"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, February 9, 2009

Mpaka waamue wao!

Naamini Adamu alikuwa haulizwi na Eva "Je unanipenda?" Kwani Adamu angempenda nani tena kama si Eva peke yake, maana walikuwa wawili tu duniani.

Hata hivyo suala la mapenzi na tendo la ndoa limekuwa likipitia hatua nyingi na vionjo tofauti tangu dunia kuumbwa hadi sasa.
Sijui miaka 50 ijayo mambo yatakuwaje.

Binadamu wa kwanza walikuwa hawajui kama ni sperm huwa ina fertilize yai ili ku create mtoto.
Wengi walidhani ni miungu au mwanamke mwenyewe ndiye alikuwa na uwezo wa kuumba mtoto tena wa jinsia fulani na kama alikuwa anazaa watoto wa kike tu au wa watoto wa kiume tu mume alikuwa anakuja juu au ndugu wa mume walikuwa wanakuja juu kumlaumu mwanamke kwa nini anazaa watoto wa jinsi moja tu.
Pia zipo jamii ziliamini watoto mapacha ni mkosi na hivyo waliuawa pindi tu wakizaliwa.

Pia baadhi ya dini (kikristo) kama (nazungumzia dini siyo wokovu maana dini na wokovu ni vitu viwili tofauti kabisa) waliingiza suala la mume na mke kuacha tendo la ndoa kwa ajili ya sababu za kidini kama vile:-
Hawakuruhusiwa kufanya sex siku ya Alhamisi kwa sababu ilikuwa ni siku ya kukumbuka kukamatwa kwa Kristo kabla ya kifo chake msalabani.
Pia hawakuruhusiwa siku ya Ijumaa kwa ajili ya kuadhimisha mateso ya Kristo.

Hawakuruhusiwa siku ya Jumamosi kwa sababu iliwekwa kama siku maalumu kumkumbuka Bikira Maria.
Siku ya jumapili hawakuruhusiwa kabisa kwani ni siku ya Bwana siku ya kufunga na kuomba pia kuupa heshima ufufuko wa Kristo.

Siku ambazo zilikuwa wazi kwa tendo la ndoa ilikuwa ni Jumatatu, Jumanne na Jumatano pia hawa viongozi walikuwa tishio kwani walikuwa pia uwezo wa kuwatangazia washirika wao kwamba hata hizo siku zilizokubaliwa zinaweza kuamriwa hakuna tendo la ndoa na watu walikuwa wanatii viongozi wao pasipo kujua maandiko yanasemaje kuhusu haki ya mume na mke kibiblia.
Je, ungalikuwapo nyakati hizi ingefanyeje?

1 comment:

Anonymous said...

Mmmmm hapo ingekuwa ngumu kabisa lakini sijui tungeweza tu kwani mbona kila siku mambo yanabadilika?
Msafiri