"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, December 28, 2008

Merry Christmas and Happy New Year 2009

Nawatakia Christmas njema na Heri ya mwaka mpya 2009 wapendwa wote na wasomaji wote wa blog hii.
Naamini mtakuwa na sherehe mbalimbali za kifamilia na kijamii kitu cha msingi ni kukumbuka kwamba baada ya mwaka kuanza kuna ada za wanafunzi na kutimiza malengo mapya ya mwaka 2009.
Mungu awabariki
@@@@@@@@@@@@@@@@@

Saturday, December 20, 2008

Nitawakumbuka sana

Wafanyakazi wa Umoja wa mataifa (UNDP)
Kunduchi Beach Hotel & Resort- Mei 2007
Dar es Salaam Tanzania
Nimefanya kazi pamoja nanyi kwa miaka 7, tangu tarehe 13 Octoba 2001 hadi tarehe 15 Desemba 2008.
Nimejifunza mengi sana kutoka kwenu na mafanikio mengi nimeyapata ni kutokana na ushauri wenu kwangu.
Nawatakia maisha mema katika kuhakikisha dunia hii ni mahali bora kuishi kwa watu wote maskini na matajiri.
Nitawakumbuka sana!
I will remember!
Je me souviens!
Ndila suhwa!
Lazarus P. Mbilinyi
Ontario - Canada

Thursday, December 18, 2008

Mawasiliano

Fikiria una chungwa moja tu na una watu wawili wanalihitaji.

Je, ni njia ipi nzuri ya kufanikisha kila mmoja kupata hitaji lake la kupata chungwa?

Naamini wewe haraka haraka jibu lako litakuwa ni kuligawa nusu kwa nusu na kuwakabidhi kila mmoja aanze mbele!

Ukweli kabla hujafanya hivyo mi vizuri ukawauliza kwanza sababu za kila mmoja kuhitaji hilo chungwa kwani inawezekana mmoja anahitaji ganda lake kwa ajili ya kutengeneza keki na mwingine inawezekana anahitaji juisi ya chungwa ili anywe hivyo kugawa nusu kwa nusu ni kitendo ambacho wote hawataridhika, ingawa kwako ni njia sahihi.

Mawasiliano ni pande mbili anayeongea na anayesikiliza na muongeaje lazima wakati mwingine atambue msikilizaji anahitaji kusikia nini na si kumwongelesha tu.
Kwa njia hii unaweza kutatua migongano, migogoro, chuki, migomo nk

Wednesday, December 17, 2008

Waliooana tu!

James na Deborah (si majina halisi) ni mke na mume wote wana miaka 28 na Mungu amewajalia kuwa na watoto wawili, miaka 2 na miaka 4.
James ni mwalimu na Deborah ni Nesi.
Jumamosi moja baada ya watoto kwenda kulala kifuatacho kilitokea kwenye sofa sebuleni.

James: (Huku akimpapasa mkewa mapaja kwa mikono yake na pia akimtazama usoni) vipi honey unajisiskiaje? Je una mood leo?
Deborah: (huku akijisikia kushtushwa) mwenzio najikisia kuchoka.

James: (huku akiwana na hofu kwamba anaweza kukataliwa) Mbona kituko! ina maana jana hukupata usingizi wa kutosha?
Deborah: Sawa ila nadhani nitakuwa nimechoka sana kwa hili leo.

James: Siku hizi naona huna hamu sana na mimi kufanya mapenzi na wewe au kwa sababu jana nilipoteza erection mapema?
Deborah: (huku akijisikia hatia kwa kumkatalia mumewe ombi lake) Kwa nini iwe issue kama hilo lilitokea jana?

James: (huku akiwa amekasirika na kujiona si lolote mbele ya mke) Ok, naenda kulala tutaonana baadae.
Deborah: (anamfuata James chumba na anavua nguo zote) Ok, nipo tayari kama tunaweza kujaribu basi.

James anambusu Deborah haraka haraka naye anajibu, James anamvuta kwake anaanza kuchezea nywele zake kumpapasa mwili kidogo then anahisi uume wake umesimama, haraka bila kupoteza muda anamlaza Deborah kitandani na kumlalia juu yake na kuanza kumwingia, inashindikana kwani Deborah bado hajawa relaxed na lubricated.

James anajaribu kuingia tena kwa nguvu na anashindwa kwani Deborah ni mkavu kabisa na anajisikia maumivu na Deborah sasa anabana miguu kwa maumivu na kumwambia stop.

James anapoteza erection wakati huohuo Deborah anajisikia hana hamu tena.
James anajisikia aibu sana na kuwa frustrated kwa kuwa kila kitu kimeshindikana.

SWALI:
je, unaweza kuhisi tatizo kubwa la James na Deborah ni nini?
Je, ili kitanda chao kiwe na moto wa kweli ni mambo gani wanahitaji kufanya?

Tuesday, December 16, 2008

"We don't love qualities,
we love persons;
sometimes by reason of their defects as well as of their qualities."
By
Jacques Maritain

Monday, December 15, 2008

Sex huko International Space Station Ngumu

Wataalamu wa NASA wanakiri kwamba si rahisi kufanya mapenzi huko kwenye space.
Tatizo kubwa ni ila hali ya kutokuwa na force of gravity kwa maana kwamba wapenzi hawawezi kushikana na kufanikisha intercourse kwani kila mmoja huelea kivyake (zero gravity)


Kumekuwa na maswali kutoka kwa watu wengi wanaouliza kama wanaweza kutembelea International Space Station pamoja a wapenzi wao na kufana sex na kuwa watu wa kwanza kufanya mapenzi huko na hatimaye kujiweka kwenye kitabu cha kumbukumba cha Guinness.

Richard Branson anatumaini mwakani anaweza kupeleka watalii zaidi huko pia zaidi ya watu kuomba wawe wa kwanza kufanya mapenzi huko bado wapo waaoomba kwenda kufanya movie.
Wataalamu wanadhani kwamba ili watu waweze kufanya mapenzi kuna ulazima wa kutengeneza kifaa mfano wa shuttle (basi) ambalo ndani yake wataweka vifaa maalumu kuwawezesha wapenzi kufanikisha ufanyaji wa mapenzi (love handles)

Kufanya mapenzi bila nguvu ya uvutano (zero gravity) hakuna uzuri wowote kwani inaweza kusababisha kuchefuchefu kwa wahusika, pia watalamu wanasema sex itakuwa ni kitendo chenye joto, wet pia kuzungukwa na matone ya jasho (messed up).
Pia hatari kubwa ni kwamba watu wakiwa Space Station hujisikia kupata low blood pressure na ni wazi kuwa low blood pressure hupelekea damu kutozunguka sehemu zote za mwili na damu kutozunguka sehemu zote za mwili maana yake ile kitu haiwezi kusimama na hata kama ikisimama si kwa muda mrefu.

Mwanaume kutumia baiskeli ambayo si sahihi huweza kuathiri utendaji wake kimapenzi (sexual life)
Soma hapa chini.
Regular cyclists also run a higher risk of testicular damage and impaired testicular function. Mountain bikers run a particular risk, says Nargund, as studies have shown that they exhibit higher levels of scrotal abnormalities than on-road cyclists.

The male cyclist should know his bicycle well and a proper fit is particularly important for high-performance cycling
"The bicycle saddle is in direct contact with the perineum and its underlying structures.
It makes contact just behind the scrotum where the nerves and blood vessels enter the back of the scrotum and penis.
This area is sensitive, with hair follicles and sweat and sebaceous glands, which are all good breeding grounds for infection," he said."Abrasions, chafing, damaged hair follicles and bruising are among the most traumatic cycling injuries.
Sweating in this area can also cause soreness and skin problems," he added.
Nargund pointed out that more than 60 per cent of male cyclists who have taken part in research studies have reported genital numbness.
He said: "Numbness is common because the pressure of the saddle can impair the blood supply to this area and put pressure on the nerves in the penis.
This can also affect the man's ability to get an erection.
"There is a greater incidence of numbness and erectile problems in men who cycle regularly and over longer training distances.
That is why it is important to rest intermittently during prolonged and vigorous cycling."Choosing the right bike is essential, stresses Nargund.
"The male cyclist should know his bicycle well and a proper fit is particularly important for high-performance cycling" he said.
"The level of pedal resistance is also very important, because riding a bike using too much resistance is a major cause of health problems in the groin area.

Cyclists can also help to ease saddle-related injuries or skin irritations by adjusting the saddle height and fore and aft position.
Padding in the saddle and shorts are also important if cyclists want to avoid saddle-related problems," he added.

Saturday, December 13, 2008

Wanaume hawapendi Mwanamke Kulalamika

Ile unarudi tu home kutoka kazini kila siku jioni kiumbe huyu ndo anakutazama hivi?
Nahisi baada ya siku kadhaa utatamani urudi yeye tayari kalala! Binadamu ni kuimbe anayependa sana kulalamika iwe ofisini, kanisani, hotelini, kazini, sokoni, darasani, mikutanoni, msibani, harusini nk watu ni kulalamika tu.

Na kwa upande wa wanandoa mwanamke ndiye anajulikana sana kwa kuwa mtu wa kulalamika kasi kwamba wanaume wengi huwa wanachoka na kuanza kujiuliza hivi mwanamke anahitaji kitu gani maana kila unachompa bado hakiweze kumfanya asilalamike zaidi au tena.
Je, ni tabia ipi huchukizana wanaume?
Ukiwauliza wanaume wengi kwenye ndoa asilimia kubwa watasema hawapendi kabisa tabia ya mwanamke kulalamika kwa kila kitu na wakati wote.

Kwa nini wanaume hawapendi mwanamke mlalamishi/mnung’unikaji?
Wanaume tangu watoto wao wamefundishwa kuwa tough, kuwa wavumilivu, kuwa unemotional, kuwa wanaume na zaidi kwamba tabia ya kulalamika si ya wanaume.
Matokeo yake wamekuwa watu dhaifu sana linapokuja suala la mtu mlalamikaji na hushindwa kuvumilia kuona mtu analalamika mnuda wote.

Wanaume pia ni watu wa ku-fix matatizo au kutoa solution na si kutafuta solution.
Mwanamke anapolalamika kwa mara ya kwanza humvuta mwanaume kuja kutatua tatizo na akiendelea kulalamika mwanaume hujisikia ameshindwa ku-fix hilo tatizo na hujina failure mkubwa.
Kulalamika si njia njema ya kuuliza au kupata kitu kwa mwanaume bali ni njia bora ya kumfanya ajisikie vibaya.

Mwanamke mlalamishi ndani ya nyuma kwa mumewe muda wote hufanya mwanaume amuone ni takataka zaidi na kwamba hawezi kukufanya uwe happy na mwanamke usipokuwa happy maana yake mwanaume ameshindwa kazi ya msingi kabisa katika mahusiano.
Anajiona ni sawa na mwindaji anayerudi mikono mitupu nyumbani baada ya siku nzima ya kuwinda.

Wanawake wengi hutegemea sana mwanaume kuwa source ya furaha zao, huo ni mzigo mzito sana ambao mwanaume anaweza kuubeba.
Pia mwanamke unawajibika kabisa kujipa furaha mwenyewe kwanza, unapochukua jukumu la wewe mwenyewe kuwa mwanamke mwenye furaha na mumeo hujiona amefanikiwa sana hata kama hakufanya lolote kwa furaha uliyonayo na zaidi unapokuwa na furaha unaruhusu moyo mumeo kufunguka kirahisi kwako kuliko kuwa jimwanamke lenye uso usio na furaha kama vile ulilazimishwa kuolewa naye.

Pia kulalamika kunafanya mwanamke usiwe attractive, mwanamke unapolalamika kwa kila kitu na kila wakati mwanaume hukuona upo ugly na huvutii kabisa ndo maana wanaume wengi wanawatoroka wake zao kisa mwanamke ni mlalamisha na mwanaume anasema nimeshindwa kujua anataka kitu gani na pia nitawezaje kumfurahisha maana ni kulalamika tu kila siku.

Usiwe Chronic complainer maana kuwe na jua unalalamika, kusiwe na jua unalalamika.
kuwe na mvua unalalamika kusiwe na mvua unalalamika.
uwe na kazi unalalamika usiwe na kazi unalalamika.
Ukiwa mnene unalalamika ukiwa mwembamba unalalamika.
Uwe na mtoto unalalamika usipokuwa na mtoto unalalamika
Utaishi na nani?
Nani anataka jitu la aina hii?
Jirekebishe!

Congratulations

Dear friends,and Family hope that it is well with you all .
I thank God that he is good to me too.
I thank God for his love and mercy to reach this day.
I thank all my friends and family for the support you gave me during my good 3yrs of Studies here in Malaysia and today Iam receiving my scroll.
I have nothing to say than praying for you and keeping in touch with you all the time.
Thank you for being close to me and I will always remember each and every friend of mine .
regards
Lisa Emmanuel Tom

Friday, December 12, 2008

The difference between School and Life is:
In School you are taught a Lesson and then given a Test.
In Life you are given a Test that teaches you a Lesson.

Thursday, December 11, 2008

Mapenzi Nayo!

Mwanafunzi wa kidato cha tano wa Shule ya Sekondari ya Bishop Daning, Barakael Charles (18) amemuua mwenzake wa kike kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Mwanafunzi aliyeuawa, mwenye umri wa miaka 17, alikuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Bang'ata.Habari kutoka katika Kijiji cha Sing'isi kilichopo wilayani Arumeru, lilikotokea tukio hilo, zinasema msichana huyo alipigwa na kitu kizito kichwani.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Basilio Matei pia alithibitisha tukio hilo na kusema lilitokea juzi saa 8 mchana.
Vyanzo vya habari vilisema kuwa Charles alimpiga na kitu kizito marehemu na yeye kukimbilia kunywa sumu ili afe lakini yuko mahututi katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru chini ya ulinzi wa polisi.

Taarifa zilisema kuwa marehemu ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo ya sekondari Bang'ata na walikuwa wakigombana mara kwa mara kutokana na madai kuwa mwenza wake wa kike alikuwa siyo mwaminifu katika mapenzi na kutembea na wanaume wengine.

Habari ziliendelea kusema kuwa mtuhumiwa hakufurahishwa na vitendo vya marehemu alivyokuwa akivifanya na kumwonya mara kwa mara lakini marehemu alikuwa akikaidi ushauri wa mpenzi wake.

Kamanda Matei alisema kuwa mtuhumiwa bado yuko katika hospitali ya mkoa akipata matibabu na yuko chini ya ulinzi mkali wa polisi kwa kosa la kuua na hali yake inaendelea vizuri.
Matei alisema wanafunzi hao wa sekondari walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu.

Source: John Mhala, ArushaDaily News;
Tuesday,December 09, 2008

Wednesday, December 10, 2008

Furaha (Happiness) -2-

Kufurahia keki si lazima iwe siku ya harusi au sherehe, any time! Furaha (happiness) ni tofauti na furaha (joy) , kutokana na kiswahili kuwa na neno moja la furaha kwa maana ya happiness na joy inakuwa ngumu kupata msamiati sahihi.
Furaha (happiness) hutegemea sana mazingira au circumstance wakati furaha (joy) hutegemea sana
emotional well-being.

Mfano mtu ni mgonjwa sana unakuta yeye ndie mwenye furaha (joy) kuliko ninyi mnayeenda kumtazama.
Au mwisho wa mwezi baada ya watu kupokea mishahara huwana furaha (happiness) na pesa zikiisha wanarudi kwenye masikitiko
Joy ni furaha kutoka kwa Bwana haijalishi upoje na unapitia mambo gani au una hali gain, na happiness ni furaha inayotokana na vitu vya duniani au vinavyotuzunguka.
Kuwa mtu wa furaha ni tabia ambayo unaweza kujifunza.

Ili uwe na furaha katika maisha yako ni vizuri kuzingatia mambo yafuatayo:-
Ridhika na kujikubali jinsi ulivyo nakwamba Mungu alikuumba uwe hivyo.
Unaweza kuwa ni mfupi sana, mrefu sana, mnene sana, mwembamba sana, mweusi sana, mweupe sana, sauti mbaya sana, au mrembo sana, au una sura wengine wanakuona unatisha.

Jiamini jikubali na kwamba hakuna mtu mwingine duniani mzuri kama wewe ila ni wewe tu.

Tafuta furaha katika sehemu sahihi.
Je, kunywa pombe na kulewa ni sehemu ya kukupa furaha? Marafiki? kwenda kanisani? kuimba?

Timiza malengo yako ya maisha kuliko kusikiliza critics wanasemaje kuhusu wewe.

Weka mtazamo wako katika mambo mazuri na uwe positive katika attitude yako.

Uwe mtu wa kuridhika na kile unacho.

Uwe na tumaini kwa future yako.
Pia fanya vitu vinavyokufanya ujisikie mtu mwene furaha kwani hakuna mtu anaweza kuondoa furaha yao hadi wewe mwenyewe uamue.

Kuwa na furaha hakuwezi kuponya ugonjwa wowote bali huweza kuzuia usipate magonjwa mengi.
Eti Nigeria ndiyo nchi yenye watu wenye furaha (happiest) duniani!
Kutabasamu (smile) ndicho kipimo cha tamaduni zote duniani kuonesha kwamba mtu ana furaha.
Watoto waliotoka kuzaliwa huonesha smile kwa watu mwenye uso usio tabasamu, kama hujajua chunguza!
Wanawake hutabasamu zaidi ya wanaume.
Hata ukitabasamu kwa geresha, au kujifanya (fake) bado hupelekea kujisikia furaha.

Tuesday, December 9, 2008

Watu wenye furaha huishi zaidi

Wengine huwa watu wa furaha tangu watoto Utafiti uliofanywa na Duke University Medical Centre huko Durham North Carolina na Beverly Brummett unaonesha kwamba emotions huadhiri moyo na pia huathiri afya.

Hii ina maana kwamba watu wazima wenye furaha huweza kuishi miaka mingi zaidi kuliko watu wasio na furaha.
Utafiti umeonesha kwamba ugonjwa wa moyo wenye furaha wana asilimia 20 (20%) ya kuishi miaka 11 zaidi ya wale ambao hawana furaha.

Brummett alifuatilia watu 866 ambao wanaumwa ugonjwa wa moyo kwa miaka 11na kuwafanyia utafiti kwa kujua ni namna gani waliishi kwa furaha na akagundua kwamba wagonjwa wale walikuwa na furaha asilimia 20 ya kupona kuliko wale wanaokula ndita muda wote.

Pia imejulikana kwamba kuwa na furaha muda wote si muhimu sana kitu cha muhimu ni kuwa na furaha hasa pale unapopata jambo linalokufanya usiwe na furaha (emotional lows). Hii ina maana unahitaji kuwa na positive views kwa jambo lolote katika maisha yako.
Unapaokuwa huwa furaha au chini ya stress mwili huweza kuzalisha homoni aina ya cortisal ambazo husababisha seli za damu kushindwa kufanya kazi vizuri.

Nini hasa husababisha watu kukosa furaha?
Asilimia kubwa ya watu hawana furaha kwa sababu ya mapato, afya na masuala ya mahusiano.
Je ni kundi gani la watu ambalo linaongoza kwa kuwa na furaha?
Vijana ndilo kundi pekee ambalo ni la watu wenye furaha (happiest) kuliko wote.
Guess why?
Hawana majukumu, no responsibility mom na dad wapo kwa ajili yao kuwapa wanachohitaji.
Kundi gani linaongoza kwa kutokuwa na furaha?
Watu wa makamo (miaka 30 - 55) ndilo kundi la watu ambalo linaongoza kwa kutokuwa na furaha
Kwa nini hawana furaha?
Wengi hawaridhiki na maisha waliyonayo,
Kuogopa kuachishwa kazi
Majukumu ya familia
kushindwa kufikia malengo na mafanikio
Migogoro ya ndoa

Pia tafiti nyingi zinaonesha kwamba bila kujali tamaduni zilizopo duniani bado watu wengi hufa baada ya siku za sikukuu au sherehe zao na si kabla.
Guess why?
Wengi huwa na positive view kwamba wanakuwepo siku za hizo sikukuu na sherehe

Kuvuta sigara huweza kupunguza umri wa kuishi kwa miaka 3, lakini kuishi bila kuwa na furaha huweza kupunguza miaka 9.

The happier a person is, the longer he/she lives.

Monday, December 8, 2008

Inashangaza

Unashangaa nini? Wanaume hutoa Jasho zaidi ya wanawake, hii inatokana na sababu kwamba wanawake huweza ku-regulate kiwango cha maji wanayopoteza mwilini.

Mtu wa kawaida ana wastani wa kilo 3 za ngozi yake.

Watoto wadogo hutumia muda mwingi kuota ndoto kuliko watu wazima.

Kwa siku mtu mzima huweza kupitisha lita 10,000 za hewa kwenye mapafu.

Tendo la ndoa huweza kuunguza burn) kati ya 35 – 60 ya calories kwa mwanamke mwenye uzito wa kilo 65 kwa saa.

Kubusu huweza kusaidia kupunguza meno kuoza kwani baada ya kubusiana kinywa hubaki safi kutokana na mate ya ziada.

Wakati mwanamke anafika kileleni huweza kuzalisha homoni aina ya endorphins ambazo ni pain killers hivyo kama unaumwa kichwa isiwe sababu ya kukataa tendo la ndoa bali iwe sababu ya kutaka tendo la ndoa ili umalize maumivu ya kichwa.

Kufanya mapenzi huku mwanamke amesisimama (vertical position) hakuwezi kuzuia mimba hata siku moja.
Uwezekano wa kupata mimba upo mbalimbali maana mbegu zitapanda tu na kufikia lilipo yai na kufanya fertilization.

Kisimi au kinembe (clitoris) ni organ pekee kwenye mwili wa mwanamke ambayo ni kwa ajili ya kumpa raha ya mapenzi hasa baada ya kusisimuliwa vizuri.

Cervix hufanya kazi mbili kwa wakati moja (multitasking) kuhakikisha inapitisha mbegu tu na si kitu kingine kwenda kwenye uterus.

Hapo zamani za kale ilijulikana kwamba mwanamke aliye bikira lazima awe na Hymen, lakini sasa imegundulikwa kwamba kutokuwa na Hymen haina maana kwamba siyo bikira kwani unaweza kuondoa Hymen Kutokana na mazoezi kama vile mwanamke kuendesha baiskeli nk.
Kuwa bikira maana yake ni kutowahi kufanya mapenzi kabisa.

Uke kuwa na harufu (scent) ni jambo la kawaida na hii huonesha kwamba uke upo katika afya njema, ingawa kukiwa na harufu mbaya (kunuka) ni vizuri kujichunguza inaweza kuwa kuna maambukizi au hakuna usalama hivyo mwone daktari.

Mwanamke akiona titi moja kubwa kuliko lingine haina haja ku-panic kwani kila mwanamke huwa na matiti ambayo wakati mwingine huweza kutofautiana shape, size na rangi ya chuchu hivyo basi tofauti yoyote si lolote, relax.

Sunday, December 7, 2008

Jumapili Njema

True love never lives happily ever after - true love has no ending.

You're the laughter in my life.

Saturday, December 6, 2008

Talaka Huharibu Mazingira

Kiwango kikubwa cha talaka huweza kuathiri mazingira, utafiti mpya umeonesha.

Taarifa za talaka kutoka nchi 12 za Marekani, Belarus, Brazil, Cambodia, Costa Rica Ecuador, Greece, Kenya, Mexico, Romania, Afrika Kusini na Spain zinaonesha kuwa nyumba ambazo zimekumbwa na talaka sasa zinatumia kiwango kikubwa cha Nishati Pesa na Maji.

Ingawa viwango vya maisha katika nchi hizo ni tofauti, ukweli unabaki kwamba kuwa na kiwango kikubwa cha talaka huweza kusababisha kaya zilizojigawa kutumia nishati nyingi na maji mengi zaidi kuliko zilipokuwa pamoja.

Wana ndoa walioachana huwa na kaya zenye idadi ndogo wa watu lakini hutumia pesa nyingi, maji mengi na nishati nyingi zaidi kuliko zile ambazo hawajatalikiana.

Huu utafiti umefanywa na Eunice Yu na mwenzake Ianguo Liu wanafunzi (PhD) katika Chuo Kikuu cha Michigan.

Kila wiki

Kupenda ni kujiajiri katika kazi ya kumpenda yule umeamua kuwa naye maisha yako yote.
Haijalishi ana udhaifu kiasi gani kwani wewe ndiye mtu pekee unayeweza kustahimili dhaifu wake hapa duniani.

Hivyo kila siku kila wiki,kila mwezi n kila mwaka unawajibika kumpenda na zaidi kumpa upendo wa kweli na ladha tofauti za upendo ili ajikisie yeye ni mtu maalumu duniani.
Kila wiki unaweza kufanya yafuatayo ili wewe na mwenzi wako mzidi kuwa kitu kimoja na kuwa na ndoa yenye afya.

Ficha love notes sehemu kwa ajili ya mwenzi wako angalau mara moja kwa wiki.
Unaweza kuficha message zako kwenye kitabu, gazeti au jarida au Biblia hasa tafuta kile anapenda kusoma mara kwa mara.
Unaweza ku-attach kwenye simu yake ya mkononi.
Pia unaweza kuweka kwenye kioo chake cha kujiangalia na akija kujitazama akute love note yako pale.
Unaweza kuweka kwenye mifuko ya suruali au shati au pochi yake au wallet.
Weka mahali popote unajua anaweza kuona.

Fanya vitu pamoja unaweza kuchagua siku kama Jumamosi wakati mpo wote pamoja, kama vile kwenda kutembea (walk), kuangalia movie pamoja, kupika pamoja au kusafisha nyumba yenu pamoja.
Hili ni ninyi wawili tu halihitaji watoto kuwepo.

Pia ni vizuri kuhakikisha kila wiki unampa mwenzi wako muda wake wa kuwa mwenyewe bila kumsemesha au kumuingilia, kwani yeye ni binadamuna kuna wakati binadamu huhitaji usiri wa kuwa mwenyewe.

Thursday, December 4, 2008

Kila siku

Kumpenda mtu ni uamuzi na ni kazi inayoendelea kila siku hivyo basi kila siku kuna mambo ambayo unapaswa kufanya.
Yafuatayo ni muhimu sana kufanywa kila siku ili kuhakikisha upendo katika ndoa yako unakuwa katika kiwango kinachofanya ujisikia kweli nina mwenzangu anayenijali na kunipenda.
1. Tumia dakika angalau 10 kuwa pamoja (quality time) bila kuingiliwa na watoto, TV, Simu nk, huu ni muda tofauti na mkiwa mmelala au mnakula chakula pamoja.
2. Mbusu kila unapoodnoka nyumbani asubuhi, unaporudi nyumbani na unapoenda kulala na wakati wowote mchana ukipenda.
3. Mwambie "Nakupenda"
4. Mkumbatie mara kadhaa kwa siku (zisipungue 6)
5. Cheka pamoja
6. Usimlaumu mwenzako bila sababu za msingi
7. Fanya jambo lolote linaloonesha unampenda na kumjali
8. Mpe maneno yanayomtia moyo na pia mpe sifa pale amefanya vizuri
9. Uwe mwema kwake.

Wednesday, December 3, 2008

You're Just my Cup of Tea
Our Love Warms My Heart

Hawajakwambia!

Hivi ndiyo huyu alikuwa ananipigia simu kunilaza na kuniamsha kila siku wakati wa uchumba! UTAMSHANGAA SANA:
Mnapooana, hasa baada ya kumpata yule unadhani ni mwenzi halisi na anayekufaa unaamini kwamba utakuwa naye kwa furaha hadi kifo kitakapo watenganisha na utakuwa mtu wa furaha milele.
Ila siku moja utaamka asubuhi na kugundua kwamba hata kama ni mtu maarufu sana duniani bado hawezi kukufanya wewe kuwa mtu wa furaha siku zote na zipo siku utakuwa uajiuliza hivi kwa nini ulikuwa na haraka kumkubali na kuoana naye.

Sasa matarajio yanapotea, unajisikia upweke, na unaaanza kujifunza kwamba ndoa si kituo kufikia baada ya maisha ya kujitafutia mtu wa kuishi naye duniani bali safari uliyojaa raha na karaha kuelekea kujuana na kujenga familia bora na imara.

UTAFANYA KAZI KUBWA ZAIDI YA ULIVYOTEGEMEA.
Mapema watu wanapokwambia ndoa ni kazi unadhani labda itakuwa ni kuvumilia kwa kuwa mwenzako anasahau kufanya wajibu wake katika kazi za kila siku ndani ya nyumba.
Na unaamini kwamba hata kama anatabia fulani fulani mbaya basi utamvumilia kwa kuwa unampenda.
Kuoana ni kudhihirisa umemaliza degree ya kwanza sasa unaingia Graduate studies (Masters au Phd) na unahitaji kazi kuliko unavyotegemea.
Ndiyo maana sasa unapambana na matatizo hayo unapitia kwani inawezekana hukudhani kwaba siku moja utajikuta katika njia panda ambayo unahisi inakuchanganya zaidi.
Hata hivyo bado nafasi unayo na ndoa yako ina uhai mkubwa

KUNA WAKATI UTAENDA KULALA OVYO KABISA
Wengi huwashauri wanandoa wapywa kwamba “usiende kulala huku umekasirika” kama vile hawajui nini hutokea kwenye vyumba vya kulala vya wanandoa.
Na wengine hujihurumia sana kwa kuwawapo single eti usingizi ni wa mang'amung'amu wakioa na kuolewa ndipo watalala vizuri vifuani mwa wapenzi wao.
Thubutu! vyumba vingine vya kulala ni kisima cha machozi na kelele za migogoro hadi usiku wa manane hata usingizi hakuna.
Kitu cha msingi ukikasirishwa just come down and be loving endelea na maisha hakuna mtu anaweza kukufanya uwe na furaha isipokwa wewe kwanza..

KUNA WAKATI UTAISHI BILA TENDO LA NDOA
Si kwamba siku zote wanandoa huwa na mood kwa ajili ya sex, anaweza kuwa mmoja au wote. Kukosa mood au sex drive ni sehemu ya maisha ya ndoa na hii haina maana kwamba hutataka sex tena bali ni kipindi kutokana na maisha yanavyoenda.
Kitu cha msingi ni kwamba hata kama hamfanyi basi kunatakiwa kuwepo na romantic life kama vile touching, kissing, hugging.
Hivyo ingia kwenye ndoa ukijua sex si chakula bali hitaji la mwili kwa ajili ya kuridhishana wawili wanaoishi pamoja.

NDOA IMARA HAINA MAANA HAKUNA MIGOGORO
Kubishana au kupingana au kupishana kimawazo au jambo lolote ni sehemu ya maisha ya ndoa.
Pia ni njia nzuri ya kujuana na kuwekana sawa tena hili inabidi lifanywe kwa upendo pia kuvumiliana na kuyamaliza ndani ya dakika 15.

Tuesday, December 2, 2008

Positive Thinking!

The difference between can and cannot are only three letters. Three letters that determine your life's direction.
Being positive or negative are habits of thoughts that have a very strong influence on life.
Positive and negative are directions. Which direction do you choose?
Positive thinking is expecting, talking and visualizing with certainty what you want to achieve, as an accomplished fact.
Riches, mediocrity and poverty begin in the mind. A positive attitude brings strength, energy and initiative.
To think negatively is like taking a weakening drug.
Positive thoughts are not enough. There have to be positive feelings and positive actions.
When you say, "I can't" and expect the worst, you become weak and unhappy.
When you say "I can", and expect success, you fill yourself with confidence and happiness.

Kipima joto cha ndoa

Kati ya mambo muhimu ambayo binadamu yeyote huota siku moja akutane nayo ni siku ya harusi kama kaka Gilbert Mongi na dada Bertha Mlay wakati ya sherehe ya harusi yao Istana jijini Dar es Salaam tarehe 26/07/2008
(Picha kwa hisani ya fomafoma blog)
Kuna mahali wanandoa waliulizwa swali hili:
Je, mke uliyenaye au mume uliyenaye sasa kama ingetokea sasa hivi iwe ni ule wakati unachumbiana naye kuwa mke au mume ungemchagua kuoana naye?

Zaidi ya asilimia 70 walisema wasingekuwa tayari kuoana nao kwani wamegundua kuna tofauti kubwa sana ya mtu aliyenaye sasa na yule alikuwa kabla ya kuoana.

Je, wewe ungeliulizwa swali hili leo ungekuwa na jibu gani?
Ukweli jibu unalo wewe ndani ya moyo wako na ni siri yako.

Ukitaka kujua ndoa yako ina joto kiasi gani unaweza kujibu maswali yafuatayo kwa usahihi na uaminifu kabisa kwa kuchagua jibu sahihi kwako.

1. Tunaweza kumaliza mgogoro au tofauti ya mgongano wa kimawazo chini ya dakika 15.
A. Hata siku moja.
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

2. Huwa tuna tabia ya kumaliza matatizo yetu kabla ya kulala
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

3. Huwa nawaza kuhusu talaka
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

4. Namkumbatia na kumpa busu mpenzi wangu kwa mahaba
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

5. Mapenzi katika ndoa yetu yanaridhisha sana
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote
Hadi hapo naamini umepata picha kamili ya wapi unaelekea na mpenzi wako.
Je, yafuatayo nayo ni wimbo wa kila siku katika ndoa yako?
Kama ni kweli basi unahitaji msaada haraka iwezekanavyo.
Mawasiliano ovyo
Hakuna tendo la ndoa na kama lipo basi ni bora wajibu hakuna ladha halisi
Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa
Hakuna mahaba
Hakuna kutiana moyo wala kupeana asante
Migogoro isiyoisha
Kuumizana kihisia
Kukosa uaminifu kati ya mwanandoa
Migogoro ya matumizi ya fedha
Tabia ya kukefyakefya