"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, November 27, 2008

Hujanielewa!

Nimewakuta hawa nao hawaelewani!
Wanachanganyana lugha!
Matokeo yake gari haliendi! Mume na mke wakiwa kwenye gari walipita sehemu ambayo wanauza soda, mke akamuuliza mume “je, unaweza kusimama kwa ajili ya kunywa soda?” mume akamjibu kwa uaminifu kabisa mke wake kwamba “hapana haina haja" na hawakusimama kwa ajili ya kunywa soda.

Matokeo?
Ukweli mwanamke alitaka wasimame wapate soda, na alikwazwa au kuumia sana kwamba mume hakukubali wasimame kwa ajili ya soda.
Alijisikia pendekezo lake halikupokelewa na mumewe, alijiona amekatishwa tamaa.

Mume naye alipohisi mke wake kakasirika na kukwazwa alifadhaishwa sana kwani alijiuliza kama alikuwa anataka kweli nisimame kwa ajili ya soda siangesema tu kwamba anataka tusimame kunywa soda kuliko kuniuliza nichague?

Hii ina maana gani?
Hii ina maana mwanaume hakujua kwamba mke wake alipouliza swali alikuwa hahitaji jibu au uamuzi (decision) bali ilikuwa ni njia ya kuanzisha mazungumzo na kuonyesha hisia zake kuhusu kusimama wapate soda.

Na mwanamke naye hakufahamu kwamba mwanaume aliposema "hapana" hii haina maana kwamba alikuwa anatoa jibu la mkato kuonesha utawala mbovu na kutojali hisia zake bali alikuwa anaelezea uamuzi wake na kile alikuwa anapenda kujibu baada ya kuulizwa swali lenye kujibu ndiyo au hapana na yote alikuwa majibu sahihi kama yangetolewa.

Wakati mwanamke na mwanaume kwenye ndoa wanapotoa majibu blue namna hii bila kujua mwanamke na mwanaume wanatakiwa kuwasiliana vipi, ukweli inaweza kuzalisha hasira na kukwazana kusiko tamkika.

Nini kitu cha msingi kuzingatia?
Ukweli ni kwamba mwanaume na mwanamke wapo tofauti sana linapokuja suala la mawasiliano baona yao.
Kwa mwanaume kuongea ni kuonesha uwezo wake katika kutoa maamuzi au status aliyonayom katika jamii au katika ndoa au katika eneo analoishi, wakati mwanamke kuongea ni kutoa hisia zake ili kuhitaji msaada wake au kuelezea kitu kijadiliwe na si kutolewa maamuzi hata kama ni swali.

Wanawake mara nyingi huongea huku wakifikiria kutaka ukaribu (closeness) na wale wanawapenda, wanawapa nafasi katika maishayao na hivyo hujitahidi sana kulinda intimacy.
Wanaume wapo focused kwenye status hivyo huongea uhuru wao, uwezo wao, maamuzi yao na hii husababisha mwanaume na mwanamke kuongea kitu kimoja na kuwa na maana tofauti na matokeo yake kutoelewana.
Wanawake wengi huumia sana pale mwanaume anapotoa majibu ya mkato na u ukali hasa kitendo cha kujibu kwa mkato na kunyamaza kama vile anam-ignore.
Kwa mwanaume kuongea ni ku-share information kwa mwanamke kuongea ni ku-share feelings. Ndiyo maana wanaume huongea sana kwenye public na kutoa jokes na stories lakini wakiwa home huwa kimya hata hivyo wao hufanya hivyo kwenye public kujipatia attention na status kwamba yeye ni mwanaume ni hero, ni kiongozi, ni mwenye nguvu yeye ni kidume.

1 comment:

Anonymous said...

A man was being chased by a lion in the jungle. As he gets tired and feels he can't run anymore he stands still and pray: 'Ohhhhh God, would you please make this lion a Christian please?
By Msafiri