"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, November 13, 2008

Kuwajibika!

Yaani unasubiri huyu jamaa akuchekeshe ndo ujisikie una furaha, mwenzio analipwa! Kuwajibika na kujitoa ni moja ya mahitaji muhimu sana ya mafanikio yoyote dunia leo.
Pia hakuna sehemu muhimu kwa kuwajibika na kujitoa kama kwenye ndoa na mambo ya familia.

Watu wanaoamua kuoana huwa wanawajibika na kuhakikisha wanajitoa kwa ajili ya uamuzi na uchaguzi wamefanya kwanza kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ili kuhakikisha ndoa inaendelea.

Kila anayeingia kwenye ndoa huwa anakuwa amebeba limfuko la matatizo binafsi na kutokukomaa katika maisha ya ndoa (immaturity), hana uzoefu na kinachofuata ni kupata uzoefu mpya.
Hivyo partners wote wanawajibika kukutana na matatizo na kuyashughulikia hayo matatizo bila kulaumiana au kumlaumu mwenzake kwa matatizo just focus to the solutions kuliko ku-focus kwenye matatizo na kuanza kulalamikiana, ingawa hapa kuna wengine huwa kichwa ngumu anajiona yeye yupo sahihi siku zote na anaweza ku-ignore kila kile mwenzake anapendekeza ili ndoa irudi kwenye amani na usalama.

"Marriage is a commitment of one imperfect person to another imperfect person".

Kila mwanandoa anahusika na kuwajibika kwa ajili ya furaha yake, hisia zake na kila reactions, hakuna mtu atakufanya uwe happy ila ni wewe kwanza, kwani ukishinda umekasirika siku nzima au mwezi mzima au hata mwaka unapata faida gani?

Furaha ni matokeo ya kukomaa kwa mtu na kufahamu kwamba yeye mwenyewe ni chanzo cha furaha na simwingine.
Wewe ukiwa na furaha na wengine watakuwa na furaha.
Watu wenye furaha hutengeneza ndoa zenye furaha na watu wasio na furaha hutengeneza ndoa zisizo na furaha.

1 comment:

Shabani Kaluse said...

Habari yako kaka Mbilinyi.

Jana wakati napitia Blog mbalimbali, nimekutana na blog yako.
Miongoni mwa mada ulizojadili nimevutiwa sana na mada hii ya kuwajibika katika ndoa, kusema kweli, sababu kubwa ya ndoa nyingi kuyumba au kama si kuvunjika ni hii ya wanandoa kutokuwajibika. Hata hivyo ipo sababu nyingine ya watu kutokuwa na upendo wa kweli wakati wanaposana.
Kukosekana kwa upendo pia kunasababisha wandoa kutokuwajibika.
Neno upendo ukiliangalia kijuujuu litakupa maana nyepesi tu, kwamba upendo wa kweli katika ndoa ni kupendana kati a mume na mke. Lakini kama neno “upendo” ukiliangalia kwa uzito wake utagundua kwamba limebeba maana pana sana kuliko mtu anavyoweza kufikiria.
Hebu jaribu kuwauliza watu waliooana miaka ya 1960, na usikilize majibu yao kwa makini.
Naamini kabisa utajua upendo ninaouzungumzia hapa, ni upendo wa namna gani.
Kabla sijendelea , hebu tutazame mfano huu wa wajapani halafu tuje tuangalie kwa upande wetu kwamba upendo wa kweli umesimamia wapi?
Kwa mujibu wa japisho moja lililotolewa hivi karibuni nchini Japan, ni kwamba ndoa nyingi zilizofungwa miaka ya 1960 ni imara sana, ingawa zilikuwa hazina upendo hata chembe.
Mama mmoja mtu mzima aliyejulikana kwa jina la Yuri Uemura alisema “ndoa yangu na mume wangu haikuwa na upendo hata kidogo tangu tumeoana, lakini tumedumu kwa miaka 40”
Mama huyo aliendelea kusema kwamba, tangu wameoana, mume wake hakuwahi kumwambia kuwa anampenda, hakuwahi kumshika mkono kuonesha ishara ya upendo wakati wakitembea barabarani, hakuwahi kumnunulia zawadi yoyote na wala hakuwahi kumwambia “Ahsante” kwa jambo lolote zuri alilomtendea na hakuwahi kufurahishwa na yeye hata siku moja.

Lakini aliweza kudumu na mume wake huyo kwa miaka 40 bila kugombana kiasi cha kutishia kuvunjika kwa ndoa yao.
Alipoulizwa, ilikuwaje akadumu kwenye ndoa hiyo? Alijibu kwamba, alichofanya ni kumzoea mume wake na kumchukulia kama alivyo kwa sabau hiyo ndio tabia aliyomkuta nayo.
Jambo lililokuwa muhimu kwake ni ile tabia ya mumewe katika kutunza familia na kuwajibika kama baba.
Kwa mujibu wa chapisho hilo, hadi kufikia miaka ya 1980, Japani ilikuwa na kiwango kidogo sana cha talaka katika nchi zinanaoendelea na zilizoendelea.
Hii haikutokana na kwamba watu walikuwa wanapendana sana, bali ndoa ilikuwa ni jambo lililosimamiwa na mila na desturi, upendo haikuwa ni mojawapo sababu muhimu za watu kuoana.
Hivyo basi kutokea watu kutalikiana lilikuwa ni jambo la aibu kubwa na ilikuwa inadhihirisha ni kwa kiasi gani wahusika ni dhaifu wa kushindwa kuhimili misukosuko ya ndoa.
Na hii yote ilitokana na dhana ya ndoa kuchukuliwa kama mgawanyo wa majukumu kati ya mume na mke kwa maana mume kuwa ni mtafutaji wa mkate wa kila siku kwa familia na mke anakuwa ni mama wa nyumbani wa kutunza nyumba na watoto.
Kwa hiyo kutalikina kuanaashiaria kwamba wote wameshindwa kutekeleza majukumu yao. Lakini tofauti na miaka ya 1960, siku hizi wanawake wengi nchini Japani wamejiingiza katika kufanyakazi, na hii imepelekea vijana wengi kuoana kwa kufuata ustaarabu wa nchi za Magharibi ambapo mume na mke wanasaidiana kazi za nyumbani kwa kuwa wote ni watafutaji, hivyo kuondoa ile dhana ya kwamba kazi za nyumbani ni za wanawake pekee.

Hata hivyo ule upendo wa kimagharibi umeongezeka kwa kiasi fulani miongoni mwa ndoa nyingi za vijana tofauti na ndoa za miaka 1960.
Nikisema upendo wa kimagharibi ninamaanisha ule upendo wa kupeana kadi mbalimbali zenye ujumbe wa mapenzi na kununuliana zawadi, kutembea pamoja, na kwenda kwenye mighahawa pamoja. `
Lakini pamoja na mabadiliko hayo hali imekuwa ni tofauti kwa upande wa talaka. Kati ya mwaka 1980 na 1994 kulikuwa na ongezeko kubwa la talaka nchini Japani, kutoka asilimia 20 hadi 29kwa mujibu wa chapisho lililotolewa na wataalamu wawil ma Kijapani Bwana Yamamoto na Kojima.
Kwa hiyo pamoja na mabadiliko hayo, haijawasaidia wajapani kudumu katika ndoa zao mkama zamani.
Je kwa upande wa hapa nchini hali ikoje? Hili ni swali ambalo kila mmoja wetu anpaswa kujiuliza. Siku hizi.
Binafsi naamini hatutofautiani sana na Wajapani na kama iko tofauti basi ni ndogo sana.
Siku nhizi vijana wengi wamekuwa wakioana baada ya kudanganyana kwa kuoneshana upendo wa wenzetu wa nchi za Magharibibila ya kuchunguzana kama kuna upendo wa kweli miongoni mwao.
Wanaoingia kwenye mtego huo mara nyingi ni wanawake. Kwani wao ndio wanaodanganywa kwa zawadi za thamani, kadi za upendo zilizoandikwa maneno mazuri na ya kuvutia, na pia kununuliwa maua na kutembezwa sehemu mbalimbali za starehe kila wiki.
Mara nyingi mbwembwe zote hizo hufanywa makusudi ili kumfanya msichana ajione kama anapendwa sana.Kwa kawada msichana akioneshwa upendowa namna hii hupofushwa kiasi kwamba hawezi kuchukuwa fursa kusoma tabia na mwenendo wa mwenzi wake.
Na baada ya kufunga ndoa upendohuo ambao mimi nauita wa bandia hutoweka taratibu na mwishowe hakuna upendo tena, na kinachofuatia ni ugomvi usioisha na mwishowe kufikia kupeana talaka.
Kama ukichunguza sana, utagundua kwamba wanawake wanofujwa na wanaume zao ni wale waliolaghaiwa na upendo wa aina hii.
Naamini wengi wataosoma mtazamo wangu huu, huenda wakaupinga na kuniona kama siendi na wakati, lakini naomba niweke wazi kwamba sipingi watu kuwapenda wenzi wao kwa mtindo huu wa nchi za Magharibi, bali najaribu kutahadharisha kwamba wakati mwingine upendo huo umebeba unafiki mkubwa.
Ni vema watu wakabeba uhalisi wao kuliko kuiga kuiga upendo wa nchi za Magharibi ambao una gharama kubwa ambazo ni ngumu kuziendeleza kipindi chote cha ndoa.

Kwa leo naomba niishie hapo, ukipata wasaa nitembelee kwenye blog yangu ya utambuzi, naamini, yapo mambo ambayo tunaendana, kwa sababu wote tunazungumzia ustawi wa wanaadamu.

Tembelea: www.kaluse.blogspot.com