"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, December 4, 2008

Kila siku

Kumpenda mtu ni uamuzi na ni kazi inayoendelea kila siku hivyo basi kila siku kuna mambo ambayo unapaswa kufanya.
Yafuatayo ni muhimu sana kufanywa kila siku ili kuhakikisha upendo katika ndoa yako unakuwa katika kiwango kinachofanya ujisikia kweli nina mwenzangu anayenijali na kunipenda.
1. Tumia dakika angalau 10 kuwa pamoja (quality time) bila kuingiliwa na watoto, TV, Simu nk, huu ni muda tofauti na mkiwa mmelala au mnakula chakula pamoja.
2. Mbusu kila unapoodnoka nyumbani asubuhi, unaporudi nyumbani na unapoenda kulala na wakati wowote mchana ukipenda.
3. Mwambie "Nakupenda"
4. Mkumbatie mara kadhaa kwa siku (zisipungue 6)
5. Cheka pamoja
6. Usimlaumu mwenzako bila sababu za msingi
7. Fanya jambo lolote linaloonesha unampenda na kumjali
8. Mpe maneno yanayomtia moyo na pia mpe sifa pale amefanya vizuri
9. Uwe mwema kwake.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Watu/wapendanao wote wangewaza kama wewe kaka Mbilinyi nadhani ndoa/wapenzi wengi wangeona raha ya maisha.

Ni kweli kumpenda mtu ni uamuzi, ni msukomo ambao tumepewa, mapenzi ni pumzi ya maisha juu ya moyo na yanaleta madaha/uzuri ndani ya roho.

Pia haya mambo tisa uliyoyatoa inategemea na huyo mpenzi wako. Kwani inawezekana yeye hapendi kwa hiyo itakuwa wewe mwingine unapoteza muda tu. Kwani inabidi wote muwe mnafanya hivyo sio mmoja tu.

Ni fikra zangu tu.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,

Asante sana kwa maoni yako ni kweli kuna wengine hata mwenzie ujitahidi inakuwa kama kumpigia mbuzi gitaa, hata hivyo mapenzi ni kujifunza hata kama hujawahi tamka neno 'mpenzi leo nakupenda sana"inabidi siku jitoe mhanga kutamka then ukirudia a kurudia inakuwa tabia yako kumwambie umpendaye maneno mazuri na matamu na hatimaye kila mmoja kujisikia raha, Nani hapendi kupendwa?

Upendo daima!

Thinker said...

Marriage has never been parfect.