"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, March 20, 2009

Bank zingine!

Mama wa Kinew zealand akiwa na mtoto ambaye amemzaa baada ya kutumia sperms za mume ambaye alikuwa ameshakufa Hata baada ya mume kufa mwanamke bado anaweza kuendelea kuzaa na mume wake.
Hilo limethibitika huku Nchini New Zealand ambako wanawake wawili wameshazaa watoto baada ya kutumia sperms za wanaume zao ambao walikuwa wameshakufa.

Kinachofanyika ni kwa mume na mke kwa hiari yao kwenda clinic (sperm bank) jaza fomu (consent form) na mwanaume hutoa sperm ambazo zitatunzwa in case mume akafa kabla hawajaamua kupata watoto.
Hata kama mume akifa, mke akitaka kuzaa hurudi clinic kuchukua sperms za mumewe na kupandikizwa kwa njia ya IVF (in-vitro fertilization)
Bado inaleta maswali kimaadili kuhusiana na haki za mtoto hasa akitaka kujua ilikuwaje tarehe yake (mtoto) kuzaliwa ikawa mbele ya tarehe ya kifo cha baba yake.

Bado ni jambo jipya katika dunia ya technolojia na inashangaza.

Wakati wajane wengine huenda kufuata benki pesa za waume zao waliokufa sasa wajane wanaenda benki kuchukua sperms ambazo waume zao waliacha.

Source:
http://www.stuff.co.nz/dominion-post/archive/national-news/1402676


7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ndio! hapo inaonyesha jinsi watu wawili walivyopendana na wanataka mtoto. lakini kweli itakuwa ni sawasawa? Mmh sijui kama nimeeleweka naona nimetingwa kidogo na hizi tekenologia za leo.

Lazarus Mbilinyi said...

Kila mtu ana maoni yake na hili suala ni gumu kimaadili na pia kwa mtoto ambaye anazawali baada ya baba kuwa alishafuka hata kabla mimba haijatungwa.

Kazi kwelikweli!

Anonymous said...

Hi, Nimeipenda hii lakini bado kuniingia akilini.Mtoto ataitwa jina la baba yupi? kwa mungu hii halali? Hapo pagumu
Msafiri.

Lazarus Mbilinyi said...

Msafiri,

Bado hili suala ni mjadala mkali je, Biblia inasemaje kuhusiana na hili, maana sperms ni za mume halali ila alishakufa, na mtoto naamini ataitwa jina la baba ambaye alishakufa kinachoshangaza ni kwamba baba hufa baada ya mtoto kuzaliwa na si mtoto kuzaliwa wakati baba alishakufa.
Pia je inakuwaje kama ndoa halali, mume huyo anaugua ghalfa na unahisi hataweza kushiriki tendo la ndoa na anaweza kufa je ukiomba madaktari wamtoe sperms kwa mume mwenyewe kukubali na bada ya kufa mke akatumia kibiblia ni sahihi?
Technolojia ya sasa ina maswali mengi sana.

kazi kwelikweli

Anonymous said...

Dear Mbilinyi, Mambo haya mimi siyajui ila ninachofahamu wazazi hukutana kimwili na kupata mtoto, yote hufanyika kwa maombi muhimu kama wakristo. Je kama mbugu hizo hazitakuwa na uwezo wa kutoa mtoto? Mi sijui ila nitachunguza zaidi.
Msafiri

Anonymous said...

Hii Kali, lakini na inakuwaje kama mke anataka kuzaa na mume wake hata baada na yeye (mke) kufa.
HG

Lazarus Mbilinyi said...

Dada HG,

Kama mume na mke wote wamekufa itakuwa ngumu kuzaa, ingawa mwanamke yeyote anaweza kuzaa na mwanaume ambaye alishalushaa kufa,

But I believe this is ungodly and an ethical.

Mungu tusaidie