"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, December 10, 2008

Furaha (Happiness) -2-

Kufurahia keki si lazima iwe siku ya harusi au sherehe, any time! Furaha (happiness) ni tofauti na furaha (joy) , kutokana na kiswahili kuwa na neno moja la furaha kwa maana ya happiness na joy inakuwa ngumu kupata msamiati sahihi.
Furaha (happiness) hutegemea sana mazingira au circumstance wakati furaha (joy) hutegemea sana
emotional well-being.

Mfano mtu ni mgonjwa sana unakuta yeye ndie mwenye furaha (joy) kuliko ninyi mnayeenda kumtazama.
Au mwisho wa mwezi baada ya watu kupokea mishahara huwana furaha (happiness) na pesa zikiisha wanarudi kwenye masikitiko
Joy ni furaha kutoka kwa Bwana haijalishi upoje na unapitia mambo gani au una hali gain, na happiness ni furaha inayotokana na vitu vya duniani au vinavyotuzunguka.
Kuwa mtu wa furaha ni tabia ambayo unaweza kujifunza.

Ili uwe na furaha katika maisha yako ni vizuri kuzingatia mambo yafuatayo:-
Ridhika na kujikubali jinsi ulivyo nakwamba Mungu alikuumba uwe hivyo.
Unaweza kuwa ni mfupi sana, mrefu sana, mnene sana, mwembamba sana, mweusi sana, mweupe sana, sauti mbaya sana, au mrembo sana, au una sura wengine wanakuona unatisha.

Jiamini jikubali na kwamba hakuna mtu mwingine duniani mzuri kama wewe ila ni wewe tu.

Tafuta furaha katika sehemu sahihi.
Je, kunywa pombe na kulewa ni sehemu ya kukupa furaha? Marafiki? kwenda kanisani? kuimba?

Timiza malengo yako ya maisha kuliko kusikiliza critics wanasemaje kuhusu wewe.

Weka mtazamo wako katika mambo mazuri na uwe positive katika attitude yako.

Uwe mtu wa kuridhika na kile unacho.

Uwe na tumaini kwa future yako.
Pia fanya vitu vinavyokufanya ujisikie mtu mwene furaha kwani hakuna mtu anaweza kuondoa furaha yao hadi wewe mwenyewe uamue.

Kuwa na furaha hakuwezi kuponya ugonjwa wowote bali huweza kuzuia usipate magonjwa mengi.
Eti Nigeria ndiyo nchi yenye watu wenye furaha (happiest) duniani!
Kutabasamu (smile) ndicho kipimo cha tamaduni zote duniani kuonesha kwamba mtu ana furaha.
Watoto waliotoka kuzaliwa huonesha smile kwa watu mwenye uso usio tabasamu, kama hujajua chunguza!
Wanawake hutabasamu zaidi ya wanaume.
Hata ukitabasamu kwa geresha, au kujifanya (fake) bado hupelekea kujisikia furaha.

1 comment:

Anonymous said...

Kaka hongereni sana.
This is the best picture I have ever seen in your blog.
Hata ungenikuwa ya harusi nisingeifurahia kama hii.
Unajua nini?
I am proud of you kwani watu wengi hata kama wana furaha wanaogopa kusema kuonekana kana kwamba wao wanajisikia furaha.
But that is obviously wrong nionavyo mimi, kwani the more unavyoonesha una furaha the more unafurahi zaidi na kukaa nayo.
Ndivyo nafikiria mimi, and of course you will live positively siku zote.

Mungu awalinde na kuwaongezea furaha kila siku

Tuombeeni nawengine tuwe na furaha.
Mbarikiwe sana.

Your sister HO