"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, November 12, 2008

Usimfananishe

Eti mbona wenzako wakivaa lemba wanapendeza!
Kuna wakati huwa inashangaza sana ukisikia yale wanandoa wanafanya au wanataka yafanyike katika ndoa zao.

Kama ni mwanamke basi una marafiki wanawake wenzako ambao waume zao inawezekana wana pesa nyingi kuliko mumeo, wamesoma kuliko mumeo, wana mali kuliko mumeo, wana akili kuliko mumeo, wanakuwa na muda zaidi na familia zao kuliko mumeo, wakivaa wanapendeza kuliko mumeo na pia wanabembeleza wake zao kuliko mumeo, au wana tabia njema kuliko mumeo au kama wewe ni mwanaume nawe una marafiki wa kiume ambao wake zao wapo hivyo.

Je, ni mara ngapi umemlalamikia mumeo au mkeo kwa kumlinganisha na wanaume wengine au wanawake wengine?
Inawezekana umemlalamikia mumeo au mkeo kwamba
“Mwenzako Kelvin au Peggy amepunguza uzito wewe umebaki umenenepeana kama kitimoto kwa nini?
“Mwenzako George amenunua gari wewe nini kinakushida , wewe ni mwanaume gani?”
Mwenzako mama Noel kila siku ukienda kwake nyumba safi wewe inakuwaje chafu namna hii”
Kama ni wewe utajisikiaje?
Hapa msipotoana ngeu au kuzuka zogo basi kati yenu mmoja hana baadhi ya homoni fulani fulani mwilini ndo maana kabaki kimya.

Kitu cha msingi ni kujikubali kwamba huwezi kupata kila kitu au mwenzako kuwa kama walivyo wengine kama vile umeoana na “mr right or mrs right”

Dunia itakuwa na ndoa za ajabu sana kama wote tungeamua kila tunachokiona kwenye ndoa zingine lazima tuwe nacho.
"Furaha si kuwa na kila kitu unachohitaji bali ni kuhitaji kile ulichonacho".

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Ndio maana MUNGU alituumba tofauti. Fikiria kama wote tungekuwa sawa DUNIA ingekuwaje.Binafsi nafurahi kama nilivyo. kazi kwelikweli