"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, November 6, 2008

Wana bacteria wengi kuliko.......

Mikono ya wanawake huvutia bacteria wengi kuliko wanaume! Utafiti unaonesha kwamba wanawake wana bacteria wengi kwenye mikono kuliko wanaume.
Na kila mwanaume au mwanamke ana aina tofauti ya bacteria kuliko mwingine tena bacteria wa aina tofauti.

Huu Utafiti umefanywa na Profesa Rob Knight wa chuo kikuu cha Colorado nchini Marekani katika Idara ya Biochemistry.
Hii ni baada ya kuchukua sample za mikono ya wanachuo 51 (mikono 102) na kutafuta kiwango cha bacteria waliomo kwa kutumia utaalamu wa juu sana wa kugundua aina ya bacteria kwa kutumia DNA.
Utafiti ulibaini aina 4,742 za bacteria (species) na kila mkono ulikuwa na zaidi ya bacteria 150 aina tofauti bacteria.
Pia wanawake wamegundulika kuwa wana bacteria wengi wanaoishi ndani ya ngozi yao hasa isiposafishwa ukilinganisha na wanaume.

Je, nini kinasababisha wanawake kuwa na bacteria wengi kuliko mwanaume?
Hii ni kutokana na tofauti ya kiwango cha acid kwenye mwili (pH), wanaume wana kiwango kikubwa cha Acid mwilini kuliko wanawake.
Pia tofauti ya kiwango na aina ya mafuta (oil) na jasho (sweat) linalozalishwa mwilini hasa kutokana na aina tofauti ya homoni mwilini (testosterone and oestrogen)
Pia matumizi mbali mbali ya vipodozi katika ngozi na miili yao.

Je, wanawake hawawaambukizi wanaume bacteria wanaposalimiana?
Watafiti wanasema haina noma kabisa kwani bacteria wengi hawana madhara hivyo unaweza kubusu hata mikono yao na miili yao kwa raha zako.
Tahadhari:
Ni jambo la msingi na muhimu kuosha mikono mara kwa mara unapoisi imeshafuka bila kujali wewe ni mwanamke au mwanaume kwa ajili ya afya zetu katika jamii zetu.
Source:University of Colorado at Boulder (2008, November 4). Women Have More Diverse Hand Bacteria Than Men. ScienceDaily. Retrieved November 5, 2008, from http://www.sciencedaily.com­ /releases/2008/11/081103192310.htm

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Ningependa kuwashuri wanawake wote kama wangepata nafasi wapite katika blog hii kwani kuna mafundisho ya kila aina. Ya kindoa ambayo kila mtu anahitaji kujua. Nimesema wanawake kwa vile nadhani idadi kubwa inaonekana ni wanaume/vijana tu.

Binafsi nilijua kuna bacteria lakini eti wanawake zaidi sikuwa na habari.Pia kwa wale waliofunga ndoa kama una pete basi unapooka mikate vua hizo/hiyo pete kwani sehemu kama hizo bacteria wanapenda sana. Asante kaka Mbilinyi.