"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, January 30, 2009

Weekend Njema

Match zetu za soccer ni gender balanced.

Funga vizuri

Hata kama ni mlango wa dhahabu kama haujafungwa wapo wanawake haijalishi huko chumbani kuna raha ajabu bado wazo la kwamba mlango upo wazi na haujafungwa linanata kichwani. Mwanaume anaweza kuongeza ladha ya mahaba kwa mke wake pale anapokuwa makini na suala la jiografia na ustadi wakati wa tendo la ndoa.
Wanawake ni viumbe ambao mara nyingi huwa distracted na mazingira waliyopo kuliko wanaume hasa linapokuja suala la faragha na usalama.

Wanawake huathirika zaidi na mazingira hasa sauti au kelele na harufu (smells) kuliko wanaume (mume) kwa wakiwa sita kwa sita, mfano hofu ya kwamba watoto watasikia hasa kama watoto wanapiga kelele,hofu ya kusikiwa na majirani au wapiti njia, hofu ya mlango kuwa haujafungwa (komeo) nk.

Mume mmoja alisafiri kwenda nchi za mbali na aliporudi nchini kwake na kupokelewa na mkewe walienda moja kwa moja nyumbani kwao na kwa kuwa hakukuwa na watoto au mtu mwingine bali wao wenyewe tu, wakaamua kwa raha zao wapeane zawadi ya miili yao kwanza kabla ya lolote kwa kuwa walikuwa na hamu kubwa kila mmoja kwa mwenzake, hata hivyo mlango walisahau kuufunga na baada ya kumaliza kupeana zawadi mke alimuuliza mume "hivi unakumbuka mlango hatukufunga?"
Hii ni ina maana gani? ni kuthibitissha kwamba muda wote wa tendo la ndoa mke alikuwa anawaza kwamba mlango haujafungwa na alikuwa anawaza hivi watoto wakirudi na kuingia moja kwa moja itakuwaje.
Mume yeye wala hakuwa na wazo hilo na wanaume wengi wapo hivyo.
Mwingine ana enjoy sex mwingine anawaza mlango haujafungwa!

Pia sijui inakuwaje tafiti nyingi zinaonesha wanaume wala huwa hawaogopi wapi ni salama kufanya tendo la ndoa.
Kwenye gari, bafuni, jikoni, sebuleni, chumbani, store, ofisini, kiwanjani, porini, makaburini na sehemu zingine unazozijua wewe.

Kuna nchi watu walikuwa wanaulizwa maeneo ambayo wamewahi kufanyia sex, ukweli majibu yaliyokuwa yanatoka yanatisha sana.


Tatizo kubwa lingine ambalo linaweza kuwa kizuizi cha kumpa hamu mke wakati wa tendo la ndoa ni wanaume kuwa wachafu au rough, au kutozingatia usafi.
Inawezekana wewe ni mwanaume unafanya kazi ambayo baada ya kazi unakuwa na majasho au unahitaji kuoga vizuri acha suala la kupiga mswaki na kuwa na kinywa kisicho na harufu.

Kucha chafu na mikono inayotisha hata unapomshika bibie na ngozi yake laini badala ya kusisimuka wewe unamuumiza na kumpa kinyaa kama si kichefuchefu.
Bahati mbaya na huko kazini uliona picha au mwanamke mrembo basi homoni nazo zikafanya kazi basi ummemkumbuka mkeo hivyo kufika nyumbani tu unataka.


Bila kujali usafi unamrukia mkeo na kwa kuwa anauwezo wa kunusa zaidi kuliko wewe unafanya a-palalyse kwa kuishiwa hamu kabisa na wewe matokeo yake na wewe unajisikia upo rejected.
Ukweli usafi ni jambo la msingi mno.
Cleanness is next to godliness

Wednesday, January 28, 2009

Mume wangu na mama yake - lao moja

Mtoto wa kiume akiwa na miaka 10 hadi 14 akawa na mama tu bila baba, huwa mtoto wa mama hata akiwa ameoa! Wapo wanawake wambao wameolewa na mume ambaye ni mototo wa mama haambiwi kitu hadi mama yake aamue na anaweza kuongea na mama yake maamuzi ya ndoa na kuacha mke kama mtekelezaji tu.

Ukweli kuwa na mume ambaye anamsikiliza mama kwa kila maamuzi ya maisha ya ndoa yenu huwa inasumbua sana kama siyo kuleta matatizo makubwa katika ndoa.
Inakuwa ngumu zaidi kwa kuwa unahitaji kutomchukiza mumeo na mama mzaa mumeo maana bila mama mkwe huyo mume usingempata.
Pia wakati mwingine mama yake (mumeo) anapoleta vurugu kwako au kukuchukia tu bila sababu au kujaribu kukuona si lolote kwa mototo wake, mumeo anatulia tu kama vile haoni na zaidi anamtetea mama yake.

Inawezekana upo kwenye uchumba, na mchumba wako (mwanaume) sasa anageuka na kusema kwamba kwa sababu ambazo mama yake hajaridhika nazo labda kabila, au ukoo au dini au elimu au basi tu si chaguo la mama, eti hamuwezi kuoana.
Usibaki kimya eti ipo siku ataacha mwenyewe au mumeo na mama yake watabadilika, unaumia bure mototo wa watu, sema usikike!

Je, njia zipi za kutumia kuishi vizuri na mume ambaye bila mama mambo hayaendi?
Kaa chini na mumeo mwambie wazi kabisa kile kinaendelea na jaribu kuhakikisha mnapata jibu (solution) kwa pamoja.
Kwa upendo na heshima zote tena kwa lugha rahisi (kama umeokoka basi huku ukiwa umefunga kwa maombi ila unatabasamu), mweleze vizuri mumeo kwamba uliolewa na yeye siyo mama yake na mwambie anavyofanya inakuumiza na toa sababu kamili inakuumiza vipi.

Uwe tayari una majibu ya nini kifanyike na mwambie ni mikakati ipi au unataka iweje halafu mwambie na yeye atoe solutions kwa hili jambo, pia uwe unamsikiliza zaidi kuliko kuongea hasa mumeo anapongea.
Pia muamue kwa pamoja nani ataenda kuongea na mama yake (kumfunga paka kengele) kama mwanamke mwoga mume anaweza kwenda mwenyewe kuongea na mama yake.

Ukifika kwa mama (wote au mmoja ambaye ameenda) kaa chini, elezea jinsi unavyojisikia au mnavyojisikia na jinsi anavyowasumbua, mpe solutions za jinsi mlivyopendekeza na pia mpe na yeye nafasi aongee bila kumkatisha anapoongea.

Tahadhari!
Kama inawezekana pata ushauri kwa mtu anayeaminika anaweza kuwa mchungaji, msimamizi wa ndoa au mtu yeyote mwenye busara na hekima katika jamii.
Wanaume wengi ambao hushikwa sana na mama zao huwa hivyo kwa sababu mara nyingi wakiwa na umri wa miaka 10 hadi 14 hawakuwa na mwanaume wa kuwa nao isipokuwa mama peke yake hivyo mwanaume yeye hajui kama ameshikwa na mama yake.
.
Pia wanaume ambao wanameshikwa na mama zao hawawezi kuweka mipaka na mama zao, hivyo inabidi asaidiwe kujua kuna mipaka mwanaume anapooa na zaidi anatakiwa aweke mipaka maana yeye ni mlinzi wa mke kimwili, kiroho na kihisia.
Mwanamke pia uwe wazi kwa mama mkwe (ingawa hii kwa jamii nyingi za Afrika ngumu sana) mwambie tabia ipi inakuchukiza anapokuwa na mwanae na tabia ipi unafurahia kwani huko pia ni kuweka mipaka.

Ikiwezekana kama mnaishi jirani hama kabisa angalia uwezekano wa kuhamia mbali au umbali kidogo au mji mwingine au kijiji kingine huko unaweza kupata amani na pia unaweza kupata muda wa kukata mzizi unaomshika mumeo kwa mama yake.
Umbali wakati mwingine hufanya maajabu.

Pia mwanamke uwe umejiandaa kupata resistance kutoka kwa mumeo au mama yake, na wote wakigoma usikate tamaa pia unaweza mwenyewe kwenda kupata ushauri kupambana na hii hali.
Pia fahamu kwamba kuna wanaume (piga ua) hatakubali kujirekebisha, ila kuna mtu mmoja tu anaweza kuwabadilisha wanaume duniani yeye anaitwa ni change agent, anaweza kuleta mabadiliko yoyote, miaka 200o iliyopita alikufa msalabani kwa ajili ya wanaume na wanawake wote, mwambie yeye anaweza, jina lake anaitwa Yesu

Tuesday, January 27, 2009

Ni kudanganyana

Kama ulivyo ni wewe jiamini na waweza kuwa vyovyote unataka na una haki ya kuzaliwa kufurahia tendo la ndoa bila kujali upoje. Jamii imezungukwa na tamaduni zinazofanya mwanamke kujiona akiwa na shape, size, uzito, rangi, lugha, cheo, elimu fulani ndipo atafurahia mapenzi na kuonekana mwanamke mrembo na anayetakiwa na wanaume katika jamii husika, huo ni uwongo na si kweli.

Pia jamii inawadanganya wanawake kwamba wakiwa vile au uzito fulani basi watakuwa wazuri kimapenzi, ukweli ni kwamba uwe mnene, uwe mwambamba, uwe mrefu au mfupi, mweupe au mweusi unaweza kuwa mzuri kwenye mapenzi.

Ukweli ni kwamba mwanamke mwenyewe akijiamini na kujiona ni mrembo (self esteem/ self image), urembo huanza na wewe mwenyewe kwenye ubongo, ukijiona sexy watu watakuona sexy vivyo hivyo ukijiona hufai watu watakukimbia.
"You are by what you think"

Naura Hayden aliwafanyia utafiti wanawake 486 kujua je wanaume hudanywa au huwa hawadanganywi linapokuja suala la kufika kileleni (orgasm).
310 Walikiri kwamba walikuwa wanawadanganya waume zao mara zote.
124 Walikuwa wanadanganya mara nyingi.
52 Walikuwa wanadanganya mara chache sana.

Hii ina maana gani?
Hii ina maana kwamba wanaume hudanganywa na wanawake kwamba wameweza kazi, kumbe …………………..

Pia jamii hasa wanaume hujidanganya kwamba (potoshwa) kwamba kitendo cha mwanaume kusugua uke kwa uume (intercourse) kwa kila aina ya style humpa mwanamke raha ya mapenzi kuliko mambo mengine kama kumuandaa na kufurahia foreplay nk kwa muda mrefu kuliko intercourse yenyewe.

Pia bado jamii inadanganywa kwamba sex ni usiku baada ya kazi na si mchana, matokeo yake mwanaume na mwanamke wanaoenda kazini na kuchoka na kazi huishia kufanya sex (tendo la ndoa) huku wamechoka na hakuna ladha.

Kwa nini msisubiri weekend mchana wakati upo safi mind, body and soul?
When you are tired, the libido goes away!

Wengine kama walichanjia hata mwanamke achoke vipi lazima atoe maana anaona ni kama birthright yake kuhakikisha ikiwa usiku tu lazima apewe.

Unapima quality ya tendo la ndoa kwa kufanya mara ngapi na si kuridhisha?
Usijidanganye!

Saturday, January 24, 2009

Hatuoni aibu loo!

Inasikitisha sana dunia ya leo kwa nchi kama Tanzania kuona na kusikia habari za baadhi ya watu kuwaua Albino kwa ajili ya kazi zao za kishirikina.
Mungu atuepushe!
Kwa habari zaidi bofya hapa chini

Friday, January 23, 2009

CONFIDENCE :
Once all village people decided to pray for rain. On the day of prayer all people gathered and only one boy came with an umbrella...... that's Confidence...

TRUST:
Trust should be like the feeling of a one year old baby when you throw him in the air; he laughs.....because he knows you will catch him........ That's Trust............

HOPE:
Every night we go to bed, we have no assurance to get up alive in the next morning but still we have plans for the coming day..........that's Hope.......... Have a wonderful day!

Checkup ya Ndoa 2009

Kama mahusiano yangekuwa yanaenda kwa daktari kupata vipimo je, ungepata Tick?
Huu ni mwaka 2009 naamini ni vizuri kujiangalia na kupata ukweli wa mahusiano yako unavyojisikia na je kuna dalili kwamba hali inakuwa nzuri au ndo mnaelekea ICU?
Jikague kwa kuangalia mambo yafuatayo then kwa uaminifu kabisa jiulize ni lipi kati ya haya bado unahitaji msaada.
Kumbuka mahusiano yakiwa mabaya unaweza kuhatarisha afya yako, utendaji wako wa kazi, kiroho chako, marafiki na hatimaye hisia zako na mwisho kufa mapema.
Jiulize hapa sasa!
Najisikia nipo huru, wazi na pia ni rahisi sana kuongea na mwenzangu kuhusu negative au positive feelings nilizzonazo.

Mwenzangu kawaida huwa hanisikilizi ninapoelezea hisia zangu.

Mara kwa mara namlalamikia, criticize, laumu mwenzangu hata kwa vitu ambavyo hajafanya.

Namwambia mwenzangu “Nakupenda” au nampa appreciation angalau kwa wiki mara moja.

Mara chache sana mimi na yeye kwa pamoja hulipuka na kuchukia pale mmoja anapoanza kutoa makosa kwa mwenzake.

Angalau kwa mwezi tunakuwa na mazungumzo si chini ya nusu saa kuongelea kutatua matatizo na migogoro inayojitokeza.

Mwaka uliopita hatukuweza kuwa na muda wa kuongea kuhusu mahusiano yetu katika tendo la ndoa
Ukweli kila mmoja ameridhika na mgawanyo wa kazi nyumbani.

Tumekuwa na maongezi bayana kuhusu kila mmoja anavyojisikia mapenzi nje ya ndoa.

Ni mara chache sana tunafikia muafaka tukianza kuzozana.

Kama nahitaji kumpa hisia ambazo anahitaji kwangu najua jinsi ya kufanya.

Tuponajaribu kutatua mgogoro ambao umejitokeza mara nyingi huishia kuamsha hata migogoro iliyipita.

Tunapokuwa kwenye tendo la ndoa wote huwa tunafika kileleni na kuridhika.

Tukigombana, ndani ya saa 24 tunakuwa tumeelewana na kuyamaliza.

Mambo ya kuzingatia ili ndoa mahusiano yako yawe ya kuridhisha na afya njema mwaka 2009.
Mawasiliano wazi (open communications) – uwezo wa kuongea kwa uwazi hisia zako za ndani tena kwa uhuru ziwe positive au negative.
Kuonesha kujali na upendo- je ni kitu gani kinamfanya mwenzako aone unampenda?
Mahaba na mapenzi – tendo la ndoa ambalo kila mmoja anaridhika, kutatua matatizo ya kitandani, kuridhika na tendo
Kutatua matatizo kwa ustadi – kutafuta jawabu kwa kila tatizo na si kuacha tatizo
Mgawanyo wa kazi – iwe ndani na nje ya nyumba kila mmoja aridhike na mgawanyo wa kazi.

Baadhi ya alama zinazoonesha kwamba una mahusiano yanayoridhisha ni:-
Unajisikia unapendwa
Unajisikia unaeleweka kwa mwenzio
Unajisikia unakubalika kwa mwenzio
Unajisikia yeye ni ukuta kukukinga na stress au maaduni wa kiroho na kimwili
Watoto wanakuwa sehemu yenu na si tatizo kwenu
Unajisikia salama kujieleza kihisia au unavyojisikia kuhusu kufanya mapenzi
Mna sehemu inaitwa "nyumbani" ambako ni kimbilio la kila mmoja kupata faraja na upendo hata kama ni nyumba ya kupanga.
Kristo ni namba moja katika maisha yako binafsi.

Thursday, January 22, 2009

Unajua kuchora

Julian Beever ni mwingereza mtaalamu wa kuchora (anamorphic art ) kwenye pavements kiasi ambacho amekuwa anazunguka dunia nzima kwa ajili ya hiyo kazi yake na watu kumshangaa kwa kipaji alichonazo.Anauwezo wa kuchora picha inayoonesha 3 dimensional kuliko kuonekana flat


Watu wanakwepa shimo ambalo halipo


Kila kitu hapa ni feki kuanzia maji hadi mpira wa maji wenyeweMnashangaa nini hapo hakuna shimo kabisa


Wednesday, January 21, 2009

Kusamehe

Kwa nini kusamehe? Kwa sababu ni faida kwako.

Kusamahe ni kitendo cha kupooza au kuacha kujisikia umekwazwa, au umekosewa au umeudhiwa au kuondoa hasira mwa mtu ambaye amekukosea.

Faida ya kusamehe imeelezwa sana katika dini, elimu ya sayansi na matibabu pia.
Wengi wamekosa kuponywa magonjwa makanisani kwa sababu wameshindwa kusamehe.
Wengine afaya zao zinazidi kuzolota kisa hawataki kusamahe wenzao
.

Watu wanaweza kutuumiza kwa njia nyingi zaidi ya milioni hata hivyo tunahitaji kuwasamehe, pia kusaheme wakati mwingine si rahisi kama wengi wanavyodhani hata hivyo inabidi kusamehe.
Wapo wanandoa wanalala mzungu wa nne kisa hawataki kusameheana, na wengine wamehama na chumba cha kulala kisa hataki kusamehe, sasa unajitesa nini kwani kuna mtu alikulazimisha kuoa au kuolewa?
Nini kujitesa na donge moyoni?
unajiona mjanja hata hivyo ukweli unajimaliza mwenyewe kiafya, kimwili na kiroho pia.
Hata hupendezi kabisa! looooooooooo

Anaweza kuwa aliyekuumiza au kukukwaza ni mume wako, mke wako, mdogo wako, boss wako kazini, mchungaji wako, polisi, mkwe wako, dada au kaka.
Hata hivyo kama vilivyo vitu vingi hasira kwa wengi ni is easier said than done.

Huwa inakuwa ngumu sana kusaheme hasa pale tunayetaka kumsamehe anaonekana hana sababu au hastahili kusamehewa.

Kwa nini kusamehe ni muhimu?
Kusaheme ni vizuri sana kwa moyon wako.
Kusaheme kuna uhusiano mkubwa na Blood pressure (BP) pamoja na kupunguza Stress hivyo kusamahe huweza kukupa faida kubwa sana kwa afya yako ya moyo.

Pia kusaheme kuna matokeo postitive na dalili za kimwili kiafya, dawa unazotumia (medication), kiwango cha usingizi, kuchoka na kulalamika.
Hii ina maana kwamba mtu asiyesamahe hupata matokeo negative kwa yaliyotajwa hapo juu.
Kusamahe huimarisha mahusiano na urafiki.

Kusamahe huimarisha roho ya kujitolea (volunteerism) na kuwa watoaji katika jamii.
Kusahamehe hupunguza uadui.
Kusamahe ni njia nzuri ya kujilinda na hasira.
Kusamehe hukuongezea kiroho chako na kujisikia vizuri mbele za Mungu
Kusamahe huimarisha saikolojia yako
Kusamehe hupunguza maumivu sugu
Kusamehe ni kukaribisha uponyaji wa mwili na roho

Forgiveness is choosing to love. It is the first skill of self-giving love.

Kusaheme ni kitu kizuri sana kwa mwili wako, mahusiano yako na mahali ulipo duniani hivyo achana na hasira za kutosamehe na badala yake samahe ili ufanye dunia mahali bora kuishi.

Wapo watu ambao husema anasamehe lakini hasahau, ukweli hasara ya kutosamehe ni kubwa sana kwa anayetakiwa kusamehe kuliko anayesamehewa.

In the Bible it says they asked Jesus how many times you should forgive, and he said 70 times 7.
Well, I want you all to know that I'm keeping a chart.
(Hillary Rodham Clinton)

Monday, January 19, 2009

Huleta hamu zaidi!

Tunda aina ya tikiti maji (watermelon) lina viasili vya citrulline ambavyo huwezesha damu kufanya kazi sawa na anayetumia vidonge vya viagra kiasi cha kutibu tatizo la mwanaume kushindwa kusimamisha uume wakati wa tendo la ndoa.

Dr. Bhimu Patil huko Texas (A&M’s Fruit and vegetable Improvement) amefanya utafiti na kugundua kwamba tunda hili linauwezo huo na faidi zingine nyingi zaidi ya kuongeza libido.

Hivyo kama unahisi unahitaji nguvu zaidi haina haja kuhangaika, kitu cha kufanya ni kubugia matikiti maji kwa speed kama ya light.
Au ukiona mzee (mumeo) hana hamu na ile kitu au mke hana hamu na ile kitu, hakikisha baada ya mlo anapata matikiti maji ya kutosha.


Saturday, January 17, 2009

Weekend Njema

When in good times, prepare for bad times

Wednesday, January 14, 2009

Divine Nectar (ii)

Hata wadudu kama nyuki wanajua sana nectar ni kitu muhimu kwa ajili ya kutengeneza asali Pia kabla ya kusoma hapa ni vizuri ukasoma kwanza hapa http://mbilinyi.blogspot.com/2009/01/divine-nectar.html
Taratibu za mwanaume kumsaidia mwanamke kutoa divine nectar:
Divine Nectar huzalishwa na glands zinazojulikana kwa jila la Skene sawa na zile za Prostate ambazo hutengeneza sperms kwa mwanaume.
Fluid inayozalishwa na Skene si mkojo lakini hufanana na mkojo ingawa yenyewe huwa na glucose na prostatic acid.
Muundo wa kikemia wa hii fluid hufanana zaidi na semen za mwanaume ila hakuna sperm kuliko mkojo ingawa huwa majimaji kama mkojo.

Hii ni kujulisha kwamba mwanamke huweza kukojoa akifika kileleni na hutoa fluid ambayo hujulikana kama divine nectar au amrita au juice.

Wakati mwanamke anasisimuliwa kimapenzi au wakati wa mapenzi glands za Skene hutoa secretions ambayo husukumwa nje kwa speed kupitia urethra (kama mwanaume anavyotoa sperms)
Glands za Skene zimejibana kwenye ukuta wa kibofu cha mkojo na zipo upande wa juu wa ukuta wa uke pia zimetengenezwa kwa erectile tissues.

Divine nectar huweza kumtoka mwanamke baada ya kuponywa (healing) eneo la G- spot (Graffenberg spot).
Kila mwanamke anauwezo wa kufika kileleni (orgasm) kwa kupitia G- spot na mwanaume ndiye anayeweza kusaidia.
Wewe mwanaume kwanza lazima uwe na mtazamo kwamba wewe ndiye healer au mtu wa karibu kumsaidia na zaidi wewe ndiye mtu wa ku-guide kwamba lazima mkeo atoe divine nectar.

Pia mwanaume lazima ufikirie pia hicho kipisi cha uume ni kitu ambacho unaweza kuingiza kwenye mwili wa mwanamke na ukishamaliza unatoa na kwenda zako.
Fikiria kwamba uume wako ni Nuru halisi ya kuangaza raha ya mwanamke katika mwili wake na kufungua roho na nafsi yake ili ajisikia ni mwanamke aliyekamilika kimwili, kiroho na kihisia.
Ili mwanamke aweze kuwa kisima cha kutoa divine nectar ni kupata uponyaji halisi wa eneo hili la G- spot au sacred area kwa kufanyiwa massage au kukandwa.

G- Spot ni eneo ambalo lipo upande wa mbele kwa ndani kwenye uke wa mwanamke na unapopitisha kidole utakugundua kwamba ni eneo vimikunjo kama lips za midomo na si smooth
Baadhi ya wanawake huweza kupatikana kirahisi na wengine ni ngumu zaidi ingawa mwanamke akiwa amesisimka huweza kupatikana kirahisi.

Hiki kitendo ni muhimu kifanywe na mwanamke kwa kujitoa kumpa raha mwanamke bila kutegemea kupata return yoyote kwake.
Kwanza mwanaume lazima ajenge trust kwa kumpa mahaba ya uhakika kwanza kwa kuanza naye kwanza kwa mwanaume kuhakikisha kucha za vidole vya mikono zipo safi na zimekakatwa vizuri then unaweza kwenda kuoga naye (kumuogesha au kuoga pamoja), pia hakikisha chumba umekiandaa na kuwa na sura ya kimahaba, unambusu passionately hakikisha mnapumua pamoja, huku mkitafakari mapenzi yenu kwa uwazi ili kuunganisha moods zenu na kupeana hamu zaidi kama si kuipa miili joto la kimapenzi.

Anza kwa kumfanyia Massage mapaja, hips, na eneo chini ya kitovu, panda tumboni na kuzunguka matiti, upande wa ndani wa mikono na rudi tena kwenye mapaja huku ukizambaza raha mwili wako wote ukirudi hadi dakika 5 hadi 10 hivi.
Hapo mwanamke atakuwa amerelax na yupo tayari kukuruhusu uendelee kwenye uke wake.
Then kwa upole kabisa anza kuchezea kwa ustadi kabisa kuta za nje za uke wake na kisimi kama vile ni vito vya thamani umepewa mikononi mwako.
Ni vizuri kumuuliza hasa ukiona ameanza kuhema tofauti kama unaweza kuingia kwenye sacred place au kwenye bustani .

Baada ya kuruhusiwa ingiza kidole (kidole cha kati huku kiganja kikiangalia juu) ndani ya uke huku ukichezesha au massage kwa alama kama vile unamuita mtu kwa kidole( njoo).
Ongeza mgandamizo kidogo ili na yeye asikie aina fulani ya mguso, endelea kuchezea kwa kuzungusha kidole chini na juu au kwa vibration, au zigzag au vyovyote hasa kutokana na yeye anavyo respond huku mkono mwingine ukichezea kisimi.
Pia unaweza kuongeza kidole kingine kwani baadhi ya wanawake hujisikia raha au kusisimka zaidi hasa kukiwa na vidole viwili.
Hakikisha macho yako na macho yake yanangaliana huku mkisamabaza umeme wa upendo baina yenu na huku kila mmoja akimsoma mwenzake anaendelea vipi
Pia wakati mnaendelea na hili zoezi ni vizuri mwanaume kuongea maneno mtamu yanayoonesha anafanya uponyaji wa hii sehemu huku mwanamke akimshukuru mwanaume kwa kazi kubwa anayofanya .

Kazi ya mwanamke kwenye hili zoezi la kufanya massage G-spot ni kulala, kuenjoy na kutoa feedback kwa mwanaume (ingawa mwanamke lazima ujiandae kwani unaweza kujisikia unataka kukojoa haja ndogo au unaweza kujisikia unataka kulia au unaweza kujikuta unakumbuka jinsi hisia zako zilivyoumizwa huko nyuma)
Hili kitendo lazima kirudiwe na kufanywa zaidi miezi miwili, mara mbili kwa wiki na kama kila kitu kipo shwari basi mwanamke anaweza kuanza kutoa divine nectar ingawa inatokana na historia yake ya mahusiano ipoje kama amewahi kubakwa au kudhalilishwa kijinsia au kuumizwa wakati wa tendo la ndoa huchukua muda mrefu kupata healing kwenye G spot.

Mambo ya msingi kuzingatia
Mwanamke au mwanaume kufahamu location ya G-spot
Uwezo wa kusababisha mwanamke akisijia raha (pleasure) anaposisimuliwa au kufanyiwa massage kwenye G spot
Mwanamke kuondoa hofu na mashaka au kujisikia anataka kutoa mkojo hasa anaposisimuliwa G-spot hivyo badala la kurelax anaweza kuwa na hofu

Picha chini inaonesha G-spot katika uke
Kama una swali unakaribishwa!

Wanaume wamejigawa katika makundi mawili linapokuja suala la kusimamisha uume wao kwa ajili ya tendo la ndoa.
Kundi la kwanza ni lile ambalo kabla hajasimamisha (sisimuliwa) huonekana kuwa na umbo kubwa na akisisimka au sisimuliwa inakuwa kawaida tu (shower).
Kundi la pili ni lile ambalo kabla ya kusisimuliwa au sisimka huonekana umbo dogo na akisisimka hukua na kuwa maradufu (grower)
Hivyo huwezi kujua nini kimo kwenye kitabu kwa kuangalia nini wameandika kwenye cover.

Monday, January 12, 2009

Ufundi, uhodari, ustadi wa kutatua matatizo ya Ndoa

Wapo wanandoa ambao ni kama hua, hata audhiwe vipi anabaki kimya anaogopa asije akasababisha mwenzake kukasirika au kuzozana.
Wengine ni mwewe kitu kidogo tu ni kuzozana hadi yaishe.
Wewe je ni mwewe au hua? MAWASILIANO YALIYO WEZA.
Wanandoa lazima waongee kwa uhakika wao wenyewe kila mmoja kwa mwenzake kuelezea hisia za ndani kabisa na kila mwanandoa lazima amtie moyo (encourage) mwenzake.

KUONESHA UPENDO WA KWELI NA KUJALI
Wanandoa lazima wawe na uwezo wa kuonesha upendo na kujali mwenzake hasa ili kuzuia hali ya kuzolota tabia ya kupenda mwenzake kila wanapoendelea na maisha na kuishi.

MAPENZI NA FARAGHA
Wanandoa ni muhimu kila wakati kuchochea mahusiano ya tendo la ndoa linaloridhisha ili kuwa na mahusiano imara na wawili kuwa na faragha pamoja (intimate partnership)

KUTATUA MATATIZO NA MIGOGORO.
Wanandoa ni muhimu kuwa na ustadi, au busara au hekima na uwezo wa juu sana kumaliza migogoro au tatizo au tofauti yoyote inapojitokeza haraka iwezekanavyo.

KUYAMALIZA
Pia ni muhimu sana kwa wanandoa kuwa na hekima ya kujua jinsi ya kumaliza mgogoro kuliko kwenda sambamba kila mmoja bila kuridhika na uamuzi wa mwenzake, kama mmoja amekosa basi akubali amekosa hata kama wewe ni mwanaume na jamii inakuona kama waziri au mbunge au kiongozi mkubwa kwani ndani ya nyumba wote ni kitu kimoja.

MGAWANYO WA KAZI
Katika ulimwengu wa sasa ambao wanawake na wanaume wote huondoka asubuhi au muda wowote kwenda kuwinda kwa ajili ya mkate wa familia bila kuwa na mgawanyo mzuri wa kazi nyumbani mmoja huweza kulemewa na zaidi kuzusha migogoro mingine.
Hivyo basi wanandoa lazima wawe wanagawana kazi na kusaidiana vizuri na kila mmoja kumtanguliza mwenzake.

JINSI YA KUZOZANA
Ni vizuri kila mmoja kutoa dukuduku alilonalo au kama kuna kitu kinamuudhi au kinamsumbua au haridhiki nacho kwa mwenzake ni vizuri kukiweka mezani na kikamalizwa kwa kujadiliana kuliko kukaa na donge moyoni huku unaangamiza na afaya yako.
Wapo wanandoa ambao hata kama kuna jambo gumu limamuumiza hayupo tayari kumuuliza mwenzake kwa kuogopa wasije wakaanza kuzozana au kuogopa mwenzake asije akakasirika. Ukweli ni kwamba afadhari umwambie akasirike na muyamalize kuliko kukaa nalo moyoni.

Friday, January 9, 2009

Tunatumia ubongo tofauti

Je, kama unaendesha gari then ukamchomekea, kati ya mwanaume au mwanamke yupi utaambulia matusi chapchap? why!Mwanaume na mwanamke hufikiria tofauti hasa kutokana na jinsi ubongo unavyofanya kazi.
Mwanaume hutumia gray matter na wanawake hutumia white matter.
Pia wanaume hutumia upande mmoja wa ubongo wakati wanawake hutumia pande zote mbili za ubongo (kushoto na kulia)
MAWASILIANO
Kawaida mwanaume husikia nusu ya kile anaambiwa na mwanamke na hukumbuka nusu ya kile amekisikia kutoka kwa mwanamke na hurudia nusu ya kile anakumbuka.
Ubongo wa mwanaume hauwezi kushika na kujihusisha kwenye mambo ya kihisia kama mwanamke ndiyo maana mwanaume anaweza kuambiwa habari za ugonjwa, harusi, ajali hata kifo amwambie mkewe na akasahau na si mwanamke akiambiwa amwambie mumewe kusahau lazima atakumbuka na atakwambia.

Wanawake wana uwezo mkubwa sana kukumbuka jambo lolote la kihisia (emotions) kutokana na ubongo wao wa eneo la amygdela kuwa na uwezo kuliko wanaume.
Daktari Stephen Hamman (University of Toronto Canada) anasema kwamba mwanaume anaweza kupokea kwenye ubongo wake sawa na mwanamke ila ujumbe wake unakuwa mweupe bila hisia (emotions & feelings) kwani maana ya hisia hupotea na kuwa ujumbe mkavu tu.

MAUMIVU
Wanawake huwa na mwitikio mkubwa wa maumivu kuliko wanaume.
Katika utafiti (University college of London) watafiti walutumia Electric shock kwa wanawake kupima mwitikio wa maumivu na baadae wakawachukua waume zao na kuwafanyia the same thing na wanaume wakaambiwa wakawaambie wake zao kwamba waliteswa na electric shock matokeo yalionesha wale wanawake waliupokea ujumbe ule kwa maumivu sawa na waume zao walivyokuwa wanapata electric shock, Hii ina maana kuambiwa tu waliumia kama vile wapo kwenye mashine yenyewe.

TENDO LA NDOA/MAHABA
Kumbumbatia mwanamke kwa sekunde 20 huweza kuzalisha oxytocin ambayo humpa mwanamke muunganiko wa hisia.
Wanaume pia huzalisha oxytocin kwa affections na tenderness wanayotoa ila ubongo wao hupeleka hisia moja kwa moja kwenye sex au tendo lenyewe.
Sehemu inayohusika na mambo ya sex kwenye ubongo kwa mwanaume ni kumbwa mara mbili ya mwanamke.
Ndiyo sababu kwa kuona tu (acha kuwa uchi chumbani) ubongo wa mwanaume huanza kulipuka kwa sex.

KUFAHAMU MAZINGIRA
Wanaume ubongo wao una uwezo mkubwa sana kusoma ramani na kutumia mwelekeo (directions) wakati wenzao wanawake ni wazuri kutumia alama (landmark) kama majengo ili kukumbuka ramani zamahali.
Mfano mwanaume atakumbuka kwamba alipaki gari mlango wamagharibi wa Mall na mwanamke atakumbuka alipaki gari mlango wenye display ya mashati ya njano.

HASIRA
Wanaume hu-react haraka kwa kufoka kwa sababu homoni zao hutumia mzunguko mfupi kwenye kwenye ubongo.
Wanawake wakikasirishwa homoni hupitia njia ndefu ya kujipima kwanza (processing) ndipo afanye reaction.
Mwanamke hu-react kwa hofu na woga wa security yale kwanza ndiyo maana si sawa na mwanaume.
Ukitaka kuangalia chunguza dereva mwanamke na dereva mwanaume anapokutana na mtu anayemchomekea barabarani.

MSONGO WA MAWAZO
Mwanaume akiwa na stress mapigo ya moyo na BP hupanda na hu-react kwa haraka na msongo wa mawazo kuyeyuka.
Mwanamke akiwa katika siku zake huwa mtulivu kuliko wakati mwingine wowote linapokuja suala la msongo wa mawazo.
Pia mwanamke huweza kuondoa stress kwa kuongea na rafiki yake au mtu wa karibu au anayemwamini. Hivyo basi ili mwanaume ajisikia vizuri huweza kufoka chapchap na mwanamke ili ajisikie vizuri huongea na mtu anayemwamini au mtu wa karibu.

MIGOGORO
Wanaume si wepesi ku-maintain relationship hii ina maana kwamba wanaume wengi (si wote) ndiyo wagumu sana linapokuja suala la kutatua matatizo ya ndoa, wanawake hupenda sana yaishe.
Unakuwaje mwanaume akifumaniwa au inakuwaje mwanamke akifumaniwa?
Naamini unaweza kujua nani hapo atamsamehe au nani atafukuzwa kabisa.

Thursday, January 8, 2009

Homoni zingine acha tu!

Muundo wa homoni ya Oxytin kikemikali Mwanaume au mwanamke anapofika kileleni (orgasm) mwili wake huzalisha (release) homoni inayoitwa Oxytin (oxytocin) ambayo husababisha kujisikia furaha na upo relaxed.
Pia hii homoni husaidia kufanya bonding ya kimapenzi kuwa strong kwa hao wawili ambayo wamefanya sex.

Wanawake huzalisha (release) kiwango kikubwa mara tano (5) zaidi ya wanaume na hii ndiyo sababu wanawake wengi huoza kabisa (addicted) na mwanaume anayetembea naye.
Mtasema sana mchana na usiku mtalala, kwani anakuwa blind and deaf indeed.
Ili kuvunja hiyo bond basi inahitajika miaka 2 mizima bila hawa wawili kukutana tena kimapenzi.

Mwanamke akiwa fertile kiwango cha estrogen huongezeka na kifikia kiwango cha juu kabisa.
Mwili wake huzalisha homoni za pheromones ambazo kupitia jasho hupaa hewani na kuwavutia wanaume, Guess what! Your on heat! And serious unataka sex ili dunia ijae!

Mengineyo!
“A man has to have sex to feel good, a woman has to feel good to have sex”
Wanaume wanaojua hili hawatumii muda wao mwingi kufikiria jinsi ya kuongeza ukubwa wa maumbile yao badala yake wanatumia muda mwingi kwa ajili ya kuandika love letter kwa wapenzi wao,
Wanawapa compliments kwa mambo wake zao wanafanya,
Wanawapa zawadi,
Wanawapa mabusu na hugs si chumbani tu, bali asubuhi wanapoagana kwenda kazini na jioni wanaporudi kutoka kazini na kila wakati,
Wanawasilikiza wake zao wanapoongea na kuwapa muda (quality time)
Wanakumbuka siku za kuzaliwa za wake zao na kufanya party.
Wake zao nao hujiona wapo sexy, hujisikia wanatakiwa na waume zao, wanapendwa, waume zao wanawajali, wanajisikia vizuri na wakifika chumbani huwa wanajisikia raha na wanataka mahaba na wakipewa wanafika kileleni.

Wednesday, January 7, 2009

Fikiria wewe ni mwanamke na upo naked mbele ya kioo chumbani,
Je, unapenda vile unajiona nywele, pua, matiti, tumbo, hips, mapaja, sehemu za siri?
Kama unajiona upo beautiful hongera mikono juu kabisa, na kama huridhiki pole hujiamini. Mwanaume huweza kusimamisha uume kila dakika 15 akiwa amelala usiku na mwanamke huweza kutoa majimaji (lubrication) kwenye uke wake kila dakika 15 akiwa amelala.

Binadamu ni wanyama pekee (primates) ambao hamu ya kufanya mapenzi au kufanya mapenzi (sex) si kwa ajili ya kuzaliana tu bali kupena raha ya kimahaba (sexual pleasure)

Pia Clitoris (kisimi) ni kiungo pekee katika mwili wa mwanamke au bindamu kipo kwa ajili ya kumpa raha ya mapenzi, hakuna kazi nyingine ni hiyo tu.

Raha ya sex kwa mwanamke si katika uke tu (genitals) kama alivyo mwanaume kwa uume wake (penis) bali ni zaidi ya hapo yaani mwili mzima.

Data zinaonesha kwamba wanawake ambao wamepatwa na matatizo ya ut wa mgongo (spinal cord injuries) na hawawezi kuhisi kitu chochote kuanzia kwenye kiuno kushuka chini bado wana uwezo wa kufika kileleni (orgasm)
Sababu kubwa ni kwamba ubongo hupokea hisia (feelings) za kusisimuliwa kimapenzi kupitia njia zingine nje ya uti wa mgongo hasa mwanamke anapochezewa matiti au kissing nk.
Hii ina maana mwanamke mwili mzima ni single sex organ tofauti na wanaume wanaowaza kwamba ili mwanamke afurahie mapenzi ni lazima uhakikishe unachimba vizuri Gold kule bondeni Afrika kusini (South pole au V – zone)

Quality ya mapenzi katika ndoa si mara ngapi mnafanya kwa siku au kwa wiki au kwa mwezi au kwa mwaka bali ni kuridhishana au kuridhika kwa wahusika kutokana tendo lenyewe.

Jamii inawadanganya wanawake kwamba wakiwa na sura fulani, au uzito fulani watakuwa wazuri katika mapenzi.
Thubutu, tafiti zinaonesha mwanamke yeyote akiwa uchi (naked) mwanaume yeyote humuona ni mrembo na huchanganyikiwa kabisa.
Haina haja kuzima taa au kutaka giza eti kwa kuwa matiti yako ni makubwa mno au madogo sana, au mwili umenenepa sana au mwembamba sana, au ngozi upo tofauti na unavyodhani.
Ukiwa uchi tu mwanaume hukuona bonge na beautiful woman.

Pia jamii inapotoshwa kwamba kitendo cha mwanaume kusugua uke kwa uume wake kwa kila aina za style ni tendo linalompa mwanamke raha ya mapenzi.

Ukweli si wanawake wote hufikishwa kileleni kwa uume kuwa ndani ya uke tu (clitoral and viginal stimulation) bali kwa mwili mzima kama single sex organ na pia kuandaliwa kwa muda unaotakiwa.

Jamii imezungukwa na tamaduni zinazofanya mwanamke kujiona akiwa na shape Fulani au size Fulani ndipo atafurahia sex kitu ambacho ni kweli kwani ili mwanamke afurahie sex kwanza lazima ajifahamu mwenyewe na kuufurahia mwili wake kama ulivyo kujiamini kuhusu self esteem na body image yake.

Kuna asilimia zaidi ya 50 ya wanawake huwadanganya waume zako kwamba wamefika kileleni kitu ambacho si kweli ili mambo yaishe.
Kwa nini wanadanganya?
kwa sababu wanaume wengi huwa hawawaandai vizuri so anaona afahadhari aone amefikishwa maana lengo la wanaume wengi huwa kumfikisha mwanaume kileleni na si kumpa raha ya mapenzi.

Kazi kwelikweli!

Tuesday, January 6, 2009

Divine nectar

Kama maji vile ila ni fluid (sweet smelling) inayotokana na mfumo urogenital pamoja na glands za prostatic za mwanamke.
Huitwa divine nectar au Amrita au the foutain of youth.
Wapo wanawake ambao akifika kileleni (G- spot stimulation) huweza kutoa fluid mfano wa mkojo kupitia urethra (gushing fluid), huwa na sweet smell, huweza kujaa hata kikombe cha chai na huruka umbali wa futi hata 8 na kugonga ukuta wa chumba.

Huu si mkojo na ni haki ya kuzaliwa ambayo mwanamke amepewa na muumba wake hasa linapokuja suala la kufurahia mapenzi na mumewe.
Pia haya maji maji huitwa Amrita au Divine Nectar, au Fountain of Youth huu si mkojo hata kama hutoka kupitia njia ya mkojo ya kawaida.

Hiki ni kitu cha kawaida kwa mwanamke yeyote ambaye anapata mapenzi ya kweli na kukubali hisia zake na kufahamu mwili wake unavyofanya kazi akisaidiana na mpenzi wake.
Hii divine nectar imefahamika pia huweza kutokea hata pale mwanamke akifurahi jambo lingine na si lazima iwe mapenzi tu.
Hujasikia mwanamke alifurahia jambo akacheka na kutoa machozi na kukojoa?

Kila mwanamke anayo potential ya kutoa amrita au divine nectar ila ni pale tu atakapojifunza ku-surrender mwenyewe na kuwa na furaha ya kweli.

Wataalamu wa mambo ya mahusiano ya kimapenzi wanandoa Caroline na Charles Muir wameweza kuhusanisha suala la sex kwamba ni kimwili, kihisia na kiroho.

Mwanamke huweza kufikishwa kileleni (orgasm) kimapenzi kwa kusisimuliwa kisimi (clitoris), uke au G- spot.
Tofauti ya mwanamke kufika kileleni kwa kuchezewa kisimi ni kwamba ile raha huja ghafla kama mwanaume anapofika kileleni (big bang) wakati kufika kileleni kwa uke au G-spot mwanamke hujisikia raha kama mawimbi (waves) kwenda mwili mzima.

Ndani ya uke sehemu ya juu ndani ya ukuta kati ya kufunguka kwa uke na cervix kuna eneo ambalo huitwa G spot na hili eneo liligunduliwa na Gynecologist Ernst Grafenberg mwaka 1944.

Hili eneo huweza kukua na kuhama ambalo wengi huliita ni sacred spot kwa mwanamke huweza kutunza kumbukumbu na hisia za kuumizwa (hurts and pains), infections, abortion, sexual abuse, magonjwa na kitendo cha kutotaka sex na kama hakuna healing huweza ku-shut down na kushindwa kutoa divine nectar.

Ili mwanamke aweze kutoa divine nectar ni lazima hili eneo liweze kuponywa au kuwa activated upya na mwanaume.
Activation hufanywa kwa mwanaume kumfanyia massage zaidi ya mwezi kwa kwa muda usiopungua nusu saa kila wakifanya mapenzi huku mwanaume akimpa wake au mpenzi wake gentle and compassionate love making.
Siku njema kwa leo!

Monday, January 5, 2009

Yanakuja yenyewe!

Kama madege yanavyotua na kuondoka ndivyo mawazo kuhusu sex huja yenyewe kwa mwanaume! Binadamu hawezi kuwa amekamilika akiwa kimwili na kiroho peke yake bila hisia (emotions).
Pia kuna tofauti kubwa sana namna mwanamke na mwanaume wanavyoweza kufanyia kazi emotions kwenye ubongo.

Bila kufahamu tofauti hizi kati ya mwanaume na mwanamke wakati mwingine hupelekea suala la mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume kuwa na matatizo hasa kutokana na upande mwingine kushindwa kuelewa mwenzake anahitaji nini au kitu gani na wakati gani.

Linapokuja suala la emotions mwanamke ana uwanja mkubwa sawa na barabara yenye uwezo wa kupitisha magari 8 kwa wakati mmoja (eight lanes super highway) wakati mwanaume ni sawa na barabara moja ya kwenda kijijini kiasi kwamba magari hata mawili kupishana ni kasheshe.

Hii ina maana kwamba kumkumbatia mwanamke huweza kumpa raha na msisimko wa ajabu kihisia na kumsikiliza akiongea humpa raha na kumpa ahuaeni kuliko kawaida.
Wakati mwanaume kuongea sana bila kutoa point kwa maneno machache anaona unampotezea muda wake.

Pia mwanamke huweza kukumbuka kutukanwa, au kupigwa na anaweza kukumbuka rangi ya chumba mlichokuwa wakati wa hilo vagi, shati mwanaume ulivaa, sura yako wakati mnapigana au kutukanana na siku, mwezi na mwaka kwa kuwa inahusishwa moja kwa moja na hisia zake kwenye hiyo super highway, wakati mwanaume anaweza akawa baadhi ya vitu hakumbuki.

Wanawake hupenda kuongea kuhusu hisia zao all the time.

Linapokuja suala la kuwaza kuhusu sex basi mwanaume huweza kuwaza kuhusu sex kila baada ya dakika mbili na mwanamke huweza kuwaza sex wengine ni siku kadhaa katika mwezi.
Je, ndo kusema mwanaume muda wote yupo kwenye foreplay na ndiyo maana huwa na dakika chake akikutana na mwanamke na kutaka kwenda south pole moja kwa moja kuchimba gold hata kabla mgodi haujawa tayari!

Kuingia na kutoka kwa mawazo kuhusu sex kwa mwanaume ni sawa na ndege zinavyoingia na kutoka katika International Airport kama vile Amsterdam, au London Heathrow na mwanamake ni kama kiwanja cha ndege kule Nduli - Iringa kiasi kwamba wakati mwingi ndege hata zikifika zinaweza zisitue hadi hali ya hewa iwe nzuri (hadi mwanamke akaribie kuwa fertile)

Hii ina maana kwa mwanaume mawazo kuhusu sex hutua kwa wingi kama madege makubwa kila baada ya dakika mbili (kutua na kuondoka) na mwanamke ni sawa na kiwanja kidogo ambapo ndege ndogo za mawazo ya sex (tena private jet) hutua kwa mwezi angalau siku chache tu au kwa siku mara moja.
Kwa mwanamke foreplay ni saa 24 kabla ya sex, wakati mwanaume foreplay ni dakika 3 kabla ya sex.
Hapa bila mwanaume kufahamu tofauti iliyopo na mwanamke mahusiano ya mapenzi huweza kuwa ya kuumiza au kutimiza wajibu tu.

Ndiyo maana linapokuja suala la kutaka sex mwanaume ndiye mara nyingi hulianzisha, ingawa hii haina maana kwamba mwanamke kama anataka sex kwa mumewe asubiri mume aanze.

Wanaume hupenda kutafakari kuhusu sex all the time.

Mengineyo!
Data zinaonesha kwamba wanawake wengi huvutiwa na wanaume ambao wamewazidi umri zaidi ya miaka miwili na kuendelea iia wanaume ambao ni warefu kidogo kuliko wanamke wenyewe ingawa wanawake wakiulizwa huwa wanaruka kimanga.

Pia wanawake wengi huvutiwa na mwanaume kwa sababu ya ukubwa wa wallet yake na reputation au status aliyonayo katika jamii na si sura, size, rangi au kitu chochote kwenye mwili wake.

New Year 2009

“Another fresh new year is here . . .
Another year to live!
To banish worry, doubt, and fear,
To love and laugh and give!

I have the opportunity
Once more to right some wrongs,
To pray for peace,
To plant a tree,
To love the unloved,
To think the unthinkable,
To pursue the impossible,
And sing more joyful songs!
And much more................."