"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, December 11, 2008

Mapenzi Nayo!

Mwanafunzi wa kidato cha tano wa Shule ya Sekondari ya Bishop Daning, Barakael Charles (18) amemuua mwenzake wa kike kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Mwanafunzi aliyeuawa, mwenye umri wa miaka 17, alikuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Bang'ata.Habari kutoka katika Kijiji cha Sing'isi kilichopo wilayani Arumeru, lilikotokea tukio hilo, zinasema msichana huyo alipigwa na kitu kizito kichwani.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Basilio Matei pia alithibitisha tukio hilo na kusema lilitokea juzi saa 8 mchana.
Vyanzo vya habari vilisema kuwa Charles alimpiga na kitu kizito marehemu na yeye kukimbilia kunywa sumu ili afe lakini yuko mahututi katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru chini ya ulinzi wa polisi.

Taarifa zilisema kuwa marehemu ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo ya sekondari Bang'ata na walikuwa wakigombana mara kwa mara kutokana na madai kuwa mwenza wake wa kike alikuwa siyo mwaminifu katika mapenzi na kutembea na wanaume wengine.

Habari ziliendelea kusema kuwa mtuhumiwa hakufurahishwa na vitendo vya marehemu alivyokuwa akivifanya na kumwonya mara kwa mara lakini marehemu alikuwa akikaidi ushauri wa mpenzi wake.

Kamanda Matei alisema kuwa mtuhumiwa bado yuko katika hospitali ya mkoa akipata matibabu na yuko chini ya ulinzi mkali wa polisi kwa kosa la kuua na hali yake inaendelea vizuri.
Matei alisema wanafunzi hao wa sekondari walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu.

Source: John Mhala, ArushaDaily News;
Tuesday,December 09, 2008

No comments: