"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, November 21, 2008

Mpe dakika 15 kwanza

Wanaume hupenda kuwa wenyewe muda fulani (kukimbilia pangoni) hasa akiwa amerudi nyumbani kutoka kazini au akiwa anatatizika na jambo lolote.
Hivyo basi inawezekana wewe kama mwanamke ndani ya ndoa umezoea mume akirudi kutoka kazini unamkaribisha home kwa kumpiga maswali na kuanza kumueleza kila aina ya matatizo na karaha ambazo zimetokea siku hiyo bila kumpa hata muda wa yeye kupumzika kidogo.

Sina maana kwamba mumeo akirudi nyumbani ule jiwe bila kumpokea au kumuuliza kazi ilikuwaje, nazungumzia suala la kutompa muda angalau dakika 15 kupumzika kabla hujaanza kutoa maswali yako na matatizo yako.

Pia naamini dunia ya sasa wote wanawake na wanaume tunafanya kazi iwe ofisini au shambani hata hivyo tukifika nyumbani kila mmoja hujitahidi kumweleza mwenzake nini kimeendelea au kupeana taarifa mbalimbali za familia ukweli ni kwamba bado mwanaume huhitaji dakika kama 15 kabla ya kujiunga na familia.

Kumbana maswali na kumwambia matatizo na shida tangu anaingia mlangoni si jambo zuri sana kwa mwanaume kwani hujisikia ainaishi na mama yake na si mke wake maana mama yake alizoea kumbana maswali tangu anaingia nyumbani kutoka shule.
Kama angekuwa anataka kuishi na mama yake basi asingekuoa wewe bali amekuoa wewe kwa sababu wewe ni tofauti na mama yake.

Baada ya kuchoshwa na kazi, na boss, au wateja au foleni za magari njiani anapowahi nyumbani anachohitaji akifika nyumbani ni busu na hugs kutoka kwa mke wake then aoge na kupumzika kidogo kama dakika 15 hivi ndipo atakuwa tayari kujibu maswali ya mkewe na kuendelea na story zingine pia.

Mpe muda wa kurelax akishafika nyumbani kwani kumbana maswali punde tu anaingia nyumbani kunaweza kusababisha yeye kuchelewa home kwani hujisikia ni usumbufu.
Akishakuwa tayari ameridhikana muda wake kuwa kwenye hilo cave unaweza kuona anaanza kuzunguza mwenyewe then anza kumpa hayo maswali yako.
Pia akigundua wewe ni msumbufu, hata siku ukiwa na point za maana anaweza kupuuzia maana umezoea kuchonga sana akiingia tu mlangoni hata kabla hajafika chumbani.
Ubarikiwe!

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Sawa kabisa. Lakini kwa nini wanawake wafanye hivi kwa waume zao na sio wanaume kwa wake zao? kwani kwa uzoefu wangu kuna wanawake ambao ni wana maswali sana na wengine ni kama maji ya mtungini. Na pia vile vile kuna wanaume wengine ni maji ya mtungini na wangine ni maswali tu. Kwani inawezekana pia mwanamke anahitaji hizo dakika kumi na tano. Maana kuna wanaume wengine hawawezi kupika, kufua kusafisha nyumba, kujua wapi ngua za watoto. Kwa hiyo hata hapo kuna kuwa na maswali pia kwa mwanamke kuhusu hivyo vyote. Je? ni haki mwanamume apatiwe dakika 15 na sio mwanamke? nilidhani ya kuwa binadamu wote ni sawa. kazi kweli kweli, hizo ni fikra zangu tu.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,

Asante sana kwa maoni yako, ukweli mwanamke anahitaji si dakika 15 tu bali anahitaji siku zote kusikilizwa na mume wake kwani mume wake ni mtu pekee ambaye anaweza kuelezea hisia zake na mwanamke akiongea yale yaliyo moyoni mwake hujisikia ahueni. Hapa tunazungumzia kuhusu mwanaume kupewa angalau muda kidogo akifika nyumbani kabla ya kujichanganya na familia. Ni asili ya mwanaume kujisikia kuwa pangoni kwa muda fulani kabla ya kuanza kusikiliza na kujichanganya na familia wakati wa kurudi kazini.
Tatizo linakuja unapomdaka mumeo mlangoni kwa maswali na kumpa lundo la yote yametokea siku nzima hata kabla hajaweka bag au kulegeza tai au kufika chumbani.

Asante sana

Yasinta Ngonyani said...

sawa, sasa je kama mwanamke anafanya kazi naye hahitaji hizo dakika 15. ni sawa tu yeye adakwe na maswali anapoingia mlangoni?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,

Mara nyingi wanawake mnapenda kuongea na sisi wanaume kuwasikiliza hasa kama una tatizo au jambo linakutatizo na tusipisikiliza mnajisikia kama vile hatuwajali au hatuwasikilizi au kuwapenda au tunawa ignore. Wanaume tukiwa na mawazo au tatizo au shida au msongo wa mawazo tunapenda sana kujitenga na kuwa wenyewe kwanza (kwenda pangoni) kabla ya kuanza kuongea na wakati mwingine unaweza kuona kweli mume wangu ana mawazo na ukimuuliza anasema sina tatizo niache tu.
Kama mwanamke unahitaji muda kama dakika 15 ukirudi home basi utapewa au ongea na mumeo kwamba unajua nikirudi kazini nahitaji personal time, ingawa wanawake wengi hujisikia vizuri mwanaume ukiwa umamsikiliza anapoongea akifika tu kazini na anavyoongea na mwanaume kumsikiliza hujisikia raha zaidi.

Kila ndoa ina namna yake hivyo kinachofaa kwa Mbilinyi kinaweza kisifae kwa Mshana.

Ubarikiwe

Yasinta Ngonyani said...

ok nimekuelewa. lakini hata hivyo ningefurahi kama wanaume wangekuwa wawazi kujaribu kuongea matatizo yao kwa wake zao. kwani kama una mke mwongeaji na mdadisi ni vizuri kutoa tatizo lako kwake anaweza kukusaidia kuliko kukaa nalo moyoni. hivi ni mimi ninavyofikiri.

Mama wa Kichagga said...

Kaka Mbilinyi,

Blog yako ni nzuri sana. Ntakuwa nakutembelea mara kwa mara kupata maarifa haya.

Ubarikiwe sana kwa kuwa baraka kwa wengine.

Lazarus Mbilinyi said...

Mama wa Kichaga,

Nashukuru sana kwa kunitembelea naamini maoni yako yatasaidia wote tujifunze na hatimaye kuwa na maisha yenye afya njema na wale tunaowapenda, ukweli kuwa wealth huanzia katika furaha na upendo katika ndoa na wale tunawapenda kwanza.

Karibu sana

Upendo daima

Anonymous said...

Je akiuomba mwenyewe huo muda wa kukaa pangoni? tena bila kusema ni lini huo muda utaisha kwamba kazi zinamsumbua.unamsaidiaje aweze kutoka haraka huko pangoni?

Lazarus Mbilinyi said...

Kama kazi zinamsumbua huko si kukaa pangoni bali ni ulevi wa kazi.

Jambo la msingi ni kujadiliana naye kwamba na wewe unahitaji muda naye as mke au mume na familia pia.

Kukaa pangoni ni pale tu anapokuwa anahitaji muda wa kujiliwaza mwenyewe kwanza kabla ya kuwa na muda na mke au familia baada ya kazi.

Ubarikiwe