"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, February 28, 2009

Dada Julia Eisele akionesha moyo wa upendo kwa watoto huku Tanzania God gave us two ears to hear,
two eyes to see and two hands to hold.
But why did God give us only one heart?

Because he wants us to find the other one.

Friday, February 27, 2009

Ni kujituma!

Unaweza kuanza vizuri katika mahusiano usipoweka jitihada zinazotakiwa inaweza kuwa kazi ngumu kama kuponda kokoto! "Any fool can fall in love, it takes wisdom to stay in love".

Ukimuuliza mtu yeyote ambaye anaanza kazi katika taaluma mpya kwa mfano Daktari, injinia, mwanafunzi, polisi, rubani, Nahodha nk; kwamba kazi au taalumu anayoingia inahitaji kuiitoa na kufanya kazi kwa kujituma kila au kazi inayoingia ni demanding bila shaka atakubali.

Lakini ukimuuliza mke mtarajaiwa au mume mtarajiwa kwenye ndoa kwamba taalumu anayoingia ni demanding (kwa maana kwamba inahitaji kujitoa kila siku na kwamba ni kuweka juhudi kila siku ili kupata matokeo mapya; ataona kama vile unafanya utani au unamuonea wivu kwani mapenzi waliyonayo ni kama maji kwenye mtelemko hivyo hakuhitaji efforts zozote ili penzi lidumu miaka na miaka.

Hii haina maana kwamba ndoa ni ngumu sana kiasi kwamba kama unataka kuolewa uogope bali ni kutoa msisitizo kwamba kuingia kwenye ndoa bila kuwa na ujuzi unaotakiwa au kutojua kwamba unatakiwa kufanya kitu gani inaweza kuwa disaster.

Ndoa si jambo ambalo ni effortless, kama muhusika iwe mke au mume unahitaji kuwa na mipango, kuhangaika, kuvumilia, fanyia kazi kila jambo linalojitokeza, kusahau ukisamehe, kuelekeza nguvu katika upande wa mambo mazuri.

Hata kama mmeoana na kujiona duniani hakuna watu ambao wamewahi kupendana kama ninyi bado katika safari ya maisha ya mahusiano ya ndoa ipo siku mambo hayatakuwa kama uynavyotarajia kwani wewe ni binadamu na umezaliwa mazingira tofauti nay eye hivyo ipo siku mambo hayatakuwa sawa.

Mara nyingi upendo huzaa ndoa njema hata hivyo kuna wakati ukiwa kwenye ndoa hata kama unajisikia hakuna upendo ipo siku ndoa huweza kuzaa upendo hasa kama wote mnafanya juhudi kuhakikisha unatia juhudi kwenye hii taalumu ya ndoa.
Wapo watu ambao wakati wanaoana hakukuwa na upendo mkubwa kama wewe hata hivyo kutokana na kujiweka sana katika taaluma hii ya ndoa matokeo yake ndoa imekuwa imara na yenye upendo wa ajabu.

Wapo walioingia kwenye ndoa kwa madaha na kujiona hakuna wanandoa wanaopendana kama wao hata hivyo baada ya kubweteka sasa ndoa inashikiriwa na uzi mwembamba sana ni kama vile ipo ICU hata hivyo juhudi zozote za kufufua ndoa huzaa matunda hasa pale kila mmoja akielekeza nguvu kwenye positive side.
Kwenye balance sheet ya ndoa siku zote tunaelekeza nguvu upande wa faida au positive au yale mambo yanayofanya ndoa isimame si hasara au mambao ambayo unahisi hayakupi kuridhika.

Ukitaka kuwa na balance sheet ya ndoa yenye bonding strong fanya yafuatayo kwa mpenzi wako
Tabasamu huku ukimwangalia usoni
Mshike au gusana naye (ngozi kwa ngozi)
Mfanyie kitu chochote kizuri bila kuombwa
Kumsifia kwa kitu kizuri amefanya huku unatabasamu
Kuangaliana usoni kwa kuangaliana usoni zaidi ya dakika 3
Kumsikiliza mwenzako kwa makini huku ukirudia kile anakwambia,
Kumsamehe leo kesho na zamani,
Mwandalie chochote ale,

Pumua kwa pamoja au weka kichwa kwa moyo wake na sikiliza mapigo ya moyo wake,
Mbusu kwa midomo na ulimi,
Kushikana zaidi ya dakika kumi,
Kumpa massage kwa lengo la kumfariji hasa miguu, mabega na kichwa,
Kumkumbatia kwa maana ya kumfariji (hii ni two-edged sword),

Kumgusa na kunyonya chuchu na matiti,
Kuweka mkono kule chini kwa mpenzi wako kwa lengo la kumfariji,
Kwenda kulala wakati mmoja hata kama baadae utaamka kwena kufanya kazi,
Uwe na hamu ya kutaka mpenzi wako akijisikie raha na karibu na wewe
.

Mengine unayajua wewe!

Thursday, February 26, 2009

Macho!

Tangu siku tulipoingia katika dunia hii tulifungua macho yalitutuwezesha kuona, kuelewa na kuwasiliana na ulimwengu.

Macho hukuwezesha kutoa machozi wakati ukijisikia kulia na hukuwezesha kuona vitu vya karibu na vile vya mbali kadri ya upeo wa macho yako.

Kitu cha thamani sana kwenye uso wako ni macho, pia kuona ni zawadi ambayo wengi hatuoni thamani yake hata hivyo huwa tunakumbuka thamani ya macho pale tunapokutana na mtu asiyeona yaani kipofu.

Macho huweza kubeba uwezo wa ajabu waingereza anasema ni sexual symbol that opens window to the soul.

Macho yana nguvu ya ajabu huweza kufungua moyo na maisha.
Nafsi ya mtu ipo kwenye macho na ni gateway kuelekea kwenye moyo wa mtu.

Mapenzi nayo yana uhusiano mkubwa na macho, hisia za mapenzi katika mwili hupitia njia nyembamba na laini iitwayo macho.

Macho kuelezea ukweli ambao ulimi wakati mwingine hushindwa kutamka.
Asilimia 80 ya nguvu ambazo tunazielekeza kwa wengine hupitia kwenye macho yetu.
Binadamu ana kawaida (nature) kukwepesha macho hasa pale kama haongei ukweli au pale anapoona hajisikii vizuri.
Watu wakiwa na hofu au kutojisikia vizuri huwa na tabia ya kuangalia pembeni.
Kama unataka kugundua je macho yanauwezo kiasi gani basi leo ukikutana na mpenzi wako mwangalie kwa kutumia macho yako kwa muda zaidi dakika 2 bila kukwepesha ukimpa tabasamu linaloendana na unavyochezesha macho huku ukichunguza nafsi yake na uzuri wake (kimwili) hakikisha mawazo yako na hisia zako unaelekeza jinsi unavyojisikia kwa mpenzi wako. (akikuuliza mwambie "nakupenda")

Ukweli ni kwamba utapokea kitu katika hisia zako na kwamba macho ni silaha muhimu sana kwenye mapenzi kwa wapendanao.
Jicho ni taa ya mwili.
Kama jicho lako ni nyofu, mwili wako wote utakuwa na nuru
Mathayo 6:22

Monday, February 23, 2009

Tunapenda muwe hivi!

Kila mwanamke huwa na ndoto za kufanikiwa maisha;
kuwa na familia, kuwa na mume ambaye atampenda maisha yake yote nk Ni hakika wanawake ni tofauti na wanaume, inawezekana hilo umelijua, kuna mambo ambayo wanaume hufanya kitandani na kumfanya mwanamke ajione ni mwenye furaha duniani na pia kuna wakati kuna mambo yanafanywa na wanaume kitandani na hupelekea mwanamke kujuta na kuumizwa hisia zake.
Mambo yafuatayo ni muhimu sana kuzingatiwa na mwanaume akiwa chumbani kwani wanawake wengi wanakiri kwamba mambo madogo kama haya wakati mwingine huwafanya kujisikia vibaya hasa linapokuja suala la mahaba.

USAFI
Kuwa msafi ni msingi wa mambo yote kitandani, ni vizuri kuoga kabla ya kulala hata kama kuna matatizo ya maji lazima uweke bajeti yako vizuri kuhakikisha unaoga kabla ya kurukia kitandani.
Usafi ni pamoja na sehemu zote za mwili wako, mikono safi na kucha zilizopunguzwa vizuri, pia kunyoa ndevu vizuri, kuna wakati kidevu kikigusa mwili wa mwanamke humkwaruza na kumuumiza, labda uwe na mke anayependa kidevu kama kile cha Osama.
Pia wapo wanaume ambao huvuta sigara na bila kuwa makini huingia chumbani na harufu ya sigara huku midomo inanuka, hapo unaharibu kila kitu.
Cleanness is second to Godliness
KUWEPO
Ni vizuri kuwepo kwenye tendo lenyewe na mhusika mwenyewe kiroho, kimwili na kiakili, kama upo kwenye tendo la ndoa mwanamke hujisikia vizuri kwa kuwa utashirikiana na mwanamke kwa kila hatua na atajiona ni sehemu ya utendaji.
Tamka jina lake, tamka maneno mazuri na kuonekana upo na yeye isiwe kama vile wewe upo na mashine fulani ya kukupa raha.
Pia wapo ambao anaanza then anaacha (anajibrekisha), mwanamke ni tofauti na mwanaume hivyo basi kama utaacha ujue lazima ukaanze square one from scratch.
Pia wapo wanaume wanajua kabisa mwanamke ni umbo dogo na yeye mwanaume ni umbo kubwa, sasa ukimlalia na kuendelea na shughuli bila kujua hapo chini anaendeleaje si anaweza akashindwa hata kupumua, wewe kuwepo ni pamoja na kujua na kumsoma anauonaje muziki wenyewe.

MAANDALIZI HUANZA TANGU NGUO ZIMEVALIWA.
Mwanaume unahitaji kuanza kumuandaa mwanamke tangu mapema (kisaokolojia) tangu asubuhi mnaamka, mchana kwa kuwasiliana, jioni kwa kuwa pamoja, then chumbani ni mahali ambapo mnamalizia mission ya siku nzima tena kwa kila mmoja kumvua mwenzake nguo (siyo lazima ila yasiwe mazoea).
Kuna raha mtu kubaki na nguo za ndani tu, na pia kuna raha kuwa naked, kila kitu kina raha yake.

KUFANYA VILEVILE NA KUACHANA NA SEHEMU ZINGINE ZA MWILI WAKE
Uwe makini kuangukia kwenye utaratibu wa ratiba ya kila siku kitu kilekile wimbo uleule, mziki ule ule na mwimbaji yuleyule.
Una mbusu, unachezea matiti then penetration, huna time hadi chumbani? makubwa!
Ukifanya hivi kwa kuzoea basi mwanamke atajisikia bored.
Unahitaji kuwa mbunifu na mtundu kujua sehemu zingine ambazo anaweza kusisimka na ukampa utamu mpya wa tofauti.
Even an old dog can learn new tricks.
Na kuna wengine hata kukiss hakuna kila siku yeye ni kurukia tu.

KUWA BUBU
Hata kama wewe ni bubu naturally linapokuja suala la mahaba unahitaji kuongea lugha unayoijua wewe ambayo itaonesha unampa appreciation kwa juhudi ambayo mke wako anafanya wakati wa tendo la ndoa.
Kama anakuuliza au anakuomba uwe unaongea ni vizuri sana ukawa unaongea wakati wa mahaba kwani kuna raha yake na utamu wake.

Kumbuka kwamba mwanamke kuathirika sana na maneno ambayo mwanaume anaongea ndiyo maana linapokuja suala la kudanganywa wanawake wengi (si wote) ni rahisi sana, hivyo basi mwanaume anayeongea wakati wa mahaba ana raha yake kwa mwanamke.
Ila uwe na kiasi usiwe unaongea tu kama radio za FM.
Pia kuna wanawake huwa wanapenda kusikia dirty words (maneno matamu) na wengine hawapendi kabisa so uwe makini na mke wako kama anapenda mpe na kama hapendi achana kabisa.

KUCHEZA RAFU
Uwe mstaarabu kwani tendo la ndoa si vita.
Hakuna mwanamke anapenda matiti yake yachezewe ovyo kwa kunyumbuliwa huko na huko kama vile unataka kuyanyofoa, pia chuchu zisibonyezwe kama vile unafungua radio ya Mkulima hasa huko Iringa mchana radio huwa hazishiki so ubonyeza tu hadi radio ikome, fanya taraatibu, pia hata kama anakuruhusu upeleke mkono wako hapo chini basi fanya kila kitu kwa uangalifu ili usimuumize.
Kama unafanya vizuri utajua na kama anahitaji mgandamizo zaidi (pressure) atakwambia hata kama ni aina ya mwanamke anayependa rough sex atakwambia tu, kwani mambo ya sex ni ya ajabu sana na yana vituko vya kila aina.
Hujasikia watu wanatukana matusi mazito wakifika kileleni?
Pia wapo ambao hufanya kama vile wapo kwenye mbio za Olympic na kujaza kama vile kuna mashindano ya hydraulic mashines.
Fanya kwa taratibu na wote mtapata utamu zaidi.

KUMALIZA MAPEMA
Kama ni mwanaume ambaye unamaliza mapema ni muhimu kuchukua tahadhari na kujifunza jinsi ya kuchelewa kumaliza mapema kwani mara nyingi mwanaume akimaliza mapema mwanamke hukatizwa utamu na anakuwa hana jinsi.
Ni vizuri kutumia utundu wako kumfikisha kileleni yeye kwanza kabla yako.

KUCHELEWA KUMALIZA
Wapo wanaume ambao hubaki wamedinda masaa na wakati huohuo mke amesharidhikaka, kitu ambacho hupelekea mchezo mzima kuwa gwaride na mwanamke humalizwa energy na kuanza kutokuwa na hamu ya tendo kila akikumbuka urefu wa gwaride alilopewa.
Ni vizuri kuwa makini kusoma saikolojia na mwendo wa tendo lenyewe ili kujua gia unayotakiwa kuweka ili kufika pamoja katika kituo cha basi kinachotakiwa.
KUTOKUSHUKURU
Mwanamke anahitaji kupewa credits kwa kazi aliyofanya, unahitaji kumshukuru, sema asante kwa hudumu yake na ili uwe mwanzo wa huduma nyingine bora zaidi.
Hujasikia tendo la ndoa ni dawa, na kama ni dawa maana yake amekupa tiba ndiyo maana hata ukiwa kazini unachangamka kwa sababu unapata kitu kizuri kwa mke wako, hivyo anastahili kupewa asante.
Shukuru kwa kila jambo!

Saturday, February 21, 2009

Weekend Njema

“Women need a reason to have sex;
men just need a place”.
Bill Crystal

Thursday, February 19, 2009

Little girl and her father were crossing a bridge.
The father was kind of scared so he asked his little daughter,
'Sweetheart, please hold my hand so that you don't fall into the river.'
The little girl said,
'No, Dad. You hold my hand.' 'What's the difference?'
Asked the puzzled father.
'There's a big difference,' replied the little girl.
'If I hold your hand and something happens to me, chances are that I may let your hand go.
But if you hold my hand, I know for sure that no matter what happens, you will never let my hand go.'
In any relationship, the essence of trust is not in its bind,
but in its bond.
So hold the hand of the person who loves you rather than expecting them to hold yours...
This message is too short......but carries a lot of Feelings.

Watoto wao wapo wazi,
Lily na Emmanuel sijui walikuwa wanaongea nini!
Je, kuna tofauti gani urafiki (friendship) na mahusuno(relationship)?
Wengi tunaamini urafiki ukiwa strong hupekea watu kuwa na mahusiano kwa watu wa jinsia tofauti?

Hata hivyo kuna kitu cha ajabu hapa, fikiria aina ya maongezi unakuwa nayo kwa mtu ambaye mna urafiki na maongezi unakuwa nayo kwa mtu ambaye una mahusiano (mpenzi0).
Kwa rafiki yako unakuwa mwepesi kueleza wazi kabisa mapungufu yako na kushindwa kwako, huoni aibu kuongelea matatizo yako na unaona rahisi sana kumuuliza maswali na unamuomba huyo rafiki akusaidie kuyatatua.

Kwenye urafiki (deep) tunategemea utajua kila kitu kuhusu yeye hata siri kubwa kubwa iwe mbaya au nzuri, ziwe za mafanikio au kushindwa.

Linapokuja suala la mahusiano binadamu wana tabia ya ajabu ambayo ni kutunza siri kutoka kwa mtu ambaye ana mahusiano naye, hatupendi kumwambia kuhusu failures tulizonazo, tunatunza siri kwenye sana bila partners kujua.
Kwenye urafiki tunakuwa kama watoto wadogo na kwenye mahusiano tunakuwa kama watu wazima, tunapokuwa kwenye mahusiano kila tunachofanya kwanza lazima calculations zifanyike wakati kwenye urafiki tunakuwa wazi kabisa kujiachia kwa mazuri na mabaya kwa kushinda na kushindwa, tupo wazi.

Inaonekana kwamba kuweka mipaka katika mahusiano na kutoongea chochote huwezesha nahusiano kudumu kuliko kuwa huru kuongea udhaifu kama kwenye urafiki.

Hata hivyo binafsi naamini mahusiano ya kweli ni pamoja na kujiweka huru kwa mwenzako kufahamu uzuri na ubaya, jinsi unavyoweza na jinsi unavyoshindwa.

Sijui wewe unasemaje kitendo cha kuwa huru sana kwa rafiki yako kuliko mpenzi wako?

Tuesday, February 17, 2009

Je, ni kweli?

Mwanamke mnene hubaguliwa zaidi kuliko mwanaume mnene, mwanamke akianza kunenepa haichukui raundi watu kuanza kumnyanyapaa au kumpa maneno ya kibaguzi, wakati mwanaume huendelea kupeta kwa muda zaidi.
Jamii huwavumilia sana wanaume wanene kuliko wanawake wanene.

Wanawake huweza kukumbuka sura (uso) ya mtu kuliko wanaume.
Pia wanawake huweza kukumbuka sura (uso) za wanawake wenzao kuliko wanaume.

Wanawake wenye rika moja huchokana mapema zaidi kuliko wanaume wa rika moja.
Kwa mfano wanawake wawili waliopanga chumba kimoja huweza kuishi pamoja kwa muda mfupi kuliko wananaume wanaishi chumba kimoja cha kupanga.

Wanawake ni wazuri sana katika kukumbuka nguo (pamba) na wanaume ni wakali kukumbuka magari na silaha.

Wanawake huota ndoto mbaya mara nyingi zaidi kuliko wanaume, hii inatokana na kupishana kwa kiwango cha joto la mwili na homoni wakati wa usiku ambapo wanawake hutokea mara nyingi zaidi kuliko wanaume.
Pia wataalamu wanasema kwamba wanawake huwa wagumu sana kuachana na hisia walizokuwa nao kabla ya kulala matokeo yake wakilala huota kuna mtu anawawinda au anawakimbiza au amepoteza wazazi au watoto na hata kujikuta amepotea na kuwa mazingira asiyoyajua.
Pia critics wanasema kwamba si kwamba wanawake huota ndoto mbaya kuliko wanaume bali wao ndo hukumbuka zaidi ndoto zao kuliko wanaume.

Si kweli kwamba wanawake ni waoga kuliko wanaume, wanawake huonekana ni waoga kuliko wanaume hasa kutokana na jinsi wanavyojieleza au wanavyowakilisha woga wao.
Wanawake ni watu wa hisia zaidi hivyo wakati mwingine huonekana ni waoga kuliko wanaume kitu ambacho si kweli ni hisia tu na huruma.

Monday, February 16, 2009

Kukaliwa

Huyu Bwana naye sijui kakaliwa!
hapo anamuaga mkee Airport moja hivi hapa duniani! Nimepata email hii na nikajifunza kitu na kucheka, wewe mwenzangu una maoni gani kuhusiana na hili hasa kwenye jamii zetu za kitanzania?
If KUKALIWA is to allow your wife to be a partner and participant in formulating the family matters, then I support it, becoz women are wiser spenders than men.

If KUKALIWA means that the family money is used by Mama Watoto to purchase stuff in Kariakoo rather than be drunk by the husband RIVERSIDE then I support that men be KALIWAD.

If a KALIWAD husband is one who won’t spend ALL the month's wages with
DOGO DOGO or at KITIMOTO Bar (while his KIDS starve) then HOORAY to
all KALIWAD husbands.

If KUKALIWA means that you are a partner to your wife, that she is your
best friend, and has a higher priority than your drinking buddies then
HOORAY to all KALIWAD husbands.

If KUKALIWA means that a HUSBAND spends quality time with his wife and
kids, instead of engaging in dubious investments where he is CONNED then;
"Watu wakaliwe forever".

If KUKALIWA means that when your wife is SICK you help her with work,
that when she is overburdened you extend a helping hand then LONG LIVE
Kukaliwa.

If KUKALIWA means that you DON'T BEAT UP your wife that you don't kick
doors when you are drunk then LONG LIVE Kukaliwa.

If KUKALIWA means that you treat your wife as a human being that you are
polite, don't bark at her like a dog, DONT growl at her like a hyena, consider that after work she is as stressed as you are then VIVA KUKALIWA.

If KUKALIWA means that you are at home after work, and that your wife
and kids are your next of KIN then HONGERA WALE WOTE WALIOKALIWA. Na ukae hivyo hivyo!


“KAMA UMEKALIWA NAMNA HII UNASTAHILI KUITWA
MWANAUME!!”

Source: Email

There is only one Happiness in Life,
to Love and be Loved.
- George Sand -

Saturday, February 14, 2009

Mtoto awa baba

Alfie ambaye ni mvulana mwenye sura ya kitoto bado na anayeonekana kama mwenye miaka 8 amekuwa baba baada ya rafiki yake wa kike jina Chantele Steadman ambaye ana miaka 15 kuzaa mtoto mwenye uzito paundi 7.3, motto anaitwa Maisie Roxanne.


Huyu baba mtoto anasema kwamba ilipofahamika kwamba Chantele ni mjamzito hawakukubali kutoa mamba na badala yake yeye aliona ni vizuri kuwa na mtoto. Ingawa hakujua itakuwaje kwani baba yake naye ana watoto tisa na hana kazi maalumu hivyo si mara zote hupata pocket money na hata akipata hupokea £10.


Waziri mkuu wa Uingereza Bwana Gordon Brown aliingia mitini kutoa maoni kuhusiana na hii issue ingawa amekiri kwamba serikali inatakiwa kujitahidi kuhusiana na mamba za teenagers.

Hi si mara ya kwanza kwa watoto kuzaa watoto nchini Uingereza kwani mwaka 1998 Sean Stewart (12) alizaa na rafiki yake wa kike Emma Webster (15) ingawa walikuja kutengena baada ya miezi 6 tu.
Huyu Bwana mdogo hujui hata nepi inauzwa kiasi gani na itabidi asahau kidogo kwenda kucheza Game na ajikite kumaliza shule na kuwa baba mzuri.

Je, hapa wa kulaumiwa ni nani, hawa watoto au wazazi au jamii?


Source:
http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/news/article2233878.ece

Friday, February 13, 2009

Weekend Njema!

“Without question the future of a nation depends on how it sees its women”

Kupata Mimba


Wengi hasa wanawake wamekuwa wakiuliza maswali mengi sana kuhusuana na jinsi ya mwanamke kupata mimba au kuzuia kutopata mimba.
Naamini maelezo yafuatayo ukisoma kwa makini unaweza kupata ufahamu na kujibiwa maswali yako yote ambayo yamekuwa yanakutatiza.

Pia ni vizuri kuzingatia na kutochanganya Kalenda ya menstrual cycle tunayoongelea hapa na ile 'kalenda ya mwaka' inayohusu tarehe za miezi 12 ya mwaka ambayo huwa tunaitundika ukutani huko nyumbani na maofisini kwetu!

Wanawake wamegawanyika katika makundi makubwa 4 linapokuja suala la siku za hedhi
Mzunguko mfupi yaani siku 22
Mzunguko wa kati yaani siku 28
Mzunguko mrefu yaani siku 35
Na mzunguko abnormal siku 15

Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavo:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd.
Kisha ahesabu kuanzia ile 22nd day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 8th day ya kalenda yake.
Hivyo 8th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 22.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!
Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavo:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 14th day.
Inamaana kwamba 14th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 28.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!
Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavo:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th, 29th, 30th, 31st, 32nd, 33rd, 34th, 35th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 35th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 21st day.
Inamaana kwamba 21st day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 35.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!
Kama mwanamke ana abnormal menstruation cycle ya siku 15
BASI KUNAUWEZEKANO WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama kawaida:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 15th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 1st day.
Inamaana kwamba, the 1st day of her bleeding ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 15.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed, na ndiyo hiyo hiyo siku ambayo mwanamke wa kundi hili anaweza kupata mimba!
Hii inamaana kwamba, siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa.
Mwanamke wa aina hii anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kubleed, kwani siku ambayo yai moja linaanza kuharibika ndio siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linakuwa tayari kurutubishwa
Na wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au ku-feel ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa kurutubishwa, kwani ute wa wanawake wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu kwa vile unatoka siku ile ile wanapoanza ku-bleed.Pia wanawake wa kundi hili huwa wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu na bleed hukatika ndani ya siku moja au mbili tu!

NB:
Mwenye uwezo wa kuhakikisha mwanamke anapata mimba ni Mungu mwenyewe, unaweza kutumia njia zote na kila uwezo wa kibinadamu nab ado mimba isitokee au unaweza kuzuia kwa njia zote na mimba bado ikapatikana.
MASWALIJe, nifanye nini ili nizae mtoto wa KIUME:
Ili mwanamke aweze kuzaa mtoto wa KIUME, inabidi alale na mwanaume siku ile ya mimba (fertile day), ambayo ni siku ya 15.
Je, nifanye nini ili nizae mtoto wa KIKE:
Ili mwanamke aweze kuzaa mtoto wa KIKE, inabidi alale na mwanaume siku 3 kabla ya ile siku ya mimba (yaani siku 3 kabla ya ile fertile day)
Hii inaondoa uwezekano wa mbegu za kiume kulirutubisha yai, kwani mbegu zote za kiume zitakuwa zimeshakufa ndani ya siku mbili za mwanzo na kuziacha zile za kike zikidunda kwa siku moja zaidi zikilisubili yai lifike!
Je, Kama menstruation cycle yangu Ni siku 15, nifanye nini ili nipate mtoto wa kike?
Ili mwanamke mwenye menstruation cycle ya siku 15 aweze kuzaa mtoto wa KIKE, inabidi alale na mwanaume siku 3 kabla ya siku ile ya bleed (yaani siku 3 kabla ya ile siku anayoanza kutokwa damu ya hedhi)!
Kwa mwanamke wa kundi hili inabidi tukumbuke kwamba, siku yake ya mimba ndiyo siku hiyo hiyo anayoanza ku-bleed!
Source: Jamii forum

Wednesday, February 11, 2009

Kazi kwelikweli!

Mwanaume mmoja aliwahi nyumbani kutoka kazini mapema zaidi ya muda wake wa kawaida ile kufika home akasikia sauti zisizo za kawaida chumbani upstairs, akaamua kukimbia haraka ili kujua kulikoni.
Kufika tu chumbani akakuta mkewe anahema na jasho linamtoka na yupo uchi kabisa, mzee akauliza
“ Vipi mke wangu kulikoni?”
mwanamke huku analia akajibu
“Nimshikwa na heart attack”

Mzee akakimbia downstairs ili kupiga simu kuita ambulance, ile anataka kupiga tu mtoto wake wa miaka 4 akaja na kumwambia
“Baba baba mdogo yupo amejificha kwenye closet chumbani kwenu) na yupo uchi”

Mzee kwa haraka akaacha simu na kukimbia tena upstairs chumbani na kwenda moja kwa moja kumfurumsha jamaa kwenye closet, akafungua mlango wake na kukuta mdogo wake huyo yupo uchi na kwa woga mkubwa amejificha chini kwenye floor ya closet.

Huna akili kabisa wewe”, mzee akafoka “mke wangu ana heart attack wewe upo busy unakimbia tu humu ndani uchi kuwatisha watoto!!!
Nenda zako huko kavae nguo!”

Kila mtu humjua!

Kuna wengine ni watu wa furaha muda wowote, mahali popote, wakati wowote na kama kuna tatizo ndani ya dakika tano unafahamu kwamba huyu ana tatizo:


Kuna watu ambao huwa hawawezi kuwa excited na kitu chochote pia hata kama wamepata kitu cha kushusha moyo wanakuwa kawaida tu.

Wakiwa kwenye tamsha, mechi ya soka, kanisani, au mahali popote kwenye sherehe wao si kawaida kuweza kushangilia na kutoa kelele yoyote, wanakuwa kimya kama vile hawapo.
Hata kama kuna habari njema kiasi gani kwao hupokea kwa hali ya kawaida tu sawa na habari mbaya.
Hata kama amefaulu mtihani au kupandishwa cheo hawezi hata kuchangailia au kuonesha kweli amefurahi na hata akipata msiba bado huwa kawaida tu.
Pia hawa watu huwa hawawezi kukatishwa tama kirahisi, jana, leo na hata kesho kwao ni sawa tu.
Hata wakiwa na shida au raha huwezi kujua.Ukimletea zawadi hata kama ni surprise kiasi gani atakwambia asante tu basi imetoka, hata hivyo si kwamba ana nia mbaya bali huo ndio mwitikio wa emotions zake n mazingir ya nje.
Kama ni graph basi mawimbi huende mwendo wa kawaida bila kufanya mzunguko wa kwenda juu na chini kuwa mkali sana.
Lakini wapo watu ambao hisia zao kuruka juu sana na kushuka chini kabisa kwenye zero.

Hawa watu huwa na furaha kwa kila kitu na hushangilia hata kitu kidogo tu, hata akiona ua huruka na kushangalia, hawa ni watu ambao mkiwa kiwanjani mnatazama mechi ya mpira wa miguu lazima ukae mbali kwani kelele zao huendana na kurusha mateke kama vile na wao wapo kiwanjani.

Hata hivyo ukweli ni kwamba hawa watu huwa hawadumu na furaha zao kwani pindi mambo yakibadilika basi huvunjika vipande vipande chini kabisa na kila mtu hutambua kwamba huyu mwenzetu ana tatizo tayari.
Hawa ni watu akiwa na furaha huwa na marafiki wengi tu na akikosa furaha hata marafiki humkimbia maana anabadilika na kuwa mwingine.


Graph zao hushuka chini kabisa na kupanda juu kabisa.
Issue inakuja je mkioana mtu wa mawimbi ya kawaida na yule wa kushuk chini kabisa na kupanda juu kabisa ndoa inakuwaje?

Monday, February 9, 2009

Mpaka waamue wao!

Naamini Adamu alikuwa haulizwi na Eva "Je unanipenda?" Kwani Adamu angempenda nani tena kama si Eva peke yake, maana walikuwa wawili tu duniani.

Hata hivyo suala la mapenzi na tendo la ndoa limekuwa likipitia hatua nyingi na vionjo tofauti tangu dunia kuumbwa hadi sasa.
Sijui miaka 50 ijayo mambo yatakuwaje.

Binadamu wa kwanza walikuwa hawajui kama ni sperm huwa ina fertilize yai ili ku create mtoto.
Wengi walidhani ni miungu au mwanamke mwenyewe ndiye alikuwa na uwezo wa kuumba mtoto tena wa jinsia fulani na kama alikuwa anazaa watoto wa kike tu au wa watoto wa kiume tu mume alikuwa anakuja juu au ndugu wa mume walikuwa wanakuja juu kumlaumu mwanamke kwa nini anazaa watoto wa jinsi moja tu.
Pia zipo jamii ziliamini watoto mapacha ni mkosi na hivyo waliuawa pindi tu wakizaliwa.

Pia baadhi ya dini (kikristo) kama (nazungumzia dini siyo wokovu maana dini na wokovu ni vitu viwili tofauti kabisa) waliingiza suala la mume na mke kuacha tendo la ndoa kwa ajili ya sababu za kidini kama vile:-
Hawakuruhusiwa kufanya sex siku ya Alhamisi kwa sababu ilikuwa ni siku ya kukumbuka kukamatwa kwa Kristo kabla ya kifo chake msalabani.
Pia hawakuruhusiwa siku ya Ijumaa kwa ajili ya kuadhimisha mateso ya Kristo.

Hawakuruhusiwa siku ya Jumamosi kwa sababu iliwekwa kama siku maalumu kumkumbuka Bikira Maria.
Siku ya jumapili hawakuruhusiwa kabisa kwani ni siku ya Bwana siku ya kufunga na kuomba pia kuupa heshima ufufuko wa Kristo.

Siku ambazo zilikuwa wazi kwa tendo la ndoa ilikuwa ni Jumatatu, Jumanne na Jumatano pia hawa viongozi walikuwa tishio kwani walikuwa pia uwezo wa kuwatangazia washirika wao kwamba hata hizo siku zilizokubaliwa zinaweza kuamriwa hakuna tendo la ndoa na watu walikuwa wanatii viongozi wao pasipo kujua maandiko yanasemaje kuhusu haki ya mume na mke kibiblia.
Je, ungalikuwapo nyakati hizi ingefanyeje?

Utafiti mpya unaonesha kwamba mwanamke akiwa mjamzito huweza kupoteza kumbukumbu (memory) hivyo basi kupoteza kumbukumbu lisiwe jambo la kujiona ni tatizo kubwa sana, ni kitu cha kawaida.
Na baada ya mwaka tangu kujifungua kumbukumbu hurudi kama kawaida.

Utafiti umeshindwa kutoa sababu kamili ni ipi kwa mwanamke mjamzito kupoteza kumbukumbu labda inatokana na homoni pia mfumo wa maisha mapya ya kuwa na mimba kama vile kukosa usingizi, kuchoka nk

Source: http://www.supernanny.co.uk/Advice/-/Pregnancy-and-Birth/-/The-postnatal-you/How-becoming-a-mum-affects-your-memory.aspx

Friday, February 6, 2009

Hii inaumiza sana!

Nani haogopi sindano?
Je umemchoma mara ngapi mumeo au mchumba wako? Ni ukweli usiopingika kwamba hata wanaume huumia sana hisia zao na mtu pekee mwenye uwezo wa kupooza maumivu ni mpenzi wake yaani mke au mchumba yake, Je inakuwaje pale inatokea mke au mchumba ndo anakuwa chanzo cha maumivu ya hisia za mwanaume?
Ni muhimu sana mwanamke (mke au mchumba) kuepuka haya;-
Kumwambia kwamba hana thamani yoyote (worthless) na kwamba hana lolote na hakusaidii lolote. Hata kama unaongea ukiwa na hasira kumwambia mwanaume yeyote kwenye mahusiano kwamba hana maana unaweza ukajutia. Ni busara kama una hasira na unajiona huwa unakuwa huna break kwa maneno unaongea baki kimya.

Kumfananisha yeye na mwanaume mwingine ambaye amefanikiwa iwe pesa au maisha kwa ujumla. Usimwambie mumeo au mchumba wako kwamba mbona mke wa fulani au mchumba wa fulani amenunuliwa hiki au kile na yeye hawezi, hiyo ni kashfa. Atakwambia uende ukaolewe naye kama wewe ni mchumba na kama ni mke atakwambia nenda kaishi naye au unawasha moto ambao kuuzima unahitahi magari ya fire ambayo tena yanakuja bila maji.

Usimwoneshe kwamba husikilizi pale anaongea hasa anapoongelea jambo lolote analoliona ni la msingi. Hata kama kama anachoongelea unaona kwako ni upuuzi (boring) jitahidi kuonesha kama unamsikiliza ikiwezekana hata kuuliza maswali kutokana na anachoongea. Ukimsikiliza atajisikia wa maana na anaweza kuongea na wewe mambo mengi ya msingi.

Usifanye utani (hasa kwa kutumia wanaume wengine hasa unatani unaomdhalilisha yeye) hata kama unatumia utani ukiongelea mwanaume ambaye ni rafiki yake. Maana akiumizwa hisia zake kumbuka kutibu ni gharama kubwa sana. Kwani kwa maneno wengine wamevunja ndoa na uchumba.

Kutoa sababu kila mara mumeo anapotaka kufanya mapenzi na wewe, hii ni pamoja na kuwa mwanamke mwenye huzuni mara zote, hakuna furaha wala kutabasamu kila wakati mwanamke ni malalamiko, huzuni na gubu, unafikiri kwa nini aliondoka kwa mama yake na baba yake kama si kukasirikiwa kila mara.
Amekuchagua wewe ili uwe faraja na akiwa na wewe ajisikia raha kama hivyo basi ni afadhari asirudi nyumbani au atumie muda wake na mtu mwingine usidhani eti kwa kukasirika au kuonesha uso wa huruma na huzuni ndipo mwanaume atakuona wa maana au kukuhitaji na kukubembeleza zaidi, ukweli anajiona hawezi kukupa furaha na hivyo afadhari awe na kitu kingine badala yako, who cares hata TV anaweza kuona inamfaa kama si kwenda kuangalia mechi za ligi kuu Uingereza.


Nakutakia weekend njema!

"A successful marriage requires falling in love many times, and always with the same person."

Mignon McLaughlin

Wednesday, February 4, 2009

Kukiwa na Mawingu tu!

Wapo wanawake ambao hata siku kukiwa na mawingu tu husababisha depression Depression ni nini?
Depression (Unyonge) ni ugonjwa ambapo mtu hujisikia huzuni na anakuwa mkari na msumbufu (misarable) kwa muda fulani katika maisha.
Ni ugonjwa ambao hutokana na mabadiliko au kuchanganyana kwa chemicals ndani ya mwili kiasi cha kuuchanganya ubongo na matokeo yake uwezo wa kufikiria (mind) na uwezo wa tukuko (emotions) huathirika.
Watu ambao wana depression wanakuwa na wakati mgumu sana kuenjoy maisha kama kawaida na wengine hufikiria hata kujinyonga ingawa depression huweza kutibika.

Nini husababisha Depression?
Depression hutokana na mabadiliko ya kikemia (brain chemistry) na hii hutokana na msongo wa mawazo katika maisha hasa husababishwa na mambo makubwa matatu ambayo ni
Pesa
Kazi na
Mahusiano

Pia kwa nchi ambazo zina kipindi cha winter watu wake kukosa jua kwa muda mrefu huweza kusababisha aina ya depression ambayo huitwa SAD (Seasonal Affective Disorder)

Nini ni dalili za kuwa depressde?
Dalili za kuwa upo depressed ni pamoja naKuwa na mood ovyo, kukosa hamu ya kufanya mapenzi, kuchoka lakini pia kukosa usingizi, kuamka mapema, kuwa ovyo kwa maana kwamba huwezi kulala na huwezi kukaa.
Kukosa kujiamini, kusahau na kupoteza kumbukumbu, kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito, kujiona hufai, kuwa na hasira zisizo na maana, kutojisikia raha na kitu chochote.
Maumivu, hofu na mashaka na kujiona maisha hayana maana.

Nini kifanayike kama upo depresseed?
Kwanza tambua tatizo na pata msaada.
Kutokana na mfumo dume wanaume ambao huwa depressed huwa wanakuwa wagumu sana kukubali kwamba wapo depressed na kwamba wanahitaji msaada.
Wanakawaida ya kukaza midomo yao kuomba msaada wakati huohuo kila mtu anajua huyu yupo depressed.
Depression na Ndoa
Katika Ndoa tafiti nyingi zinaonesha kwamba mmoja ya wanandoa anapopata depression basi ndoa nzima huanza kuathirika kwa sababu depression huathiri ubongo (mental health) wa mwanandoa mmoja na kuathirika kwa utendanji wa ubongo husababisha ndoa kuwa ovyo.

Mwanandoa ambaye yupo depressed anakuwa amepoteza furaha, kuridhika, hamu ya mambo mazuri ambayo wanandoa wanatakiwa kufanya pamoja ili ndoa iwe tamu.
Hisia zake na libido hupotea na huweza kuthani upendo katika yao umekwisha na hapo ndoa huwa tayari ICU.

Pia asilimia 30 – 50 ya ndoa zenye matatizo sababu kubwa ya hayo matatizo ni mmoja ya wanandoa kuwa depressed.
Wapo wanandoa wakiwa depressed basi amepata tiketi ya kutafuta mpenzi mpya, ukweli hapo unaongeza matatizo jambo la msingi ni wanandoa wote kila mmoja kumjua mwenzake ili hata akiwa depressed ujue jinsi ya kumsaidia au kusaidiana hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza tatizo permanently.

Monday, February 2, 2009

Je unajua binadamu ni kiumbe peke katika wanyama (animal kingdom) ambaye huendelea kuishi hata baada ya muda wa kuzaa kukoma.

Hivyo basi mwanamke binadamu huweza kuendelea kuishi hata baada ya kukoma kizaa wakati wanyama wanawake wote hufa pindi tu wakiwa hawana uwezo wa kuzaa tena.

Si kweli!

Source: