"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, October 11, 2008

Urembo na mvuto

Kijiji kwetu mwanamke mzuri ni yule anajua kushika jembe na kulima pamoja na tabia njema hata hivyo huko Thailand uzuri wa mwanamke ni Shingo yenye rings, hapo mchumba hakosi!

Suala la ndoa ni suala la kiutamaduni zaidi.
Katika jamii nyingi kuwa romantic na uzuri wa kimwili (physical attraction) jambo la muhimu sana.
Afya, umri na mwonekano pia huwa jambo linalotazamwa sana kila mmoja anapotafuta mwenzi wake.
Pia mwanamke kuonekana anavutia hutofautiana sana katokana na utamaduni, jadi na mitazamo ya jamii husika.
Kwa mfano kama umezaliwa huko Thailand, mwanamke anayevutia ni mwanamke mwenye shingo ndefu iliyovalisha rings (tazama picha hapo juu).
Pia kama umezaliwa jamii za Afrika au Amerika ya kusini na katika visiwa vya karibean, basi mwanamke mwenye umbo nene na makalio makubwa huonekana ndiye anayevutia kuliko aliye kimbaumbau ambaye huonekana mgonjwa.

Ingawa Ulaya na Amerika kaskazini pamoja na vijana wa kizazi kipya bado wanaona mwanamke mnene hapendezi na ana umbo lisilo na afya.
Na huko China mwanamke mwenye umbo la uso wa mviringo kama mwezi huwachanganya wanaume bado wanamke mwenye mguuu wa nguvu huonekana si lolote na wakati huohuo wanaume wenzao wa Afrika mwanamke mwenye mguu wa nguvu huonekana wa uhakika.
Pia suala la umri katika kuoana kwa sasa halina tatizo sana
Hata hivyo kutokana na kupanuka kwa mawasiliano ya mitandao na mwingiliano wa jamii globally mtazamo wa kizazi kipya kuhusu urembo na uzuri linakuwa suala kubwa na la kibiashara zaidi kwani wanawake na wanaume wengi sasa wanafanya upasuaji ili krekebisha mwonekano iwe mguu, matiti, makalio au uso na wengine hushinda saloon.

Uzuri na urembo wa kweli huanzia moyoni na tabia pamoja na kujifahamu kwamba kama ulivyo umekamilika na upo kwa ajili ya utukufu wa aliyekuumba.
Je, kwenu mwanamke mrembo ni yupi?

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mmh hapo ipo kazi kubwa: Nimejiuliza je? atapotoa hizo rings hiyo shingo itakuwa salama? au anavaa hizi rings usiku na mchana na maisha yake yote?. Kuhusu urembo kwa mwanamke kwa kweli naweza kusema sisi binadamu hatutosheki kabisa na tulivyoumba hii hata mimi bado sijaelewa kwa nini kama ulivyosema watu wengi siku hizi wanajirekebisha katika miili yao. Halafu pia kuna hii ya kubadili rangi waafrika wanataka kuwa weupe na wazungu wanataka kuwa waafrika. Bado sijaelewa kwa nini Binadamu tupo hivi. Zamani ilikuwa zaidi kwa wanawake lakini sasa hata vijana wengi wanafanya hivi. Mmh kazi kweli kweli.

Lazarus Mbilinyi said...

Naamini maandiko yanatimia kwamba siku za mwisho watu watajipenda wenyewe kuliko kawaida.

Bwaya said...

Kwangu mwanamke mrembo ni yule anayejiamini vile alivyo pasipo kuongeza nakshi zisizo na sababu.