"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, November 10, 2008

Je, Unajua haya?

Nusu ya ajali za barabarani ni kutokana na madereva kuutwika wakati wanaendesha magari, hata hivyo likija suala la ndoa ulevi na kuvuta sigara husababisha ajali mbaya sana. Hakuna tofauti ya muda unaotakiwa kwa mwanamke mwenye afanya njema na mwanaume mwenye afya njema wote ni kiwango cha dakika 10 tu kuwa wamesisimka na tayari kwa mapenzi.

Asilimia 1 ya watu wazima hawana hamu ya mapenzi (zero sex drive) na wala hawapo attracted na mwanaume au mwanamke yeyote.
Pia asilimia 3 hadi 6 ya watu wazima katika jamii wapo addicted na tabia fulani ya mambo ya sex kama vile kunusa chupi, soksi au viatu vya mpenzi wao, au kunyonya nyayo za mpenzi wao, au kuiba chupi za wanawake au wanaume na kutembea nazo nk.

Ukiacha harufu mbaya na ladha chafu ya mdomo kwa mpenzi wao wanaume wanavuta sigara husababisha kuongezeka (double) kiwango cha mwanaume kushindwa kusimamisha uume (erectile dysfunction) wakati wa kufanya mapenzi.

Hysteria ni ugonjwa ambao huwapata sana wanawake na tiba iliyopo ni kwa daktari kumsisimua mwanamke kimapenzi hadi afike kileleni (orgasm) kwa kutumia vifaa maalumu (vibrator). Inaaminika kwamba hii ni Kutokana na irregular movement ya damu kutoka kwenye uterus kwenda kwenye ubongo.
Kwa sasa daktari akigundua mwanamke unaumwa hysteria anakupeleka kwa sex therapist akupe tiba.

Watu walipoulizwa kwa nini wanafanya mapenzi, utafiti unaonesha walitoa sababu tofauti zaidi ya 237 na moja ya hizo sabab ni “kwa sababu nampenda (yaani love)” na wastani ilikuwa ni sababu ya namba 7 kwa wanawake na namba 17 kwa wanaume.
Je unapata picha gani hapo?

Kufanya mapenzi mara moja kwa wiki kwa mwanamke humsaidia kuimairisha fertility hasa kwa kulinganisha (stabilize) vizuri kiwango cha homoni na mzunguko wa siku zake.

Jasho la mwanaume lina androstadienone, kemikali inayoimarisha mood nzuri na kusisimka kimapenzi kwa mwanamke na pia ina boosts kiwango cha homoni zinazipambana na stress kwa mwanamke.
je, mwanaume ni dawa akiwa anatoa jasho? Mmmmmmm!!!! walakini

Kusisimka kimapenzi (sexual arousal) na upendo (romantic love) vina sehemu tofauti kwenye ubongo na romantic love ni imara zaidi na hudumu kwa muda mrefu kuliko kusisimuliwa kimapenzi.

Source: Wing Sze (FASHION Magazine)

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kwani ndoa nyingi zinakufa kutokana na mmoja katika ndoa anakunywa sana kwa hiyo akisha kunywa basi hawezi tena ile kazi ya chumbani yaani kufanya mapenzi yeye sasa ndo inakuwa kama amepata dawa ya usingizi. NDOA KAZI KWELI