"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, November 26, 2008

Tamaduni!

Kwetu bila mshenga mke hupati!
Asia:
Vijana hukaa na wazazi hadi anapofikia wakati wa kuoa na akisha oa au kuolewa huchagua mzazi mmoja na kuishi kwake kwa muda fulani ndipo huanza maisha.

Australia:
Mabinti huwaomba vijana wa kiume kwenda nao “outing” kwa ajili kuombwa uchumba na analipa gharama zote kama vile chakula na vinywaji.

Columbia:
Kama msichana unatoka naye kwenda kuongea kwa mara ya kwanza kawaida huambatana na rafiki yake mmoja wa kike unawajibika kuwalipia gharama zote.

Finland:
Vijana wa kiume na kike huenda kwa kundi moja kama 30 hivi lengo likiwa ni kutafuta wachumba (matching).

Latin America:
Kaka au dada yeyote atakaye muomba mwenzake kutoka naye kwa ajili ya mazungumzo ya faragha (uchumba) anawajibika kulipa gharama zote za vinywaji na chakula.

Japan:
Siku Valentine wanwake huwapa zawadi wanaume na baada ya mwezi kuna white day ambayo wanaume nao hutoa zawadi kwa wapenzi wao wa kike.

India Kaskazini:
Hakuna uchumba hadi wazazi wamkubali msichana ambaye unataka kumuoa kama wewe ni kijana wa kiume, wazazi wakikataa umeumia na kama wakikubali unaruhusiwa full speed kuoa.

Je, sehemu unayoishi wewe tamaduni za kuoana zipoje?
Au hakuna kanuni na taratibu rasmi?
Je, njia mnazotumia zinasaidia vipi kuhakikisha wachumba wanafahamiana na kujuana ili kuwa na maisha ya ndoa yenye mshikamano na si migongano?

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Kama nilivyoona mimi hapa Sweden wazazi hawana la kuingilia katika uchumba wa watoto wao. Ni kijana na binti wo ndio waamuzi. Kwani wanaamini hakuna haja ya kuwashirikisha wazazi wakati wao ndio wanaopendana na ndio watakaoishi pamoja.