"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, February 27, 2009

Ni kujituma!

Unaweza kuanza vizuri katika mahusiano usipoweka jitihada zinazotakiwa inaweza kuwa kazi ngumu kama kuponda kokoto! "Any fool can fall in love, it takes wisdom to stay in love".

Ukimuuliza mtu yeyote ambaye anaanza kazi katika taaluma mpya kwa mfano Daktari, injinia, mwanafunzi, polisi, rubani, Nahodha nk; kwamba kazi au taalumu anayoingia inahitaji kuiitoa na kufanya kazi kwa kujituma kila au kazi inayoingia ni demanding bila shaka atakubali.

Lakini ukimuuliza mke mtarajaiwa au mume mtarajiwa kwenye ndoa kwamba taalumu anayoingia ni demanding (kwa maana kwamba inahitaji kujitoa kila siku na kwamba ni kuweka juhudi kila siku ili kupata matokeo mapya; ataona kama vile unafanya utani au unamuonea wivu kwani mapenzi waliyonayo ni kama maji kwenye mtelemko hivyo hakuhitaji efforts zozote ili penzi lidumu miaka na miaka.

Hii haina maana kwamba ndoa ni ngumu sana kiasi kwamba kama unataka kuolewa uogope bali ni kutoa msisitizo kwamba kuingia kwenye ndoa bila kuwa na ujuzi unaotakiwa au kutojua kwamba unatakiwa kufanya kitu gani inaweza kuwa disaster.

Ndoa si jambo ambalo ni effortless, kama muhusika iwe mke au mume unahitaji kuwa na mipango, kuhangaika, kuvumilia, fanyia kazi kila jambo linalojitokeza, kusahau ukisamehe, kuelekeza nguvu katika upande wa mambo mazuri.

Hata kama mmeoana na kujiona duniani hakuna watu ambao wamewahi kupendana kama ninyi bado katika safari ya maisha ya mahusiano ya ndoa ipo siku mambo hayatakuwa kama uynavyotarajia kwani wewe ni binadamu na umezaliwa mazingira tofauti nay eye hivyo ipo siku mambo hayatakuwa sawa.

Mara nyingi upendo huzaa ndoa njema hata hivyo kuna wakati ukiwa kwenye ndoa hata kama unajisikia hakuna upendo ipo siku ndoa huweza kuzaa upendo hasa kama wote mnafanya juhudi kuhakikisha unatia juhudi kwenye hii taalumu ya ndoa.
Wapo watu ambao wakati wanaoana hakukuwa na upendo mkubwa kama wewe hata hivyo kutokana na kujiweka sana katika taaluma hii ya ndoa matokeo yake ndoa imekuwa imara na yenye upendo wa ajabu.

Wapo walioingia kwenye ndoa kwa madaha na kujiona hakuna wanandoa wanaopendana kama wao hata hivyo baada ya kubweteka sasa ndoa inashikiriwa na uzi mwembamba sana ni kama vile ipo ICU hata hivyo juhudi zozote za kufufua ndoa huzaa matunda hasa pale kila mmoja akielekeza nguvu kwenye positive side.
Kwenye balance sheet ya ndoa siku zote tunaelekeza nguvu upande wa faida au positive au yale mambo yanayofanya ndoa isimame si hasara au mambao ambayo unahisi hayakupi kuridhika.

Ukitaka kuwa na balance sheet ya ndoa yenye bonding strong fanya yafuatayo kwa mpenzi wako
Tabasamu huku ukimwangalia usoni
Mshike au gusana naye (ngozi kwa ngozi)
Mfanyie kitu chochote kizuri bila kuombwa
Kumsifia kwa kitu kizuri amefanya huku unatabasamu
Kuangaliana usoni kwa kuangaliana usoni zaidi ya dakika 3
Kumsikiliza mwenzako kwa makini huku ukirudia kile anakwambia,
Kumsamehe leo kesho na zamani,
Mwandalie chochote ale,

Pumua kwa pamoja au weka kichwa kwa moyo wake na sikiliza mapigo ya moyo wake,
Mbusu kwa midomo na ulimi,
Kushikana zaidi ya dakika kumi,
Kumpa massage kwa lengo la kumfariji hasa miguu, mabega na kichwa,
Kumkumbatia kwa maana ya kumfariji (hii ni two-edged sword),

Kumgusa na kunyonya chuchu na matiti,
Kuweka mkono kule chini kwa mpenzi wako kwa lengo la kumfariji,
Kwenda kulala wakati mmoja hata kama baadae utaamka kwena kufanya kazi,
Uwe na hamu ya kutaka mpenzi wako akijisikie raha na karibu na wewe
.

Mengine unayajua wewe!

1 comment:

shyrose said...

Upo sahihi brother' i would like also to emphasize the following points to men for their marriage/womens:

Men need to do some of the things the woman wants, such as prioritize their relationship and listen more. Men need to do the same things at home that they do at work. A wife is the million-dollar client. If she walks out the door, the business is closed.