"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, February 13, 2009

Kupata Mimba


Wengi hasa wanawake wamekuwa wakiuliza maswali mengi sana kuhusuana na jinsi ya mwanamke kupata mimba au kuzuia kutopata mimba.
Naamini maelezo yafuatayo ukisoma kwa makini unaweza kupata ufahamu na kujibiwa maswali yako yote ambayo yamekuwa yanakutatiza.

Pia ni vizuri kuzingatia na kutochanganya Kalenda ya menstrual cycle tunayoongelea hapa na ile 'kalenda ya mwaka' inayohusu tarehe za miezi 12 ya mwaka ambayo huwa tunaitundika ukutani huko nyumbani na maofisini kwetu!

Wanawake wamegawanyika katika makundi makubwa 4 linapokuja suala la siku za hedhi
Mzunguko mfupi yaani siku 22
Mzunguko wa kati yaani siku 28
Mzunguko mrefu yaani siku 35
Na mzunguko abnormal siku 15

Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavo:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd.
Kisha ahesabu kuanzia ile 22nd day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 8th day ya kalenda yake.
Hivyo 8th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 22.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!
Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavo:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 14th day.
Inamaana kwamba 14th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 28.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!
Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavo:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th, 29th, 30th, 31st, 32nd, 33rd, 34th, 35th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 35th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 21st day.
Inamaana kwamba 21st day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 35.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!
Kama mwanamke ana abnormal menstruation cycle ya siku 15
BASI KUNAUWEZEKANO WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama kawaida:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 15th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 1st day.
Inamaana kwamba, the 1st day of her bleeding ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 15.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed, na ndiyo hiyo hiyo siku ambayo mwanamke wa kundi hili anaweza kupata mimba!
Hii inamaana kwamba, siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa.
Mwanamke wa aina hii anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kubleed, kwani siku ambayo yai moja linaanza kuharibika ndio siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linakuwa tayari kurutubishwa
Na wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au ku-feel ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa kurutubishwa, kwani ute wa wanawake wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu kwa vile unatoka siku ile ile wanapoanza ku-bleed.Pia wanawake wa kundi hili huwa wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu na bleed hukatika ndani ya siku moja au mbili tu!

NB:
Mwenye uwezo wa kuhakikisha mwanamke anapata mimba ni Mungu mwenyewe, unaweza kutumia njia zote na kila uwezo wa kibinadamu nab ado mimba isitokee au unaweza kuzuia kwa njia zote na mimba bado ikapatikana.
MASWALIJe, nifanye nini ili nizae mtoto wa KIUME:
Ili mwanamke aweze kuzaa mtoto wa KIUME, inabidi alale na mwanaume siku ile ya mimba (fertile day), ambayo ni siku ya 15.
Je, nifanye nini ili nizae mtoto wa KIKE:
Ili mwanamke aweze kuzaa mtoto wa KIKE, inabidi alale na mwanaume siku 3 kabla ya ile siku ya mimba (yaani siku 3 kabla ya ile fertile day)
Hii inaondoa uwezekano wa mbegu za kiume kulirutubisha yai, kwani mbegu zote za kiume zitakuwa zimeshakufa ndani ya siku mbili za mwanzo na kuziacha zile za kike zikidunda kwa siku moja zaidi zikilisubili yai lifike!
Je, Kama menstruation cycle yangu Ni siku 15, nifanye nini ili nipate mtoto wa kike?
Ili mwanamke mwenye menstruation cycle ya siku 15 aweze kuzaa mtoto wa KIKE, inabidi alale na mwanaume siku 3 kabla ya siku ile ya bleed (yaani siku 3 kabla ya ile siku anayoanza kutokwa damu ya hedhi)!
Kwa mwanamke wa kundi hili inabidi tukumbuke kwamba, siku yake ya mimba ndiyo siku hiyo hiyo anayoanza ku-bleed!
Source: Jamii forum

8 comments:

Anonymous said...

Ukiwa utatoa masomo kama haya ,tutapenda sana kusoma lakini sometimes unaandika vitu amabavyo ni none sense na amabavyo vinatufanya tujiulize ivi unafikiri nini hata uanaze kyaandika hayo. mengine si ya kuyaandika ila ni mtu binafsi akikuuliza basi unaweza mpa experience yako lakini siyo kutuandikia hapa. Somo la leo nimelipenda kwanza ni la kitaaluma na linamgusa kila mtu. lakini mambo ya fanya hivi ,hapa na wapi naona ni kupitiliza.

Anonymous said...

Brother,Your star, Hope God will bless you all the way to your fillings and commitments to help others,I like the way how you take your time to educate people including me and for those who wish to have Kids, God bless you. Quick question my friend are you a doctor? by any means.
MSAFIRI

Anonymous said...

Du!
Asante kwa darasa

Hilda

Fikirikwanza said...

heeee!!! lecture ya leo ni kiboko ,nimesinzia hadi nikuchoka .

lakini mie nataka kuwauliza ,sasa wale wavivijijin wasio na net vii tawasaidieaje?, nafkiri wangefurahi sana nao wakazipata couscous like these.

pili hivi watu wote wanao oana huwa wanafundiwshwa haya yote au ndo mambo yatajijua yenyewe tukifika ?

Anonymous said...

Kaka sante kwa darasa, lakin je ambao mzunguko wetu ni siku 24 tunakuw katika kundi lipi?

Lazarus Mbilinyi said...

Kama mzunguko wako ni siku 24 siku yako ya kupata mimba ni siku ya 10 baada ya kuanza MP kwa utaratibu wa kanunie yetu ni kama ifuatavyo;

Kama una mzunguko wako ni siku 24 kalenda yako itakuwa 1st, 2nd , 3rd , 4th , 5th , 6th , 7th , 8th , 9th , 10th , 11th , 12th , 13th , 14th , 15th , 16th , 17th , 18th , 19th , 20th , 21st, 22nd, 23rd and 24th.
Kisha hesabu kuanzia 24th kurudi nyuma mpaka ifike 15 na utaona inaangukia siku ya 10th ambayo ndiyo siku yako ya kupata mimba.
Kumbuka 1st day yako ni siku ya kwanza kupata MP au bleeding

Anonymous said...

Je Kama mzunguko wangu Ni wasiku 30?lini nitapata mtoto wa kiume?

Anonymous said...

Kama nilibleed 28/11/2013 Na pia 28/12/2013 je inamaana Ni mzunguko wa siku 30?Kama Ni hivyo je lini nitapata mtoto wa kiume tafadhali?