"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, December 18, 2008

Mawasiliano

Fikiria una chungwa moja tu na una watu wawili wanalihitaji.

Je, ni njia ipi nzuri ya kufanikisha kila mmoja kupata hitaji lake la kupata chungwa?

Naamini wewe haraka haraka jibu lako litakuwa ni kuligawa nusu kwa nusu na kuwakabidhi kila mmoja aanze mbele!

Ukweli kabla hujafanya hivyo mi vizuri ukawauliza kwanza sababu za kila mmoja kuhitaji hilo chungwa kwani inawezekana mmoja anahitaji ganda lake kwa ajili ya kutengeneza keki na mwingine inawezekana anahitaji juisi ya chungwa ili anywe hivyo kugawa nusu kwa nusu ni kitendo ambacho wote hawataridhika, ingawa kwako ni njia sahihi.

Mawasiliano ni pande mbili anayeongea na anayesikiliza na muongeaje lazima wakati mwingine atambue msikilizaji anahitaji kusikia nini na si kumwongelesha tu.
Kwa njia hii unaweza kutatua migongano, migogoro, chuki, migomo nk

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Au labda je mimi nata´ka chungwa lote nzima nzima bila kugawana na mtu.

Shabani Kaluse said...

HABARI ZA SIKU KAKA.
NIMEPITA HAPA KIBARAZANI KWAKO LEO,
ILI KUJIFUNZA MAWILI MATATU.
AHSANTE KWA MAARIFA HAYA YA NDOA.
KUSEMA KWELI NIMEJIFUNZA MENGI HUMU.

YASINTA USIWE MCHOYO, KWA NINI UTAKE KULA CHUNGWA PEKE YAKO?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,
Kabla sijakupa chungwa zima je unataka kwa ajili ya nini?

Kaka Shabani,
Nashukuru sana kwa kupita hapa.
asante sana