"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, November 17, 2008

Matatizo makubwa yanajenga Ndoa!

Hata ndoa zenye afya njema bado hukutana na matatizo na tofauti kati ya ndoa imara na zile zisizo imara ni namna matatizo yanavyoshughulikiwa hasa matatizo madogomadogo.
Pia wapo wana ndoa ambao mmoja wao (hasa mwanaume) hata kama kuna matatizo (problems) katika ndoa huendelea kukataa kwamba hakuna tatizo lolote, ukweli ni kwamba ku-ignore tatizo hakufanyi tatizo liondoke bali linazidi kuwa tatizo kubwa.
Matatizo makubwa ya ndoa nyingi ni kushindwa kutatua tatizo lililopo wakat bado linaonekana dogo kama vile kukosa mawasiliano mazuri kati ya wanandoa.
Utafiti mwingi unaonesha kwamba matatizo makubwa kama kufiwa mtoto, kupunguzwa kazi, kuuungua nyumba, ajali, kufilisika business, kuugua ugonjwa mzito nk kawaida huimarisha ndoa zaidi tofauti na wengi wanavyofikiria na matatizo madogomadogo kama vile kutomsikiliza mwenzako, kuwa mwongo, kutomjali mwenzako, kutomzungumzia mambo ya sex kama mmoja haridhiki na kuacha matatizo haya matatizo madogo kana kwamba hayapo huweza kuharibu ndoa na kuifikisha mahali ambapo wengi hawakutegemea.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

matatizo, sisi watu ni tofauti sana wengine kama ulivyosema wakiwa na tatizo kubwa au ndogo kwao ni sawa tu. Na wengine wanakuwa vichaa kabisa na kuanza kunywa pombe, kuacha kula na pia kwenda hata kwa daktari ili wapewe dawa za usingizi. lakini wengine ni kinyume kabisa. Nisaidieni nimekwama