"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, December 2, 2008

Kipima joto cha ndoa

Kati ya mambo muhimu ambayo binadamu yeyote huota siku moja akutane nayo ni siku ya harusi kama kaka Gilbert Mongi na dada Bertha Mlay wakati ya sherehe ya harusi yao Istana jijini Dar es Salaam tarehe 26/07/2008
(Picha kwa hisani ya fomafoma blog)
Kuna mahali wanandoa waliulizwa swali hili:
Je, mke uliyenaye au mume uliyenaye sasa kama ingetokea sasa hivi iwe ni ule wakati unachumbiana naye kuwa mke au mume ungemchagua kuoana naye?

Zaidi ya asilimia 70 walisema wasingekuwa tayari kuoana nao kwani wamegundua kuna tofauti kubwa sana ya mtu aliyenaye sasa na yule alikuwa kabla ya kuoana.

Je, wewe ungeliulizwa swali hili leo ungekuwa na jibu gani?
Ukweli jibu unalo wewe ndani ya moyo wako na ni siri yako.

Ukitaka kujua ndoa yako ina joto kiasi gani unaweza kujibu maswali yafuatayo kwa usahihi na uaminifu kabisa kwa kuchagua jibu sahihi kwako.

1. Tunaweza kumaliza mgogoro au tofauti ya mgongano wa kimawazo chini ya dakika 15.
A. Hata siku moja.
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

2. Huwa tuna tabia ya kumaliza matatizo yetu kabla ya kulala
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

3. Huwa nawaza kuhusu talaka
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

4. Namkumbatia na kumpa busu mpenzi wangu kwa mahaba
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

5. Mapenzi katika ndoa yetu yanaridhisha sana
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote
Hadi hapo naamini umepata picha kamili ya wapi unaelekea na mpenzi wako.
Je, yafuatayo nayo ni wimbo wa kila siku katika ndoa yako?
Kama ni kweli basi unahitaji msaada haraka iwezekanavyo.
Mawasiliano ovyo
Hakuna tendo la ndoa na kama lipo basi ni bora wajibu hakuna ladha halisi
Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa
Hakuna mahaba
Hakuna kutiana moyo wala kupeana asante
Migogoro isiyoisha
Kuumizana kihisia
Kukosa uaminifu kati ya mwanandoa
Migogoro ya matumizi ya fedha
Tabia ya kukefyakefya

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nashukuru kwa mtihani mzuri nimepima na nimeona nipo wapi. Watu wengi wanafikiri maisha ya ndoa ni lelemama, kazi kweli kweli.
kazi nzuri endelea hivyo hivyo kwani kuna wengi wanahitaji kujifunza mambo kama hayo.

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli ndoa ni kazi na kazi kubwa ni kumpenda mwenzako ambaye umeamua kuishi naye hadi kifo kitakapowatenganisha.
jambo la msingi ni kuwa makini kabla hujatoa hicho kiapo mbele ya mwenzako na mbele ya Mungu kwamba utaishi naye katika hali zote.
Upendo daima