"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, November 4, 2008

Si kila kitu kinakuhusu

Utaniambia leo ulipitia wapi na ulikuwa na nani! Kila mtu duniani ana siri zake binafsi na kuwa wakati hapendi mtu yeyote ajue ila ni yeye na Mungu wake.
Si siri tu bali hupenda kuwa mwenyewe na kujiamulia mambo yake mwenyewe kwa kadri anavyotaka.
Unapokubali kuoana na mwanaume au mwanamke maana yake unaruhusu kuanza maisha ya pamoja (sharing) katika hisia, emotions, kazi, kitanda, bafu, harufu, nguo nk.
Hata hivyo hii haina maana kwamba tunawajibika upande mwingine yaani mume au mke kujua kila kitu kwani kila mmoja huhitaji kuwa na siri au kufanya kitu mwenyewe.

Hapa ninazungumzia vitu ambavyo ni vizuri havina uhusiano na tabia mbaya kama ulevi au kukosa uaminifu.

Hata hivyo wapo wanaume zetu au wake zetu hutaka kujua kila kitu tunachofanya na kila mahali tulikuwa zaidi ya mama zetu walivyokuwa wanatuchunga wakati watoto.

Kama mwanaume umeenda kazini, mkeo anataka kujua kwanza wakati unaenda kazini uliongea na nani, umefanya nini, umekula nini na nani, ulipotoka kazini ulipitia wapi, na mlikuwa na nani na atachukua simu ya mkono na kuanza kuangalia nani alipiga, nani alipigiwa na nani alikutumia sms na nani alitumiwa, ni kuchunguzana na kuulizana zaidi ya FBI.
Maswali mengi utafikiri ndoa ni mahakamani.
Mume anaogopa hadi kurudi nyumbani maana anaona ni usumbufu.
Kwani ni lazima ujue kila kitu?
Ukweli kama wewe ni mwanamke si lazima ujue kila kitu kuhusu mume wako, alikuwa wapi, alikuwa na nani, amefanya nini na ilikuwaje nk, kuna vitu ni non of your business.

Inawezekana unajua kutoka kazini hadi nyumbani huwa anatumia dakika 20 lakini sasa ametumia dakika 50, ile anafika nyumbani tu unambana na maswali ajieleze alikuwa wapi, alikuwa na nani, na analikuwa anafanya nini na ilikuwaje, inawezekana alipitia kwa rafiki zake aliosoma nao pia si lazima ujue kila kitu yeye ni mtu mzima si mototo tena, yaani anajisikia kama vile wewe ni mama yake kitu ambacho kinakupunguzia alama na anahisi hujiamini na pia msumbufu na humuamini.
Kama anataka kuishi na mtu anayetaka kujua kila kitu kuhusu yeye, basi angebaki kwa mama yake na si kuoana na wewe.

Ukweli si lazima ujue kila kitu kuhusu yeye, mwamini, mpende, mfurahie hata kama amechelewa kwa muda kidogo zaidi na alivyo kwambia.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hii yote ni kukosa uaminifu tu. Kwani kama mtu umeoa/olewa kwa nini uwe na wasiwasi na mke/mume wako wakati unajua ni wako

Anonymous said...

Hii msg ila umependelea upande mmoja, tu yani mke asijue kila kitu kuhusu mumewe japo ulianza kwa wote. Its true but unfortunately mara nyingi inatokea kuhusu mambo ya uaminifu ktk mapenzi. na wenzi huanza kuchunguza baada ya kuona mkewe/mumewe kabadilika tabia.