"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, January 9, 2009

Tunatumia ubongo tofauti

Je, kama unaendesha gari then ukamchomekea, kati ya mwanaume au mwanamke yupi utaambulia matusi chapchap? why!Mwanaume na mwanamke hufikiria tofauti hasa kutokana na jinsi ubongo unavyofanya kazi.
Mwanaume hutumia gray matter na wanawake hutumia white matter.
Pia wanaume hutumia upande mmoja wa ubongo wakati wanawake hutumia pande zote mbili za ubongo (kushoto na kulia)
MAWASILIANO
Kawaida mwanaume husikia nusu ya kile anaambiwa na mwanamke na hukumbuka nusu ya kile amekisikia kutoka kwa mwanamke na hurudia nusu ya kile anakumbuka.
Ubongo wa mwanaume hauwezi kushika na kujihusisha kwenye mambo ya kihisia kama mwanamke ndiyo maana mwanaume anaweza kuambiwa habari za ugonjwa, harusi, ajali hata kifo amwambie mkewe na akasahau na si mwanamke akiambiwa amwambie mumewe kusahau lazima atakumbuka na atakwambia.

Wanawake wana uwezo mkubwa sana kukumbuka jambo lolote la kihisia (emotions) kutokana na ubongo wao wa eneo la amygdela kuwa na uwezo kuliko wanaume.
Daktari Stephen Hamman (University of Toronto Canada) anasema kwamba mwanaume anaweza kupokea kwenye ubongo wake sawa na mwanamke ila ujumbe wake unakuwa mweupe bila hisia (emotions & feelings) kwani maana ya hisia hupotea na kuwa ujumbe mkavu tu.

MAUMIVU
Wanawake huwa na mwitikio mkubwa wa maumivu kuliko wanaume.
Katika utafiti (University college of London) watafiti walutumia Electric shock kwa wanawake kupima mwitikio wa maumivu na baadae wakawachukua waume zao na kuwafanyia the same thing na wanaume wakaambiwa wakawaambie wake zao kwamba waliteswa na electric shock matokeo yalionesha wale wanawake waliupokea ujumbe ule kwa maumivu sawa na waume zao walivyokuwa wanapata electric shock, Hii ina maana kuambiwa tu waliumia kama vile wapo kwenye mashine yenyewe.

TENDO LA NDOA/MAHABA
Kumbumbatia mwanamke kwa sekunde 20 huweza kuzalisha oxytocin ambayo humpa mwanamke muunganiko wa hisia.
Wanaume pia huzalisha oxytocin kwa affections na tenderness wanayotoa ila ubongo wao hupeleka hisia moja kwa moja kwenye sex au tendo lenyewe.
Sehemu inayohusika na mambo ya sex kwenye ubongo kwa mwanaume ni kumbwa mara mbili ya mwanamke.
Ndiyo sababu kwa kuona tu (acha kuwa uchi chumbani) ubongo wa mwanaume huanza kulipuka kwa sex.

KUFAHAMU MAZINGIRA
Wanaume ubongo wao una uwezo mkubwa sana kusoma ramani na kutumia mwelekeo (directions) wakati wenzao wanawake ni wazuri kutumia alama (landmark) kama majengo ili kukumbuka ramani zamahali.
Mfano mwanaume atakumbuka kwamba alipaki gari mlango wamagharibi wa Mall na mwanamke atakumbuka alipaki gari mlango wenye display ya mashati ya njano.

HASIRA
Wanaume hu-react haraka kwa kufoka kwa sababu homoni zao hutumia mzunguko mfupi kwenye kwenye ubongo.
Wanawake wakikasirishwa homoni hupitia njia ndefu ya kujipima kwanza (processing) ndipo afanye reaction.
Mwanamke hu-react kwa hofu na woga wa security yale kwanza ndiyo maana si sawa na mwanaume.
Ukitaka kuangalia chunguza dereva mwanamke na dereva mwanaume anapokutana na mtu anayemchomekea barabarani.

MSONGO WA MAWAZO
Mwanaume akiwa na stress mapigo ya moyo na BP hupanda na hu-react kwa haraka na msongo wa mawazo kuyeyuka.
Mwanamke akiwa katika siku zake huwa mtulivu kuliko wakati mwingine wowote linapokuja suala la msongo wa mawazo.
Pia mwanamke huweza kuondoa stress kwa kuongea na rafiki yake au mtu wa karibu au anayemwamini. Hivyo basi ili mwanaume ajisikia vizuri huweza kufoka chapchap na mwanamke ili ajisikie vizuri huongea na mtu anayemwamini au mtu wa karibu.

MIGOGORO
Wanaume si wepesi ku-maintain relationship hii ina maana kwamba wanaume wengi (si wote) ndiyo wagumu sana linapokuja suala la kutatua matatizo ya ndoa, wanawake hupenda sana yaishe.
Unakuwaje mwanaume akifumaniwa au inakuwaje mwanamke akifumaniwa?
Naamini unaweza kujua nani hapo atamsamehe au nani atafukuzwa kabisa.

4 comments:

Anonymous said...

Kaka Mbilinyi, NIMEKUELEWA Vizuri sana na mada yako ila utata kidogo hapo?
Je yawezekana mwanamke ana akili nyimgi kuliko mwanaume? Je kama ni kweli mbona huwa wepesi sana kurubuniwa na wanaume na kujikuta wanajutia badae? Nini hasa HAPO? Have a nice weekend,Mungu akubariki its me Msafiri

Lazarus Mbilinyi said...

Mwanamke na mwanaume wana akili tofauti ila linapokuja suala la mapenzi ni kweli mwanamke huwa victim wa kudanganywa kuliko mwanaume hata hivyo pia mwanaume huwa anashangaza sana kwa tabia zake za kubaka hadi watoto.
Mwanamke huathirika sana na maneno mwanaume anaongea wakati mwanaume huathiriwa sana na kile anaona.
Kitu cha msingi ni kwamba kuna tofauti sana kimwili, kihisia na kiroho kati ya mwanaume na mwanamke.

Anonymous said...

Kaka mbilinyi nashukuru sana kwa Hili ila napenda kusema kusema kuwa wale wanaume wanaobaka watoto nazani si hisia tu za mapenzi bali yawezekana pia kukawa na imani za kishirikina au kuchanganyikiwa hayo ni mawazo tu. Ni mimi Msafiri.

Anonymous said...

Kawaida mwanaume husikia nusu ya kile anaambiwa na mwanamke na hukumbuka nusu ya kile amekisikia kutoka kwa mwanamke na hurudia nusu ya kile anakumbuka.
Ubongo wa mwanaume hauwezi kushika na kujihusisha kwenye mambo ya kihisia kama mwanamke ndiyo maana mwanaume anaweza kuambiwa habari za ugonjwa, harusi, ajali hata kifo amwambie mkewe na akasahau na si mwanamke akiambiwa amwambie mumewe kusahau lazima atakumbuka na atakwambia.

Wanawake wana uwezo mkubwa sana kukumbuka jambo lolote la kihisia (emotions) kutokana na ubongo wao wa eneo la amygdela kuwa na uwezo kuliko wanaume.


Salama kaka?. Yani hayo maneno hapo juu ni ya kweli kabisa na nimeyathibitisha kwasababu jana mke wangu ktk kuongea nilishangaa alinikumbusha vitu vya zamani sana ambavyo mimi nilikua navisema juu juu tu kumbe mwenzangu anatunza kumbukumbu si kawaida. Kuanzia sasa nimejifunza kua makini sana na kauli zangu kwake.

Asante kaka endelea kutuelimisha.

Mdau Jesse,
Dar es salaam.