"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, November 3, 2008

Walisema haoi, Ameoa!

Manuel Uribe jitu la nusu tani Mwanaume mzito kuliko wanaume wote duniani (guinness record) mwenye uzito wa Kg 560, nusu tani (88 stone) Manuel Uribe (43) amemuoa rafiki yake wa kike Caludia Solis (38) mbele ya mashahidi 400 huko mexico katika mji wa Monterrey tarehe 26 octoba 2008.

Bibi na Bwana wakifurahia jambo Manuel alikutana na binti mrembo Claudia tangu mwaka 2006 na tangu akutane na huyu mwanamke kwa pamoja wamesaidiana kuhakikisha manuel anapunguza uzito na amejitahidi kupunguza Kg 250 (39 stones) rekodi ambayo inaweza kumuweka tena kwenye kitabu cha guinness kwa kupunguza uzito mkubwa.

Picha chini Bibi harusi Claudia Solis siku ya harusi Manuel alibubujikwa na machozi pale msajili alipotamka kwamba wao sasa ni mume na mke.
Na hakusita kutamka maneno haya huku akibubujikwa na machozi
Nimefurahi sana leo ni siku yangu maalumu Mungu ameruhusu siku nzuri kama hii mimi na mrembo Claudia kuoana”.
Huyu bwana hajawahi kutoka kindani mwaka kwa miaka 6 mfululizo na harusi yake ilifanyika kitandani baada ya kubebwa kuelekea sehemu ya harusi na gari la kuvuta.
Pia harusi yao imekuwa documented na Discovery Channnel

Inawezekana umenenepa au kuwa mwambamba sana au hali yoyote ile na imepelekea usijiamiini kwamba huwezi kuoa au kuolewa, hayo ni mawazo potofu, bado kuna mtu anakupenda duniani ni wewe tu.
Ukweli unabaki kwamba kuna mwanamke yupo kwa mwanaume yoyote bila kujali ni mnene kiasi gain, mwembamba kiasi gani au kilema kiasi gain, au sura mbaya kiasi gain, upendo wa kweli ukiwa kazini hakuna lisilowezekana.

Picha chini maharusi wakibusiana siku ya harusi yao "It goes to show you it is not the size of the nail that counts, it is the size of the hammer".

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli penzi sio pesa,Penzi ni uamuzi wa mtu, penzi ni moyo wa mtu. Na pia watu wanasema afadhali kuolewa na mume/mke mbaya au mzuri na pia labda mnene au mwambamba nina maana muwe tofauti. kwani mkiwa sawa inakuwa furugu ndani ya nyumba.

Sababu ya kupenda kazi kwelikweli.
nawatakia maisha mema

Thinker said...

Namani jamani huu ni uchokozi ,hivi kuna mtu mbaya hapa duniani. Au kuna mtu anaye jisikia vizuri kuitwa mbaya.Binadamu wote tuliubwa vizuri barabara kabisa. Kama ni vivyo inawezekana wote ni wabaya. Huyu jamaa si mbaya bali ni mnene. Na wanawake wote ni wazuri ila wao wanahisi kuna wanawake wazuri zaidi kuliko wengine. Mtu anaweza kuwa mweupe,mweusi,hana meno yote ,kipofu, hacheki siku zote lakini mtu hawezi kuwa mbaya. Nafikiri huyu mwanamke anaweza kuwa na raha maisha mwake kuliko wanawake wanao jibidisha kutafuta wanaume wazuri kwa zura na umbo kama wapo.

Lazarus Mbilinyi said...

Thinker,

Hapo umenea, duniani hakuna mtu mbaya wote ni wazuri na ni kweli huyu dada Claudia kampata mume ambaye ni kweli ni mzuri naamini ndoa yao itakuwa na upendo wa kweli.
Asante sana