"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, January 23, 2009

Checkup ya Ndoa 2009

Kama mahusiano yangekuwa yanaenda kwa daktari kupata vipimo je, ungepata Tick?
Huu ni mwaka 2009 naamini ni vizuri kujiangalia na kupata ukweli wa mahusiano yako unavyojisikia na je kuna dalili kwamba hali inakuwa nzuri au ndo mnaelekea ICU?
Jikague kwa kuangalia mambo yafuatayo then kwa uaminifu kabisa jiulize ni lipi kati ya haya bado unahitaji msaada.
Kumbuka mahusiano yakiwa mabaya unaweza kuhatarisha afya yako, utendaji wako wa kazi, kiroho chako, marafiki na hatimaye hisia zako na mwisho kufa mapema.
Jiulize hapa sasa!
Najisikia nipo huru, wazi na pia ni rahisi sana kuongea na mwenzangu kuhusu negative au positive feelings nilizzonazo.

Mwenzangu kawaida huwa hanisikilizi ninapoelezea hisia zangu.

Mara kwa mara namlalamikia, criticize, laumu mwenzangu hata kwa vitu ambavyo hajafanya.

Namwambia mwenzangu “Nakupenda” au nampa appreciation angalau kwa wiki mara moja.

Mara chache sana mimi na yeye kwa pamoja hulipuka na kuchukia pale mmoja anapoanza kutoa makosa kwa mwenzake.

Angalau kwa mwezi tunakuwa na mazungumzo si chini ya nusu saa kuongelea kutatua matatizo na migogoro inayojitokeza.

Mwaka uliopita hatukuweza kuwa na muda wa kuongea kuhusu mahusiano yetu katika tendo la ndoa
Ukweli kila mmoja ameridhika na mgawanyo wa kazi nyumbani.

Tumekuwa na maongezi bayana kuhusu kila mmoja anavyojisikia mapenzi nje ya ndoa.

Ni mara chache sana tunafikia muafaka tukianza kuzozana.

Kama nahitaji kumpa hisia ambazo anahitaji kwangu najua jinsi ya kufanya.

Tuponajaribu kutatua mgogoro ambao umejitokeza mara nyingi huishia kuamsha hata migogoro iliyipita.

Tunapokuwa kwenye tendo la ndoa wote huwa tunafika kileleni na kuridhika.

Tukigombana, ndani ya saa 24 tunakuwa tumeelewana na kuyamaliza.

Mambo ya kuzingatia ili ndoa mahusiano yako yawe ya kuridhisha na afya njema mwaka 2009.
Mawasiliano wazi (open communications) – uwezo wa kuongea kwa uwazi hisia zako za ndani tena kwa uhuru ziwe positive au negative.
Kuonesha kujali na upendo- je ni kitu gani kinamfanya mwenzako aone unampenda?
Mahaba na mapenzi – tendo la ndoa ambalo kila mmoja anaridhika, kutatua matatizo ya kitandani, kuridhika na tendo
Kutatua matatizo kwa ustadi – kutafuta jawabu kwa kila tatizo na si kuacha tatizo
Mgawanyo wa kazi – iwe ndani na nje ya nyumba kila mmoja aridhike na mgawanyo wa kazi.

Baadhi ya alama zinazoonesha kwamba una mahusiano yanayoridhisha ni:-
Unajisikia unapendwa
Unajisikia unaeleweka kwa mwenzio
Unajisikia unakubalika kwa mwenzio
Unajisikia yeye ni ukuta kukukinga na stress au maaduni wa kiroho na kimwili
Watoto wanakuwa sehemu yenu na si tatizo kwenu
Unajisikia salama kujieleza kihisia au unavyojisikia kuhusu kufanya mapenzi
Mna sehemu inaitwa "nyumbani" ambako ni kimbilio la kila mmoja kupata faraja na upendo hata kama ni nyumba ya kupanga.
Kristo ni namba moja katika maisha yako binafsi.

No comments: