"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, February 17, 2009

Je, ni kweli?

Mwanamke mnene hubaguliwa zaidi kuliko mwanaume mnene, mwanamke akianza kunenepa haichukui raundi watu kuanza kumnyanyapaa au kumpa maneno ya kibaguzi, wakati mwanaume huendelea kupeta kwa muda zaidi.
Jamii huwavumilia sana wanaume wanene kuliko wanawake wanene.

Wanawake huweza kukumbuka sura (uso) ya mtu kuliko wanaume.
Pia wanawake huweza kukumbuka sura (uso) za wanawake wenzao kuliko wanaume.

Wanawake wenye rika moja huchokana mapema zaidi kuliko wanaume wa rika moja.
Kwa mfano wanawake wawili waliopanga chumba kimoja huweza kuishi pamoja kwa muda mfupi kuliko wananaume wanaishi chumba kimoja cha kupanga.

Wanawake ni wazuri sana katika kukumbuka nguo (pamba) na wanaume ni wakali kukumbuka magari na silaha.

Wanawake huota ndoto mbaya mara nyingi zaidi kuliko wanaume, hii inatokana na kupishana kwa kiwango cha joto la mwili na homoni wakati wa usiku ambapo wanawake hutokea mara nyingi zaidi kuliko wanaume.
Pia wataalamu wanasema kwamba wanawake huwa wagumu sana kuachana na hisia walizokuwa nao kabla ya kulala matokeo yake wakilala huota kuna mtu anawawinda au anawakimbiza au amepoteza wazazi au watoto na hata kujikuta amepotea na kuwa mazingira asiyoyajua.
Pia critics wanasema kwamba si kwamba wanawake huota ndoto mbaya kuliko wanaume bali wao ndo hukumbuka zaidi ndoto zao kuliko wanaume.

Si kweli kwamba wanawake ni waoga kuliko wanaume, wanawake huonekana ni waoga kuliko wanaume hasa kutokana na jinsi wanavyojieleza au wanavyowakilisha woga wao.
Wanawake ni watu wa hisia zaidi hivyo wakati mwingine huonekana ni waoga kuliko wanaume kitu ambacho si kweli ni hisia tu na huruma.

No comments: