"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, December 20, 2008

Nitawakumbuka sana

Wafanyakazi wa Umoja wa mataifa (UNDP)
Kunduchi Beach Hotel & Resort- Mei 2007
Dar es Salaam Tanzania
Nimefanya kazi pamoja nanyi kwa miaka 7, tangu tarehe 13 Octoba 2001 hadi tarehe 15 Desemba 2008.
Nimejifunza mengi sana kutoka kwenu na mafanikio mengi nimeyapata ni kutokana na ushauri wenu kwangu.
Nawatakia maisha mema katika kuhakikisha dunia hii ni mahali bora kuishi kwa watu wote maskini na matajiri.
Nitawakumbuka sana!
I will remember!
Je me souviens!
Ndila suhwa!
Lazarus P. Mbilinyi
Ontario - Canada

5 comments:

Bwaya said...

Mbilinyi, nimekuwa nikikusoma kila siku. Habari hii nadhani ni ya kibinafsi zaidi lakini nadhani si vibaya wasomaji wako tunafahamu: mwenzetu uko wapi kwa sasa na unafanya nini. Ni ombi.

Nikutakie Krismass njema kaka.

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka Bwaya,

Nashukuru sana kwa swali zuri la kufahamu kwa sasa nipo wapi na nafanya nini.

Nipo Ontario Canada kwa masomo tangu Septemba 1, 2007 pamoja na familia (mke wangu Gloria na mtoto wangu Emmanuel)
Mimi ni mwanamazingira na kwa sasa nasoma Forestry Management.
Tuzidi kuwasiliana.

Upendo daima

Yasinta Ngonyani said...

Kwa nini unasema nitawakumbuka sana sio ninawakumbuka sana je hutafanya kazi na wao tena?

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Yasinta,

Ni kweli nitrakuwakumbuka sana kwa sababu sitaenda kufanya kazi nao tena kwani nikimaliza masomo yangu nitarudi nchini kwangu kuendelea kufanya business zangu ambazo nimekuwa nafanya na ndiyo maana nimekuja kusoma zaidi ili kupata uwezo zaidi ya kuendesha business zangu mwenyewe baada ya kuwekeza zaidi ya miaka 15 iliyopita na sasa ni wakati wa mimi mwenyewe kuwa na ofisi yangu.
Nakukaribisha sana ofisini.

God bless u

Bwaya said...

Hongera sana kaka Mbilinyi. Nimefurahi kusikia hivyo. Nakupongeza kwa kuwa karibu sana na familia yako kama ambavyo umekuwa ukituelmisha. Hongera kwa kuyatembea maneno yako.

Masomo mema kaka yetu