"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, January 27, 2009

Ni kudanganyana

Kama ulivyo ni wewe jiamini na waweza kuwa vyovyote unataka na una haki ya kuzaliwa kufurahia tendo la ndoa bila kujali upoje. Jamii imezungukwa na tamaduni zinazofanya mwanamke kujiona akiwa na shape, size, uzito, rangi, lugha, cheo, elimu fulani ndipo atafurahia mapenzi na kuonekana mwanamke mrembo na anayetakiwa na wanaume katika jamii husika, huo ni uwongo na si kweli.

Pia jamii inawadanganya wanawake kwamba wakiwa vile au uzito fulani basi watakuwa wazuri kimapenzi, ukweli ni kwamba uwe mnene, uwe mwambamba, uwe mrefu au mfupi, mweupe au mweusi unaweza kuwa mzuri kwenye mapenzi.

Ukweli ni kwamba mwanamke mwenyewe akijiamini na kujiona ni mrembo (self esteem/ self image), urembo huanza na wewe mwenyewe kwenye ubongo, ukijiona sexy watu watakuona sexy vivyo hivyo ukijiona hufai watu watakukimbia.
"You are by what you think"

Naura Hayden aliwafanyia utafiti wanawake 486 kujua je wanaume hudanywa au huwa hawadanganywi linapokuja suala la kufika kileleni (orgasm).
310 Walikiri kwamba walikuwa wanawadanganya waume zao mara zote.
124 Walikuwa wanadanganya mara nyingi.
52 Walikuwa wanadanganya mara chache sana.

Hii ina maana gani?
Hii ina maana kwamba wanaume hudanganywa na wanawake kwamba wameweza kazi, kumbe …………………..

Pia jamii hasa wanaume hujidanganya kwamba (potoshwa) kwamba kitendo cha mwanaume kusugua uke kwa uume (intercourse) kwa kila aina ya style humpa mwanamke raha ya mapenzi kuliko mambo mengine kama kumuandaa na kufurahia foreplay nk kwa muda mrefu kuliko intercourse yenyewe.

Pia bado jamii inadanganywa kwamba sex ni usiku baada ya kazi na si mchana, matokeo yake mwanaume na mwanamke wanaoenda kazini na kuchoka na kazi huishia kufanya sex (tendo la ndoa) huku wamechoka na hakuna ladha.

Kwa nini msisubiri weekend mchana wakati upo safi mind, body and soul?
When you are tired, the libido goes away!

Wengine kama walichanjia hata mwanamke achoke vipi lazima atoe maana anaona ni kama birthright yake kuhakikisha ikiwa usiku tu lazima apewe.

Unapima quality ya tendo la ndoa kwa kufanya mara ngapi na si kuridhisha?
Usijidanganye!

No comments: