"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, February 4, 2009

Kukiwa na Mawingu tu!

Wapo wanawake ambao hata siku kukiwa na mawingu tu husababisha depression Depression ni nini?
Depression (Unyonge) ni ugonjwa ambapo mtu hujisikia huzuni na anakuwa mkari na msumbufu (misarable) kwa muda fulani katika maisha.
Ni ugonjwa ambao hutokana na mabadiliko au kuchanganyana kwa chemicals ndani ya mwili kiasi cha kuuchanganya ubongo na matokeo yake uwezo wa kufikiria (mind) na uwezo wa tukuko (emotions) huathirika.
Watu ambao wana depression wanakuwa na wakati mgumu sana kuenjoy maisha kama kawaida na wengine hufikiria hata kujinyonga ingawa depression huweza kutibika.

Nini husababisha Depression?
Depression hutokana na mabadiliko ya kikemia (brain chemistry) na hii hutokana na msongo wa mawazo katika maisha hasa husababishwa na mambo makubwa matatu ambayo ni
Pesa
Kazi na
Mahusiano

Pia kwa nchi ambazo zina kipindi cha winter watu wake kukosa jua kwa muda mrefu huweza kusababisha aina ya depression ambayo huitwa SAD (Seasonal Affective Disorder)

Nini ni dalili za kuwa depressde?
Dalili za kuwa upo depressed ni pamoja naKuwa na mood ovyo, kukosa hamu ya kufanya mapenzi, kuchoka lakini pia kukosa usingizi, kuamka mapema, kuwa ovyo kwa maana kwamba huwezi kulala na huwezi kukaa.
Kukosa kujiamini, kusahau na kupoteza kumbukumbu, kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito, kujiona hufai, kuwa na hasira zisizo na maana, kutojisikia raha na kitu chochote.
Maumivu, hofu na mashaka na kujiona maisha hayana maana.

Nini kifanayike kama upo depresseed?
Kwanza tambua tatizo na pata msaada.
Kutokana na mfumo dume wanaume ambao huwa depressed huwa wanakuwa wagumu sana kukubali kwamba wapo depressed na kwamba wanahitaji msaada.
Wanakawaida ya kukaza midomo yao kuomba msaada wakati huohuo kila mtu anajua huyu yupo depressed.
Depression na Ndoa
Katika Ndoa tafiti nyingi zinaonesha kwamba mmoja ya wanandoa anapopata depression basi ndoa nzima huanza kuathirika kwa sababu depression huathiri ubongo (mental health) wa mwanandoa mmoja na kuathirika kwa utendanji wa ubongo husababisha ndoa kuwa ovyo.

Mwanandoa ambaye yupo depressed anakuwa amepoteza furaha, kuridhika, hamu ya mambo mazuri ambayo wanandoa wanatakiwa kufanya pamoja ili ndoa iwe tamu.
Hisia zake na libido hupotea na huweza kuthani upendo katika yao umekwisha na hapo ndoa huwa tayari ICU.

Pia asilimia 30 – 50 ya ndoa zenye matatizo sababu kubwa ya hayo matatizo ni mmoja ya wanandoa kuwa depressed.
Wapo wanandoa wakiwa depressed basi amepata tiketi ya kutafuta mpenzi mpya, ukweli hapo unaongeza matatizo jambo la msingi ni wanandoa wote kila mmoja kumjua mwenzake ili hata akiwa depressed ujue jinsi ya kumsaidia au kusaidiana hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza tatizo permanently.

2 comments:

Thankful Paul said...

Do you believe in miracles?

Anonymous said...

Yes, I do believe in Miracles through Jesus Christ for nothing is impossible on earth.