"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, January 30, 2009

Funga vizuri

Hata kama ni mlango wa dhahabu kama haujafungwa wapo wanawake haijalishi huko chumbani kuna raha ajabu bado wazo la kwamba mlango upo wazi na haujafungwa linanata kichwani. Mwanaume anaweza kuongeza ladha ya mahaba kwa mke wake pale anapokuwa makini na suala la jiografia na ustadi wakati wa tendo la ndoa.
Wanawake ni viumbe ambao mara nyingi huwa distracted na mazingira waliyopo kuliko wanaume hasa linapokuja suala la faragha na usalama.

Wanawake huathirika zaidi na mazingira hasa sauti au kelele na harufu (smells) kuliko wanaume (mume) kwa wakiwa sita kwa sita, mfano hofu ya kwamba watoto watasikia hasa kama watoto wanapiga kelele,hofu ya kusikiwa na majirani au wapiti njia, hofu ya mlango kuwa haujafungwa (komeo) nk.

Mume mmoja alisafiri kwenda nchi za mbali na aliporudi nchini kwake na kupokelewa na mkewe walienda moja kwa moja nyumbani kwao na kwa kuwa hakukuwa na watoto au mtu mwingine bali wao wenyewe tu, wakaamua kwa raha zao wapeane zawadi ya miili yao kwanza kabla ya lolote kwa kuwa walikuwa na hamu kubwa kila mmoja kwa mwenzake, hata hivyo mlango walisahau kuufunga na baada ya kumaliza kupeana zawadi mke alimuuliza mume "hivi unakumbuka mlango hatukufunga?"
Hii ni ina maana gani? ni kuthibitissha kwamba muda wote wa tendo la ndoa mke alikuwa anawaza kwamba mlango haujafungwa na alikuwa anawaza hivi watoto wakirudi na kuingia moja kwa moja itakuwaje.
Mume yeye wala hakuwa na wazo hilo na wanaume wengi wapo hivyo.
Mwingine ana enjoy sex mwingine anawaza mlango haujafungwa!

Pia sijui inakuwaje tafiti nyingi zinaonesha wanaume wala huwa hawaogopi wapi ni salama kufanya tendo la ndoa.
Kwenye gari, bafuni, jikoni, sebuleni, chumbani, store, ofisini, kiwanjani, porini, makaburini na sehemu zingine unazozijua wewe.

Kuna nchi watu walikuwa wanaulizwa maeneo ambayo wamewahi kufanyia sex, ukweli majibu yaliyokuwa yanatoka yanatisha sana.


Tatizo kubwa lingine ambalo linaweza kuwa kizuizi cha kumpa hamu mke wakati wa tendo la ndoa ni wanaume kuwa wachafu au rough, au kutozingatia usafi.
Inawezekana wewe ni mwanaume unafanya kazi ambayo baada ya kazi unakuwa na majasho au unahitaji kuoga vizuri acha suala la kupiga mswaki na kuwa na kinywa kisicho na harufu.

Kucha chafu na mikono inayotisha hata unapomshika bibie na ngozi yake laini badala ya kusisimuka wewe unamuumiza na kumpa kinyaa kama si kichefuchefu.
Bahati mbaya na huko kazini uliona picha au mwanamke mrembo basi homoni nazo zikafanya kazi basi ummemkumbuka mkeo hivyo kufika nyumbani tu unataka.


Bila kujali usafi unamrukia mkeo na kwa kuwa anauwezo wa kunusa zaidi kuliko wewe unafanya a-palalyse kwa kuishiwa hamu kabisa na wewe matokeo yake na wewe unajisikia upo rejected.
Ukweli usafi ni jambo la msingi mno.
Cleanness is next to godliness

3 comments:

Anonymous said...

Kaka, Hii mimi mimeipenda kwani wengi wanahisi wanawake wapo kwa ajili ya kuwapa wao raha tu,yabidi watu wajiandae kwa kila jambo.wasimuache mungu wao kabla na baada ya kila shunguli kwani kupewa nguvu ulizotumia si mchezo, Mbarikiwe sana,
Msafiri

Anonymous said...

Upo sahihi' lo'

Ashura

Anonymous said...

Upo sahihi' lo'

Ashura