"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, February 11, 2009

Kila mtu humjua!

Kuna wengine ni watu wa furaha muda wowote, mahali popote, wakati wowote na kama kuna tatizo ndani ya dakika tano unafahamu kwamba huyu ana tatizo:


Kuna watu ambao huwa hawawezi kuwa excited na kitu chochote pia hata kama wamepata kitu cha kushusha moyo wanakuwa kawaida tu.

Wakiwa kwenye tamsha, mechi ya soka, kanisani, au mahali popote kwenye sherehe wao si kawaida kuweza kushangilia na kutoa kelele yoyote, wanakuwa kimya kama vile hawapo.
Hata kama kuna habari njema kiasi gani kwao hupokea kwa hali ya kawaida tu sawa na habari mbaya.
Hata kama amefaulu mtihani au kupandishwa cheo hawezi hata kuchangailia au kuonesha kweli amefurahi na hata akipata msiba bado huwa kawaida tu.
Pia hawa watu huwa hawawezi kukatishwa tama kirahisi, jana, leo na hata kesho kwao ni sawa tu.
Hata wakiwa na shida au raha huwezi kujua.Ukimletea zawadi hata kama ni surprise kiasi gani atakwambia asante tu basi imetoka, hata hivyo si kwamba ana nia mbaya bali huo ndio mwitikio wa emotions zake n mazingir ya nje.
Kama ni graph basi mawimbi huende mwendo wa kawaida bila kufanya mzunguko wa kwenda juu na chini kuwa mkali sana.
Lakini wapo watu ambao hisia zao kuruka juu sana na kushuka chini kabisa kwenye zero.

Hawa watu huwa na furaha kwa kila kitu na hushangilia hata kitu kidogo tu, hata akiona ua huruka na kushangalia, hawa ni watu ambao mkiwa kiwanjani mnatazama mechi ya mpira wa miguu lazima ukae mbali kwani kelele zao huendana na kurusha mateke kama vile na wao wapo kiwanjani.

Hata hivyo ukweli ni kwamba hawa watu huwa hawadumu na furaha zao kwani pindi mambo yakibadilika basi huvunjika vipande vipande chini kabisa na kila mtu hutambua kwamba huyu mwenzetu ana tatizo tayari.
Hawa ni watu akiwa na furaha huwa na marafiki wengi tu na akikosa furaha hata marafiki humkimbia maana anabadilika na kuwa mwingine.


Graph zao hushuka chini kabisa na kupanda juu kabisa.
Issue inakuja je mkioana mtu wa mawimbi ya kawaida na yule wa kushuk chini kabisa na kupanda juu kabisa ndoa inakuwaje?

No comments: