"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, January 12, 2009

Ufundi, uhodari, ustadi wa kutatua matatizo ya Ndoa

Wapo wanandoa ambao ni kama hua, hata audhiwe vipi anabaki kimya anaogopa asije akasababisha mwenzake kukasirika au kuzozana.
Wengine ni mwewe kitu kidogo tu ni kuzozana hadi yaishe.
Wewe je ni mwewe au hua? MAWASILIANO YALIYO WEZA.
Wanandoa lazima waongee kwa uhakika wao wenyewe kila mmoja kwa mwenzake kuelezea hisia za ndani kabisa na kila mwanandoa lazima amtie moyo (encourage) mwenzake.

KUONESHA UPENDO WA KWELI NA KUJALI
Wanandoa lazima wawe na uwezo wa kuonesha upendo na kujali mwenzake hasa ili kuzuia hali ya kuzolota tabia ya kupenda mwenzake kila wanapoendelea na maisha na kuishi.

MAPENZI NA FARAGHA
Wanandoa ni muhimu kila wakati kuchochea mahusiano ya tendo la ndoa linaloridhisha ili kuwa na mahusiano imara na wawili kuwa na faragha pamoja (intimate partnership)

KUTATUA MATATIZO NA MIGOGORO.
Wanandoa ni muhimu kuwa na ustadi, au busara au hekima na uwezo wa juu sana kumaliza migogoro au tatizo au tofauti yoyote inapojitokeza haraka iwezekanavyo.

KUYAMALIZA
Pia ni muhimu sana kwa wanandoa kuwa na hekima ya kujua jinsi ya kumaliza mgogoro kuliko kwenda sambamba kila mmoja bila kuridhika na uamuzi wa mwenzake, kama mmoja amekosa basi akubali amekosa hata kama wewe ni mwanaume na jamii inakuona kama waziri au mbunge au kiongozi mkubwa kwani ndani ya nyumba wote ni kitu kimoja.

MGAWANYO WA KAZI
Katika ulimwengu wa sasa ambao wanawake na wanaume wote huondoka asubuhi au muda wowote kwenda kuwinda kwa ajili ya mkate wa familia bila kuwa na mgawanyo mzuri wa kazi nyumbani mmoja huweza kulemewa na zaidi kuzusha migogoro mingine.
Hivyo basi wanandoa lazima wawe wanagawana kazi na kusaidiana vizuri na kila mmoja kumtanguliza mwenzake.

JINSI YA KUZOZANA
Ni vizuri kila mmoja kutoa dukuduku alilonalo au kama kuna kitu kinamuudhi au kinamsumbua au haridhiki nacho kwa mwenzake ni vizuri kukiweka mezani na kikamalizwa kwa kujadiliana kuliko kukaa na donge moyoni huku unaangamiza na afaya yako.
Wapo wanandoa ambao hata kama kuna jambo gumu limamuumiza hayupo tayari kumuuliza mwenzake kwa kuogopa wasije wakaanza kuzozana au kuogopa mwenzake asije akakasirika. Ukweli ni kwamba afadhari umwambie akasirike na muyamalize kuliko kukaa nalo moyoni.

4 comments:

Fikirikwanza said...

kama hakuna mizozano hakuna maendeleo na kaa hakuna tofauti ni the same hakuna maendeleo.
tatizo ni namna ya kutatua !

Anonymous said...

mbilinyi nina swali,
nimesikia kuwa ukiwa mbali na mkeo,mpz nk kwamuda labda miaka 5.mtapokutana mnakuwa hamna hamu na mwenzie?napia knakuwa hakuna mapenzi kabisa unamwona mwenzio kama dada au kaka yako.ni ya kweli hayo

Anonymous said...

Asante saan kwa ujumbe mzuri.upo sahihi kaka' mungu akubariki.endeleza ushauri..tunakutegemea mwana Njombe.
Daidiyo hapa shyrose-

Lazarus Mbilinyi said...

Aliyeuliza kuishi mbali ya mke miaka 5 na matokeo yake.
Kwanza inatokana na mawasiliano kati ya mke na mume kwa miaka mitano yapoje.
Kama mawasiliano mazuri naamini siku ya kuonana lazima mwanamke atoe divine nectar kwa kumfurahia mpenzi wake aliyekuwa mbali miaka 5.
Kwenye mapenzi ya kweli kuna kuvumiliana bila kujali ni muda gani hasa kama aliyewaumba anakuwa msingi wa kuimarisha mapenzi yao.

Upendo huvumilia na ukweli kukaa miaka 5 bila mwenzake naamini siku wakikutana kama kila mmoja alikuwa mwaminifu na alivumilia mwenzake itakuwa ni kama honeymoon mpya kwao.

Sidhani kama haiwezi kuwezekana kama kuna upendo wa kweli.

Kama wachumba wanaweza je mke na mume ambao wameshakubaliana mbele za Mungu kuwa mke na mume.


Upendo daima