"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, October 8, 2008

Raha na vikwazo!

Huanzia kwenye ubongo kwanza! Uumbaji wa Mungu ni wa ajabu sana hasa linapokuja suala la mahusiano Kati ya mwanamke na mwanaume katika ndoa.
Ili kuridhishana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume jambo la msingi ni kufahamu vizuri hatua kamili ambazo ili tendo la ndoa likamilike lazima zifuatwe na hasara zake.

Hata hivyo wakati mwingine wanandoa hujikuta katika mgogoro katika eneo lingine la ndoa na matokeo yake masuala ya kitandani pia huwa ovyo na zaidi kuanza kulalamikiana kila mmoja akimlaumu mwenzake.
Kawaida tendo la ndoa hupitia hatua tatu muhimu ambazo ni vizuri kila mwanandoa kufahamu na pia ni muhimu kufahamu kwamba kila hatua huwa na vikwazo vyake na hili lisipozingatiwa unaweza kujisikia wewe tu ndiye unayepunjwa kwenye ndoa.

Hizi hatua tatu muhimu kila moja ina uwezo wake na mzunguko wake binafsi na vikwazo vyake.
Hatua ya kwanza ni hamu (desire) ya tendo la ndoa na ili kupata hamu ya tendo la ndoa lazima ubongo uhusike kwani kwenye ubongo kuna mfumo maalumu wa fahamu (neural) ambao kutokana na hali iliyopo mtu hujisikia hamu.

Hatua ya pili ni kusisimka (excitement) hii ni hatuas ambayo baada ya kuwa na hamu damu huweza kusambaa sehemu muhimu kama vile matiti, uke au uume kwa ajili ya kuhakikisha sex inafanyika.

Hatua ya mwisho ni kufika kileleni (orgasm) hii hutokana na kukaza kwa misuli ya uke au uume na kutoa raha isiyoelezeka na baada ya hapo ni kama mwisho ya furaha ya tendo lenyewe.

Nini vikwazo vya hatua hizo muhimu?

Wasiwasi, hofu, mashaka, woga, kuogopa na uadui hupelekea mtu kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Fadhaa zozote kuhusu sex hupelekea kukosa kusisimka na kuwa tayari kwa mapenzi pia ku-concentrate kwenye skills na techniques au style za sex kuliko kufurahia tendo lenyewe hupelekea kushindwa kufika kileleni.

Kumbuka utendaji wa sex katika ndoa huonesha hali ya ndoa nzima katika mambo yote kwani mara nyingi ndoa ikiwa na mgogoro hata tendo la ndoa huwa ni bora liende, si kuridhishana bali wajibu na ukweli unabaki kwamba sex katika ndoa huelezea ndoa ipoje.

Kama kuna mgogoro ambao haujapata jibu au kutokuelewana katika ndoa basi mfumo mzima wa sex hubadilika.

Je, unajisikia raha na hamu kubwa na kusisimka kwa ajabu kama zile siku za kwamba wakati mnaoana?
Je, jinsi unavyoridhika na tendo la ndoa ni sawa na ulivyokuwa unategemea? Au ni kama wajibu na si kupeana raha?
Ukweli unao mwenyewe.

Uzoefu unaonesha jinsi wanandoa wanavyozidi kuishi pamoja; tendo la ndoa huwa zuri zaidi na la kuridhisha zaidi kuliko mwanzo au miaka ya mwanzo.

2 comments:

Anonymous said...

Kaka hapo upo sawa kabisa ila napenda kusema kuwa kama mwezio hajisikii basi muache au jitahidi kumfanya ajisikie kufanya si unajua namna ya kumbembeleza kwa akili?? misuli haihitajiki hapo!!!!????. Anza mapenzi asubuhi na yamalize jioni si unajua ndo muda wa hesabu huooo.
Msafiri

Yasinta Ngonyani said...

mmh ila hapo naona mambo si mabaya mapenzi kwa kweli ni kitu cha ajabu sana.