"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, February 19, 2009

Watoto wao wapo wazi,
Lily na Emmanuel sijui walikuwa wanaongea nini!
Je, kuna tofauti gani urafiki (friendship) na mahusuno(relationship)?
Wengi tunaamini urafiki ukiwa strong hupekea watu kuwa na mahusiano kwa watu wa jinsia tofauti?

Hata hivyo kuna kitu cha ajabu hapa, fikiria aina ya maongezi unakuwa nayo kwa mtu ambaye mna urafiki na maongezi unakuwa nayo kwa mtu ambaye una mahusiano (mpenzi0).
Kwa rafiki yako unakuwa mwepesi kueleza wazi kabisa mapungufu yako na kushindwa kwako, huoni aibu kuongelea matatizo yako na unaona rahisi sana kumuuliza maswali na unamuomba huyo rafiki akusaidie kuyatatua.

Kwenye urafiki (deep) tunategemea utajua kila kitu kuhusu yeye hata siri kubwa kubwa iwe mbaya au nzuri, ziwe za mafanikio au kushindwa.

Linapokuja suala la mahusiano binadamu wana tabia ya ajabu ambayo ni kutunza siri kutoka kwa mtu ambaye ana mahusiano naye, hatupendi kumwambia kuhusu failures tulizonazo, tunatunza siri kwenye sana bila partners kujua.
Kwenye urafiki tunakuwa kama watoto wadogo na kwenye mahusiano tunakuwa kama watu wazima, tunapokuwa kwenye mahusiano kila tunachofanya kwanza lazima calculations zifanyike wakati kwenye urafiki tunakuwa wazi kabisa kujiachia kwa mazuri na mabaya kwa kushinda na kushindwa, tupo wazi.

Inaonekana kwamba kuweka mipaka katika mahusiano na kutoongea chochote huwezesha nahusiano kudumu kuliko kuwa huru kuongea udhaifu kama kwenye urafiki.

Hata hivyo binafsi naamini mahusiano ya kweli ni pamoja na kujiweka huru kwa mwenzako kufahamu uzuri na ubaya, jinsi unavyoweza na jinsi unavyoshindwa.

Sijui wewe unasemaje kitendo cha kuwa huru sana kwa rafiki yako kuliko mpenzi wako?

No comments: