"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, March 11, 2009

Hata kuchagua pazia kwake ni usalama! Mwanamke huhitaji kujisikia yupo salama kwa mume wake, rafiki au yeye mwenyewe.
Pia mwanamke hujisikia raha na salama zaidi anapoona mwanaume anayempenda anaonesha kweli yupo committed kwake.

Pia mwanamke anapoolewa hutazamia nyumba yake kuwa salama, na nyumba kuwa salama kwake ina maana kuwa na maamuzi ya jinsi mpangilio wa nyumba (ndani) unatakiwa kuwa (physically).
Mfano mwanamke huwa na hisia kamili ya jinsi mpangilio na aina ya fanicha zinahitajika ndani ya nyumba, rangi ya mapazia, rangi za kuta, vyombo vya chakula, jiko aina ya kabati nk.
Kwake ni muhimu kujua na kuhusika kutengeneza mwonekano mzima ndani ya nyumba kuanzia sebuleni, jikoni, chumbani nk, kwani huwa na ndoto zake na kutimiza ndoto kwake ni kujisikia salama (security) katika maisha yake na yule ampendae.

Kama mwanaume hataweza kujua hili basi mwanamke anaweza kujisikia hapendwi au kujisikia mume hamjali hata kama amenunuliwa kila kitu.
Issue hapa ni kumshirikisha kikamilifu katika maamuzi yote kuhusu vitu vya ndani ya nyumba labda awe ni mwanamke ambaye umwambia au usimwambie yeye hana tatizo.
Mfano
Mwanaume mmoja alinunua nyumba mpya nchi fulani, then akanunua fanicha zote na kuziweka ndani ya nyumba hiyo, hata hivyo mke walipofika na kuambiwa mzee kanunua nyumba na ameshaweka fanicha zote, mwanamke alilia sana.
Je kwa nini alikuwa analia wakati mzee kafanya kazi nzuri?
Aliuugua ugonjwa wa (nest syndrome siyo empty nest syndrome) alikuwa anaumwa kukosa kutengeneza kiota chake mwenyewe (own nest) alijiona humo ndani ni kama si kwake kwa kuwa hakushirikishwa katika kununua nyumba na vitu vya ndani.
Alipenda sana na yeye kujisikia amehusika (responsible) katika kuijenga nyumba na kuingia humo.
Mwanamke huyu alipatwa na msongo wa kimawazo kwamba hathaminiwi wala kupendwa ndiyo maana hakuhusishwa katika maamuzi ya kununua fanicha ndani.

Hata hivyo si wanawake wote huwa smart linapokuja suala la mambo ya ndani kama vile fanicha, rangi za nyumba nk.

Tafakari!

Kama wewe ni mwanamke utajisikiaje/ulijisikiaje pale unakuta unaingia nyumba ya mwanaume kuishi naye ameshanunua kila kitu wewe ni kuishi tu?


5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Inategemea; Kuna wanaume wengine wanapenda kujiandaa yaani wanapenda mambo ya nyumba na kuna wengine hawapendi kabisa. Binafsi nadhani ningejisikia raha nusu nusu. Kwa sababu, nami ningependa tukae na kujadili ni nini tunahitaji. USHIRIKIANO na hapo ndo utaona kila kitu ni chenu. Kwasababu ukikuta kila kitu kipo ndani utajuaje kama amenunua yeye kwa ajili yetu. mawazo yangu tu.

Anonymous said...

mimi nimemkuta mume wangu ana kila kitu yani nyumba kila kitu na anaupendo kweli na wala siku doubt kuhusu hilo, cha msingi nilimwomba Mungu anipatie ambae yeye mwenyewe Mungu amenichagulia, na tunaishi kwa upendo sana hamna mwenye dharau kwa mwenzie. dharau ni tabia ya mtu tu, kama mtu ni mcha Mungu na amebarikiwa wala haina majivuno hapo

Ms GBennett

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli kumjua Mungu na nguvu zake ni msingi namba moja wa ndoa imara.
Kila mmoja akina na hofu ya Mungu lazima atampenda mwenzake na kumpa kile anahitaji na ndoa itakuwa yenye baraka pia wote hujishusha ili kumuinua Kristo juu.
Muhimu pia ni kushirikiana na zaidi kuwa na mawasiliano ya kila wazo na mipango ya yale wanandoa wanataka kufanya.
Awe amenunua kila kitu au hajanunua jambo la msingi ni kushirikiana na kila mmoja kujiona ni sehemu ya mwenzake, ingawa kila wana ndoa ni tofuati na kila ndoa ina namna yake.

Upendo daima

Anonymous said...

Wala si jambo la kuchangua mwanaume anatakiwa anunue vyote, mwanamke naye anatakiwa aje mikono mitupu, ni wasiwasi tuu ,wala wasiogope,tatizo ni wanawake wenyewe wanafikiria eti wataoneka wanatumia vya watui,kama ni hovyo walipe na mahali basi kama wanataka usawa. Mwanamke akisha fika basi ni lugha moja "vya kwetu". Na siku zote ukiwaachia wanawake waingie na vya kwao utaona cha moto ndio maana watu wanaogopa kuoa wanawake wasomi,wanye vifedha mifukoni na hata wale wanajiweza kwa namna nyingine . labda tu wale wenye imani safi na wanao jua nini wanafanya wanaweza kuruhusiwa kuchangia kama makubaliano ya yeye na huyo comredi wake.
By FIKIRIKWANZA

Fikirikwanza said...

jongeza kwa kunawanawake ambao kuchangia kwao hawata kutamka kamwe ndani ya ndoa ,ni kama vile mwanamke anapo amua kukusaidia kulipa mahali sio kwa sababau anataka kuchangia ila ni kwasababu zake na wewe. kwa hiyo sometimes mamabo yananoga kwa kuwa wanaofanya wanajua what if?
ila nasisitiza wanawake wasiwe na wasiwasi ni kazi ya kina adam kuandaa kila kitu.