"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, February 26, 2009

Macho!

Tangu siku tulipoingia katika dunia hii tulifungua macho yalitutuwezesha kuona, kuelewa na kuwasiliana na ulimwengu.

Macho hukuwezesha kutoa machozi wakati ukijisikia kulia na hukuwezesha kuona vitu vya karibu na vile vya mbali kadri ya upeo wa macho yako.

Kitu cha thamani sana kwenye uso wako ni macho, pia kuona ni zawadi ambayo wengi hatuoni thamani yake hata hivyo huwa tunakumbuka thamani ya macho pale tunapokutana na mtu asiyeona yaani kipofu.

Macho huweza kubeba uwezo wa ajabu waingereza anasema ni sexual symbol that opens window to the soul.

Macho yana nguvu ya ajabu huweza kufungua moyo na maisha.
Nafsi ya mtu ipo kwenye macho na ni gateway kuelekea kwenye moyo wa mtu.

Mapenzi nayo yana uhusiano mkubwa na macho, hisia za mapenzi katika mwili hupitia njia nyembamba na laini iitwayo macho.

Macho kuelezea ukweli ambao ulimi wakati mwingine hushindwa kutamka.
Asilimia 80 ya nguvu ambazo tunazielekeza kwa wengine hupitia kwenye macho yetu.
Binadamu ana kawaida (nature) kukwepesha macho hasa pale kama haongei ukweli au pale anapoona hajisikii vizuri.
Watu wakiwa na hofu au kutojisikia vizuri huwa na tabia ya kuangalia pembeni.
Kama unataka kugundua je macho yanauwezo kiasi gani basi leo ukikutana na mpenzi wako mwangalie kwa kutumia macho yako kwa muda zaidi dakika 2 bila kukwepesha ukimpa tabasamu linaloendana na unavyochezesha macho huku ukichunguza nafsi yake na uzuri wake (kimwili) hakikisha mawazo yako na hisia zako unaelekeza jinsi unavyojisikia kwa mpenzi wako. (akikuuliza mwambie "nakupenda")

Ukweli ni kwamba utapokea kitu katika hisia zako na kwamba macho ni silaha muhimu sana kwenye mapenzi kwa wapendanao.
Jicho ni taa ya mwili.
Kama jicho lako ni nyofu, mwili wako wote utakuwa na nuru
Mathayo 6:22

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kaka mbilinyi. hakuna kitu muhimu kama macho.