"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, March 30, 2009

Nimeachwa, nimepata mwingine!

Mimi na wewe milele Duniani kuna wakati wa kutoa machozi, wakati wa kucheka, wakati wa kuhuzunika, wakati wa kufurahi, wakati wa kuchukiwa, wakati wa kupendwa, wakati wa kuponya nk.

Kama umewahi kupendwa na mwanaume au mwanamke then akakupiga chini bila sababu za msingi au kwa mgogoro mkubwa, ukweli hali hii huumiza na huweza kuzidi maumivu ya operation hospitalini kama si kuwa na mawazo hadi unanusurika kugongwa na magari barabarani.


Kupendwa kutamu na kuacha kuchungu !


Ni kawaida kujisikia huzuni, kuvunjika moyo, kujisikia hatia na hata kuwa na siku za machozi na hata kushindwa kufanya kazi kama kwenda kazini maana love is greater than faith and hope.


Ni kweli uliwekeza muda wako wote hata rasilimali zako kuhakikisha unampa umpendaye kile ambacho kinatoka ndani ya moyo wako, hata hivyo amekukimbia na kukuacha.


Ni kweli umeumizwa, umekasirishwa, hata unajiuliza una tatizo gani hata hivyo jambo la msingi ni kumshukuru Mungu kwamba sasa una nafasi ya kusahihisha makosa na kwamba alikuacha kabla ya kuwa ndoa hivyo una nafasi nzuri zaidi kufanya maamuzi ya kweli.

Wengine akishaachwa, kwa haraka anajiingizwa mahusiano na mtu mwingine ili kuziba pengo au nafasi iliyoachwa wazi moyoni na kuendelea kumlaumu aliyeachana naye kwamba ndiye alikuwa chanzo na sababu.

Kabla ya kuingia kwenye mahusiano mapya ni jambo la msingi kuwa makini zaidi kwani unaweza kuingia kwenye mahusiano mapya na ukagundua kwamba umefanya terrible mistake kuliko mara ya kwanza ukaishia kujuta zaidi nakujikuta umebadilisha sura, rangi, kimo na shape hata hivyo mwanaume au mwanamke ni yuleyule na tabia zake.

Data zinaonesha kwamba ukiwa na mahusiano na yakavunjika ukienda haraka unaweza kuishia kwa mtu wa aina ile ile na kuendelea kuumizwa zaidi.

Maswali mawili ya msingi kujiuliza kabla ya mengine ni kwanza je, nitawezaje kumpata mwingine ambaye hataniumiza kama yule wa kwanza?

Na pili je, nitawezaje kubadilika na kuwa mtu mwingine tofauti na nilivyokuwa mara ya kwanza kabla ya mahusiano kuvunjika?

Tunatakiwa kujifunza kutokana na mahusiano ya kwanza na kujua tulihusika vipi kusababisha mahusiano kushindikana au je ni kitu gani kinatakiwa kubadilisha?

Yafuatayo ni maswali ya kujiuliza kabla hujaingia kwenye mahusiano mapya
Je, nimekuwa na muda wa kutosha kuponya (heal) majeraha yangu kabla sijajiingiza kwenye mahusiano mapya?
Je, nimefahamu kwa nini mahusiano ya kwanza yalivunjika?
Je, nimebadilika katika tabia, mitazamo, maneno, kufikiria na mawazo yangu kabla ya mahusiano haya?
Je, nipo wazi na huru katika mahusiano haya ninayotaka kuanza?

Tumeshaongelea malengo ya baadae, dini, pesa?
Je, nataka kuanza mahusiano mapya kwa sababu ni mpweke au nataka kufanya naye mapenzi au namuhitaji sana kifedha, au ni mtu sahihi kwangu?

Je, nimemuomba Mungu?

Friday, March 27, 2009

Mazoezi

Si lazima uende Gym Mwili wako uliumbwa kwa ajili ya kufanya kazi (manual labour) kama vile kusukuma, kuvuta, kubeba, kutembea, kuruka, kuimba, kucheza, kusakata rhumba, kuinama, kuinuka, kukimbia, kukusanya, kupanda (climb) kuwinda nk.

Tunapofanya kazi yoyote kimwili ubongo huweza kutoa aina za kemikali (endocrines) ambazo hutuwezesha kuji-balance na kutupa hisia za kuwa well being.
Unajua kuna watu wabishi inawezekana na wewe msomaji ni mmoja wao, hivi ni lini umefanya zoezi?
na kwa nini hufanyi?
halafu unajiuliza mbona mwili unanilemea, mbona sijisikii vizuri, mbona stress kila siku? wakati mwingine tunawasumbua madaktari bure kumbe dawa zipo ni wewe kufanya mazoezi.

Ni kweli kufanya mazoezi kutakufanya ujisikia vizuri na lazima ufanye hivyo kwa faida yako, hata hivyo wengi wetu hutumia muda mwingi kufanya kazi ambazo tunakuwa tumekaa tu kwenye kiti kwa muda mrefu bila kuufanyisha kazi mwili na ikifika weekend unashinda unatazama Tv full speed bila kujishughulisha na manual work.

Pia ukitoka ofisi unaingia kwenye gari hadi nyumbani kama unaishi maisha ya aina hii lazima ufanye mazoezi otherwise unaweza kuharibu afya yako, kitaalamu mazoezi mara mbili kwa wiki muhimu.

Kufanya mazoezi husaidia kupunguza uzito, kuondoa nyama zembe mwilini, kupunguza mafuta (fat), kubalance blood pressure, pia kisukari.

Kufanya mazoezi (siyo magumu)hukuwezesha wakati wa kulala kuweza kufumba macho haraka na kuingia nchi ya ahadi ya usingizi haraka.
Mazoezi huongeza mental skills.

Ukiwa na afya yenye mgogoro maana yake hata mambo ya sita ka sita yataleta mgogoro hivyo basi fanya mazoezi ili uwe na afya njema na ukiwa na afaya njema maana yake better sex life.
Mwanamke ambaye misuli ya kegel imejikaza anakuwa na wakati mzuri linapokuja suala la sex kuliko Yule ambaye misuli imelegea na huweza kuwa na misuli iliyokaza kama hufanyi mazoezi, unataka kushinda bahati nasibu wakati hukucheza, thubutu!

Na mwanaume ambaye anafanya mazoezi ni hivyo hivyo atampeperusha kipepeo hadi anapotakiwa kufika.

Kama upo nchi za magharibi summer hiyo inakuja, huna sababu ya kujitetea eti baridi ooh snow nyingi..... nk hukosi sababu!

Na sisi tulio tropics wengi shughuli zetu ni zoezi tosha, ila fanya mazoezi kwa ajili ya kuweka sawa ubongo pia kujiweka social na wengine.

Huwezi kuogelea nenda for walking,
Jogging,
Gym
Soccer
Volleyball
Boxing
Biking
Na mengine mengi tu!

Wednesday, March 25, 2009

Ni nguvu ya ajabu!

Baada ya kupendana watu huoana, hata hivyo wakati mwingine baada ya kuoana watu hupendana, usishangae muulize babu yako na bibi yako kama si baada ya kuoana ndipo walianza kupendana.

Hebu fikiria umewakutanisha watu wawili mume na mke, baada ya muda wataanza kila mmoja kutaka kumjua zaidi mwenzake.
Hata kama hawana uzoefu wowote kimahusiano, wataanza kila mmoja kuvutiwa na mwenzake kikemia, wasiwe na ukaribu wa damu, hakikisha unazidi kuwaweka pamoja kama mawe mawili unayoyatupwa sehemu hadi somethings happens.

Wataanza kila mmoja kujawa na mawazo na kuanza kumfikiria mwenzake, concentration itaongezeka kila mmoja kwa mwenzake kama tiger anayekimbiza kasungura.
Matokeo yake wataanza kutumia muda pamoja kuongea, kucheka na kutembea, wakati mwingine hawajui hata wakikutana watafanya kitu gani au kila mmoja anataka kufanya nini kwa mwenzake ila wanajisikia nguvu ya ajabu inayomfuta kila mmmoja kwa mwenzake.

Kila wanachofanya hakina maana, kitu chenye maana ni kuwa pamoja, wanaanza kujisikia nguvu ya ajabu ya kutaka kurukia kitandani pamoja, kila mmoja sasa anahamu ya kumgusa mwenzake, wanatamani kuanza kuziondoa layers moja badi nyingine kuanzia nguo walizovaa nje hadi za ndani, kila mmoja anataka kumjua mwenzake hahaha yaani hadi awe uchi wawe wawili tu.
Kila wakiwa karibu kila mmoja ni raha na kila mmoja anapenda kuendelea kugundua hazina za uzuri wa mwenzake, wanahangaika kuwa pamoja tu hata for doing nothing muhimu wapo pamoja.

Unaonaje ukiwasambaratisha na kila mmoja kwenda kuishi nchi tofauti kama vile Finland na Tanzania?
Kama wana mapenzi ya kweli hapo itakuwa disaster na watakuchukia maisha yao yote na baada ya dakika chache wataanza kuwa depressed kwa kila mmoja kumkosa mwenzake.

Romantic love is composed of some very strong human fibers, once formed, it is not easily broken.
(Song of Solomon 8:6 -7)


"Marriage is perhaps the most vital of all the decisions and has the most far-reaching effects, for it has to do not only with immediate happiness, but also with eternal joys.
It affects not only the two people involved, but also their families and particularly their children and their children’s children down through the many generations."

There is no such thing as a successful divorce...

Tuesday, March 24, 2009

Sikujua kuna Upweke!

Binadamu si kisiwa!
Unahitaji watu ili ku-socialize na hatimaye kuondokana na upweke.
Pichani ni Kole, Gloria, Lilly, Emmanuel na Jody.Kujisikia upweke ni suala la wote, umeolewa, hujaolewa au umeoa au hujaoa.

Swali muhimu je upweke ni kwa wanawake peke yao?
Ukweli hata wanaume hujisikia upweke ingawa matokea ya upweke hutofautiana kwani mwanaume akishakuwa na mahusiano ya kijamii (social network) huweza kuondokana na upweke wakati mwanamke anaweza kuwa na mahusiano ya jamii (social network) na bado akawa na upweke emotionally.

Linapokuja suala la emotions wanawake ni sawa na barabara yenye njia 8 (8 lanes) wakati wanaume ni mfano wa barabara iliyotota inayoenda msituni (forest access road).

Pia jinsi tunavyowasiliana wanawake na wanaume ni tofauti, wanaume tupo direct to the point wakati wanawake hupendelea kuongea kunakoelewesha, kitu amacho automatically mwanamke akiongea na mwanaume hujikuta mpweke maana jamaa yupo mkatomkato tu.

Pia kama umeolewa inawezekana ndoa yako ipo kwenye stage ya repair, huwa tunajidanganya kwamba tukiolewa au kuoa basi kila kitu kitakuwa shwari kama mwindaji nyikani hakuna milima wala mabonde bali tambarare.
Hata tukikutana na matatizo badala ya kushambulia tatizo tunashambuliana wenyewe kwa nini tusiwe wapweke?
Kujua tatizo ni mtaji wa ushindi wa tatizo lolote katika ndoa.

Kawaida watu hukutana na upweke wa aina mbili ule wa kijamii (social) na ule wa tukuko (emotional)
Upweke wa kijamii hutokana na kukosa mtandano wa kijamii, kila mmoja anahitaji wmingine awe mwanaume au mwanamke pasipo suala la sex, hakuna mtu ni kisiwa kwamba hahitaji mwingine.
Wanawake ambao wapo active kijamii ni mara chache sana huwa na upweke wa kijamii, hata hivyo wapo wengine kutokana na kuwa na aibu, au kuwa wapya katika eneo jipya hawana mtandao wa marafiki na hujikuta wapweke.

Hivyo jambo la kwanza mahali popote ni kutengeneza mtandao wa marafiki ili kuondoa upweke wa kijamii.

Kwa upande mwingine upweke wa tukuko (emotions) ni upweke unaotokana na kukosa ukaribu wa kihisia katika mahusiano, hata kama upo socially active bado kuna nafasi ya ndani ambayo lazima ujazwe na mtu wako wa karibu mume umpendaye au mke umpendaye.
Ndiyo maana watu wanaweza kulala wanafanya party, lakini bado ndani yao asubuhi wakajikuta ni wapweke wa ajabu.

Pia kujenga emotional relationship ni ngumu kwani watu huogopa unaweza kujiachia kwa mwanaume au mwanamke then akaja akakuumiza (rejection factor) kwani lazima ujiweke wazi kwake ili muwe na mahusiano ya karibu kabisa.
Pia kumpata mtu ambaye anakufaa emotionally kuna hitaji kazi kubwa kumfahamu na zaidi chemistry ziendane.

Hata wanawake ambao wameolewa bado wakati mwingine hujikuta kwenye upweke wa kupindukia kwa sababu wanaume walionao bado hawajazi nafasi ile ya ndani ambayo mwanamke anahitaji kujisikia ili upweke umtoke.

Wanawake wengine ni wapweke kwa sababu hawapo wazi kwa waume zao na kwa kuwa wanaume kihisia ni tofauti na mwanamke basi huwa hawajui kwamba something is wrong ni ngumu mwanaume kusoma uso na kujua mwanamke anahitaji kitu gani kwenye mahusiano ingawa wengine wapo smart ila si wote.
Ni vizuri mwanamke ambaye ameolewa kuongea na mumewe jinsi anavyojisikia kwani kubaki kimya na kudhani kwamba mume atajua jinsi unavyojisikia na kwamba atajirekenisha huwezi jua ndo imetoka hiyo.
Siku njema....................................

Sunday, March 22, 2009

Jumapili Njema

A Muslim man in Egypt killed his wife because she was reading the Bible and then buried her with their infant baby and an 8-year old daughter.
The girls were buried alive! He then reported to the police that an uncle killed the kids.15 days later, another family member died. When they went to bury him, they found the 2 little girls under the sand - ALIVE!
The country is outraged over the incident, and the man will be executed.
The older girl was asked how she had survived and she says:-
'A man wearing shiny white clothes, with bleeding wounds in his hands, came every day to feed us.
He woke up my mom so she could nurse my sister,' she said.
She was interviewed on Egyptian national TV, by availed Muslim woman news anchor.
She said on public TV,
'This was none other than Jesus, because nobody else does things like this!'
Muslims believe Isa (Jesus) would do this, but the wounds mean He really was crucified, and it's clear also that He is alive!
But, it's also clear that the child could not make up a story like this, and there is no way these children could have survived without a true miracle. Muslim leaders are going to have a hard time to figure out what to do with this, and the popularity of the Passion movie doesn't help!
With Egypt at the center of the media and education in the Middle East , you can be sure this story will spread.Christ is still turning the world upside down! Please let this story be shared.
The Lord says, 'I will bless the person who puts his trust in me.
'Jeremiah 17

Friday, March 20, 2009

Bank zingine!

Mama wa Kinew zealand akiwa na mtoto ambaye amemzaa baada ya kutumia sperms za mume ambaye alikuwa ameshakufa Hata baada ya mume kufa mwanamke bado anaweza kuendelea kuzaa na mume wake.
Hilo limethibitika huku Nchini New Zealand ambako wanawake wawili wameshazaa watoto baada ya kutumia sperms za wanaume zao ambao walikuwa wameshakufa.

Kinachofanyika ni kwa mume na mke kwa hiari yao kwenda clinic (sperm bank) jaza fomu (consent form) na mwanaume hutoa sperm ambazo zitatunzwa in case mume akafa kabla hawajaamua kupata watoto.
Hata kama mume akifa, mke akitaka kuzaa hurudi clinic kuchukua sperms za mumewe na kupandikizwa kwa njia ya IVF (in-vitro fertilization)
Bado inaleta maswali kimaadili kuhusiana na haki za mtoto hasa akitaka kujua ilikuwaje tarehe yake (mtoto) kuzaliwa ikawa mbele ya tarehe ya kifo cha baba yake.

Bado ni jambo jipya katika dunia ya technolojia na inashangaza.

Wakati wajane wengine huenda kufuata benki pesa za waume zao waliokufa sasa wajane wanaenda benki kuchukua sperms ambazo waume zao waliacha.

Source:
http://www.stuff.co.nz/dominion-post/archive/national-news/1402676


Thursday, March 19, 2009

Mume kutoweka!

Kwa mwanamke ambaye alikuwa na ndoto za maisha bora ya ndoa kuondokewa na mume huleta maumivu makali sana, ni janga na hasara kubwa sana kwake.
Kuachwa mwenyewe ni badiliko kubwa katika maisha linalokuacha unahangaika mwenyewe na kujikuta ghafla unahusika kifedha, kulea watoto na kuendeleza taaluma kama si kuanza taaluma mpya.

Kama umepitia hali hii au unapitia hali hii ya kutalikiwa au mume kufa au mume kutoweka na kukuacha wewe na watoto au hata namna yoyote basi fahamu kwamba si nina yangu kutonesha kidonda ulichonacho bali ni katika kusaidiana ili uweze kukabiliana na kushinda na hatimaye kusimama katika changamoto hii kubwa uliyonayo.

Kumbuka hukuchagua iwe hivyo, na mume kutoweka si mwisho wa yote (end of the road), bado kuna uamuzi na chaguo wawezafanya.

Kila mwanamke mwenye ndoa ni mjane mtarajiwa hivyo hata kama una mume bado unahitaji kusoma na kuelewa na zaidi sana kujifahamu wewe ni nani na lolote laweza kutokea.

Inawezekana unajisikia kila kitu hakiendi, unajiona maisha ni shagalabagala, asilimia 80 ya uwezo wako na nguvu zako unatumia kutafakari emotions zako zilivyoharibiwa, ndiyo maana unajisikia kuwa confused na pia umepoteza self esteem or self image, hujiamini tena, marafiki wote wanakukwepa na unajiona mpweke na depressed and stressed.

Hata hivyo mara nyingi ukiachwa na mume marafiki wengi ulikuwa nao hukimbia na hilo linakufanya uwe mpweke na kukaliwa na msongo wa mawazo maana hata ndugu nao hawaoni thamani yako tena.
Umeshaanza kupata matatizo ya ajira na fedha pia.

Kumbuka kutoweka kwa mume wako hakujabadilisha kitu chochote ambacho Mungu alikuumba kuwa, thamani yako ipo palepale, kuachwa ni uamuzi wake si wako na hiyo haiwezi kuondoa kile unastahili kuwa (worth).
Bado wewe ni mwanamke tofauti (unique), mzuri, mrembo, mwanamke mwenye malengo, mipango kamili, mwenye talents na mawazo mazuri ya kukufanya kuwa vyovyote unataka kuwa, wewe ni mbunifu, mwanamke mwenye ndoto na mwenye uwezo wa kufanya vitu vya uhakika na tofauti duniani.

Nakutia moyo kwamba achana na mawazo yanayoongea ndani yako kwamba
Huna lolote, maisha kwisha, maisha hayana maana tena, hakuna mtu anakujali tena, unataka kukata tama”

Anza kuchukua hatua madhubuti kuwa na uamauzi mpya ili uweze kukua na kuendelea kusonga mbele katika mwelekeo sahihi na halisi kwa furaha na ujasiri.
“Hakuna mtu anaweza kuondoa furaha yako ndani yako hadi uamue mwenyewe”

Jaribu kufanya yafuatayo:
Pata ushauri kwa mtu unayemwamini kama vile mchungaji wako.
Andika kwenye karatasi hisia na kila linalokusumbua hata kama utaandika kwa machozi utajisikia kupata relief.
Kama huna ajira tafuta ajira/kazi yoyote ya kufanya hasa ile unapenda.
Weka malengo – long term or short term na anza kuyatimiza.

Kubali kwamba maisha yako ni changamoto na zitazame changamoto kwa jicho la opportunities kwako kukua kiimani na kupata new skills za maisha hata kuweza kufundisha wengine.
Kubali kwamba huna mume kwa sasa na kwamba usijiingize haraha haraka kutafuta mwanaume mwingine kuziba pengo unaweza kuingia kwenye moto mkali zaidi.

Katika jambo gumu kama hili Mungu anaweza kukurejesha kwenye matumaini na wewe kuwa strong baada ya kuvunjika moyo.

Tambua kwamba Mungu anaweza kutenda kazi hata katika giza nene, anaweza kujibu maombi yako na kukurejesha katika maisha mapya pole pole na baadae kujenga msingi imara kimaisha na kiroho ili kuweza kugundua baraka, hazina mpya na hata wewe kuwa mtu mpya kabisa.

Ubarikiwe na Bwana!

Mumeo aridhike!

Kunywa maji katika kisima ulichochimba mwenyewe Kumfanya mume wako aridhike kimapenzi maana yake ni kufanya akuangukie kimapenzi zaidi.
Kufanya mapenzi kwa wanandoa ni njia nzuri ya kuwaunganisha kinafsi na kujipa raha na ukaribu.

Ukijifunza sanaa ya kumkaribisha na kuwa tender kwa mwenzako basi mnaweza kutengeneza bond ambayo ni strong na mume au mke atakufurahia siku zote za maisha yenu.
Kumfanya mwanaume awe na furaha kwa mke wake huonesha jinsi unavyompenda na pia inampa msukumo wa kuhakikisha anakuwa karibu na wewe kimahaba na kuwa na muda na wewe kama wapenzi (quality time).
Kuna vitu vingi ambavyo mwanmke huhitaji kufanya kwa mume wake hata hivyo kila mwanaume ana tofauti na mwingine na kila mwanaume ana ladha yake linapokuja suala la mapenzi au tendo la ndoa.

Hivyo ni jukumu la wewe mwanamke kujifunza na zaidi kufanya utafiti wa kutosha kujua mume wako anapenda kitu gani kwako na pia mwili wako upo sensitive wapi na zaidi jiografia yake maana
"without geography we are nowhere",
usiniulize jiografia ya mume nini, sugua ubongo!

Kila mwanaume hupenda kuona mke wake akionekana sexy na nguo amevaa, inawezekana mpo wawili tu yeye na wewe, kwa nini usimtanie mzee na kinguo cha uhakika then pima libido meter yake itasoma vipi?
Kuna vinguo vya kuogea, kuna vinguo vya chumbani, kuna nguo za kuvaa ofisini au kazini nk kila nguo huvaliwa mahali pake.
Huwezi kuvaa nguo ya kazini chumbani!

Unajua kuchezesha sauti kuna raha yake kumfanya mwanaume joka litoke pangoni, siyo kila siku kulalamika tu, lawama tu, manung’uniko tu, acha hizo jaribu siku hata kama anakosea kila siku anza kumsifia hata kwa vitu vidogo tu, mpe asante, mkumbatie na kumpa romantic touch, uwe mbunifu.
Siamini kama kuna mwanaume ameoa mke ambaye siku zote ni kelele au kununa tu, au kulalamika tu au kuongea tu makosa na kusahihisha, kwa nini asikukwepe, hata kama anakosa siku zingine geuza udhaifu wake kuwa kitu kizuri au uwe na mtazamo positive.

Hata siku moja hujamchezea kifua au kidevu chake, mfanye ajisikie yeye ni mwanaume special.
Mwanamke anatakiwa kumlinda mumewe na maadui wote kiroho na kimwili lakini wakati mwingine mke hujisahau na kuzoea ndoa hadi mume ana fall in love kihisia na mwanamke mwingine (nyumba ndogo).

Hata hivyo inawezekana mume huwa haja fall I love na yule mwanamke bali ame-fall in love na hisia zile wewe humpi na akikutana na huyo mwanamke anajisikia raha na kupata kile love tank yake ndani ya moyo wake huhitaji hata kama mwanamke mwenyewe hampendi ila emotionally ameoza kwa huyo mwanamke na anajikuta anavutwa na yeye badala ya wewe kumvuta.

Wednesday, March 18, 2009

Katika afya njema na Ugonjwa!

Nilienda Muhimbili hadi siku ya mwisho wake! Ndoa ni kazi na wakati mwingine huweza kuwa kazi nzito nay a ziada.
Watu wengi hukumbana na wakati mgumu kwenye ndoa wakati fulani inawezekana hata wewe msomaje upo kwenye wakati mgumu sana wa ndoa yako, hata hivyo swali gumu ambalo linahitaji majibu ni
je, mume wako au mke wako anapokuwa amepata tatizo kubwa la kiafya kwa mfano hawezi kushiriki tendo la ndoa na wewe, hawezi kula mwenyewe, ameharibika sura kwa sababu ya ugonjwa au inabidi umbebe kwa ajili ya haja zote ndogo na kubwa,
Je, utakimbia?, utakaa naye?,
utamuomba Mungu?
Utaomba talaka?
Utakimbilia kwenye kifua cha mwanaume au mwanamke mwingine?
Au ndo wakati wako wa kujirusha?

Unaweza kuangalia maswali hayo na kujiuliza
hivi ni nani anaweza kufikiria kufanya vitu kama hivyo?”

Ukweli kuna mifano hai ambapo baada ya mmoja ya wanandoa afya kuzolota mwingine amefanya moja ya hayo hapo juu.

Wakati wanandoa wapo mbele ya kanisa na mbele ya mchungaji, kutoa viapo vyao mara nyingi ni rahisi sana kusema
“katika afya au ugonjwa nakubali”
au
‘Katika utajiri na umaskini nakubali”,
Wakati wote mna afya njema ni rahisi sana kukubali lakini wakati ukifika umaskini ukaanza kuwakalia kwa kasi ya ajabu, au mmoja afya kuzolota ndipo unaweza kukumbuka kile kiapo kilikuwa kina maana gani.

Moyo wangu ulikufa ganzi pale niliposikia mume wangu mpenzi ana Cancer na ipo hatua ya 4 ambayo hakuna dawa duniani.
Hadi hapa tulikuwa wanandoa wazuri na wenye raha pamoja na watoto wetu na tulipenda na kila mmoja kujisikia raha kwa mwenzake.
Mume wangu mpenzi alianza kuugua alianza kupunguza uwezo wa kwenda kufanya kazi kila siku hadi ikafika siku hawezi kula chakula mwenyewe hadi nimlishe huku amelazwa Hospitalini.
Wengine waliona ni udhaifu wa mume wangu kshindwa hata kula mwenyewe ila mimi nilimuona jinsi anavyojitahidi kutumia nguvu zake na ilishindikana, niliona anavyoteseka kwa maumivu hadi nikamuomba Mungu anipe nguvu kuvumilia kuona mume wangu katika ugonjwa namna hii.
Ilibaki mimi kuwa pembeni kwake usiku na mchana na kumuonesha mume wangu upendo mkuu na kwamba bado namuhitaji kuliko wakati mwingine hata kama alikuwa kwenye kitanda cha mgonjwa, Mungu aliniwezesha kunipa nguvu na ujasiri kuendelea kumuona mume wangu bado ni mume wangu hata kama alikuwa amebadilika sana kwa jinsi ugonjwa ulivyomharibu.

Ili niweze kupita katika haya yote nilikuwa namuomba Mungu ili niwe strong na anilinde kupita katikati ya kipindi hicho kigumu na Mungu alinionesha njia ya kumsaidia mume wangu na njia pekee ilikuwa ni mimi kuendelea kumhudumia “Kama Mume wangu” bila kujali alikuwa katika hali gani.
Alikuwa anaongea mama mmoja kwa uchungu na moyo wa machozi kuonesha kwamba kweli ndoa ni kujitoa na alikuwa anajua kuwepo wakati mumewe afya imezolota".

Swali Je utakuwa pamoja na mume wake au mke wako akiwa katika ugonjwa?

Jibu ni
Endelea kumpenda kama ulivyokuwa unampenda
Omba Mungu akupe uwezo na nguvu na uvumilivu,
Uwe pamoja nay eye,
Usikimbie,
Usikate tama,
Simama na toa upendo wako maalumu na
Mpende mpende na endelea kumpenda.

Hongera Sana!

Hongera sana dada Upendo na kaka Perfect sasa ni Mr & Mrs P. Mwasiwelwa tangu tarehe 14/02/2009 mlipounganisha na Mungu kuwa mwili mmoja.
Mungu awabariki na kuwapa maisha marefu yenye furaha katika ndoa yenu.

Tuesday, March 17, 2009

Wenye Wallet nzito!

Mwanaume akiwa na wallet kubwa basi wakiwa kwenye sita kwa sita mwanamke hufika haraka kileleni.
Je, ni kweli sex pleasure anayopata mwanamke ina uhusiano mkubwa na ukubwa wa wallet ya mzee ?
Je, ni kutafsiri kwamba mwanamke hupunguza uwezo wa kufika kileleni akiwa na mwanaume ambaye akilala naye bado anaendelea kuwaza shida ya pesa na jinsi ya kulipa bills na manunuzi ya vitu mbalimbali anavyohitaji?

Wanawake 1,534 huko China walifanyiwa utafiti (Chinese Health and Family Life Survey) wanawake 121 walikiri kufika kileleni kila wakati, 408 mara kwa mara, 762 mara chache na 243 hawakuweza kufika kileleni kabisa.
Hata hivyo iligundulika kwamba kuongezekana kwa kipato cha mwanaume kulikuwa na matokeo ya kuongezeka kwa mwanamke kufika kileleni.
Mwanaume alivyozidi kuwa na pesa mwanamke alifika haraka kileleni.

Hata hivyo utafiti wa aina hii umetoka matokeo yanayofanana si kwa wachina tu bali hata Ulaya na Amerika sijui hapa Afrika utafiti kama huu ukifanyika matokeo yatakuwaje.

Hata hivyo utafiti haokuonesha je, hawa wanawake wanaofika kileleni haraka kwa sababu mzee ana pesa furaha yao hudumu kwa muda gani?
au ni kuwadanganya wanaume waone mwanamke anajituma na kwamba ameridhika?

Hapa nahisi wanaume hudanganywa tu na mwanamke kwamba amefika kileleni ili atoe pesa.

Ila hata hivyo kuna kaukweli fulani ndani yake fikiria mwanaume ana pesa na amemwambia wakitoka hapo atamkabidhi funguo za gari, mwanamke akishafikiria jinsi atakavyoringa na usafafiri wake, kwa nini usifike kileleni!
Kazi kwelikweli!

Saturday, March 14, 2009Je, wajua!
Wanawake wengi huanza kusisimka kwa maongezi tu, kama vile kuongelea jinsi anavyokuvutia, au vitu unapenda kufanya na yeye mkiwa wawili tu, na ukishaanza kumkumbatia na kumbusu you may lose her hahahaha!

Wanawake wengine hawapendi kuanza kusisimuliwa clit… moja kwa moja kwanza kabla ya kusisimuliwa sehemu zingine na wengine huwa wanapenda kusuguliwa kwa pembeni kwanza na si moja kwa moja juu kwa mgandamizo mkubwa, uliza kabla ya kurukia huko!

Wanawake hupenda mwanaume kuendelea na stimulation hata kama yupo kileleni tayari au hata kama ameshafika, kama upo ndani (usiniulize ndani ya nini kwani tunaongelea kitu gani hapa) usitoe endelea kumpa stimulation kwani ukitoa anaweza kupoteza raha yake au atadondoka kileleni!

Wanawake wengi hawawapi sifa sana wanaume wanaoendelea kusimamisha zaidi ya saa moja huku wanawake wenyewe wakiwa hoi wamechoka, eti kwa sababu bado amesimamisha huendelea tu bila kujali, hayo ni mateso na inaweza kuwa sababu ya mwanamke kugoma next time!
Mwanaume lazima ajue kusoma mazingira!

Wanawake wengi huwa na matiti ambayo ni sensitive sana kabla na baada ya kupata siku zao, hata hivyo raha na msisimko anaopata umetenganishwa na uzi mwambamba sana na kuumizwa, hivyo kama mwanaume hatakuwa gentle na hilo watermelon lake anaweza kumuumiza badala ya kumpa raha mpenzi wake!

Eti baadhi ya wanawake hugoma oral sex kwa sababu ya kuhofia mwanaume anaweza kukutana na harufu au taste ya ajabu, hata hivyo mwanaume anahitajika kutoa sifa kwa jinsi anavyijisia kuhusiana na smell/taste ya huko, kwa wote usafi ni kiroho pia.

Wanawake wengi hawaridhiki sana na miili yao, hivyo mwanaume akimwambia mwanamke ana mapaja mazuri kuliko mwanamke yeyote duniani mwanamke hujisikia yupo turned on, mmm bila kusifiwa najisikii raha?
kweli mambo ya word of praise mkiwa faragha muhimu!
Mimi simo!

Ute wa yai (egg white) ni natural lubricant salama, bure na ya uhakika kuliko K-Y Jelly.

Friday, March 13, 2009

'To get something you never had, you have to do something you never did.'
When God takes something from your grasp, He's not punishing you, but merely opening your hands to receive something better.
Concentrate on this sentence...
The will of God will never take you where the Grace of God will not protect you.'
Something good will happen to you today; something that you have been waiting
to hear.

Thursday, March 12, 2009

Ni kujifunza!

Tendo la ndoa au kufanya mapenzi (sex) kwa watu wawili wanaopendana (Ndoa) ni moja ya vitu vya asili duniani vinavyowapa wahusika raha ya ajabu ambayo bado lugha za kawaida tunazotumia binadamu hazitoshelezi kuelezea.

Ingawa ni kweli mwanamke na mwanaume wapo tofauti linapokuja suala la sex bado kujifunza na kuwa equipped kwa ajili ya sex ni muhimu.

Miili yetu ni complex machines ambazo zinahitaji kutumia Owners Manual kusoma mara kwa mara ili kuelewa na kuwa wazuri kuitumia.

Wakati wanaume hujisikia vizuri baada ya sex wanawake mara nyingi hupenda kujisikia vizuri ili wajishughulishe na sex.

Pia mwanaume akiwa amesisimka kimwili ndipo hujisikia kusisimka kisaikolojia mwanamke akisisimka kisaikolojia ndipo hujisikia kusisimka kimwili.

Sex yenye utamu wa kweli hutokana na kujiachia katika fahamu zetu na kutojiachia fahamu huweza kufanya blocking ambayo huweza kuiba hamu ya kufanya mapenzi.

Ni kweli kwamba ubongo wako ni most important sex organ na kwa ubongo tunaweza kuhusanisha mwili, nafsi na roho kuumba raha ya mapenzi ambayo haiwezi kusaulika katika maisha yote tunayoishi.

Hakuna binadamu anazaliwa anajua kila kitu, hivyo basi kujifunza ndiyo silaha ya kwanza kabisa ya kufahamu mwili wako na wa Yule umpendae una react vipi linapokuja suala la kufanya mapenzi.

Wala huhitaji kununua libido meter ili kuhakikisha kitanda chenu kinakuwa na moto mambo ya msingi ni kwamba:

Hakikisha kufanya mapenzi ni moja ya priority kati yako na mume/mke

Jifahamu mwenyewe kama vile unapenda kitu gani na wapi katika mwili wako

Mfahamu vizuri partner wako

Fahamu aina mbali mbali za style za kufanya mapenzi (sex position) hiyo hiyo kila siku inakuwa mazoea, muwe wabunifu.

Hakikisha mnapata suluhisho kwa matatizo kabla ya kwenda chumbani ( wakati mwingine jifunze kukubaliana kutokubaliana.

Hakuna kitu muhimu kama romance.

Afterplay ni muhimu kama foreplay- huwezi kumaliza mazungumzo bila kutoa hitimisho.

Hakikisha unaimarisha mawasiliano.

Pia kubali mabadiliko au kutafuta kitu kipya.

Wednesday, March 11, 2009

Hata kuchagua pazia kwake ni usalama! Mwanamke huhitaji kujisikia yupo salama kwa mume wake, rafiki au yeye mwenyewe.
Pia mwanamke hujisikia raha na salama zaidi anapoona mwanaume anayempenda anaonesha kweli yupo committed kwake.

Pia mwanamke anapoolewa hutazamia nyumba yake kuwa salama, na nyumba kuwa salama kwake ina maana kuwa na maamuzi ya jinsi mpangilio wa nyumba (ndani) unatakiwa kuwa (physically).
Mfano mwanamke huwa na hisia kamili ya jinsi mpangilio na aina ya fanicha zinahitajika ndani ya nyumba, rangi ya mapazia, rangi za kuta, vyombo vya chakula, jiko aina ya kabati nk.
Kwake ni muhimu kujua na kuhusika kutengeneza mwonekano mzima ndani ya nyumba kuanzia sebuleni, jikoni, chumbani nk, kwani huwa na ndoto zake na kutimiza ndoto kwake ni kujisikia salama (security) katika maisha yake na yule ampendae.

Kama mwanaume hataweza kujua hili basi mwanamke anaweza kujisikia hapendwi au kujisikia mume hamjali hata kama amenunuliwa kila kitu.
Issue hapa ni kumshirikisha kikamilifu katika maamuzi yote kuhusu vitu vya ndani ya nyumba labda awe ni mwanamke ambaye umwambia au usimwambie yeye hana tatizo.
Mfano
Mwanaume mmoja alinunua nyumba mpya nchi fulani, then akanunua fanicha zote na kuziweka ndani ya nyumba hiyo, hata hivyo mke walipofika na kuambiwa mzee kanunua nyumba na ameshaweka fanicha zote, mwanamke alilia sana.
Je kwa nini alikuwa analia wakati mzee kafanya kazi nzuri?
Aliuugua ugonjwa wa (nest syndrome siyo empty nest syndrome) alikuwa anaumwa kukosa kutengeneza kiota chake mwenyewe (own nest) alijiona humo ndani ni kama si kwake kwa kuwa hakushirikishwa katika kununua nyumba na vitu vya ndani.
Alipenda sana na yeye kujisikia amehusika (responsible) katika kuijenga nyumba na kuingia humo.
Mwanamke huyu alipatwa na msongo wa kimawazo kwamba hathaminiwi wala kupendwa ndiyo maana hakuhusishwa katika maamuzi ya kununua fanicha ndani.

Hata hivyo si wanawake wote huwa smart linapokuja suala la mambo ya ndani kama vile fanicha, rangi za nyumba nk.

Tafakari!

Kama wewe ni mwanamke utajisikiaje/ulijisikiaje pale unakuta unaingia nyumba ya mwanaume kuishi naye ameshanunua kila kitu wewe ni kuishi tu?


Tuesday, March 10, 2009

Watoto wa tiger wapata mama

Ilipotokea hurricane ijulikanayo kwa Jina la Hannah huko South Carolina USA watoto wawili wa tiger walitelekezwa na mama yao hata hivyo Chimpanzee ajulikanaye kwa jina la Anjana aliendelea kuwalea kwa upendo wa hali ya juu kama watoto wake.
Anjana anajulikana kwa style yake ya kuwa mlezi na ameshawahi kulea watoto wa simba pia

Monday, March 9, 2009

Hutazama kwa undani

Ni baby boy au baby girl?
Mwanaume hupenda kujua hilo! Mwanamke siku zote hujihusisha zaidi na undani wa kitu kuliko mwanaume.
Hebu fikiria pale mtoto akizaliwa, mwanaume kitu ambacho atauliza siku zote “je mtoto ni wa kiume au wa kike?”
Hicho ndicho kinachomhusu wakati huo na ndicho kinachomhusu kuhusu mtoto ambaye amezaliwa na mara nyingi akishajua hilo basi imetoka.

Lakini mwanamke atamshika (hold) mtoto wake na kumuangalia (chunguza) kila kila kitu ataanza na vidole vya mkono na miguuni, sura kamili ya mtoto na atajua mtoto anafanana na nani baba (au baba anayemjua yeye mwanamke), nywele za mtoto, midomo, pua, mguu, kila kitu kuhusu mtoto.
Mwanamke huwa sensitive hata kujua hisia mbalimbali za mtoto hadi aina ya mlio anaotoa akilia na zaidi anajiweka tayari kuwa mama na mlezi wa mtoto.

Fikiria suala la harusi, mwanaume anachojua ni kuwa na harusi then mke ndani ya nyumba, lakini mwanamke huwaza na kutaka kujua kila kitu kuhusiana harusi kama vile rangi za nguo za harusi, aina za pete na duka gani wanaweza kupata, aina za nguo, maua, wapi watafanyia sherehe za harusi, aina ya wageni, nani atafungisha ndoa na kwa nini, atataka kujua nani atatoa huduma ya chakula na chakula gani kiwepo nk.
Yupo tayari kuzunguka mji Mzima kujua ni duka gani atapata kile anataka kwa ajili ya harusi yake.
Naamini ukimwachia mwanaume kila kitu kuhusu harusi anaweza ku-ruin au screw siku yako muhimu duniani maana mwanaume anachosubiri ni kukuvalisha pete na mwanamke kuwa ndani ya nyumba.
Wapo wanaume ambao pia wapo makini sana na details za kila kitu ila wanawake wao ni wengi zaidi.

Ukinunua gari mwanamke atataka kujua ni rangi gani. Ingawa mwanaume anaweza kuona rangi ya gari ni rangi tu muhimu ni aina ya gari linalodumu.

Pia wanawake hukumbuka sana mambo yote yanayohusiana na kalenda, kama vile birthday, anniversary na appointments.
kama ni mwanaume ni vizuri kukumbuka siku maalumu za maisha yako na ya mpenzi wako kwani ukijisahau anaweza kuhisi humjali.

Hata mkishaoana mwanamke huwa bado anakumbuka undani wa mwanaume jinsi alivyokuwa anafanya wakati wa wachumba au wakati unafanya juhudi za kumpata, anakumbuka siku amekutana na wewe mwanaume, anaweza kukwambia hata shati ulilokuwa umevaa, kiatu na hata mahali na mpangilio wa vitu ulivyokuwa sehemu mlipokutana mara ya kwanza.

Anakumbuka sana jinsi ulivyokuwa unamkumbatia na kumpa sifa zote kwamba yeye ni mwanamke bora duaniani na hakuna kama yeye.
Anakumbuka sana ulivyokuwa unamsifia mbele za rafiki zako na kila aina ya maneno matamu ulikuwa unamwambia ndiyo maana sasa anashangaa mbona upo hivyo.

Kumbuka mwanamke na mwanaume ni tofauti na hizi tofauti ndizo zinatufanya tuwe na mahusiano mazuri ya ya kudumu na yanayoridhisha kiroho, kimwili na kiakili na pale tunapojisahau ndipo tunarudisha nyumba maendeleo ya kukua kwa mahusiano yetu na matokeo yake kila mmoja anaanza kushangaa vipi upendo mbona unapoa.

Pia kumbuka vitu vidogo sana ambavyo zamani ulikuwa unafanya ni muhimu sana nab ado unahitaji kufanya tena na tena bila kuacha.
Upendo daima!

Friday, March 6, 2009


Those that have some means think that the most important thing in the world is Love.
The poor know that it is Money.
Gerald Brenan

Kumbe mnawaza chakula!

Picha kwa hisani ya Dada A. Hamidu Ripoti mpya imedhihirisha kwamba wanawake hutumia muda mwingi kufikiria kuhusu chakula kuliko sex na wanaume hutumia muda mwingi kufikiria kuhusu sex kuliko chakula.

Uchunguzi uliofanywa na tume ijulikanayo kama Weight Watchers, iligundua kwamba asilimia 58 ya wanawake huko Uingereza waliweza kufikiria kuhusu sex angalau mara 1o kwa siku na asilimia 70 walikiri kwamba walikuwa wanafikiria kuhusu chakula.
Pia ilidhihirika kwamba wanawake wengi walikuwa wanafikiria kuhusu body image (mwonekano wa miili yao) kama walikuwa hawafikiria (waza) kuhusu chakula.

Chakula ni complex issue kwa wanawake, hii haina maana sana wanwake wanakula sana bali inadhihirisha kwamba linapokuja suala la nini ale mwanamke huhusisha sana mawazo yake kuliko masuala ya sex ambapo mwanaume hujihisisha zaidi kufikiria.

Wanawake wengi hutumia muda mwingi kufikira chakula na body image kwa maana kwamba wengine hushinda njaa wakiogopa kunenepeana na kuonekana wana sura na miili ya ajabu.
Na wengine huishia kula chocolate tu au biscuits siku nzima wakiogopa kuwa na miili ya ajabu.

Source:
YellowBrix, The Scotsman

Thursday, March 5, 2009

Kabla hujaolewa!

Ndege wa tabia moja huruka pamoja! Ujana ni fahari pia ni wakati wa kufanya maamuzi muhimu kumchagua yule utatumia muda wako wote unaobaki duniani.
Pia mapenzi ni matamu, na kupendwa kutamu, wakati mwingine mapenzi huanza polepole na inafika siku yanakuja yanakufagia miguu yote, hata kabla hujajitambua vizuri unajikuta tayari upo kwenye ndoa kupitia kasi ya ajabu kwa jina la "Love is Blind"

Ndoa ni kupenda, ni commitment ya maisha, kukubali ndoa maana yake ni kukubali kwamba upo tayari kutoa kila kitu na kijikabidhi kwa mtu mmoja tu maisha yako yote, ndoa ni ahadi na agano la kumpenda yeye sasa na hadi kifo kitakapo watenganisha.

Ndoa ni zaidi ya unavyojisikia (feelings) ni zaidi ya mguso unaoupata ndani ya nafsi yako, ndoa ni kuudhihirishia ulimwengu kwamba umechagua kumpenda mtu mmoja, maisha yako yote, na kabla hujaanza kuvuna unachopanda sasa ni vizuri kufikiria kwanza huku ukiwa na akili timamu ili usije siku ukamlaumu mtu hahaha nisikutishe hakuna kitu kitamu kama ndoa!

UMERIDHIKA NA TABIA YAKE?
Naamini mpenzi wako ni the sweetest, cutest, lovable, barafu la moyo wako, is a real honey na majina mengine mengi tu, anakupa raha na unajisikia hakuna mwanaume kama yeye duniani anayekupa ridhiko la moyo ila ni yeye tu, kweli uchumba ni mtamu, ukitaka chochote anakupa, anapenda akuone kila wakati.

Kabla hujafika mbali na kutoa maamuzi jaribu kufikiria kwanza kwa makini zaidi zile tabia ambazo unahisi hujaridhika nazo.
Unajifariji kwa kuwa anakupenda basi ukiolewa naye utambadilisha au ataacha tu.

Uzoefu unaonesha kwamba vitu vingi ambavyo unaona sasa ndiyo vinakuvutia kwake kama vile jinsi anavyoongea, jokes zake, n.k vinaweza kukupa raha kwa muda mfupi sana wakati huu lakini ukishazoena naye baada ya kuoana naye, utatamani awe na kitu kipya kitu ambacho kwake haitawezekana na wewe utaanza kuwa bored.

Utani na jokes ni raha kwa unaposikia kwa mara ya kwanza au kwa mtu unayekuwa naye kwa mara ya kwanza, ila akishazoeleka ukajua kila kitu kuhusu yeye inakuwa kwisha kabisa anakukinai.
Kama ni mwanaume mwenye utani na jokes basi inabidi uwe una develop new skills za jokes zako kila baada ya muda fulani kabla ya expire date.

Vile vitu umekuwa unavipenda kwake sasa vinaweza kuwa usumbufu miaka 2 ijayo.

Ni vizuri kuangalia tabia endelevu ambazo hata baada ya miaka 10, 15 au 20 bado kwako hazitaleta shida.

Wazo kuu ni kwamba angalia miaka 10 ijayo maisha na yeye yatakuwaje kama unaona yatakuwa supper basi ingia kichwakichwa maana hakuna shida ila ukihisi unaona mawingu please think twice!

Inawezekana anamwamini mama yake kuliko wewe mke mtarajiwa na amekwambia bayana linapokuja suala la maamuzi mama yake ndiye top,
Inawezekana amekuahidi kwamba yupo tayari kuacha dini yake kwa ajili yako, hata hivyo uwe makini kwani suala la dini ndilo linafanya watu wauane duniani,
Inawezekana anajua kuutwika na sasa ametulia kidogo anasubiri uingie ndani ya 18 na wewe umejifariji kwamba utambadilisha, mara nyingi baada ya kuingia kwenye ndoa wanawake ndio hubadilika.
Inawezekana anavuta sana sigara na kwa sasa anavuta sigara moja kwa siku kwa sababu anakupenda, kumbuka wote wanaovuta sigara ukiwauliza watakwambia wanataka kuacha kuvuta sigara, fikiria maana bedroom inaweza kuwa tray vipisi vya sigara zake.

Inawezekana unajidanganya eti anakupenda hivyo tabia zake mbovumbovu ataacha unajifariji tu au unawezekana ume-fall in love na image, au hisia zako (feelings) ambazo zimezikosa upendo wa mwanaume.

Ndoa si 50/50 wala 100/100 bali ni 150/150 yaani kujitoa kwa ajili ya mwenzako zaidi ya asilimia mia, kwamba umechagua kazi ya kumpenda huyo mwanaume hapa duniani yeye tu bila kujali amefanya nini.

Pia usikubali kuolewa kwa sababu ndugu zako wanakushauri kwamba uolewe au kwa sababu sasa unahisi mwili unawasha sana unahitaji mume wa kukuridhisha au kwa sababu rafiki zako wanakusema sana kwamba mbona huolewi.
Au kwa sababu kiongozi wako wa dini anasema uolewe, olewa kwa sababu ni wakati wako na kwamba umekubali mwenyewe baada ya kukaa na kufikiria kwa makini na kumkubali mwanaume huyo.
Kawaida dunia nzima inaweza kukushauri na kukusema hata hivyo mwamuzi wa mwisho ni wewe maana wewe ndiye utakaye kuwa na huyo mwanaume siku meli yenu ya ndoa itakapokuwa inapita kwenye kina kirefu cha maji wakati wa dharuba kali, usiwategemee wanadamu kwani ndivyo walivyo ni vigeugeu.

Zaidi omba Mungu akupe amani ya kweli na huyo mwanaume ili uwe na uhakika na uamuzi unaenda kuutoa.

“Marriage is a school in which the pupil learns too late.”

Kama hupo makini kuchagua partner mzuri wakati wa kuolewa basi hiyo sentensi inaweza kuwa ni ukweli mtupu.

Wednesday, March 4, 2009

Live simply
Love generously
Care deeply
Speak kindly
Leave the rest to God.

Sunday, March 1, 2009

Wallet nayo!

Mwanaume akiwa na wallet kubwa husababisha mwanamke kufika kileleni kirahisi, au tuseme sexual pleasure ya mwanamke ina uhusiano mkubwa sana na ukubwa wa bank account ya mwanaume ( wealth).

Sijui kwa sababu huwa wanajua baada ya kumaliza mzee atamnunulia gari, au midhahabu, au pamba za nguvu au bills zote zitalipwa.

Au mwanamke anakuwa hana stress za kifedha so anakuwa relaxed na mzee!
Au wenye pesa ndo kuliwa maana asilimia kubwa ya wanawake wakiwa na wenye pesa hudanganya kuwa wamefika kileleni kumridhisha mzee, kumbe target ni kumtoa ngawira zake, golddigger hufanya lolote kuhakikisha wanapata.

Pia utafiti haujaonesha je kufika kileleni ndo kuwa na furaha katika maisha ya mahusiano na wahusika na pia ulifanyika nchi gani, hata hivyo wanawake ndo wenye ukweli na huu utafiti.
Unaweza kuwa na mwanaume mwenye pesa gunia lakini anaweza kuwa kitandani hana uwezo wowote kulinganisha na mwanaume ambaye hata wallet hana na mwanamke akafurahi.

Huu utafiti una walakini ndani yake sijui wengine mnasemaje?

Kwa maelezo zaidi soma hapa

Thina sithi Amen - Mthunzi Namba