"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, February 14, 2009

Mtoto awa baba

Alfie ambaye ni mvulana mwenye sura ya kitoto bado na anayeonekana kama mwenye miaka 8 amekuwa baba baada ya rafiki yake wa kike jina Chantele Steadman ambaye ana miaka 15 kuzaa mtoto mwenye uzito paundi 7.3, motto anaitwa Maisie Roxanne.


Huyu baba mtoto anasema kwamba ilipofahamika kwamba Chantele ni mjamzito hawakukubali kutoa mamba na badala yake yeye aliona ni vizuri kuwa na mtoto. Ingawa hakujua itakuwaje kwani baba yake naye ana watoto tisa na hana kazi maalumu hivyo si mara zote hupata pocket money na hata akipata hupokea £10.


Waziri mkuu wa Uingereza Bwana Gordon Brown aliingia mitini kutoa maoni kuhusiana na hii issue ingawa amekiri kwamba serikali inatakiwa kujitahidi kuhusiana na mamba za teenagers.

Hi si mara ya kwanza kwa watoto kuzaa watoto nchini Uingereza kwani mwaka 1998 Sean Stewart (12) alizaa na rafiki yake wa kike Emma Webster (15) ingawa walikuja kutengena baada ya miezi 6 tu.
Huyu Bwana mdogo hujui hata nepi inauzwa kiasi gani na itabidi asahau kidogo kwenda kucheza Game na ajikite kumaliza shule na kuwa baba mzuri.

Je, hapa wa kulaumiwa ni nani, hawa watoto au wazazi au jamii?


Source:
http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/news/article2233878.ece

1 comment:

Anonymous said...

laws must be changed to allow these kids to take resposibilty as elder.