"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, December 3, 2008

Hawajakwambia!

Hivi ndiyo huyu alikuwa ananipigia simu kunilaza na kuniamsha kila siku wakati wa uchumba! UTAMSHANGAA SANA:
Mnapooana, hasa baada ya kumpata yule unadhani ni mwenzi halisi na anayekufaa unaamini kwamba utakuwa naye kwa furaha hadi kifo kitakapo watenganisha na utakuwa mtu wa furaha milele.
Ila siku moja utaamka asubuhi na kugundua kwamba hata kama ni mtu maarufu sana duniani bado hawezi kukufanya wewe kuwa mtu wa furaha siku zote na zipo siku utakuwa uajiuliza hivi kwa nini ulikuwa na haraka kumkubali na kuoana naye.

Sasa matarajio yanapotea, unajisikia upweke, na unaaanza kujifunza kwamba ndoa si kituo kufikia baada ya maisha ya kujitafutia mtu wa kuishi naye duniani bali safari uliyojaa raha na karaha kuelekea kujuana na kujenga familia bora na imara.

UTAFANYA KAZI KUBWA ZAIDI YA ULIVYOTEGEMEA.
Mapema watu wanapokwambia ndoa ni kazi unadhani labda itakuwa ni kuvumilia kwa kuwa mwenzako anasahau kufanya wajibu wake katika kazi za kila siku ndani ya nyumba.
Na unaamini kwamba hata kama anatabia fulani fulani mbaya basi utamvumilia kwa kuwa unampenda.
Kuoana ni kudhihirisa umemaliza degree ya kwanza sasa unaingia Graduate studies (Masters au Phd) na unahitaji kazi kuliko unavyotegemea.
Ndiyo maana sasa unapambana na matatizo hayo unapitia kwani inawezekana hukudhani kwaba siku moja utajikuta katika njia panda ambayo unahisi inakuchanganya zaidi.
Hata hivyo bado nafasi unayo na ndoa yako ina uhai mkubwa

KUNA WAKATI UTAENDA KULALA OVYO KABISA
Wengi huwashauri wanandoa wapywa kwamba “usiende kulala huku umekasirika” kama vile hawajui nini hutokea kwenye vyumba vya kulala vya wanandoa.
Na wengine hujihurumia sana kwa kuwawapo single eti usingizi ni wa mang'amung'amu wakioa na kuolewa ndipo watalala vizuri vifuani mwa wapenzi wao.
Thubutu! vyumba vingine vya kulala ni kisima cha machozi na kelele za migogoro hadi usiku wa manane hata usingizi hakuna.
Kitu cha msingi ukikasirishwa just come down and be loving endelea na maisha hakuna mtu anaweza kukufanya uwe na furaha isipokwa wewe kwanza..

KUNA WAKATI UTAISHI BILA TENDO LA NDOA
Si kwamba siku zote wanandoa huwa na mood kwa ajili ya sex, anaweza kuwa mmoja au wote. Kukosa mood au sex drive ni sehemu ya maisha ya ndoa na hii haina maana kwamba hutataka sex tena bali ni kipindi kutokana na maisha yanavyoenda.
Kitu cha msingi ni kwamba hata kama hamfanyi basi kunatakiwa kuwepo na romantic life kama vile touching, kissing, hugging.
Hivyo ingia kwenye ndoa ukijua sex si chakula bali hitaji la mwili kwa ajili ya kuridhishana wawili wanaoishi pamoja.

NDOA IMARA HAINA MAANA HAKUNA MIGOGORO
Kubishana au kupingana au kupishana kimawazo au jambo lolote ni sehemu ya maisha ya ndoa.
Pia ni njia nzuri ya kujuana na kuwekana sawa tena hili inabidi lifanywe kwa upendo pia kuvumiliana na kuyamaliza ndani ya dakika 15.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kama mtu unakuwa katika kumpenda mtu unakuwa kipofu kabisa huoni yale mabaya unaona mazuri tu. Sasa inakuja mnapoishi pamoja mabaya yote yanatokea hapo ndo inapokuwa kazi kweli kweli.

Na hili jambo la kulazana na kuamsha wakati wa uchumba na simu. Mmh hapo kaka Mbilinyi ni kazi kweli maana inaonyesha jinsi wanavyotamaniana.

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli dada Yasinta,

Kwa wale ambao bado hawajaoa au kuolewa ni vizuri wakatumia muda wao tena kwa uangalifu kuchambua vizuri kuhakikisha unamkubali mtu ambaye ni yeye tu ataweza kubeba udhaifu wake.

Upendo daima