"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, December 17, 2008

Waliooana tu!

James na Deborah (si majina halisi) ni mke na mume wote wana miaka 28 na Mungu amewajalia kuwa na watoto wawili, miaka 2 na miaka 4.
James ni mwalimu na Deborah ni Nesi.
Jumamosi moja baada ya watoto kwenda kulala kifuatacho kilitokea kwenye sofa sebuleni.

James: (Huku akimpapasa mkewa mapaja kwa mikono yake na pia akimtazama usoni) vipi honey unajisiskiaje? Je una mood leo?
Deborah: (huku akijisikia kushtushwa) mwenzio najikisia kuchoka.

James: (huku akiwana na hofu kwamba anaweza kukataliwa) Mbona kituko! ina maana jana hukupata usingizi wa kutosha?
Deborah: Sawa ila nadhani nitakuwa nimechoka sana kwa hili leo.

James: Siku hizi naona huna hamu sana na mimi kufanya mapenzi na wewe au kwa sababu jana nilipoteza erection mapema?
Deborah: (huku akijisikia hatia kwa kumkatalia mumewe ombi lake) Kwa nini iwe issue kama hilo lilitokea jana?

James: (huku akiwa amekasirika na kujiona si lolote mbele ya mke) Ok, naenda kulala tutaonana baadae.
Deborah: (anamfuata James chumba na anavua nguo zote) Ok, nipo tayari kama tunaweza kujaribu basi.

James anambusu Deborah haraka haraka naye anajibu, James anamvuta kwake anaanza kuchezea nywele zake kumpapasa mwili kidogo then anahisi uume wake umesimama, haraka bila kupoteza muda anamlaza Deborah kitandani na kumlalia juu yake na kuanza kumwingia, inashindikana kwani Deborah bado hajawa relaxed na lubricated.

James anajaribu kuingia tena kwa nguvu na anashindwa kwani Deborah ni mkavu kabisa na anajisikia maumivu na Deborah sasa anabana miguu kwa maumivu na kumwambia stop.

James anapoteza erection wakati huohuo Deborah anajisikia hana hamu tena.
James anajisikia aibu sana na kuwa frustrated kwa kuwa kila kitu kimeshindikana.

SWALI:
je, unaweza kuhisi tatizo kubwa la James na Deborah ni nini?
Je, ili kitanda chao kiwe na moto wa kweli ni mambo gani wanahitaji kufanya?

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

nafikiri kumekosekana kupeana habari. kwani kama Dedorah angemwambia mwenzake ni shida gani anayo mambo yangeenda safi tu. Au kinyume pia

Anonymous said...

Hapo kuna tatizo la mawasiliano.
Siwezi kuandika mengi kwa sasa ila mawasiliano ni kutoa wazo kwa busara na kupokelewa na kufanyiwa kazi na kupewa positive feedback.
Tatizo linakuja pale ambapo mmoja anafanya juhudi na kutumia akili busara nyingi kuonesha kuna tatizo na mwenzake baada ya kugundua hilo basi anaona kuwa huyu mwanamke/mwanaume kumbe kanifia sana basi anaanza maringo na kujiona bora sana hivyo anaanza kujifanya kuwa scarse kwa mwenzie na kufanya hiyo nani hii yake kama ndiyo dhahabu huku akimtishia mwenzio kuwa atampa mwengine.

That is stupid and it will never solve the problem.
Kinachotokea hapo ni kuwa yule anayefanya bidii anajiona kuwa mwenzie anamchora hivyo hawi free tena na hata kujiona hahitajiki na msisimko kupungua sana.
Matokeo yake anakata tamaa kuwa tatizo la mwenzie haliwezi kutatulika na pengine kushindwa kumwamini hata kama huyo mwenzie hagawi nje.
Nakumbuka mama mmoja aliwahi kutoa kauli na kusema kuwa akiwa mbele ya mumewe hata kama yuko tupu kabisa hujisikia kama amevaa magwanda mazito, kuliko hata anavyojisia mbele ya bosi wake ambaye huwa ana appreciate sana miguu yake.

Mawasiliano ni two way, kama hakuna response basi yule anayeleta ideas na nia njema na kwa kutumia lugha, vitendo au approch ya busara na kuona haipokelewi na kufanyiwa kazi basi anapoteza imani kuwa yanaweza kubadilika au pengine anaweza kuanza kushindwa kujiamini yeye badala yake kutafuta approval from outside.
Ni maoni yangu

Anonymous said...

Ukweli James na Deborah wana matatizo ambayo ndoa nyingi ndivyo zilivyo na hakuna ladha kabisa ya mapenzi.
Jambo la kwanza naamini sytle ya maisha yao kimawasiliano si nzuri kiasi kwamba James anashsindwa kujua ni wakati gani Mkewe ana mood au la hadi aulize hii ni kithibitisha bado hajamfahamu.
Pia tendo la ndoa kwako halina maandalizi kiasi kwamba mwingine anafanya just kumfanya mwenzake asikasirike wakati tendo la ndoa ni kwa ajili yao wote (intimacy).
Pia style ya James kumuandaa Mkewa wake is too short kwani yupo too much genital focused.
Bottom line ni kwamba hawana upendo wa kweli katika maisha yao ya kila siku.
Thanks

Anonymous said...

PLEASE MATATIZO HAYA NAKUMBANA NAYO KILA SIKU

PLEASE NIAMBIE JINSI GANI INATAKIWA TUFANYE

Ndoa yangu bado changa hata mwaka haijamaliza na ninakumbana na matatizo kama haya je kweli hata kupata mimba kupo kweli.
Please endeleza darasa ili tujifunze zaidi.

Anonymous said...

Kwa kweli imeniuma sana,wanandoa tunatakiwa kuhudumiana hata kama wewe hujisikii mwenzako anajisikia kusex hebu vuta hisia zitakuja tu ili uweze kumfurahisha mwenzako,nani wa kumpa raha mwenzi wako zaidi ya wewe?imagine hiyo ni ndoa ya kikristo,ni forever,hutakiwi kwenda nje,sasa utafanyaje,mume/mke apige mastabertion wakani ameoa/olewa,thats very bad,wanandoa we have to change,ndio maana tunaambiwa research zinaonyesha wanandoa wanaongoza kwa kuwa na ukimwi,ni kwa sababu ya staili hii ya kunyimana wakati umeshasimamisha,akina dada/mama hebu tubadilikeni,ikibidi mwambie honey weka mate au weka yako ili pawe wet mr aweze kukuingizia kirahisi.msome mumeo kama yeye ni mpaka aingize kunako ndio anaridhika basi mwachie,ukimnyima utakuwa unamkosea haki yake ya msingi,please wanawake wenzangu naomba tubadililke jamani,sisi wenyewe ndio wachawi wa ndoa zetu.
Na wakina baba hebu muwe mnawaandaa wake zenu vizuri,kama hayuko kwenye mood,mlete taratibu ili awe kwenye good mood,then ndio utake ile kitu,kwanza automatically atakupokea tu vizuri maana hata yeye atakuwa anataka.
Mwisho jamani pale unapojisikia kufanya mapenzi,as long as panafaragha,basi iwe ni hapohapo,maana kitendo cha kusema tu ngoja kwanza,tayari unakuwa umehamisha hisia za mwenzi wako,ni hayo tu kwa leo,nitarudi tena.
Nawapenda wana blog hii!
Mrembo wa Mr I.

Lazarus Mbilinyi said...

Mrembo wa Mr I,

Asante sana kwa maoni yako mazuri na jinsi unavyoweza kushauri wengine.

Ukweli ndoa nyingi huvunjwa na kuvurugwa hasa kuanzia suala la kitandani.

Ndiyo maana kila siku tunakumbushana kwamba ni vizuri kumjua mwenzako ndani na nje na pia lazima umtangulize yeye kwanza badala ya wewe kuwa mbinafsi.
Tupo katika kizazi kipya kiasi kwamba huko nje ya ndoa si salama kabisa kwa magonjwa na tunatakiwa kuhakikisha ndani ya ndoa zetu kila mmoja anaridhika na suala la unyumba.

Asante sana kwa mawazo mazuri na Mungu akubariki sana

Upendo daima