"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, October 31, 2008

Ndoa Mpya

Inawezekana wakati wa uchumba alikuwa anaonja wine tu kwenye kijiko baada ya kuingia ndani ya nyumba analala njiani, nyumbani hadi aletwe, ni wako huyo! mtunze, mpende! Kuna mambo au vitu kama hujaolewa au kuoa huwezi kuelewa tukiongea hadi siku ukiwa kwenye ndoa na hata ukielewa huwezi kuamini hadi siku yakikukuta.

Ukweli ni kwamba ni muhimu kuelewa na kujifunza kwamba tunavyoongea ni uzoefu si hadithi.
Mara nyingi wanandoa wapya hukata tamaa kabisa kwani ni kama baada ya honeymoon mambo huanza kubadilika polepole na yale ulitegemea kuwa kama unavyotaka anakuwa tofauti kabisa.
Jambo ya msingi ni kufuata kanuni na kanuni mojawapo ni:


USITAFUTE MAKOSA KWA VITU AMBAVYO TANGU UCHUMBA ULIJUA ANAVIFANYA:
Inawezekana anakula sana kuliko ulivyotegemea, inawezekana anakunywa sana kuliko ulivyotegemea, inawezekana anapenda mahaba hadi unahisi nguvu kukuishia, au anatumia pesa ovyo kama maji, au yupo antisocial hadi unaogopa, au ni mvivu hadi unaona future haina maana kuwa na yeye, au anavuta sigara kama gari moshi, au anapenda michezo hadi unakosa muda wa kuwa naye, au ni mchafu hadi rafiki zako wanakusema, au ana kelele nyumbani hata hamuhitaji radio za FM au ana ganda kwenye TV kama vile ana mkataba na vituo vya TV au anatabia ambayo inakukera mimi siijui!
Inawezekana anakula sana hadi unaamua kuficha chakula chini ya kitanda lakini wapi ananusa utadhani ana sensor ya chakula.

Kumbuka wakati wa uchumba ilikuwa rahisi sana kwako kupuuzia matatizo (uliyoyaita madogomadogo) na vile vitabia vibaya kwa sababu ulitaka kuoana naye na kweli umeoana naye.
Labda ulidhani kwamba utambadilisha siku moja kwa siri au atabadilika, ni kweli wapo ambao hubadilika ila wa kwako imeshindikana.
Pia unajitahidi kumbadilisha matokeo yake anazidi kuzama kwenye hizo tabia mbaya
.

Bottom line ni kwamba ulimpenda ukakubali kuoana naye hivyo ulifahamu kwamba yupo hivyo sasa kelele nyingi za nini?

Kumbuka ulimkubali katika raha na shida, ugonjwa na afya.
Habari njema kwako ni kwamba hakuna unaloweza kufanya kumbadilisha isipokuwa kumkubali kwanza kama alivyo.
Pia fahamu kwamba tabia zake mbaya au vitu ambavyo unaona kwako ni usumbufu kamwe haviwezi kukufanya ujisikie vibaya hadi wewe mwenyewe uamue.

Ukitaka abadilike njia ni moja tu kumuomba yule aliyemuumba ambadilishe na njia sahihi ni maombi mbele za Mungu huku ukimpenda kuliko wakati wowote.

Upendo wako ndio unaweza kumrudisha kwenye mstari unaotaka na si vita, au kumlaumu au kumsema, au kupigishana kelele au kulalamika au kutukanana.

Mathayo 19:24-26
Kwa Mungu hakuna lisilowezekana.

Tutaendelea na kanuni Zingine…………………

No comments: