"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, January 21, 2009

Kusamehe

Kwa nini kusamehe? Kwa sababu ni faida kwako.

Kusamahe ni kitendo cha kupooza au kuacha kujisikia umekwazwa, au umekosewa au umeudhiwa au kuondoa hasira mwa mtu ambaye amekukosea.

Faida ya kusamehe imeelezwa sana katika dini, elimu ya sayansi na matibabu pia.
Wengi wamekosa kuponywa magonjwa makanisani kwa sababu wameshindwa kusamehe.
Wengine afaya zao zinazidi kuzolota kisa hawataki kusamahe wenzao
.

Watu wanaweza kutuumiza kwa njia nyingi zaidi ya milioni hata hivyo tunahitaji kuwasamehe, pia kusaheme wakati mwingine si rahisi kama wengi wanavyodhani hata hivyo inabidi kusamehe.
Wapo wanandoa wanalala mzungu wa nne kisa hawataki kusameheana, na wengine wamehama na chumba cha kulala kisa hataki kusamehe, sasa unajitesa nini kwani kuna mtu alikulazimisha kuoa au kuolewa?
Nini kujitesa na donge moyoni?
unajiona mjanja hata hivyo ukweli unajimaliza mwenyewe kiafya, kimwili na kiroho pia.
Hata hupendezi kabisa! looooooooooo

Anaweza kuwa aliyekuumiza au kukukwaza ni mume wako, mke wako, mdogo wako, boss wako kazini, mchungaji wako, polisi, mkwe wako, dada au kaka.
Hata hivyo kama vilivyo vitu vingi hasira kwa wengi ni is easier said than done.

Huwa inakuwa ngumu sana kusaheme hasa pale tunayetaka kumsamehe anaonekana hana sababu au hastahili kusamehewa.

Kwa nini kusamehe ni muhimu?
Kusaheme ni vizuri sana kwa moyon wako.
Kusaheme kuna uhusiano mkubwa na Blood pressure (BP) pamoja na kupunguza Stress hivyo kusamahe huweza kukupa faida kubwa sana kwa afya yako ya moyo.

Pia kusaheme kuna matokeo postitive na dalili za kimwili kiafya, dawa unazotumia (medication), kiwango cha usingizi, kuchoka na kulalamika.
Hii ina maana kwamba mtu asiyesamahe hupata matokeo negative kwa yaliyotajwa hapo juu.
Kusamahe huimarisha mahusiano na urafiki.

Kusamahe huimarisha roho ya kujitolea (volunteerism) na kuwa watoaji katika jamii.
Kusahamehe hupunguza uadui.
Kusamahe ni njia nzuri ya kujilinda na hasira.
Kusamehe hukuongezea kiroho chako na kujisikia vizuri mbele za Mungu
Kusamahe huimarisha saikolojia yako
Kusamehe hupunguza maumivu sugu
Kusamehe ni kukaribisha uponyaji wa mwili na roho

Forgiveness is choosing to love. It is the first skill of self-giving love.

Kusaheme ni kitu kizuri sana kwa mwili wako, mahusiano yako na mahali ulipo duniani hivyo achana na hasira za kutosamehe na badala yake samahe ili ufanye dunia mahali bora kuishi.

Wapo watu ambao husema anasamehe lakini hasahau, ukweli hasara ya kutosamehe ni kubwa sana kwa anayetakiwa kusamehe kuliko anayesamehewa.

In the Bible it says they asked Jesus how many times you should forgive, and he said 70 times 7.
Well, I want you all to know that I'm keeping a chart.
(Hillary Rodham Clinton)

2 comments:

Anonymous said...

Hah thats right brother'.
u know what ?
Forgiveness is very important in relationship.
Forgiveness is a choice to let resentment go.
We choose to accept and enjoy another person.
We choose to distill the helpful and positive out of the total experience of a relationship.

Ashura M
USA

Anonymous said...

Forgiving is a process on the hands of humain being but forgetting is another process which we can not force it.