"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, November 20, 2008

Mwanaume kushindwa kitandani

Haijalishi wewe maarufu namna gani linapokuja suala la kitandani huwezi kujua hadi uwe hapo Tunapozungumzia mwanaume kushindwa kitandani (impotency) tuna maana kwamba ni mwanaume kutokuwa na uwezo kusisimamisha uume ili kuweza kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi unaotakiwa, au kuwahi kukojoa (immature ejaculation) ua mwanaume kusimamisha uume kwa muda mrefu zaidi ya saa moja na kushindwa kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Kama mwanaume anaweza kumaliza tendo zima la ndoa kwa muda wa dakika 5 au chini ya dakika 10 na kuwa hana uwezo wa kuendelea tena basi hiyo ni dalili kwamba something is wrong.
Data zinaonesha asilimia 10 ya wanaume mahali popote wana tatizo hili, kwa mfano nchini Marekani inakisiwa kwamba wanaume milioni 30 wanakumbana na tatizo hili na ulimwenguni kuna wanaume zaidi ya milioni 150 wana tatizo hili na pia kila mwanaume anaweza kukutana na tatizo hili angalau mara moja katika maisha yake.

Nini husababisha?
Ili uume uweze kusimama lazima damu iende kwa wingi huko na kusababisha kuwa mgumu na kusismama na kuwa tayari kwa huduma.

Sababu kubwa ya mwanaume kushindwa kusimamisha uume wakati wa tendo la ndoa mara nyingi huwa ni mawazo (anxiety)
Pia Inawezekana ni dalili ya ugonjwa mwingine kama Diabetes.
Mwanaume anaweza kuwa na hofu kwamba hawezi vizuri sex na hii hupelekea kutojiamini na hatimaye uume kushindwa kabisa kusimama.
Pia Inawezekana ndoa ina matatizo na kupelekea kichwa kuwa na limzigo la mawazo na hatimaye kushindwa kabisa kusababisha utendaji wa kazi huko south pole.

Inawezakana mwanaume amefiwa na mtu wa karibu aliyekuwa anampenda.
Kuchoka
Pia stress
Kuwa na hatia ya kitu chochote.
Inawezekana mwanamke aliye naye havutiii kabisa
Kufilisika biashara au kufukuzwa kazi hupelekea kuwa na mawazo.
Kupungukiwa homoni zinazowezesha uume kusimama hasa umri ukienda sana.
Matatizo ya mirija ya damu kushindwa kusafirisha damu kwenda sehemu zote za mwili, hii uweza kusababishwa na magonjwa kama BP na arteriosclerosis.
Kuvuta sigara
Magonjwa ya nerves
Kufanyiwa upasuaji hasa ule wa prostate

Wanaume ambao huonekana labda ni maarufu sana katika fani zingine bado likija suala la kitandani ni kitu kingine hivyo mwanamke anatakiwa kujua kwamba lazima atoe ushirikiano wa kutosha kwani mwanaume anahitaji kutiwa moyo na mwanamke aliyenaye kwani Inawezekana ni mawazo kichwani mwake ndo hupelekea kushindwa.

Je, unaweza vipi kuepuka hili tatizo?
Hakuna kitu kinachoshushia mwanaume hadhi mbele ya mwanamke kama hili tatizo hivyo basi mwanaume akiona hili tatizo linajitokeza mara kwa mara kwanza ajiamini na kuangalia linaweza kuwa nini kimesababisha kama ni msongo wa mawazo inahitaji kwenda kwa washauri (counselling) na kama ni suala la kimatibabu awaone madaktari.

4 comments:

Anonymous said...

upo sahihi yakheeeeeeeee

Yasinta Ngonyani said...

Kwa nini aande kwa washauri na asiongee na mke wake na wakasaidiana kutatua tatizo. Ni wazo langu.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,

Upo sahihi kabisa na kwa kweli hilondo jambo la kwanza kwa wanandoa, kwa nini mpeleke siri zenu kwa mtu mwingine? fanya kila njia kuhakikisha mnapata jibu, ila ikisindikana waone wataalamu.

Asante sana

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,

Upo sahihi kabisa na kwa kweli hilondo jambo la kwanza kwa wanandoa, kwa nini mpeleke siri zenu kwa mtu mwingine? fanya kila njia kuhakikisha mnapata jibu, ila ikisindikana waone wataalamu.

Asante sana