"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, November 28, 2008

Mvuto nao!

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Bristol umebaina kwamba mwanaume au mwanamke akiutwika huwaona wengine wanavutia sana.
Mwanaume huona wanawake wanavutia na ni warembo kwelikweli, na wanawake huona wanaume ni handsome wa nguvu.
Pombe zikimtoka Guess what? ............................

Tume ya uchaguzi hapa Canada mwaka 1974 iligundua kwamba wagombea uchuguzi wenye sura zinazovutia walipata kura mara mbili na nusu ya wale ambao sura zao zilikuwa za kutisha hasa pale wanapolingana uwezo.
Hivi hii Tanzania haijawahi kutokea watu wakampigia kura mgombea kwa ushindi wa Tsunami? Maisha bora kwa kila mtanzania
Sura inayovutia acha kabisa!

Mwanamke anapotumia pills husababisha kupunguza uwezo wa kunusa, hii inatokana na utafiti uliofanywa a chuo kikuu cha Liverpool kwa wanawake kunusa (sniff) mashati 100 ya wanaume.
Kawaida mwanamke huvutiwa na mwanaume tofauti na genetics zake (harufu tofauti).
Hawa nao kazi kwelikweli, inamaana walikuwa wananusa vikwapa?????

Tafiti za kisayansi zinasema si binadamu wote huvutiwa na binadamu wengine, inasemakana kuna binadamu ambao huvutiwa na vitu wala si wanyama bali vitu visivyo na uhai.
Hawa watu huweza kusisimka, kupenda (fall in love) na pia huwa committed kuishi navyo au kuishi hapo vilipo.
Eija-Riita Berliner-Mauer yeye ameolewa na ukuta wa Berlin tangu mwaka 1979.
Duniani kuna vituko!

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Pennsylvania mwaka 1980 waligundua kwamba watuhumiwa waliokuwa wanavutia sura zao walipata adhabu laini zaidi ukilinganisha na watuhumiwa wenye sura zilizikuwa zinatisha.
Yaani kwa sura nzuri wanakuhurumia?

Wanawake wanapojipamba sana kwa vipodozi huweza kupunguza uwezo wa wanaume kuvutiwa nao hasa wakiwa wapo fertile.
Wanawake huwa na aina ya harufu (scent) ambayo huvutia wanaume hasa mwanamke anapokuwa kwenye siku za ovulation.
Kama hutaki kusumbuliwa na wanaume basi ukiwa fertile siliba vipodozi (makeup) vya nguvu finish!

Unavyojionesha kwa mara ya kwanza ni muhimu sana (first impressions).
Wengi huweza kutoa uamuzi wa mwenzake kuwa partner hasa kutokana na alivyojieleza dakika 4 za kwanza kuonana.
Siyo kujieleza maneno tu bali ni vitendo vya mwili unapoongea, maneno unayoongea na sauti unayoongea.
Maneno unayoongea kwa mara ya kwanza huvutia asilimia 7 tu, vitendo vya mwili unapoonga (body language) ni asilimia 55 na aina ya sauti na jinsi unavyoongea ni asilimia 38.

Je, unadhani mpenzi wako alikuvutia kitu gani siku ya kwanza ulipokutana naye?

Weekend Njema!


Thursday, November 27, 2008

Hujanielewa!

Nimewakuta hawa nao hawaelewani!
Wanachanganyana lugha!
Matokeo yake gari haliendi! Mume na mke wakiwa kwenye gari walipita sehemu ambayo wanauza soda, mke akamuuliza mume “je, unaweza kusimama kwa ajili ya kunywa soda?” mume akamjibu kwa uaminifu kabisa mke wake kwamba “hapana haina haja" na hawakusimama kwa ajili ya kunywa soda.

Matokeo?
Ukweli mwanamke alitaka wasimame wapate soda, na alikwazwa au kuumia sana kwamba mume hakukubali wasimame kwa ajili ya soda.
Alijisikia pendekezo lake halikupokelewa na mumewe, alijiona amekatishwa tamaa.

Mume naye alipohisi mke wake kakasirika na kukwazwa alifadhaishwa sana kwani alijiuliza kama alikuwa anataka kweli nisimame kwa ajili ya soda siangesema tu kwamba anataka tusimame kunywa soda kuliko kuniuliza nichague?

Hii ina maana gani?
Hii ina maana mwanaume hakujua kwamba mke wake alipouliza swali alikuwa hahitaji jibu au uamuzi (decision) bali ilikuwa ni njia ya kuanzisha mazungumzo na kuonyesha hisia zake kuhusu kusimama wapate soda.

Na mwanamke naye hakufahamu kwamba mwanaume aliposema "hapana" hii haina maana kwamba alikuwa anatoa jibu la mkato kuonesha utawala mbovu na kutojali hisia zake bali alikuwa anaelezea uamuzi wake na kile alikuwa anapenda kujibu baada ya kuulizwa swali lenye kujibu ndiyo au hapana na yote alikuwa majibu sahihi kama yangetolewa.

Wakati mwanamke na mwanaume kwenye ndoa wanapotoa majibu blue namna hii bila kujua mwanamke na mwanaume wanatakiwa kuwasiliana vipi, ukweli inaweza kuzalisha hasira na kukwazana kusiko tamkika.

Nini kitu cha msingi kuzingatia?
Ukweli ni kwamba mwanaume na mwanamke wapo tofauti sana linapokuja suala la mawasiliano baona yao.
Kwa mwanaume kuongea ni kuonesha uwezo wake katika kutoa maamuzi au status aliyonayom katika jamii au katika ndoa au katika eneo analoishi, wakati mwanamke kuongea ni kutoa hisia zake ili kuhitaji msaada wake au kuelezea kitu kijadiliwe na si kutolewa maamuzi hata kama ni swali.

Wanawake mara nyingi huongea huku wakifikiria kutaka ukaribu (closeness) na wale wanawapenda, wanawapa nafasi katika maishayao na hivyo hujitahidi sana kulinda intimacy.
Wanaume wapo focused kwenye status hivyo huongea uhuru wao, uwezo wao, maamuzi yao na hii husababisha mwanaume na mwanamke kuongea kitu kimoja na kuwa na maana tofauti na matokeo yake kutoelewana.
Wanawake wengi huumia sana pale mwanaume anapotoa majibu ya mkato na u ukali hasa kitendo cha kujibu kwa mkato na kunyamaza kama vile anam-ignore.
Kwa mwanaume kuongea ni ku-share information kwa mwanamke kuongea ni ku-share feelings. Ndiyo maana wanaume huongea sana kwenye public na kutoa jokes na stories lakini wakiwa home huwa kimya hata hivyo wao hufanya hivyo kwenye public kujipatia attention na status kwamba yeye ni mwanaume ni hero, ni kiongozi, ni mwenye nguvu yeye ni kidume.

Wednesday, November 26, 2008

Tamaduni!

Kwetu bila mshenga mke hupati!
Asia:
Vijana hukaa na wazazi hadi anapofikia wakati wa kuoa na akisha oa au kuolewa huchagua mzazi mmoja na kuishi kwake kwa muda fulani ndipo huanza maisha.

Australia:
Mabinti huwaomba vijana wa kiume kwenda nao “outing” kwa ajili kuombwa uchumba na analipa gharama zote kama vile chakula na vinywaji.

Columbia:
Kama msichana unatoka naye kwenda kuongea kwa mara ya kwanza kawaida huambatana na rafiki yake mmoja wa kike unawajibika kuwalipia gharama zote.

Finland:
Vijana wa kiume na kike huenda kwa kundi moja kama 30 hivi lengo likiwa ni kutafuta wachumba (matching).

Latin America:
Kaka au dada yeyote atakaye muomba mwenzake kutoka naye kwa ajili ya mazungumzo ya faragha (uchumba) anawajibika kulipa gharama zote za vinywaji na chakula.

Japan:
Siku Valentine wanwake huwapa zawadi wanaume na baada ya mwezi kuna white day ambayo wanaume nao hutoa zawadi kwa wapenzi wao wa kike.

India Kaskazini:
Hakuna uchumba hadi wazazi wamkubali msichana ambaye unataka kumuoa kama wewe ni kijana wa kiume, wazazi wakikataa umeumia na kama wakikubali unaruhusiwa full speed kuoa.

Je, sehemu unayoishi wewe tamaduni za kuoana zipoje?
Au hakuna kanuni na taratibu rasmi?
Je, njia mnazotumia zinasaidia vipi kuhakikisha wachumba wanafahamiana na kujuana ili kuwa na maisha ya ndoa yenye mshikamano na si migongano?

Tuesday, November 25, 2008

Type Of Women!

HARD-DISK Woman:
She remembers everything, FOREVER.
RAM Woman:
She forgets about you, the moment you turn her off.
WINDOWS Woman:
Everyone knows that she can't do a thing right, but no one can live without her.
EXCEL Woman:
They say she can do a lot of things but you mostly use her for your four basic needs.
SCREENSAVER Woman:
She is good for nothing but at least she is fun to look at!
INTERNET Woman:
Difficult to access.
SERVER Woman:
Always busy when you need her.
MULTIMEDIA Woman:
She makes horrible things look beautiful.
CD-ROM Woman:
She is always faster and faster.
E-MAIL Woman:
Every ten things she says, eight are nonsense.
Which type of woman is yours?

Monday, November 24, 2008

Love is blind, but marriage restores its sight.

Matiti ni Mali ya nani?

Matiti ni chakula cha mtoto!Linapokuja suala la matiti wanaume wengi (si wote) hunyang'anyana hati miliki ya matiti na watoto wanaonyonya hata hivyo wanawake nao kila mmoja ana mtazamo wake tofauti, hebu angalia maoni ya wanawake hawa wa Nigeria wanavyojibu swali la nani ni mmiliki halali wa matiti ya mwanamke.
Mrs. Arogundade
Mume wangu ndiye anamiliki matiti yangu kwa sababu mume alikuja kabla ya mtoto.
Baada ya mtoto kunyonya kwa muda inakuwa zamu ya mume wangu kwani tunalala kitanda kimoja.
Mtoto wangu ana access ya matiti yangu kwa muda tu wakati mume wangu ni mali yake maisha yetu yote.
Matiti yangu ni kitu ambacho mume wangu huchezea na pia ni mto wake wa kulalia.
Ukweli ni kwamba mume wangu hujisikia wivu kama mtoto wangu ataendelea kunyonya zaid ya muda aliopewa.
Linapokuja suala la matiti yangu mume wangu huwa anachanganyikiwa, hawezi kufanya ile kitu (sex) bila matiti yangu.

Mrs. Omisade
Mume wangu ni mmiliki ya matiti yangu.
Mume wangu akiyakamata tu matiti yangu basi huwa tunakuwa na mahaba ya nguvu katika uso wa dunia
Mume wangu hawezi kuanza chochote bila kugusa matiti na pia hunisisimua sana kwa ajili ya kufanya mapenzi pia mume wangu hunambia huwa anamuazima mtoto wetu matiti na akimaliza anatakiwa kurudishiwa mali zake kutoka kwa mtoto.

Mrs. Alhaja Sadiku
Kitu kimoja ninachopenda kuhusu mume wangu ni pale anapochezea matiti yangu kama vile machungwa, pia huwa namruhusu mtoto wangu kuchezea matiti kwa kadri anavyoweza.
Najua mume wangu alilipa mahari kitu inachompa access ya mwili wangu wote.
Matiti ni kwa ajili ya chakula cha mtoto wangu.

Mrs. Olagbaju
Ukweli mume wangu ndiye anamiliki matiti yangu.
Ila lazima akubaliane nami kwamba wakati tunayonyesha mtoto lazima aache kwa ajili ya mtoto wetu.
Wakati ninaponyonyesha naweza kumruhusu mume wangu kuyachezea kwa mikono na si kunyonya.
Mume wangu anamiliki matiti yangu permanently na pia anamiliki kila kitu nilichonacho pamoja na matiti.

Mrs. Agunbiade
Mtoto wangu ndiye anamiliki matiti yangu.
Mume wangu ana mtazamo tofauti kwani huwa hapendi kabisa kuyanyonya, wakati nanyonyesha hapende kabisa hata kula chakula changu yeye hapendi kabisa harufu ya maziwa kutoka kwenye matiti yangu.

Mrs. Amadi
Mume wangu hawezi kufanya bila matiti, kabla kitu chochote kutokea yaani kufanya mapenzi lazima achezee matiti yangu na bila matiti siwezi kusisimka.
Mume wangu husahau huzuni zote akianza kunyonya matit yangu.

Mrs. Ganiu
Mume wangu ndiye anayemiliki matiti yangu, mtoto wangu hunyonya kwa muda tu, then automatically matiti hurudi kwa mume wangu.

Mrs. Daniel
Mume wangu anamiliki matiti yangu kwa sababu alinioa kihalali.
Tunapotaka kuwa kwenye huduma ya pamoja ya usiku kila mara ni utukufu, huanza kwa mume wangu kunichezea matiti yangu na kuyakandakanda halafu tendo huanza.

Mrs. Omole
Mume wangu aliniambia kwamba nilipokutana naye kwa mara ya kwanza matiti ndiyo kitu kilimvutia sana yeye, hivyo ni mali yake, najua matiti yangu ni sehemu ambayo mume wangu ni dhaifu, siwezi kumnyima mali zake, hata kama mtoto wangu anayanyonya, mume wangu bado huyanyonya na kuyachezea.

Mrs. Ojo
Kabla ya mtoto kuzaliwa matiti yangu yalikuwa ni toy la mume wangu kuchezea.
Baada ya mtoto matiti ni kwa ajili ya mtoto, mume wangu anaishia kuchezea tu si kuyanyonya.

Mrs. Alao
Mume wangu anamiliki matiti yangu kwa sababu tulikuwa pamoja kabla ya mtoto kuzaliwa.
Moto anaweza kuazima matiti kwa muda tu, mume wangu anamiliki matiti yangu permanently na mtoto huwa yake kwa muda.

Mrs Salome
Mume wangu ni owner wa matiti yangu.
Hawezi kufanya mapenzi bila matiti yangu.
Mume wangu huniambia matiti yangu ni chakaazi (succulent ).
Matiti yangu humpeleka mbali sana mume wangu na husisimka hadi kufika juu sana hata kabla hatujaanza kitu chenyewe.
Mtoto wangu ipo siku atayacha na kwenda kuanza nyumba yake hivyo lazima nimridhishe mume wangu kwa matiti yangu.
Mungu alinipa matiti ili kumridhisha mume wangu katia suala la tendo la ndoa.
Siwezi kunyonyesha mtoto miezi 7 bila kuyarudisha kwa mmiliki wake ambaye ni mume wangu mpenzi.

Je, wewe kama ni mwanamke matiti yako ni mali ya nani? Mtoto au mume wako?

Source: Modupe Okanlawon & Omowunmi Owoyomi
Daily Sun News, Sunday, June 8 , 2008

Sunday, November 23, 2008

Jumapili Njema

Jacqueline Ngowi
Morogoro Tanzania Love is patient, love is kind.
It does not envy, it does not boast, it is not proud.
It is not rude, it is not self-seeking, it is not easily angered, it keeps no record of wrongs.
Love does not delight in evil but rejoices with the truth.
It always protects, always trusts, always hopes, always perseveres.
(1Corinthians 13: 4-7)

Saturday, November 22, 2008

Kukefyakefya!

Kukefyakefya (nagging) ni nini?
Ni kitendo cha kutafuta makosa na kuendelea kulaumu, kulalamika, kusumbua, kutesa, kuchokoza , kuudhi, kushutumu, kuleta mzozo ndani ya wanandoa.
Mara nyingi wanawake ndiyo wenye hii tabia ingawa imegundulika kwamba wapo wanaume wenye tabia hii katika ndoa.

Pia kukefyakefya ni kitendo cha kumsumbua mwanaume kwa maswali, au kumtuma kitu au kumwambia afanye kitu kama vile ni bosi wa kihindi na mfanyakazi wake au mama na watoto wake wakati ni mke na mume ndani ya nyumba.

Inawezekana mume wako anatabia ya kuacha bathroom kuwa chafu baada ya kutumia, akila anaacha meza na vyombo ovyo na vichafu, Inawezekana huwa anatupa nguo ovyo na kusambaa sakafuni utadhani chumba cha watoto wa shule, Inawezekana anakaa tu huku anazidi kunenepeana kama wachezaji wa sumo, au anaangalia TV kama vile ana mkataba na vituo vya TV na umekuwa unamwambia kubadilika lakini habadiliki na umeona dawa nikuendelea kumsema.

Au umekuwa ni mwanamke mwenye maswali hata yasiyo na kichwa na miguu tangu asubuhi wewe ni kuuliza tu nakuendelea kuuliza.
"Unamuuliza, je Ulitoa zile takataka, ulilipa ile bill, umetengeneza lile dirisha, umemwambia fundi kuhusu tatizo la umeme hata hajajibu umeshampachika swali lingine"
Kawaida wanaume huwa hawapendi kuambiwa nini cha kufanya.

Kwa nini kukefyakefya si vizuri?
Kwa sababu husababisha mwanaume kukwazika, kwani hujiona yeye ni mtoto (child role) na mke ni mzazi au mama (parent role), Hakuna mwanaume anapenda mke wake kuwa kama mama yake mzazi.
Mwanaume hujisikia haheshimiwa na mkewe (disrespectful)
Mwanaume hujisikia kushambuliwa na kudharauliwa nakujiona hafai (inadequate)

Kwa nini wanawawake hupenda tabia ya kukefyakefya?
Wanaume hawafanyi vile wanawake wanawaambia wafanye.
Pia wanawake hudhani kwa kurudia kukumbushia na kusutana basi mwanaume atafanya.
Wapo wanawake wamekulia mazingira ambayo mama zao walikuwa ni watu wa kukefyakefya kwa baba zao hivyo basi nao wanaamini hiyo ndiyo njia pekee ambayo wanaume wanaweza kufanya yale wanasema au wanataka wafanye.
Wengine ni asili yao kufanya hivyo.

Nini matokea ya tabia ya kukefyakefya?
Mwanaume huanza kumkwepa mke wake na kuchelewa kurudi nyumbani au kujibakia ofisini au kazini au kupitia sehemu hadi ahakikishe akirudi nyumbani mke amelala.
Mwanaume anaweza kuanza tabia mbaya za ulevi au kukosa uaminifu katika ndoa
Mwanaume huanza tabia ya kutosikiliza mke wake kwani anamchuja (filter) kwamba huyu ni tabia yake kukefyakefya so msumbufu.
Kuchokana katika ndoa maana hakuna ukaribu (intimacy) pamoja na mawasiliano kuwa ovyo maana mume sasa uwa si msikilizaji mzuri.
Mwanaume hukosa hamu na huyo mwanamke mwenye hii tabia.

Je, mwanamke afanyeje asiwe na tabia ya kukefyakefya?
Kwanza mwanamke lazima akubali kwamba yeye na mume wake wapo tofauti na azikubali tofauti, akubali upungufu uliopo na kuchukua maisha kama yalivyo.
Siku mwanaume akifanya vizuri ampe appreciation.
Lazima mwanamke awe positive kama mwanaume amefanya alichoambiwa afanye kwa maana kwamba usilaumu, shutumu, au kukasirika au kumfanya aonekane stupid.
Kawaida Hakuna kitu kibaya duniani kinachofanya tuone kitu ni kibaya bali ni jinsi tunavyofikiri (thinking)
Shirikisha hisia zako kwake kama ungekuwa wewe kila siku unaambiwa kama mtoto mdogo ungejisikiaje.

Inawezekana mumeo huchelewa kurudi nyumbani au kukupa sababu eti anapitia sehemu kumbe anakwepa tabia yako ya kukefyakefya.

Ni afadhari kukaa kwenye jangwa kuliko mwanamke mgomvi na mchokozi
(Mithali 21:19)
Ni afadhari kuishi pembe ya darini kuliko kukaa katika nyumba pana pamoja na mwanamke anayekefyakefya
(Mithali 19:9)

Friday, November 21, 2008

Mpe dakika 15 kwanza

Wanaume hupenda kuwa wenyewe muda fulani (kukimbilia pangoni) hasa akiwa amerudi nyumbani kutoka kazini au akiwa anatatizika na jambo lolote.
Hivyo basi inawezekana wewe kama mwanamke ndani ya ndoa umezoea mume akirudi kutoka kazini unamkaribisha home kwa kumpiga maswali na kuanza kumueleza kila aina ya matatizo na karaha ambazo zimetokea siku hiyo bila kumpa hata muda wa yeye kupumzika kidogo.

Sina maana kwamba mumeo akirudi nyumbani ule jiwe bila kumpokea au kumuuliza kazi ilikuwaje, nazungumzia suala la kutompa muda angalau dakika 15 kupumzika kabla hujaanza kutoa maswali yako na matatizo yako.

Pia naamini dunia ya sasa wote wanawake na wanaume tunafanya kazi iwe ofisini au shambani hata hivyo tukifika nyumbani kila mmoja hujitahidi kumweleza mwenzake nini kimeendelea au kupeana taarifa mbalimbali za familia ukweli ni kwamba bado mwanaume huhitaji dakika kama 15 kabla ya kujiunga na familia.

Kumbana maswali na kumwambia matatizo na shida tangu anaingia mlangoni si jambo zuri sana kwa mwanaume kwani hujisikia ainaishi na mama yake na si mke wake maana mama yake alizoea kumbana maswali tangu anaingia nyumbani kutoka shule.
Kama angekuwa anataka kuishi na mama yake basi asingekuoa wewe bali amekuoa wewe kwa sababu wewe ni tofauti na mama yake.

Baada ya kuchoshwa na kazi, na boss, au wateja au foleni za magari njiani anapowahi nyumbani anachohitaji akifika nyumbani ni busu na hugs kutoka kwa mke wake then aoge na kupumzika kidogo kama dakika 15 hivi ndipo atakuwa tayari kujibu maswali ya mkewe na kuendelea na story zingine pia.

Mpe muda wa kurelax akishafika nyumbani kwani kumbana maswali punde tu anaingia nyumbani kunaweza kusababisha yeye kuchelewa home kwani hujisikia ni usumbufu.
Akishakuwa tayari ameridhikana muda wake kuwa kwenye hilo cave unaweza kuona anaanza kuzunguza mwenyewe then anza kumpa hayo maswali yako.
Pia akigundua wewe ni msumbufu, hata siku ukiwa na point za maana anaweza kupuuzia maana umezoea kuchonga sana akiingia tu mlangoni hata kabla hajafika chumbani.
Ubarikiwe!

Thursday, November 20, 2008

Mwanaume kushindwa kitandani

Haijalishi wewe maarufu namna gani linapokuja suala la kitandani huwezi kujua hadi uwe hapo Tunapozungumzia mwanaume kushindwa kitandani (impotency) tuna maana kwamba ni mwanaume kutokuwa na uwezo kusisimamisha uume ili kuweza kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi unaotakiwa, au kuwahi kukojoa (immature ejaculation) ua mwanaume kusimamisha uume kwa muda mrefu zaidi ya saa moja na kushindwa kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Kama mwanaume anaweza kumaliza tendo zima la ndoa kwa muda wa dakika 5 au chini ya dakika 10 na kuwa hana uwezo wa kuendelea tena basi hiyo ni dalili kwamba something is wrong.
Data zinaonesha asilimia 10 ya wanaume mahali popote wana tatizo hili, kwa mfano nchini Marekani inakisiwa kwamba wanaume milioni 30 wanakumbana na tatizo hili na ulimwenguni kuna wanaume zaidi ya milioni 150 wana tatizo hili na pia kila mwanaume anaweza kukutana na tatizo hili angalau mara moja katika maisha yake.

Nini husababisha?
Ili uume uweze kusimama lazima damu iende kwa wingi huko na kusababisha kuwa mgumu na kusismama na kuwa tayari kwa huduma.

Sababu kubwa ya mwanaume kushindwa kusimamisha uume wakati wa tendo la ndoa mara nyingi huwa ni mawazo (anxiety)
Pia Inawezekana ni dalili ya ugonjwa mwingine kama Diabetes.
Mwanaume anaweza kuwa na hofu kwamba hawezi vizuri sex na hii hupelekea kutojiamini na hatimaye uume kushindwa kabisa kusimama.
Pia Inawezekana ndoa ina matatizo na kupelekea kichwa kuwa na limzigo la mawazo na hatimaye kushindwa kabisa kusababisha utendaji wa kazi huko south pole.

Inawezakana mwanaume amefiwa na mtu wa karibu aliyekuwa anampenda.
Kuchoka
Pia stress
Kuwa na hatia ya kitu chochote.
Inawezekana mwanamke aliye naye havutiii kabisa
Kufilisika biashara au kufukuzwa kazi hupelekea kuwa na mawazo.
Kupungukiwa homoni zinazowezesha uume kusimama hasa umri ukienda sana.
Matatizo ya mirija ya damu kushindwa kusafirisha damu kwenda sehemu zote za mwili, hii uweza kusababishwa na magonjwa kama BP na arteriosclerosis.
Kuvuta sigara
Magonjwa ya nerves
Kufanyiwa upasuaji hasa ule wa prostate

Wanaume ambao huonekana labda ni maarufu sana katika fani zingine bado likija suala la kitandani ni kitu kingine hivyo mwanamke anatakiwa kujua kwamba lazima atoe ushirikiano wa kutosha kwani mwanaume anahitaji kutiwa moyo na mwanamke aliyenaye kwani Inawezekana ni mawazo kichwani mwake ndo hupelekea kushindwa.

Je, unaweza vipi kuepuka hili tatizo?
Hakuna kitu kinachoshushia mwanaume hadhi mbele ya mwanamke kama hili tatizo hivyo basi mwanaume akiona hili tatizo linajitokeza mara kwa mara kwanza ajiamini na kuangalia linaweza kuwa nini kimesababisha kama ni msongo wa mawazo inahitaji kwenda kwa washauri (counselling) na kama ni suala la kimatibabu awaone madaktari.

Tuesday, November 18, 2008

Mwanamke kuwa baridi kitandani

Ukweli wakati wa snow kuna baridi kali, ingawa lile baridi la mwanamke kitandani huchanganya ndoa! Linapokuja suala la mapenzi, upendo na ndoa asilimia kubwa ya kila binadamu huwa na ndoto kubwa.
Hata hivyo hizi ndoto wakati mwingine huyeyuka pale mtu anapokutana na mambo ambayo ni kinyume chake mojawapo ni mwanamke au mwanaume uliyenaye kuwa baridi kabisa linapokuja suala la tendo la ndoa ukiongelea sex tu ni wa baridi na pia hafurahii kabisa tendo la ndoa.
Mwanamke kuwa wa baridi na kukosa kabisa hamu ya tendo a ndoa na kushindwa kabisa kufika kileleni au kwa kingereza frigidity, sexual paralysis, to be frozen, locked in state of nonresponsive, au mwanamke kuwa baridi kuhitaji mapenzi, kukosa moto wa kutaka mapenzi.
Mambo mengi sana husababisha mwanamke kuwa na frigidity mojawapo ni:HATIAWapo ambao kutokana na malezi ya dini na jadi zao wamedumazwa na mafundisho kwamba sex ni uchafu na dhambi hivyo wakiingia kwenye ndoa bado hujisikia ni dhambi na uchafu pia mwanamke huwa na wakati mgumu sana kubadilisha gear na kujisikia sex ni haki yake na ni baraka ambazo Mungu amewapa wanandoa.

Pia huyu mwanamke anaweza kuwa na mzigo wa hisia na kuumizwa kama vile kubakwa au kunajisiwa wakati mtoto au kabla ya kuolewa hivyo akikmbuka tu mwili unakuwa barafu kuhusu sex.
Pia inawezeana mwanaume aliyenae anamuudhi sana na kumtesa na mwanamke hujisikia hatia kwamba amedanganywa kuingia kwenye hiyo ndoa na matokea ana freeze kabisa kuhusu sex.
Au inawezekana wameoana baada ya kudanganya wakat bado hawajaoana na kwa kuwa walidaganya na mimba ikapatikana na wakaozeshwa kwa nguvu sasa mwanamke haridhiki na mwanaume so anajisikia ama kauziwa mbuzi kwenye gunia hivyo hisia za mapenzi kwa mwanaume zimekufa.

HOFU, MASHAKA NA WASIWASIInawezakana mwanamke anapata hofu na mashaka au wasiwasi na kuumizwa (uke) na mwanamke hasa kama mwanaume yupo rough katika tehcnis zake za mahaba.

Pia inawezekana uke ni mkavu kiasi cha kumuumizwa.
Pia kama mwanaume ana maneno ya kutisha na kukatisha tamaa wakati wamapenzi au badala ya kuwa tender yeye anakuwa na hard.

Wanawake huwa na hofu hasa kutkana na mwanaume kuwa ignorant kwenye suala zia la tendo a ndoa kiasi kwamba wanamke hujikuta amejawa na hofu na mashaka kwani mwanaume hana uhakika na kile anafanya.

Wanaume wengi hujifanya wanajua kila kitu kumbe si hivyo na ukweli wanawake hujua zaidi na kwa kuwa wakionesha wanajua wataulizwa nani kakufundisha na matokeo yake ni balaa.
Pia wapo wanawake ambao hujiweka kwenye kundi la zero linapokuja suala la mahaba pia inawezekana ni kutokana na jinsi mwanaume anavyomkandia kwamba hajui.

Pia inawezekana mwanamke anatumia Tv, films, movies na media zingine kupima uwezo wake kitandani sasa akishindwa hujiona failure na matokea hukosa libido.
Dunia ina vipimo vyake ya kuonesha unajua sex hata hivyo hujaitwa kuja kwenye ndoa kujilinganisha na vipimo vya dunia (world sex performance standars) bali kumridhisha mumeo. Muhimu ni ku-focus kwa mumeo au mkeo na si kujilinganisha na masuperstar wa sex duniani.

Pia mwanamke anaweza kuwa frigidy pale anapokuwa na hofu hasa akiwa anahisi kuna watu wanawaona au wanachungulia au watoto wanawaona au watu wanasikiliza wakati wa sex hasa kutokana na mazingira ya chumba cha mahaba kilivyo, wanaume wengi huwa hawajali ila kwa mwanamke ni issue nzit sana ambayo huwezakufanya awe wa baridi.
Kumbuka privacy is a basic need to sex
Pia mwanamke anaweza kuwa frigidy has kama anakuwa na hofu ya kupata mimba hasa kama mimba yake huishia kwenye miscarriage, hivyo emotions zake huwa zimeumizwa kiasi kwamba zina overrule hamu ya sex na mwili kuwa baridi kabisa kuhusu sex.Pia inaweza kuwa ni stress, anxiety, depression.
Pia inaweza kuwa hofu ya kuambukizwa magonjwa ya zinaaa.

Nini tiba yake? Tiba halisi kama una tatizo la kuwa baridi kuhusu tendo la ndoa ni kuwaona washauri wa saikolojia au madaktari wa taaluma za wanawake na sex.

Monday, November 17, 2008

Usitumie neno talaka

Unaweza ukapaka lipstick ya nguvu na bado kinywa kikatoa maneno yasiyo ya baraka! Usitumie neno talaka
Naomba jiulize kidogo hivi ni mara ngapi kunapotokea mgogoro katika ndoa yako umekuwa unawaza au kutishia kwamba utaachana (talaka) na huyo mume wako au mke wako?

Inawezekana unaishi katika wakati mgumu sana katika ndoa yako umeumizwa sana, umekatishwa tamaa sana, hupendwi, hakujali tena, umejawa na stress kiasi kwamba hata unapotamka kwamba afadhari kupata talaka na kujianzia maisha mapya kivyako huoni uzito wa neno talaka unavyolitamka.
Ukweli ni kwamba kwa maneno yetu tunayotamka tunaweza kuweka mustakabali wa maisha yetu ya baadae.
Maneno hushibisha nafsi sawa na chakula
(Mithali 18:20)

Maneno tunayoongea yana uwezo wa ajabu ndani yake; yana uwezo kuponya au kuua au kuumiza, yana uwezo wa kutia moyo au kukatisha tamaa kabisa, yana uwezo wa kusema ukweli au kudanganya kwa uwongo wa ajabu, yanauwezo kutoa sifa au kulaumu, yana uwezo wa kubariki au kulaani nk.

Neno talaka ni neno lenye sumu na neno baya sana kulitumia katika ndoa yako na zaidi ya yote huweza kuumba kwenye akili na mawazo yako zaidi ya wewe unavyofikiria na kutoa matokeo sawa na mbegu iliyopandwa.

Unapotamka maneno mabaya kwa ndoa yako au katika maisha yako ya kila siku unamwaga sumu na ipo siku itakuwa kweli kwani kila unachopanda lazima utavuna.

Kawaida maneno tunayoongea kwenye ndoa wetu ni kama kioo kwa mwingine (mwanandoa mwenzako).
Ukisema nakupenda, mwenzako anajisikia vizuri na kujihisi kweli anapendwa;
Ukisema umependeza, atajisikia vizuri na kujiona amependeza;
Ukisema ndoa chungu, na mwenzako atajisikia ndoa chungu,
Ukisema nitakufa ni kweli utakufa kabla ya muda wako.

Hivyo ni vizuri kila mmoja kuongea maneno yanayojenga ambayo ni positive ili ndoa zetu zidumu.
Ukizoea kutamka neno talaka ni kweli usishangae siku ndoa inaishia kule unaitamkia hata kama ulikuwa unatania.
Ndoa haitaniwi!
Neno talaka inabidi lifutwe kwenye misamiati yako hasa baada ya kuoa au kuolewa

Duniani tuna watu wa aina tatu tu:
Kwanza wale wanafikiri chakuongea kabla ya kuongea
Pili wale wanafikiri cha kuongea huku wanaongea
Tatu wale wanaongea kwanza ndo wanafikiria nini wameongea
Wewe upo kundi gani na unatumia vipi uwezo wako wa maneno?
Unajua wewe.................................

“Divorce is more Painful than Death”

Matatizo makubwa yanajenga Ndoa!

Hata ndoa zenye afya njema bado hukutana na matatizo na tofauti kati ya ndoa imara na zile zisizo imara ni namna matatizo yanavyoshughulikiwa hasa matatizo madogomadogo.
Pia wapo wana ndoa ambao mmoja wao (hasa mwanaume) hata kama kuna matatizo (problems) katika ndoa huendelea kukataa kwamba hakuna tatizo lolote, ukweli ni kwamba ku-ignore tatizo hakufanyi tatizo liondoke bali linazidi kuwa tatizo kubwa.
Matatizo makubwa ya ndoa nyingi ni kushindwa kutatua tatizo lililopo wakat bado linaonekana dogo kama vile kukosa mawasiliano mazuri kati ya wanandoa.
Utafiti mwingi unaonesha kwamba matatizo makubwa kama kufiwa mtoto, kupunguzwa kazi, kuuungua nyumba, ajali, kufilisika business, kuugua ugonjwa mzito nk kawaida huimarisha ndoa zaidi tofauti na wengi wanavyofikiria na matatizo madogomadogo kama vile kutomsikiliza mwenzako, kuwa mwongo, kutomjali mwenzako, kutomzungumzia mambo ya sex kama mmoja haridhiki na kuacha matatizo haya matatizo madogo kana kwamba hayapo huweza kuharibu ndoa na kuifikisha mahali ambapo wengi hawakutegemea.

Friday, November 14, 2008

Massage

Massage (kukandwa) ni neno linalotokana na neno la kiarabu massa lenye maana touch, feel and handle.
Wakati wa kufanyiwa massage tissue zifuatazo huwa huhusika moja kwa moja klufanyiwa kazi. Muscles, tendons, ligaments, skin, joints, connective tissue na lymphatic vessels.
Maasage huweza kufanyika kwa kutumia mikono, vidole, elbow, forearm na miguu pia


Kwa nini massage ni muhimu?
Kwanza watu wanapenda kufnyiwa massage na pia massage imeonekana ni njia muhimu clinically kuwa effective kimwili na kihisia.
Maaasage ni tiba ya mwili na nafsi pia huhusika katika emotions na mental needs and wants.
Kwa kuwan touch ni hitaji la msingi la mwili kuunganishwa na mtu mwingine basi massage ni njia nzuri kwa wanandoa kufanyiana wakiwa faragha angalau mara moja kwa wiki hasa kutokana na vurugu za maisha na kuchoka na wakati huohuo kutaka kutimiziwa mahitaji ya tendo la ndoa.

Nini faida za massage kwenye mwili?
Huimarisha immune system
Ina stimulate kutokea kwa endorphins ambazo ni body natural painkiller.
Husaidia kuwezesha kupumua vizuri.
Husaidia kuimarisha mzunguko wa damu na oxygen kwenda kwenye cell zote za mwili na tishu.
Inasaidia kuipa mwendo process ya kutoa uchafu mwilini (metabolic wastes)
Huimarisha muscles.
huimarisha joints na kuzipa uwezo wa kuwa flexible.
hupunguza maumivi ya joints.
Huimarisha mapozi.
pia inafanya uwe athletic mzuri.
Hupunguza stress na anxiety.
Hufanya ujisikie relaxed.
Huimarisha usingizi.
Huondoa matatizo ya depression.
Hufanya ujisikia well being.
Hutoa uwezo wa mind na body upya
Hufanya ujisikia katika hitaji la kuwa cared, safe na nurtured.
Pia kama upo na mumeo au mkeo hufanya ujisikia tayari kwa mahaba.

je, ni mafuta gani yanafaa kwa kufanyia massage?
Sweet almond oil.
Apricot kernel oil.
Jojoba oil.
Fractionated coconut oil
Sunflower oil.
Avocado oil
Cocoa butter,
Grapeseed oil.
Olive oil
Shea butter nk
Weekend Njema!


Thursday, November 13, 2008

Kuwajibika!

Yaani unasubiri huyu jamaa akuchekeshe ndo ujisikie una furaha, mwenzio analipwa! Kuwajibika na kujitoa ni moja ya mahitaji muhimu sana ya mafanikio yoyote dunia leo.
Pia hakuna sehemu muhimu kwa kuwajibika na kujitoa kama kwenye ndoa na mambo ya familia.

Watu wanaoamua kuoana huwa wanawajibika na kuhakikisha wanajitoa kwa ajili ya uamuzi na uchaguzi wamefanya kwanza kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ili kuhakikisha ndoa inaendelea.

Kila anayeingia kwenye ndoa huwa anakuwa amebeba limfuko la matatizo binafsi na kutokukomaa katika maisha ya ndoa (immaturity), hana uzoefu na kinachofuata ni kupata uzoefu mpya.
Hivyo partners wote wanawajibika kukutana na matatizo na kuyashughulikia hayo matatizo bila kulaumiana au kumlaumu mwenzake kwa matatizo just focus to the solutions kuliko ku-focus kwenye matatizo na kuanza kulalamikiana, ingawa hapa kuna wengine huwa kichwa ngumu anajiona yeye yupo sahihi siku zote na anaweza ku-ignore kila kile mwenzake anapendekeza ili ndoa irudi kwenye amani na usalama.

"Marriage is a commitment of one imperfect person to another imperfect person".

Kila mwanandoa anahusika na kuwajibika kwa ajili ya furaha yake, hisia zake na kila reactions, hakuna mtu atakufanya uwe happy ila ni wewe kwanza, kwani ukishinda umekasirika siku nzima au mwezi mzima au hata mwaka unapata faida gani?

Furaha ni matokeo ya kukomaa kwa mtu na kufahamu kwamba yeye mwenyewe ni chanzo cha furaha na simwingine.
Wewe ukiwa na furaha na wengine watakuwa na furaha.
Watu wenye furaha hutengeneza ndoa zenye furaha na watu wasio na furaha hutengeneza ndoa zisizo na furaha.

Wednesday, November 12, 2008

Usimfananishe

Eti mbona wenzako wakivaa lemba wanapendeza!
Kuna wakati huwa inashangaza sana ukisikia yale wanandoa wanafanya au wanataka yafanyike katika ndoa zao.

Kama ni mwanamke basi una marafiki wanawake wenzako ambao waume zao inawezekana wana pesa nyingi kuliko mumeo, wamesoma kuliko mumeo, wana mali kuliko mumeo, wana akili kuliko mumeo, wanakuwa na muda zaidi na familia zao kuliko mumeo, wakivaa wanapendeza kuliko mumeo na pia wanabembeleza wake zao kuliko mumeo, au wana tabia njema kuliko mumeo au kama wewe ni mwanaume nawe una marafiki wa kiume ambao wake zao wapo hivyo.

Je, ni mara ngapi umemlalamikia mumeo au mkeo kwa kumlinganisha na wanaume wengine au wanawake wengine?
Inawezekana umemlalamikia mumeo au mkeo kwamba
“Mwenzako Kelvin au Peggy amepunguza uzito wewe umebaki umenenepeana kama kitimoto kwa nini?
“Mwenzako George amenunua gari wewe nini kinakushida , wewe ni mwanaume gani?”
Mwenzako mama Noel kila siku ukienda kwake nyumba safi wewe inakuwaje chafu namna hii”
Kama ni wewe utajisikiaje?
Hapa msipotoana ngeu au kuzuka zogo basi kati yenu mmoja hana baadhi ya homoni fulani fulani mwilini ndo maana kabaki kimya.

Kitu cha msingi ni kujikubali kwamba huwezi kupata kila kitu au mwenzako kuwa kama walivyo wengine kama vile umeoana na “mr right or mrs right”

Dunia itakuwa na ndoa za ajabu sana kama wote tungeamua kila tunachokiona kwenye ndoa zingine lazima tuwe nacho.
"Furaha si kuwa na kila kitu unachohitaji bali ni kuhitaji kile ulichonacho".

Tuesday, November 11, 2008

Ni U-Shape

Ndoa ni msingi wa jamii yoyote duniani.
Pia malezi ya watu katika jamii huanzia katika ndoa.
Hii ina maana ndoa bora tunpata taifa bora.

Linapokuja suala la ndoa mambo mengi hushangaza sana watu na wanandoa wenyewe.
Wengi hujikuta na mauzauza ya kushangaa yule alikuwa naye mbele ya kanisa na mbele za mungu kufungishana ndoa kuuthibitisha ulimwengu kwamba nimepaa liubav langu, na baada ya kukaa kwenye ndoa miezi, au mwaka au miaka anakuta ni mtu mwingine kabisa kwa tabia na kila kitu kama vile kabla ya ndoa alikuwa mwingine na baada ya ndoa ni mwingine.

Habari njema ni kwamba maisha ya ndoa yapo mfano wa U shape kwa maana kwamba wakati wanandoa wanakutana kabla ya kuoana upendo huwa juu sana na mahaba huwa katika kiwango cha juu, then yanakuja mauzauza na jinsi miaka inavyoenda basi huko mbele mahaba na upendo huanza kurudi na upanda juu tena kukamilisha umbo la U.
Hata kama ndoa yako inakukatisha tamaa namna gani bado tumaini lipo na kwa msaada wa Mungu unaweza kurudi na kukamilisha umbo.

Monday, November 10, 2008

Je, Unajua haya?

Nusu ya ajali za barabarani ni kutokana na madereva kuutwika wakati wanaendesha magari, hata hivyo likija suala la ndoa ulevi na kuvuta sigara husababisha ajali mbaya sana. Hakuna tofauti ya muda unaotakiwa kwa mwanamke mwenye afanya njema na mwanaume mwenye afya njema wote ni kiwango cha dakika 10 tu kuwa wamesisimka na tayari kwa mapenzi.

Asilimia 1 ya watu wazima hawana hamu ya mapenzi (zero sex drive) na wala hawapo attracted na mwanaume au mwanamke yeyote.
Pia asilimia 3 hadi 6 ya watu wazima katika jamii wapo addicted na tabia fulani ya mambo ya sex kama vile kunusa chupi, soksi au viatu vya mpenzi wao, au kunyonya nyayo za mpenzi wao, au kuiba chupi za wanawake au wanaume na kutembea nazo nk.

Ukiacha harufu mbaya na ladha chafu ya mdomo kwa mpenzi wao wanaume wanavuta sigara husababisha kuongezeka (double) kiwango cha mwanaume kushindwa kusimamisha uume (erectile dysfunction) wakati wa kufanya mapenzi.

Hysteria ni ugonjwa ambao huwapata sana wanawake na tiba iliyopo ni kwa daktari kumsisimua mwanamke kimapenzi hadi afike kileleni (orgasm) kwa kutumia vifaa maalumu (vibrator). Inaaminika kwamba hii ni Kutokana na irregular movement ya damu kutoka kwenye uterus kwenda kwenye ubongo.
Kwa sasa daktari akigundua mwanamke unaumwa hysteria anakupeleka kwa sex therapist akupe tiba.

Watu walipoulizwa kwa nini wanafanya mapenzi, utafiti unaonesha walitoa sababu tofauti zaidi ya 237 na moja ya hizo sabab ni “kwa sababu nampenda (yaani love)” na wastani ilikuwa ni sababu ya namba 7 kwa wanawake na namba 17 kwa wanaume.
Je unapata picha gani hapo?

Kufanya mapenzi mara moja kwa wiki kwa mwanamke humsaidia kuimairisha fertility hasa kwa kulinganisha (stabilize) vizuri kiwango cha homoni na mzunguko wa siku zake.

Jasho la mwanaume lina androstadienone, kemikali inayoimarisha mood nzuri na kusisimka kimapenzi kwa mwanamke na pia ina boosts kiwango cha homoni zinazipambana na stress kwa mwanamke.
je, mwanaume ni dawa akiwa anatoa jasho? Mmmmmmm!!!! walakini

Kusisimka kimapenzi (sexual arousal) na upendo (romantic love) vina sehemu tofauti kwenye ubongo na romantic love ni imara zaidi na hudumu kwa muda mrefu kuliko kusisimuliwa kimapenzi.

Source: Wing Sze (FASHION Magazine)

Ile ya Asubuhi!

Kama wewe upo kwenye ndoa basi utafiti unaonesha kwamba kufanya sex asubuhi hukuweka kwenye afya njema zaidi.

Kutokana na utafiti kutoka chuo kikuu cha Queen Belfast watafiti wanasema kwamba sex mara tatu asubuhi kwa wiki hupunguza uwezekano wa kupata heart attack, au stroke kwa nusu nzima na kufanya mapenzi mara kwa mara asubuhi huimarisha mzunguko wa damu na kupunguza blood pressure.

Kufanya mapenzi asubuhi husaidia kupunguza kupata kisukari kwani kwa kitendo hicho unaweza kuchoma idadi ya calories 300.

Pia sex asubuhi huweza kupunguza arthritis (maumivu kwenye viungo kama magoti nk) pia husaidia kuzalisha homoni za testosterone ambazo husaidia mifupa na mishipa kuwa imara.
Pia mahaba ya asubuhi pia husaidia nywele kung’aa na kunawiri vizuri pamoja na ngozi kwa kusaidia uzalisha kiwango kikubwa cha oestrogen na homoni zingine zinazofanana na hiyo
.

Pia utafiti ulionesha kwamba wanawake ambao waume zao hawakutumia condom walikuwa ngangari linapokuja suala la stress na depression ukilinganisha na wale ambao waliuwa wanatumia condom wakati wa sex.

Pia watafiti wana onya kwamba mahaba ya asubuhi yasiwe yale ya kuchosha kwani yanaweza kusababisha kuwa na immune system dhaifu.

Friday, November 7, 2008

Punguza matarajio

Wakati wa uchumba noti zinatoka kirahisi, ukiolewa tu bajeti inabana! Baadhi ya wanandoa wapya mwaka wa kwanza wote huwa bado ni wakati wa honeymoon pia, kwa ndoa zingine unapoisha mwaka tayari tofauti huanza kujitokeza na kama si tofauti basi baadhi ya ahadi ziliahidiwa wakati wa ndoa huanza kuota mabawa.

Habari njema ni kwamba kati yao wanandoa hakuna aliye na kosa wote wapo sahihi kwa kuwa hakuna mzoefu wa ndoa wote wanaanza kupata uzoefu mpya hivyo tofauti lazima ziwepo ili wapate uzoefu.
Inawezekana wewe unapenda kusikiliza muziki kwa sauti ya chini na mwenzako anapenda husikiliza muziki kwa sauti kubwa kama vile ni Dj.
Inawezekana wewe unapenda kutazama movie kimya kimya ila yeye anataka kuielezea hadi kila hatua movie inavyoenda hadi inakuwa usumbufu na hakuna maana ya kuangalia hiyo movie. Inawezekana yeye anapenda sex kabla ya kulala na wewe unapenda sex kabla ya kuamka asubuhi sasa inakuwa vurugu maana hakuna maelewano.
Inawezekana yeye anapeda maombi (kuomba Mungu) kabla ya kulala wewe unapenda maombi kabla ya kuanza siku asubuhi.
Inawezekana kabla ya kuoana ulikuwa anajitahidi kujiweka portable lakini sasa amenenepeana kama kitimoto.

Matatizo mengi ya mwaka wa kwanza katika ndoa mpya huweza kuepukika kwa kupunguza matarajio juu ya mwenzako na juu ya ndoa yako na kwamba kila kitu kitakuwa kama unavyotaka wewe.
Pia usitegemee kwa kuwa anakupenda basi kila kitu atafanya na kuwaza kama unavyotaka wewe.
Punguza matarajio!

Mfano:
Kelvin alikuwa mwema sana linapokuja suala la pesa wakati wa uchumba kabla hajamuoa Peggy.
Alikuwa tayari kumnunulia zawadi yoyote, kitu chochote, na wakati mwingine alimpa pesa Peggy atumieanavyotaka yeye na afanyie kitu chochote anachojisikia kufanya kama vile kwenda saloon kujiweka sawa au kununua pamba anazotaka nk.
Baada ya kuoana ndani ya mwaka mmoja, Kelvin amekuwa mchungu wa pesa hadi Peggy anahisi kama ni mwanaume tofauti na yule wa wakati wa uchumba.

Sasa ni mgogoro kila linapokuja suala la matumizi ya pesa na Kelvin kila mara aamlaumu mkewe Peggy kwamba hajui kutumia pesa vizuri na anatumia ovyo kwa vitu visivyo na maana kama kwenda saloon kutengeneza kucha na nywele.

Ukweli ni kwamba mwanaume akiwa kwenye uchumba huwa anajitahidi sana kumfurahisha mwanamke ili avutike na hatimaye aoe na akisha oa anaanza kuwaza kuhusu watoto shule, kujenga nyumba, kuwekeza nk. na mipango mingie endelevu ya maisha.

Mwanamke anahitaji kupunguza matarajio otherwise awe na pesa zake mwenyewe kwa ajili ya mambo ya ziada.
Jambo la busara ni kuacha kuzozana kwa issues ndogo kama hizo (petty) jaribu kupunguza expectations na jenga familia.
Kumbuka hakua mtu anaweza kuondoa furaha yako au kukufanya ujione inferior hadi uamue mwenyewe so be you.
God bless you so much!

Thursday, November 6, 2008

Wana bacteria wengi kuliko.......

Mikono ya wanawake huvutia bacteria wengi kuliko wanaume! Utafiti unaonesha kwamba wanawake wana bacteria wengi kwenye mikono kuliko wanaume.
Na kila mwanaume au mwanamke ana aina tofauti ya bacteria kuliko mwingine tena bacteria wa aina tofauti.

Huu Utafiti umefanywa na Profesa Rob Knight wa chuo kikuu cha Colorado nchini Marekani katika Idara ya Biochemistry.
Hii ni baada ya kuchukua sample za mikono ya wanachuo 51 (mikono 102) na kutafuta kiwango cha bacteria waliomo kwa kutumia utaalamu wa juu sana wa kugundua aina ya bacteria kwa kutumia DNA.
Utafiti ulibaini aina 4,742 za bacteria (species) na kila mkono ulikuwa na zaidi ya bacteria 150 aina tofauti bacteria.
Pia wanawake wamegundulika kuwa wana bacteria wengi wanaoishi ndani ya ngozi yao hasa isiposafishwa ukilinganisha na wanaume.

Je, nini kinasababisha wanawake kuwa na bacteria wengi kuliko mwanaume?
Hii ni kutokana na tofauti ya kiwango cha acid kwenye mwili (pH), wanaume wana kiwango kikubwa cha Acid mwilini kuliko wanawake.
Pia tofauti ya kiwango na aina ya mafuta (oil) na jasho (sweat) linalozalishwa mwilini hasa kutokana na aina tofauti ya homoni mwilini (testosterone and oestrogen)
Pia matumizi mbali mbali ya vipodozi katika ngozi na miili yao.

Je, wanawake hawawaambukizi wanaume bacteria wanaposalimiana?
Watafiti wanasema haina noma kabisa kwani bacteria wengi hawana madhara hivyo unaweza kubusu hata mikono yao na miili yao kwa raha zako.
Tahadhari:
Ni jambo la msingi na muhimu kuosha mikono mara kwa mara unapoisi imeshafuka bila kujali wewe ni mwanamke au mwanaume kwa ajili ya afya zetu katika jamii zetu.
Source:University of Colorado at Boulder (2008, November 4). Women Have More Diverse Hand Bacteria Than Men. ScienceDaily. Retrieved November 5, 2008, from http://www.sciencedaily.com­ /releases/2008/11/081103192310.htm

Tuesday, November 4, 2008

Si kila kitu kinakuhusu

Utaniambia leo ulipitia wapi na ulikuwa na nani! Kila mtu duniani ana siri zake binafsi na kuwa wakati hapendi mtu yeyote ajue ila ni yeye na Mungu wake.
Si siri tu bali hupenda kuwa mwenyewe na kujiamulia mambo yake mwenyewe kwa kadri anavyotaka.
Unapokubali kuoana na mwanaume au mwanamke maana yake unaruhusu kuanza maisha ya pamoja (sharing) katika hisia, emotions, kazi, kitanda, bafu, harufu, nguo nk.
Hata hivyo hii haina maana kwamba tunawajibika upande mwingine yaani mume au mke kujua kila kitu kwani kila mmoja huhitaji kuwa na siri au kufanya kitu mwenyewe.

Hapa ninazungumzia vitu ambavyo ni vizuri havina uhusiano na tabia mbaya kama ulevi au kukosa uaminifu.

Hata hivyo wapo wanaume zetu au wake zetu hutaka kujua kila kitu tunachofanya na kila mahali tulikuwa zaidi ya mama zetu walivyokuwa wanatuchunga wakati watoto.

Kama mwanaume umeenda kazini, mkeo anataka kujua kwanza wakati unaenda kazini uliongea na nani, umefanya nini, umekula nini na nani, ulipotoka kazini ulipitia wapi, na mlikuwa na nani na atachukua simu ya mkono na kuanza kuangalia nani alipiga, nani alipigiwa na nani alikutumia sms na nani alitumiwa, ni kuchunguzana na kuulizana zaidi ya FBI.
Maswali mengi utafikiri ndoa ni mahakamani.
Mume anaogopa hadi kurudi nyumbani maana anaona ni usumbufu.
Kwani ni lazima ujue kila kitu?
Ukweli kama wewe ni mwanamke si lazima ujue kila kitu kuhusu mume wako, alikuwa wapi, alikuwa na nani, amefanya nini na ilikuwaje nk, kuna vitu ni non of your business.

Inawezekana unajua kutoka kazini hadi nyumbani huwa anatumia dakika 20 lakini sasa ametumia dakika 50, ile anafika nyumbani tu unambana na maswali ajieleze alikuwa wapi, alikuwa na nani, na analikuwa anafanya nini na ilikuwaje, inawezekana alipitia kwa rafiki zake aliosoma nao pia si lazima ujue kila kitu yeye ni mtu mzima si mototo tena, yaani anajisikia kama vile wewe ni mama yake kitu ambacho kinakupunguzia alama na anahisi hujiamini na pia msumbufu na humuamini.
Kama anataka kuishi na mtu anayetaka kujua kila kitu kuhusu yeye, basi angebaki kwa mama yake na si kuoana na wewe.

Ukweli si lazima ujue kila kitu kuhusu yeye, mwamini, mpende, mfurahie hata kama amechelewa kwa muda kidogo zaidi na alivyo kwambia.

Ungefanyeje?

Unarudi nyumbani umechoka kutoka kazini ile kufika tu unakutana na kazi ya ubunifu ya akina dogo namna hii.
Je, utafanya nini?

Monday, November 3, 2008

Walisema haoi, Ameoa!

Manuel Uribe jitu la nusu tani Mwanaume mzito kuliko wanaume wote duniani (guinness record) mwenye uzito wa Kg 560, nusu tani (88 stone) Manuel Uribe (43) amemuoa rafiki yake wa kike Caludia Solis (38) mbele ya mashahidi 400 huko mexico katika mji wa Monterrey tarehe 26 octoba 2008.

Bibi na Bwana wakifurahia jambo Manuel alikutana na binti mrembo Claudia tangu mwaka 2006 na tangu akutane na huyu mwanamke kwa pamoja wamesaidiana kuhakikisha manuel anapunguza uzito na amejitahidi kupunguza Kg 250 (39 stones) rekodi ambayo inaweza kumuweka tena kwenye kitabu cha guinness kwa kupunguza uzito mkubwa.

Picha chini Bibi harusi Claudia Solis siku ya harusi Manuel alibubujikwa na machozi pale msajili alipotamka kwamba wao sasa ni mume na mke.
Na hakusita kutamka maneno haya huku akibubujikwa na machozi
Nimefurahi sana leo ni siku yangu maalumu Mungu ameruhusu siku nzuri kama hii mimi na mrembo Claudia kuoana”.
Huyu bwana hajawahi kutoka kindani mwaka kwa miaka 6 mfululizo na harusi yake ilifanyika kitandani baada ya kubebwa kuelekea sehemu ya harusi na gari la kuvuta.
Pia harusi yao imekuwa documented na Discovery Channnel

Inawezekana umenenepa au kuwa mwambamba sana au hali yoyote ile na imepelekea usijiamiini kwamba huwezi kuoa au kuolewa, hayo ni mawazo potofu, bado kuna mtu anakupenda duniani ni wewe tu.
Ukweli unabaki kwamba kuna mwanamke yupo kwa mwanaume yoyote bila kujali ni mnene kiasi gain, mwembamba kiasi gani au kilema kiasi gain, au sura mbaya kiasi gain, upendo wa kweli ukiwa kazini hakuna lisilowezekana.

Picha chini maharusi wakibusiana siku ya harusi yao "It goes to show you it is not the size of the nail that counts, it is the size of the hammer".

Mpende, Mtunze, Mlinde, Mbusu

Siku zinayeyuka kama barafu kwenye jua na mwaka huooo una katika.
Je, mke wako au mume wako ameweza kukupa muda (quality time) kuwa na wewe kiasi gani tangu January 2008?
Wewe ndo unajua.