza.

Kitu cha msingi ili uonekane sexy lazima uanze mwenyewe kujiamini na kujiona ukivaa vile unajifurahi utaonekana sexy, kwenye post yangu ni utafiti wa jumla jinsi wanaume wanavyowaona wanawake katika rangi na mavazi yao. Ukweli unabaki kwamba kila mtu na rangi yake na kitu cha msingi sana unataka kuwa sexy kwa nani kama ni mumeo muulize anapenda uvaaje.

Upendo daima