"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, November 11, 2008

Ni U-Shape

Ndoa ni msingi wa jamii yoyote duniani.
Pia malezi ya watu katika jamii huanzia katika ndoa.
Hii ina maana ndoa bora tunpata taifa bora.

Linapokuja suala la ndoa mambo mengi hushangaza sana watu na wanandoa wenyewe.
Wengi hujikuta na mauzauza ya kushangaa yule alikuwa naye mbele ya kanisa na mbele za mungu kufungishana ndoa kuuthibitisha ulimwengu kwamba nimepaa liubav langu, na baada ya kukaa kwenye ndoa miezi, au mwaka au miaka anakuta ni mtu mwingine kabisa kwa tabia na kila kitu kama vile kabla ya ndoa alikuwa mwingine na baada ya ndoa ni mwingine.

Habari njema ni kwamba maisha ya ndoa yapo mfano wa U shape kwa maana kwamba wakati wanandoa wanakutana kabla ya kuoana upendo huwa juu sana na mahaba huwa katika kiwango cha juu, then yanakuja mauzauza na jinsi miaka inavyoenda basi huko mbele mahaba na upendo huanza kurudi na upanda juu tena kukamilisha umbo la U.
Hata kama ndoa yako inakukatisha tamaa namna gani bado tumaini lipo na kwa msaada wa Mungu unaweza kurudi na kukamilisha umbo.

1 comment:

Anonymous said...

Kaka upo sawa kila wakati kwani nafikiri kuwa habari hizi huwa ni baada ya uchunguzi. Tusisahau kuwa kuna kupanda na kushuka,Kufanya makosa na kutoku kufanya ndio maana tunatubu kila mara kwa hiyo hayo yote ni mapito tuu. Cha muhimu UVUMILIVU NA SALA.
MSAFIRI