"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, November 14, 2008

Massage

Massage (kukandwa) ni neno linalotokana na neno la kiarabu massa lenye maana touch, feel and handle.
Wakati wa kufanyiwa massage tissue zifuatazo huwa huhusika moja kwa moja klufanyiwa kazi. Muscles, tendons, ligaments, skin, joints, connective tissue na lymphatic vessels.
Maasage huweza kufanyika kwa kutumia mikono, vidole, elbow, forearm na miguu pia


Kwa nini massage ni muhimu?
Kwanza watu wanapenda kufnyiwa massage na pia massage imeonekana ni njia muhimu clinically kuwa effective kimwili na kihisia.
Maaasage ni tiba ya mwili na nafsi pia huhusika katika emotions na mental needs and wants.
Kwa kuwan touch ni hitaji la msingi la mwili kuunganishwa na mtu mwingine basi massage ni njia nzuri kwa wanandoa kufanyiana wakiwa faragha angalau mara moja kwa wiki hasa kutokana na vurugu za maisha na kuchoka na wakati huohuo kutaka kutimiziwa mahitaji ya tendo la ndoa.

Nini faida za massage kwenye mwili?
Huimarisha immune system
Ina stimulate kutokea kwa endorphins ambazo ni body natural painkiller.
Husaidia kuwezesha kupumua vizuri.
Husaidia kuimarisha mzunguko wa damu na oxygen kwenda kwenye cell zote za mwili na tishu.
Inasaidia kuipa mwendo process ya kutoa uchafu mwilini (metabolic wastes)
Huimarisha muscles.
huimarisha joints na kuzipa uwezo wa kuwa flexible.
hupunguza maumivi ya joints.
Huimarisha mapozi.
pia inafanya uwe athletic mzuri.
Hupunguza stress na anxiety.
Hufanya ujisikie relaxed.
Huimarisha usingizi.
Huondoa matatizo ya depression.
Hufanya ujisikia well being.
Hutoa uwezo wa mind na body upya
Hufanya ujisikia katika hitaji la kuwa cared, safe na nurtured.
Pia kama upo na mumeo au mkeo hufanya ujisikia tayari kwa mahaba.

je, ni mafuta gani yanafaa kwa kufanyia massage?
Sweet almond oil.
Apricot kernel oil.
Jojoba oil.
Fractionated coconut oil
Sunflower oil.
Avocado oil
Cocoa butter,
Grapeseed oil.
Olive oil
Shea butter nk
Weekend Njema!






10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ooh! inaonekana Kaka Mbilinyi ni mzoefu sana wa kazi hii labda nibuku muda ili nipate massage kwa mtu mzoefu kama wewe. ha ha haaaaa

Anonymous said...

Hapo nimeelewa Je waweza tueleza namna ya kufanya hiyo massage Thanks.
Msafiri

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,

Nitaongea na baba Camilla ajue jinsi ya kukupa massage ya uhakika. Nitamfundisha A - Z kuhusu massage na naamini atakuwa mzoefu sana kwani najua kichwa chake chepesi sana kushika mambo.

Hata hivyo nimeanzisha kituo cha kufanyia massage hapa Njombe so ukipita napoenda Mbinga usisahau kusimama kwani kuna watu nimewa train vizuri sana, ila ukitaka mambo mazuri ni kwa baba Camilla usiku kabla hamjalala.

Upendo daima

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka msafiri,

Nashukuru sana kwa swali lako naamin kuanza kufundisha jinsi ya kufanyiaa massage itachukua muda sana kwani hili ni suala rahisi na la vitendo zaidi kuliko maneno, unaweza kwenda na mkeo mahali popote kwenye spa, au saloon au sehemu ambayo wanatoa huduma ya massage ukajifunza na kwenda kumfanyia mkeo. Au unaweza ku-google neno Massage then ukasoma na kujifunzazaidi.
Kumbuka kumfanyia massage mpenzi wako ni tiba ya bure na huweza kusaidia sana kuwaweka karibu zaidi wanandoa.
Unaweza kuwa hujui ila ukianza kujifunza unaweza kuwa fundi kama mimi na mikono yako ikawa na healing power ya hakika kwa mpenzi wako.
Anza leo usingoje kesho!

Asante sana

Yasinta Ngonyani said...

nimeghaili basi naomba kazi kwani afadhali nikaishi huko njombe

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta.

Kuhusu kuja kufanya kazi Njombe sahau nafasi zimejaa kwa wazawa kwanza.

Jitahidi fanya kazi yako kwa juhudi na kuifurahia.

Upendo daima

Yasinta Ngonyani said...

jamani uchoyo huo. haya bwana nasi nikipita njombe nitapitia hapo spa ili nipate massage. kwani napenda sana

Shabani Kaluse said...

Habari yako kaka Mbilinyi,

jana katika kupitia Blog mbalimbali, nilibahatika kupitia Blog yako.
Kati mada zote nilizo soma, nilivutiwa sana na mada yako ya Kuwajibika katika ndoa, hivyo nimeona na mimi nichangie kidogo.
Kusema kweli ndoa nyingi zinayumbasa na au kama si kuvunjika kwa sababu wanandoa wengi hawawajibiki katika ndoa zao.
Hata hivyo ipo sababu nyingine ya wanandoa kutokuwa na upendo wa kweli.

Neno upendo ukiliangalia kijuujuu litakupa maana nyepesi tu, kwamba upendo wa kweli katika ndoa ni kupendana kati a mume na mke. Lakini kama neno “upendo” ukiliangalia kwa uzito wake utagundua kwamba limebeba maana pana sana kuliko mtu anavyoweza kufikiria.
Hebu jaribu kuwauliza watu waliooana miaka ya 1960, na usikilize majibu yao kwa makini.
Naamini kabisa utajua upendo ninaouzungumzia hapa, ni upendo wa namna gani.
Kabla sijendelea , hebu tutazame mfano huu wa wajapani halafu tuje tuangalie kwa upande wetu kwamba upendo wa kweli umesimamia wapi?
Kwa mujibu wa japisho moja lililotolewa hivi karibuni nchini Japan, ni kwamba ndoa nyingi zilizofungwa miaka ya 1960 ni imara sana, ingawa zilikuwa hazina upendo hata chembe.
Mama mmoja mtu mzima aliyejulikana kwa jina la Yuri Uemura alisema “ndoa yangu na mume wangu haikuwa na upendo hata kidogo tangu tumeoana, lakini tumedumu kwa miaka 40”
Mama huyo aliendelea kusema kwamba, tangu wameoana, mume wake hakuwahi kumwambia kuwa anampenda, hakuwahi kumshika mkono kuonesha ishara ya upendo wakati wakitembea barabarani, hakuwahi kumnunulia zawadi yoyote na wala hakuwahi kumwambia “Ahsante” kwa jambo lolote zuri alilomtendea na hakuwahi kufurahishwa na yeye hata siku moja.

Lakini aliweza kudumu na mume wake huyo kwa miaka 40 bila kugombana kiasi cha kutishia kuvunjika kwa ndoa yao.
Alipoulizwa, ilikuwaje akadumu kwenye ndoa hiyo? Alijibu kwamba, alichofanya ni kumzoea mume wake na kumchukulia kama alivyo kwa sabau hiyo ndio tabia aliyomkuta nayo.
Jambo lililokuwa muhimu kwake ni ile tabia ya mumewe katika kutunza familia na kuwajibika kama baba.
Kwa mujibu wa chapisho hilo, hadi kufikia miaka ya 1980, Japani ilikuwa na kiwango kidogo sana cha talaka katika nchi zinanaoendelea na zilizoendelea.
Hii haikutokana na kwamba watu walikuwa wanapendana sana, bali ndoa ilikuwa ni jambo lililosimamiwa na mila na desturi, upendo haikuwa ni mojawapo sababu muhimu za watu kuoana.
Hivyo basi kutokea watu kutalikiana lilikuwa ni jambo la aibu kubwa na ilikuwa inadhihirisha ni kwa kiasi gani wahusika ni dhaifu wa kushindwa kuhimili misukosuko ya ndoa.
Na hii yote ilitokana na dhana ya ndoa kuchukuliwa kama mgawanyo wa majukumu kati ya mume na mke kwa maana mume kuwa ni mtafutaji wa mkate wa kila siku kwa familia na mke anakuwa ni mama wa nyumbani wa kutunza nyumba na watoto.
Kwa hiyo kutalikina kuanaashiaria kwamba wote wameshindwa kutekeleza majukumu yao. Lakini tofauti na miaka ya 1960, siku hizi wanawake wengi nchini Japani wamejiingiza katika kufanyakazi, na hii imepelekea vijana wengi kuoana kwa kufuata ustaarabu wa nchi za Magharibi ambapo mume na mke wanasaidiana kazi za nyumbani kwa kuwa wote ni watafutaji, hivyo kuondoa ile dhana ya kwamba kazi za nyumbani ni za wanawake pekee.

Hata hivyo ule upendo wa kimagharibi umeongezeka kwa kiasi fulani miongoni mwa ndoa nyingi za vijana tofauti na ndoa za miaka 1960.
Nikisema upendo wa kimagharibi ninamaanisha ule upendo wa kupeana kadi mbalimbali zenye ujumbe wa mapenzi na kununuliana zawadi, kutembea pamoja, na kwenda kwenye mighahawa pamoja. `
Lakini pamoja na mabadiliko hayo hali imekuwa ni tofauti kwa upande wa talaka. Kati ya mwaka 1980 na 1994 kulikuwa na ongezeko kubwa la talaka nchini Japani, kutoka asilimia 20 hadi 29kwa mujibu wa chapisho lililotolewa na wataalamu wawil ma Kijapani Bwana Yamamoto na Kojima.
Kwa hiyo pamoja na mabadiliko hayo, haijawasaidia wajapani kudumu katika ndoa zao mkama zamani.
Je kwa upande wa hapa nchini hali ikoje? Hili ni swali ambalo kila mmoja wetu anpaswa kujiuliza. Siku hizi.
Binafsi naamini hatutofautiani sana na Wajapani na kama iko tofauti basi ni ndogo sana.
Siku nhizi vijana wengi wamekuwa wakioana baada ya kudanganyana kwa kuoneshana upendo wa wenzetu wa nchi za Magharibibila ya kuchunguzana kama kuna upendo wa kweli miongoni mwao.
Wanaoingia kwenye mtego huo mara nyingi ni wanawake. Kwani wao ndio wanaodanganywa kwa zawadi za thamani, kadi za upendo zilizoandikwa maneno mazuri na ya kuvutia, na pia kununuliwa maua na kutembezwa sehemu mbalimbali za starehe kila wiki.
Mara nyingi mbwembwe zote hizo hufanywa makusudi ili kumfanya msichana ajione kama anapendwa sana.Kwa kawada msichana akioneshwa upendowa namna hii hupofushwa kiasi kwamba hawezi kuchukuwa fursa kusoma tabia na mwenendo wa mwenzi wake.
Na baada ya kufunga ndoa upendohuo ambao mimi nauita wa bandia hutoweka taratibu na mwishowe hakuna upendo tena, na kinachofuatia ni ugomvi usioisha na mwishowe kufikia kupeana talaka.
Kama ukichunguza sana, utagundua kwamba wanawake wanofujwa na wanaume zao ni wale waliolaghaiwa na upendo wa aina hii.
Naamini wengi wataosoma mtazamo wangu huu, huenda wakaupinga na kuniona kama siendi na wakati, lakini naomba niweke wazi kwamba sipingi watu kuwapenda wenzi wao kwa mtindo huu wa nchi za Magharibi, bali najaribu kutahadharisha kwamba wakati mwingine upendo huo umebeba unafiki mkubwa.
Ni vema watu wakabeba uhalisi wao kuliko kuiga kuiga upendo wa nchi za Magharibi ambao uan gharama kubwa ambazo ni ngumu kuziendeleza kipindi chote cha ndoa.

Kwea leo naona niishie hapo, nikipata nafasi nitachangia wakati mwingine.
naomba ukipata nafasi upitie Blog yangu ya utambuzi, naamini wote tunazungumzia jambo moja linalohusu ustawi wa wanaadamu.

Tembelea: www.kaluse.blogspot.com

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Shabani Kaluse,
Nashukuru sana kwa kuntembelea na zaidi nashukuru sana kwa comments zako, nakumbuka nilikuwa nasoma makala zako kwenye gazeti la Jitambue, naamini una mengi zaidi ya uchangia nashukuru sana na karibu sana.
Nimeshaunganisha blog yako sasa tunaweza kuwasiliana bila shida.

Upendo daima

Shabani Kaluse said...

Nakushukuru sana kwa kunikaribisha na kuniunganisha na blog yako.
Na mimi vilevile nitakuunganisha kwenye blog yangu ili wadau wa utambuzi wanufaike na makala zako ambazo naona zimekaa kiutambuzi utambuzi.

Ahsante na tuzidi kuwasiliana.